Mimi nataka ndoa, yeye anataka shule

Mimi nataka ndoa, yeye anataka shule

Habari zenu mabibi na mabwana!
Nina mchumba wangu mrembo sana,tulikutana mwaka uliopita, sasa kutokana na familia yake hakupata nafasi ya kusoma aliishia darasa la saba kutokana na kutengana kwa wazazi wake,alimaliza muda mrefu akaendelea kutafuta maisha tu, mimi nina miaka 27 najua hatupishani sana umri na yeye! aliniambia anatamani sana kusoma na angependa kusoma angalau mpaka kidato cha nne ndipo nimuoe, nikamwambia nimuoe tu halafu atasoma tukiwa tayari kwenye ndoa, akasema hawezi kusoma akiwa na mimba, sasa katika kuendelea nikashtukia ananiambia pastor kajitolea kumsomesha na akaanza masomo ya QT, elimu yangu degree
Tukaendelea na maisha,sasa akawa yuko busy sana mpaka akawa anaona kumpigia simu ni kumsumbua, mara hapokei simu akidai yuko busy! okay! sasa hataki kuzungumzia mambo ya uhusiano na juzi kaniambia kama naona ananichelewesha nitafute mwingine wa kuoa!
malengo yangu yalikuwa ni kuoa mwaka huu ikishindikana sana mwakani! sitaki kufika 30 sijaoa,
sasa naona mwenzangu hana mpango tena wa ndoa hata mwakani!

sasa je, niachane nae nitafute mwingine au nimsubiri mpaka atakapoona inafaa? mwenzangu kabadilika
Achana naye huyo. Kukuambia tafuta mwingine naye mwisho wa siku atakuambia nimepata mwingine!
 
Kwanin ujiwekee limitations? Unasema unataka kuoa kabla hujafika 30, una ahadi na Mungu? Una uhakika utapata ndoa bora ukilazimisha kuoa sasa hivi?
Kwanin usijiachie? Kuanza upya sio vibaya. Tafuta mwingine ujipange naye,.
Kulazimisha ndoa ni ujinga.
 
Habari zenu mabibi na mabwana!
Nina mchumba wangu mrembo sana,tulikutana mwaka uliopita, sasa kutokana na familia yake hakupata nafasi ya kusoma aliishia darasa la saba kutokana na kutengana kwa wazazi wake,alimaliza muda mrefu akaendelea kutafuta maisha tu, mimi nina miaka 27 najua hatupishani sana umri na yeye! aliniambia anatamani sana kusoma na angependa kusoma angalau mpaka kidato cha nne ndipo nimuoe, nikamwambia nimuoe tu halafu atasoma tukiwa tayari kwenye ndoa, akasema hawezi kusoma akiwa na mimba, sasa katika kuendelea nikashtukia ananiambia pastor kajitolea kumsomesha na akaanza masomo ya QT, elimu yangu degree
Tukaendelea na maisha,sasa akawa yuko busy sana mpaka akawa anaona kumpigia simu ni kumsumbua, mara hapokei simu akidai yuko busy! okay! sasa hataki kuzungumzia mambo ya uhusiano na juzi kaniambia kama naona ananichelewesha nitafute mwingine wa kuoa!
malengo yangu yalikuwa ni kuoa mwaka huu ikishindikana sana mwakani! sitaki kufika 30 sijaoa,
sasa naona mwenzangu hana mpango tena wa ndoa hata mwakani!

sasa je, niachane nae nitafute mwingine au nimsubiri mpaka atakapoona inafaa? mwenzangu kabadilika
Uhusiano na binti anaesoma tena unaemsaidia katika masomo yake ili aje awe mkeo kunahitaji akili ya mwendawazimu. Ni kujipotezea muda, pesa na kujikosesha warembo sahihi na stahiki wa kuoa. Mkuu kama yeye anasoma, moango wako wa kumuoa achana nao kabisa na tafuta tu mwingine.
 
Sijui vijana wa hii karne tumejazwa nini vichwani. Mtu jana tu kaja na Uzi wa kusomesha na kupigwa china, kenge nyingine inaomba ushauri hapa. Em shtuka bana tafuta mwingine mbona wapo wengi tu.
 
Digrii holder unakuwa kama hujasoma Piga chini tafuta njia nyingine wewe Sio loan bord
 
kamata mwingine...
au tukufundishe uwindaji?
 
Back
Top Bottom