Mimba imemfanya amtoroke mumewe | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mimba imemfanya amtoroke mumewe

Discussion in 'Mahusiano, mapenzi, urafiki' started by BASHADA, Feb 8, 2012.

 1. BASHADA

  BASHADA JF-Expert Member

  #1
  Feb 8, 2012
  Joined: Jul 13, 2011
  Messages: 487
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 35
  Wana JF, heshima mbele.

  Nina rafiki yangu wa karibu mno kiasi cha kuitana ndugu. Alifunga ndoa mwaka jana october. Mwisho wa mwezi December mkewe akapata ujauzito. Kazini kwake ni Mikoani lakini yuko Dar kimasomo. Jamaa anasoma masters na mrs ni graduate and degree moja.
  Mwezi november alienda kazini kwake akiwa anashughulikia ujenzi wa nyumba yake ambayo sasa anapaua, akakaa mpaka january.
  Hakupanga chumba ila akawa amefikia kwa rafiki yake wa karibu sana ambaye ana nyumba kubwa ambako muda wote amekuwa akifikia hapo, tangia aende masomoni, ukizingatia kuwa wakati wa kwenda shule alirudisha nyumba aliyokuwa amepanga.

  Tatizo lake, mkewe tangu apate mimba hataki kumwona wala kusikia sauti yake. She just hate him. Hivi majuzi mkewe alipangiwa kutuo cha kazi hapo hapo ambapo ni karibu na kazini kwa jamaa, baada ya jamaa kuhangaikia ili awe karibu na mkewe. Kwa kuwa alikuwa Dar, akamuomba huyo rafiki yake kuwa mkewe aendelee kukaa kwake kwa muda wakati anamalizia finishing ya nyumba yake. Jamaa akamkubalia na huyo mwanamke akaja. Ikawa jamaa akimpigia simu mwanamke hapokei, msg hajibu, akitumiwa hela hata hasemi kama amepata na hakuna kumshukuru kwa jinsi amavyomjali sana.

  To make story short, wakakaa siku nne hakuna mawasiliano, jamaa akaamua kumtafuta huyo mwenye nyumba ili amfikishie ujumbe. Siku iliyofuata, binti akachukua taxi akachukua kilicho chake akakomba kila kitu akaondoka wakati mwenye nyumba hayupo, akaaga kwa majirani kuwa anaenda kuripoti kazini then anasafiri. Mumewe alipoanza kumtafuta mwenye nyumba akatoa ripoti kamili, jamaa akapigwa na butwaa. Kumbe huyo mwanamke hakusafiri wala nini, ni kwamba alipanga chumba sehemu nyingine. Jamaa alipoona hivyo, akapanda gari kuja kushuhudia kilichotokea, wakanza kumtafuta binti next day wakisaidiana na mwenye nyumba huyo, binti alivyogundua kuwa mumewe kaja, yeye akapanda gari kwenda Dar, wakati jamaa yuko mkoani.
  Jamaa yangu huyu amechanganyikiwa wadau nimsaidieje?
   
 2. Lizzy

  Lizzy JF-Expert Member

  #2
  Feb 8, 2012
  Joined: May 25, 2009
  Messages: 22,224
  Likes Received: 244
  Trophy Points: 160
  Labda mimba sio yake na mke hana tu ujasiri wa kumwambia/kuomba talaka.

  Wenye ndoa mna kazi kweli!!
   
 3. BADILI TABIA

  BADILI TABIA JF-Expert Member

  #3
  Feb 8, 2012
  Joined: Jun 13, 2011
  Messages: 30,873
  Likes Received: 6,226
  Trophy Points: 280
  mimba nyingine balaa, hata mumeo hutaki kumuona, unaona kero yaani ukimtia machoni tu nafsi inachafuka...
   
 4. fazaa

  fazaa JF-Expert Member

  #4
  Feb 8, 2012
  Joined: May 20, 2009
  Messages: 2,986
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 0
  Sioni ajabu mwanamke kama yuko kwenye mimnba anaweza kufanya lolote.
   
 5. k

  kisukari JF-Expert Member

  #5
  Feb 9, 2012
  Joined: Jul 16, 2010
  Messages: 3,754
  Likes Received: 1,042
  Trophy Points: 280
  hata kama ni mimba,lakini huyu m.ke amezidi.au labda kuna kisa kingine.ndio unaweza uka behave tofauti,lakini hee anayofanya huyu m.ke ni over the top.bora huyo mume,amsubiri mpaka atakapojifungua
   
 6. C

  Cosmas Lawrence Member

  #6
  Feb 9, 2012
  Joined: Jan 22, 2012
  Messages: 27
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Huyo ana afadhali, nina shemegi yangu huyo anatuma kama muhindi! Istoshe hachagui amtume nani atakae katiza ndo huyo huyo. Chamsingi mwambie avumilie ndivyo mimba zilivyo.
   
