MIMI: Hivi ni kweli kupenda kutumia sana neno hili ni ishara ya ubinafsi?

Wakuu salaam.

Natumai mko vizuri,mkiendelea na majukumu mbalimbali.

Kama kichwa cha mada kinanyosema.

Hivi ni kweli mtu anayependa sana kutumia neno "mimi", katika mazungumzo yake, ni ishara ya kuwa ni mbinafsi?
Katika historia ya kuumbwa mwanaadamu,baada ya kutoka tangazo la kuumbwa mwanaadamu,likatolewa agizo toka kwa Muumba "mpe heshima Adamu....." Ibilisi akakataa,na akatia kibri na akasema,,,,,MIMI ni Bora kuliko huyu...! Sasa tangu wakti huo kila anayetumia neno "Mimi" huwa atafuatisha tabia ya majivuno,dharau,kibri kwani muanzilishi ni Shetwani.
 
Ahsanta.
 
Haya ni matumizi ya kawaida ya "mimi", hebu soma vizuri mada.
Wee ndo hujanielewa... Nilimaanisha yule mtangazaji pia ana ubinafsi???! Napenda jinsi anavyohitimisha katika habari zake siki zote lazima aanze na MMIMI....... Inavutia sana Kama angekua msanii basi Mimi ni shabiki wake namba moja
 
Nimekuelewa ndio maana nimekwambia hivyo.

Kusema kupenda sana kutumia "Mimi" ni ishara ya ubinafsi, haimaanishi ya kuwa kila anayetamka "Mimi" basi ni mbinafsi, hapana.

Tunafahamu ya kuwa "mimi " huwa tunaitumia katika mazungumzo yetu ya kila siku.

Lakini "mimi" hiyo hiyo inaweza ikawa ni ishara ya ubinafsi pale itakapo tumika katika muktaza flani.
 
Matumizi yaliyokithiri ya mimi ni ishara ya ubinafsi sana. Hata kwenye mahusiano, mtu akishaanza kuwa na mimi, mimi nyingi ninaona ni mtu asiyeweza kuwa 'humble'.
 
Umesema kweli.
 
Wakuu salaam.

Natumai mko vizuri,mkiendelea na majukumu mbalimbali.

Kama kichwa cha mada kinanyosema.

Hivi ni kweli mtu anayependa sana kutumia neno "mimi", katika mazungumzo yake, ni ishara ya kuwa ni mbinafsi?
Kwa jinsi ulivyoweka hapo haionyeshi kuwa ni ubinafsi.ila likitumika mahali kama,'hata mimi mwenyewe/pia...' au 'kama mimi mwenyewe/pia...' n.k.....
 
Kwa jinsi ulivyoweka hapo hainyoshi kuwa ni ubinafsi.ila likitumika mahali kama,'hata mimi mwenyewe/pia...' au 'kama mimi mwenyewe/pia...' n.k.....
Linakuwa linaashiria ubinafsi.
 
Back
Top Bottom