Ndugu WanajamiiForum, hamjambo? Mimi ni mgeni hapa, sana. Siku ya leo, Jumamosi 26 Desemba, 2009, ni siku yangu ya kumi (10) tu. Kwa hiyo bado sina hakika kama ninalotaka kuuliza linaulizika au vipi, kama linaruhusiwa au vipi, iwapo mgeni kama mimi naruhusiwa kuuliza hivi, au sina budi kuishia kujitambulisha tu. Mtanielimisha kwa yote. Na natanguliza shukrani zangu za dhati kwa uvumilivu wenu kuhusiana na umbumbumbu wangu.
Nina kaswali kadogo tu naomba kusaidiwa. Nakitafuta kitabu cha Mheshimiwa Jayantilal Keshavji Chande (Andy Chande) kinachoitwa "Whither directing your course". Ni e-book ya mkusanyiko wa kazi zake ambao upo katika tovuti yake ya http://www.andychande.com. Nimeshindwa kuipata, na naomba wajuzi wanielimishe namna ya kukipata, au wanipatie kama wanacho. Natanguliza shukrani za dhati kwa Wanajamii Forum. Manq