Mimba ya mke wangu inanitesa

Pole kaka, Mimi nilikua mjamzito mwaka jana mume wangu nilikua simpendi akiwepo nyumbani ni full maugomvi yaani nilikua nasikia kumpiga kabisa, ila asipokuwepo naumia roho na namkumbuka sana. Ole wake akionja pombe siku hiyo hatutalala chumbani namwagia kitanda maji halafu nalala sebuleni hadi asubuhi,alichokua anafanya anaondoka home asubuhi anarudi usiku na wala haniulizi kabisa. Sasa hivi nimebadilika nampenda na wala simsumbui tena, hivyo vumilia tu yataisha
 
Kaka wala husiwe na wasiwasi,hilo ni la kawaida kabisa kwa akina mama pindi wanapokuwa wajawazito,cha msingi endelea kumpenda zaidi na kuwa naye karibu,baada ya kujifungua atakuwa katika hali yake ya kawaida.mungu akubariki
 
hahahah
 
inakuwaje
wale
walopewa
mimba
nje
ya
ndoa
si
wanatesekeka
sana?
 
wengine wanajifanyisha tu mm wife ni mjamzito na ni memwambia asiniletee drama zozote mbona katulia tu ,na tunalea mimba kwa amani tu
 
Acha mchezo na mimba!

Juzi nimeenda pokea mihogo stendi imetumwa kutoka dar, eti ya hapa haina ladha! mihogo ya elfu 5, inasafirishwa kwa elfu 10, unawasha gari unatembea 25km kuifuata!

Mimba zinatesa sana.

Mimba oyeeeeeeee
 
sory nimetumia maneno ya kuchanganya kidogo.., mimba kaibeba yeye na mim ndo nili-isababisha.

Bado hujanijibu swali langu, hiyo mimba siyo yako? Uliisababishaje? Ulimtafutia mwanamme halafu akaja akampa hiyo mimba?
 
Hii kitu sijui kama ina ukweli mbona mke hajawahi kunisumbua? Mimba inakuwa sababu ys fujo badala ta amani na upendoo?
 
wengine wanajifanyisha tu mm wife ni mjamzito na ni memwambia asiniletee drama zozote mbona katulia tu ,na tunalea mimba kwa amani tu

Huo ndo uwanaume, wakati mwingine wanawake tunajiendekeza tu hamna cha sababu ya mimba wala nini. Mi mimba zangu zote sijafanya ujinga huo unamsumbua mtoto wa mwenzio hivyo kisa nini? Mimba sio ugonjwa bwana
 
Sitasahau kuna wakati nilikuwa na hamu ya kusikia harufu ya mavi ya kuku wa kisasa, ila mume bamsapu ashukuru mwenyewe nilikuwa najua nitapita wapi niisikie..
 
Halafu wana makusudi sana aisee lazima ubebe pochi kubwa muende wote Clinic hahaha
 
Mimba za wanawake tukiziendekeza wanaweza hata kutukalia kichwani... Kuna rafiki yangu siku alizunguka mji mzima anatafuta mahindi ya kuchomwa....
Mi siendekezi huo upuuzi...
 
Kaka wala husiwe na wasiwasi,hilo ni la kawaida kabisa kwa akina mama pindi wanapokuwa wajawazito,cha msingi endelea kumpenda zaidi na kuwa naye karibu,baada ya kujifungua atakuwa katika hali yake ya kawaida.mungu akubariki
asante sana kwa kunitia moyo
 
Mimba za wanawake tukiziendekeza wanaweza hata kutukalia kichwani... Kuna rafiki yangu siku alizunguka mji mzima anatafuta mahindi ya kuchomwa....
Mi siendekezi huo upuuzi...
mkuu wew utakuwa bandidu asiye na huruma hata chembe.., hivi unaweza kulala na kumuacha mkeo analia usiku kucha sababu kakosa miwa..., na usingiz ukaja kabisa!!!!!!. sidhan kama unamaanisha ulichosema
 
Reactions: BAK
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…