mapenzi yana wenyewe jamani!!
mi nanawa mikono
tangu niyajue furaha ni 40% wenge na huzuni 60%
mda mwingine yananiharibia status yangu kwa watu wangu wa karibu...nakuwa na hasira.kila mtu namjibu kwa ukali.
chakula nakiona hakina ladha nkila nakuwa kama nataka kukitapika.usiku nashindwa lala vizuri.nakonda
sijui wenzangu mnahimili vipi?
niko very royal...one man chick...michepuko sijawahi but ananizingua
najitahidi kuwa mwema,kuspend quality time...hata kwa simu...
nilimkubalia ye msela tu ndo anaanza tuyajenge tufike mbali..kwa juhudi na mungu akijalia.nkawakatalia waliokwisha settle down na minoti yao sababu yako..
but we msela unazingua..unazingua vibaya mno
we unanitemea shit thn unanipotezea..mimi nakufariji kwa matatizo unayopitia unadai nakupigia kelele..
mi nkitembea mtaani tu muuza duka ananililia..muuza mkaa anachombeza.muuza bucha nae hayupo nyuma.
..muuza genge kila nkifika anakonyeza mfululizo...vibanda vya mpesa ndo wanachukua bila kujua namba na kusumbua....msugua kucha ananibembeleza niwe wake..eti tangu aanze hiyo kaz katengeneza kucha wadada kwa mamia ila mimi tu ndo kanipenda..nkipanda daladala makonda si tamdika si mnaz mmoja si tegeta wakinipa risiti wanajibanza wanaomba namba..kila mtaa ntaoingia mi nageukiwa..kila mgeni kijana ataekuja home ananitaka
we kwanini unaninyanyasa mwana wa mwenzio? kisa kukupenda?
wakaka mkipendwa pendekeni basi..au mnatakaje??