Mimi mwalimu,Mafanikio niliyoyapa mwaka 2014 na ya 2015 na matarajio yangu 2016

Nimeajiriwa serikalini mwaka 2013.mwaka 2014 niliweza kununua kiwanja chenye thamani ya milioni sita(hapa dsm),na nikaanzisha ujenzi ambao ulinigharimu milioni kumi nne hadi kufika kwenye mkanda wa juu(lenta). mwaka 2015 namshukuru mungu nimeweza kuipaua yote ambapo imenigharimu kama milioni saba pia nimeweka grili sehemu zote ambazo zimenigharimu kama milioni moja na laki saba.pia nimeweza kufanya wiring nyumba yote,na kuipiga plasta baadhi ya vyumba kwa ndani. malengo yangu 2016,mungu akinisaidia ni kuimalizia nyumba yangu pia nataka kufungua kampuni ambayo itakuwa inahusika na maswala ya ajira. kama wewe unaamini ajira yako haikulipi,kwa nini ulionao wanapata maendeleo? be care

Hongera sana mkuu!!,lkn naomba nikuulize kidogo;Hivi lengo la hii post yako nini,Maana haujaelezea ni kwa namna gani(mbinu),uliweza kupata pesa za kujengea nyumba yako ili wengine nao waige kwako,kinyume chake ni km umejisifusifu jambo ambalo si zuri maana huwezi jua labda humu JF kuna Walimu waliofanya makubwa zaidi.
 
Mimi nilishindwa kuwa mnafiki, sitaki unafiki na sitaki kubeba dhambi ya kuto concetrate kwenye kazi yangu na kupiga deal! Ni aibu na ni hatari sana kubeba dhambi ambayo itakutafuna daima! Imagine kila watakapokuwa wanapata shida maishani mwao watakukumbuka kwa kutowafundisha vizuri. Naogopa na ndio maana niliacha ualimu! Ualimu ni dhamana kubwa maana unabeba maisha ya watu familia zao. Inahitaji moyo wa kujitoa sana. Sasa huku unafundisha huku una kampuni! Huwezi kutumikia mabwana wawili kwa wakati mmoja. Acha ualimu unawapoteza watoto ambao hawana hatia.
 
Ni vizuri kumuuliza anafanya biashara gani kuliko kumkashifu.Isije ikawa jamaa anapokea mirungi kutoka Kenya na kuuza baada ya mda wa kazi.
 
Mkuu mwalimu,

Kwanza hongera kwa mafanikio.Naomba ututendee haki walimu wenzio kwa kutuambia mbinu ulizotumia hadi kufikia hapo ili nasi tubadili mtazamo kuwa ualimu ni umasikini na tufuate nyayo

Karibu.
 
Hongera sana mkuu!!,lkn naomba nikuulize kidogo;Hivi lengo la hii post yako nini,Maana haujaelezea ni kwa namna gani(mbinu),uliweza kupata pesa za kujengea nyumba yako ili wengine nao waige kwako,kinyume chake ni km umejisifusifu jambo ambalo si zuri maana huwezi jua labda humu JF kuna Walimu waliofanya makubwa zaidi.

ni kweli ila naweza nikashukuru kwa hiki nilichokifanya kwa huu muda ndugu.najua wapo wenye uwezo zaidi ya huu tena ni mkubwa lakini naweza kumshukuru mungu kwa hapa nilipofikia
 
Mkuu mwalimu,

Kwanza hongera kwa mafanikio.Naomba ututendee haki walimu wenzio kwa kutuambia mbinu ulizotumia hadi kufikia hapo ili nasi tubadili mtazamo kuwa ualimu ni umasikini na tufuate nyayo

Karibu.

mkuu najua unapenda nikupe siri ya mafanikio yangu.ngoja nikuPM kwa sabab kuna vitu ninavyovifanya lakini sipendi wote wafaham.nakuPM mkuu
 
Labda kama private sector. Ila kama ni govt.something wrong somewhere. Hayo yanafanywa na waajiliwa labda wa bandari, tra, takukuru au traffic au wanyamapori. In education sector your playing unknown game
 
kwa wastan wa gharama ya hyo nyumba kila mwez amejiwekea sh 869,697 mbali ya fedha za chakula na mavaz na malaz kwa sasa,hebu weka vyanzo vyako vya mapato mbali na mdhahara wa ualimu
 
We ni mwalimu
Tuseme unapokea 750,000 kwa mwezi
750,000x12x3=27,000,000 iyo pesa net kama hujatumia chochote
Haya kiwanja -6m
Ujenzi hadi renta-14m
Kupauwa-7m
Grill-1m laki saba
Jumla 28m na laki saba
Kwa hesabu izo mshahara wako huwezi kufikia hapo unabishara zingine otherwise magufuri akutembelee
 
unafiki mbaya mwalimu umejitahidi.. maana shughuli ya kumiliki nyumba mjini.. ni kupambana sana
Ila sasa kwa mshara wa bei gani mpaka wewe kufikia hapo.? hongera

atakuwa ni mwalimu by profession lkn msimamizi wa walimu na ana masters, hivyo analipwa kama mkuu wa idara of which is not less than 2,000,000/- basic salary.

na atakuwa anechukua mkopo, kwa miezi 60, anaweza pata 30,000,000/-
 
Msimuhukumu inawezekana ni mkuu wa shule so lile jipu alilolitumbua magufuli la elimu bure kwa kutoa michango ambayo baadhi ya wakuu ilkuwa ndio dili lao inawzezekana kabisa hvyo vyumba vlivyobaki ikawa ndo majaaliwa tena
 
Back
Top Bottom