Mimi na wewe tunatumia kipi kutoka Urusi?

roadmaster

JF-Expert Member
Mar 21, 2023
1,484
2,572
Watanzania wa kawaida kama mm ,wewe na yule tunatumia bidhaa Gani kutoka urusi!?

Mitumba ya nguo inatoka western Europe. Mitumba ya fridge, pasi, tv, radio, phone ni kutoka western Europe.
Magari ni western, Asia, USA nk.

Madukani ni Asia yani China, Pakistan, India, Bangladesh, n.k.

Sasa Urusi vipi?
 
Russia-Tanzania In 2021, Russia exported $161M to Tanzania. The main products that Russia exported to Tanzania are Wheat ($100M), Nitrogenous Fertilizers ($26.5M), and Semi-Finished Iron ($7.79M).

Sent from my SM-G998B using JamiiForums mobile app

Hizo bidhaa kutoka Russia ni MTUMBA ??!!, manake Watz kwa kuhusudu mitumba kutoka west Europe hatujambo.😀😀
 
Watanzania wa kawaida kama mm ,wewe na yule tunatumia bidhaa Gani kutoka urusi!?

Mitumba ya nguo inatoka western Europe. Mitumba ya fridge, pasi, tv, radio, phone ni kutoka western Europe.
Magari ni western, Asia, USA nk.

Madukani ni Asia yani China, Pakistan, India, Bangladesh, n.k.

Sasa Urusi vipi?
Zaidi ya app ya telegram,hakuna kingine
 
Urusi hawapendwi na wenzao sababu wana tabia za kiswahili, Ulaya marufuku Rais kung'ang'ania madaraka, lakini Putin hataki kuelewa hilo ana miaka 28 madarakani yeye suala la kungatuka halimuhusu kabisaa

Ulaya chakula ni haki ya kila mtu, ila yeye ukimuudhii huli, ukisikia Rais anang'ang'ania madaraka sehemu yoyote ile, basi jua anaemsapoti ni Mrusi na ndo uadui mkubwa unaanzia hapo kati ya Mrusi na Marekani, Marekani pamoja na ushenzi wake wote ,lakini lazima tumshukuru ana vitu vya msingi sana

Fikiri vipi kama kungekuwa hakuna mahakama za kimataifa, serikali ya Kenya ingewafanyeje raia wake wanaondamana, maana uwezo wanao,na ninavyozijua serikali za watu weusi,

Hitimisho hakuna muislam anaweza ona lolote zuri toka kwa Marekani maana wao wanaamini kuwa mwarabu ni ndugu yao na Marekani ana ugomvi na ndugu yao
 
Hizo bidhaa kutoka Russia ni MTUMBA ??!!, manake Watz kwa kuhusudu mitumba kutoka west Europe hatujambo.😀😀
Nani kawakataza kutengeneza nguo mpaka mvae nguo zilizotupwa na watu wengine (Kafa Ulaya Mazishi Afrika).
 
Hitimisho hakuna muislam anaweza ona lolote zuri toka kwa Marekani maana wao wanaamini kuwa mwarabu ni ndugu yao na Marekani ana ugomvi na ndugu yao

mkuu unaweza kuthibitisha juu ya hilo la waislam wote duniani kuwachukia wamarekani
 
Uislam umeingiaje hapa?
 
Watanzania wa kawaida kama mm ,wewe na yule tunatumia bidhaa Gani kutoka urusi!?

Mitumba ya nguo inatoka western Europe. Mitumba ya fridge, pasi, tv, radio, phone ni kutoka western Europe.
Magari ni western, Asia, USA nk.

Madukani ni Asia yani China, Pakistan, India, Bangladesh, n.k.

Sasa Urusi vipi?
Watu weusi wanaishi Urusi wanakuambia ukitembea mtu moja mweusi ni hatari kunaubaguzi wa rangi sana wanatembea makundi.
 
Yaani ukiamka asbhi ukala chochote kitokanacho na ngano ni murusi ukiona mazao yamestawi huko vijijini jua mbolea ya mrusi kwa kifupi uhai wako ameushika

Maana msosi ndio msingi
Watanzania wangapi wanakula hiyo ngano, wewe mwenyewe hapo unashindia chai ya rangi na mihogo au viazi au sana sana vitumbua au uji.

Maeneo mengi Tanzania wala hawatumii mbolea labda ya samadi na wengi bado wanalima hivyo hivyo na hiyo mbolea ya hao warusi ni bora sana kwa kuua rutuba. Russia hana lolote.
 
Back
Top Bottom