Umeme mwingi na bei nafuu umeifanya Bangladesh kuwavutia zaidi wawekezaji na viwanda

Maghayo

JF-Expert Member
Oct 5, 2014
13,716
29,072
Mzuka wanajamvi.

Miaka ya karibuni Bangladesh imepiga hatua sana kiuchumi.

Hii ni kwasababu wanazalisha umeme mwingi na bei nafuu.

Wawekezaji wengi kutoka majirani India na Pakistan wamewekeza sana Bangladesh kwenye viwanda.

Pia nchi za Asia na ulaya zinawekeza sana sasa hivi Bangladesh kwasababu ya unafuu wa umeme na bei rahis.

Umeme mwingi na wa bei nafuu imemfanya Bangladesh ipige hatua kiuchumi.

Matajiri na middle class Bangladesh sasa hivi wanaongezeka kwa kasi ukilinganisha miaka ya nyuma.

Kupitia umeme wanawake wengi Bangladesh wameajiriwa kwenye viwanda vya kushona nguo ambazo zinavaliwa kila mahali duniani.

Sisi tumezubaa. Sasa hivi Afghanistan chini ya Taliban nayo inakuja kwa kasi kwenye uchumi. Baada ya miaka mfano wachumi wametabiri Afghanistan itapiga hatua kubwa sana.

Maghayo is a senior JF local and international analyst and correspondent and a London based Chatham house think tank.
 
Pia Bangladesh meli nyingi chakavu hazitumiki tena zinapelekwa Bangladesh ambapo wanazidimantle machuma chakavu na vitu vingine. Hii imeajiri vijana wengi sana wa Bangladesh.
 
Niliandika kwenye jukwaa la kimataifa kuhusu uchumi wa Bangladesh kwamba ni mkubwa kuliko uchumi wa taifa lolote la Africa. Lakini watu walinikejeli. Nilijaribu kuwaonyesha kwamba wenzetu Asia wanapiga hatua tofauti na Sisi Africa
 
Sasa hawa wasomi wetu na ma Phd na ma Master yao wanatupeleka wapi?
Naamini kusoma sio kazi, kazi ni baada ya kusoma kwenye uga wa maisha
 
Hivi ilikuwaje sisi tukashindwa kuliteka soko nguo baada ya kulima pamba nyingi kadri tuwezavyo?
 
Mzuka wanajamvi.

Miaka ya karibuni Bangladesh imepiga hatua sana kiuchumi.

Hii ni kwasababu wanazalisha umeme mwingi na bei nafuu.

Wawekezaji wengi kutoka majirani India na Pakistan wamewekeza sana Bangladesh kwenye viwanda.

Pia nchi za Asia na ulaya zinawekeza sana sasa hivi Bangladesh kwasababu ya unafuu wa umeme na bei rahis.

Umeme mwingi na wa bei nafuu imemfanya Bangladesh ipige hatua kiuchumi.

Matajiri na middle class Bangladesh sasa hivi wanaongezeka kwa kasi ukilinganisha miaka ya nyuma.

Kupitia umeme wanawake wengi Bangladesh wameajiriwa kwenye viwanda vya kushona nguo ambazo zinavaliwa kila mahali duniani.

Sisi tumezubaa. Sasa hivi Afghanistan chini ya Taliban nayo inakuja kwa kasi kwenye uchumi. Baada ya miaka mfano wachumi wametabiri Afghanistan itapiga hatua kubwa sana.

Maghayo is a senior JF local and international analyst and correspondent and a London based Chatham house think tank.
Yani kwa msingi huo unatuambia Watanzania kwamba, tunasuasua na miradi ya kuzalisha ugavi na hivyo tunashindwa kuwashawishi wawekezaji kuja hapa kuwekeza?

Je, tuna mlaumu nani?

Unawaambia nini wale wenye hoja ya kwamba, ni wingi wa Wawekezaji ndio unafanya umeme kutokutosheleza ujio wao?

Je, bado Hayat Rais alifanya makosa na mradi wa stiegler?
 
Back
Top Bottom