Mimi nataka ndoa, yeye anataka shule

chief1

JF-Expert Member
May 4, 2015
1,415
1,409
Habari zenu mabibi na mabwana,

Nina mchumba wangu mrembo sana, tulikutana mwaka uliopita, sasa kutokana na familia yake hakupata nafasi ya kusoma aliishia darasa la saba kutokana na kutengana kwa wazazi wake, alimaliza muda mrefu akaendelea kutafuta maisha tu, mimi nina miaka 27 najua hatupishani sana umri na yeye.

Aliniambia anatamani sana kusoma na angependa kusoma angalau mpaka kidato cha nne ndipo nimuoe, nikamwambia nimuoe tu halafu atasoma tukiwa tayari kwenye ndoa, akasema hawezi kusoma akiwa na mimba, sasa katika kuendelea nikashtukia ananiambia pastor kajitolea kumsomesha na akaanza masomo ya QT, elimu yangu degree.

Tukaendelea na maisha,sasa akawa yuko busy sana mpaka akawa anaona kumpigia simu ni kumsumbua, mara hapokei simu akidai yuko busy! okay! sasa hataki kuzungumzia mambo ya uhusiano na juzi kaniambia kama naona ananichelewesha nitafute mwingine wa kuoa.

Malengo yangu yalikuwa ni kuoa mwaka huu ikishindikana sana mwakani! sitaki kufika 30 sijaoa,sasa naona mwenzangu hana mpango tena wa ndoa hata mwakani! Sasa je, niachane nae nitafute mwingine au nimsubiri mpaka atakapoona inafaa? Mwenzangu kabadilika.
 
Uzuri ni kwamba hata huyo anayesomesha, hatooa huyo dada! Kumbuka kutokumsomesha wewe, mchumba hasomeshwi na mme wake mtarajiwa.
 
Uzuri ni kwamba hata huyo anayesomesha, hatooa huyo dada! Kumbuka kutokumsomesha wewe, mchumba hasomeshwi na mme wake mtarajiwa.
f18f2c920a3edc3ad84287e07301236d.jpg
 
maneno hujaelewa hata picha huelewi. unasubiri movie la kihindi.
 
Kwa hiyo kilichokuvutia kwake ni urembo wake na sio tabia. Haya sasa kizuri kula na wenzio. Kwa wale wote ambao wachumba au wake zao wa umri wa chini ya miaka 40 waliopo vyuoni au mashuleni kubali moja eiza Unachapiwa au ndio jumla kazamia kwa njemba nyingine. Wakati nipo chuoni huko dodoma miaka sita iliyopita wanawake na ndoa zao wanaficha pete zao wanaanza maisha mapya chuoni kana kwamba hajawai olewa kabisa, kumbe baba anaangaika na watoto nyumbani.
 
Back
Top Bottom