Watunduru
Senior Member
- Dec 29, 2011
- 170
- 39
Imekuwa ni jambo la kawaida mzazi kukamatwa,kutozwa faini au hata kifungo kwa sababu tu eti mtoto wake wa kike {mwanafunzi}kapewa mimba,au mtoto wa kiume katia mimba.tusiojua sheria tunashindwa kuelewa kigezo kinachotumika kumtia hatiani mzazi kwa kosa ambalo kimsingi hakulifanya yeye binafsi na pengine hata wakati kitendo kinafanyika hakuwa na habari na au asingependezwa nacho.hebu wana sheria nisaidieni ktk hili.