Mimi nataka ndoa, yeye anataka shule

Mimi nataka ndoa, yeye anataka shule

Mimba, nikitu kinapangwa. tatizo lako unataka umpe mimba akiwa bado anasoma kwa imani yako kuwa hawezi kukukimbia. Ungempa nafasi asome miaka miwili siyo mingi. kwa elimu yake na yako vigumu kweli mkaelewana mawazo. mwanamke huwa hakosei wewe ndo unakosea. tatizo niwewe na mawazo yako ya kukosa. Mwanamke uliyempenda kwa dhati anadi shule tena Q.T. mpaka zengwe ! ! ! je? angetaka kwenda elimu ya juu ingekuwaje? ? Mapenzi ni gharama, yapaswa umteende mwanamke ajue kuwa hapo alipo kafikishwa nanani.
 
Yani degree holder unataka kuoa mtu wa la saba,na tena bado anakudrive craizy?pathetic
love haina elimu mkuu, ukimuona IQ yake ni tofauti na elimu yake, ni mzuri kichwani pia
 
Habari zenu mabibi na mabwana,

Nina mchumba wangu mrembo sana, tulikutana mwaka uliopita, sasa kutokana na familia yake hakupata nafasi ya kusoma aliishia darasa la saba kutokana na kutengana kwa wazazi wake, alimaliza muda mrefu akaendelea kutafuta maisha tu, mimi nina miaka 27 najua hatupishani sana umri na yeye.

Aliniambia anatamani sana kusoma na angependa kusoma angalau mpaka kidato cha nne ndipo nimuoe, nikamwambia nimuoe tu halafu atasoma tukiwa tayari kwenye ndoa, akasema hawezi kusoma akiwa na mimba, sasa katika kuendelea nikashtukia ananiambia pastor kajitolea kumsomesha na akaanza masomo ya QT, elimu yangu degree.

Tukaendelea na maisha,sasa akawa yuko busy sana mpaka akawa anaona kumpigia simu ni kumsumbua, mara hapokei simu akidai yuko busy! okay! sasa hataki kuzungumzia mambo ya uhusiano na juzi kaniambia kama naona ananichelewesha nitafute mwingine wa kuoa.

Malengo yangu yalikuwa ni kuoa mwaka huu ikishindikana sana mwakani! sitaki kufika 30 sijaoa,sasa naona mwenzangu hana mpango tena wa ndoa hata mwakani! Sasa je, niachane nae nitafute mwingine au nimsubiri mpaka atakapoona inafaa? Mwenzangu kabadilika.
Mkuu kama wa kwangu ananikomalia aende degree licha ya kuwa nilimvumilia kasoma certificate hadi diploma ualimu..
 
Hivi hapo hujaelewa nini Jamani?au ndio utaki kukubali matokeo kuwa huyo hana mpango na wewe?
hivi wanawake mkoje??? hapo ni kwa sababu kajua nampenda sana, hajui kwamba nina uwezo wa kuachana nae kabisa
 
Yani degree holder unataka kuoa mtu wa la saba,na tena bado anakudrive craizy?pathetic
Za wa darasa la 7 huwaga tamu sana maana hazijawa too much used huko vyuoni😛😛😛😛😛
 
Hakika pastor "anamsomesha"... kama huajaelewa hapo, rudisha hicho cheti chako chuoni.
 
Kubali yaishe bro..huna chako apo
siyo kirahisi mkuu, imagine kuna mwingine ananibembeleza nimuoe lakini sina interest nae, na ni mzuri tu wa kuonekana katikati ya wengi na ana kazi yake..
mkuu life is viceversa sometimes
i am in prayers
 
Hakika pastor "anamsomesha"... kama huajaelewa hapo, rudisha hicho cheti chako chuoni.
mkuu anaishi kwa pastor, so, mama mchungaji anajua pia, na huyo pastor kashawahi kuwasaidia wengi kuwasomesha
na najua she is very decent, i trust her, ameokoka, akili inasizi sometimes... but i can let her go..
 
Kwanin ujiwekee limitations? Unasema unataka kuoa kabla hujafika 30, una ahadi na Mungu? Una uhakika utapata ndoa bora ukilazimisha kuoa sasa hivi?
Kwanin usijiachie? Kuanza upya sio vibaya. Tafuta mwingine ujipange naye,.
Kulazimisha ndoa ni ujinga.
Words,
 
Back
Top Bottom