 7. sister

  sister JF-Expert Member

  #7
  Feb 9, 2012
  Joined: Nov 23, 2011
  Messages: 9,027
  Likes Received: 3,933
  Trophy Points: 280
  avumilie tu mana mimba zina vituko sana, mie rafiki yangu alikuwa anapenda miguu ya kuku kila siku mumewe lazima arudi na miguu ya kuku asiporudi nayo ni balaa mpaka mumewe akaitafute ampatie na roho itulie, so avumilie tu.
   
 8. daughter

  daughter JF-Expert Member

  #8
  Feb 9, 2012
  Joined: Jun 22, 2009
  Messages: 1,274
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 135
  Mtasingizia na mimba sasa,hata kupokea simu?haya mimba haimtaki mumewe na huyo shemeji je,alishindwa nini kumuaga?am not buying this..
   
 9. N

  Nsuri JF-Expert Member

  #9
  Feb 9, 2012
  Joined: Oct 3, 2011
  Messages: 996
  Likes Received: 183
  Trophy Points: 60
  Jamani acheni kumdanganya huyu jamaa,hiyo mimba sio yake na hakuna mke hapo. Mpaka mtu ukapange bado mnasema mimba?? kuna kitu anaficha huyo mwanamke...labda anaogopa kuzaa mzungu....hahhh
   
 10. Maundumula

  Maundumula JF-Expert Member

  #10
  Feb 9, 2012
  Joined: Nov 4, 2010
  Messages: 7,055
  Likes Received: 74
  Trophy Points: 145
  Duh! hiyo mimba imepitiliza lakini
   
 11. Mabagala

  Mabagala JF-Expert Member

  #11
  Feb 9, 2012
  Joined: Nov 27, 2009
  Messages: 1,465
  Likes Received: 42
  Trophy Points: 145
  basi avumilie tu amuache ajifungue
   
 12. BRO LEE

  BRO LEE JF-Expert Member

  #12
  Feb 9, 2012
  Joined: Dec 25, 2011
  Messages: 580
  Likes Received: 42
  Trophy Points: 45
  Anachotakiwa ni kukaa chini na huyo mkewe ili waliongelee, mwanamke anatakiwa aweke wazi namna anavyojisikia. Inawezekana kukawa na jambo ila mwanamke anatumia ujauzito wake km kinga.
   
 13. BPM

  BPM JF-Expert Member

  #13
  Feb 9, 2012
  Joined: Mar 10, 2011
  Messages: 2,766
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 135
  hayo mambo ya mbadala si sahihi haiwezekani mimba ikahusishwa na masuala ya simu hata salam ni tabia na utukutu wa mtu ..

  huyo jamaa mwambie asihangaike wala nini akae atulie aendelee na ratiba zake za kila siku
   
 14. BPM

  BPM JF-Expert Member

  #14
  Feb 9, 2012
  Joined: Mar 10, 2011
  Messages: 2,766
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 135
  isije kuwa mwanamke alitaka sherehe maana siku hizi kuna ndoa za sherehe (muonekano)
   
 15. Fidel80

  Fidel80 JF-Expert Member

  #15
  Feb 9, 2012
  Joined: May 3, 2008
  Messages: 21,976
  Likes Received: 104
  Trophy Points: 145
  Ushauri wa bure jamaa akapime viungo vya uzazi kama vinaweza kutungisha mimba.
  Akikuta safi basi mimba changa hiyo inamkataa mmewe
   
 16. Wingu

  Wingu JF-Expert Member

  #16
  Feb 9, 2012
  Joined: Jan 14, 2011
  Messages: 4,326
  Likes Received: 23
  Trophy Points: 135
  Chakufanya apige kimya hakuna kumtafuta wala kumtumia hela ndo atatia akili manake ukionyesha sana mapenzi ndo madhara yake haya.Amwache angaike yeye mwenyewe atarudi.Atakuja kujua upumbafu anao fanya baadae.Kujiendekeza tu eti mimba inamchukia ni upumbafu tu tuliojijengea vichwani pambaf angenifanyia mimi mbona angejuta
   
 17. BASHADA

  BASHADA JF-Expert Member

  #17
  Feb 9, 2012
  Joined: Jul 13, 2011
  Messages: 487
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 35
  Asanteni kwa ushauri, lakini kuna wadau hapa wamechangia kuwa wakae waongee, mii nadhani hawajaelewa mada. Ni kwamba Hataki hata kumwona, hapokei simu, na akishajua kuwa jamaa kaja yeye anasafiri sasa wataonanaje? Inanitia huruma because jamaa amekuja na anakesha usiku anaomba (anasali) na analia mpaka tunakosa raha sisi wenyewe. Jamaa anampenda sana mke wake mpaka nahisi it is a deep love, kitu ambacho kwa mkewe hakipo. Ukiwa pembeni unaweza kuchukulia simple lakini ikiwa ndo wewe, sijui itakuwaje.
   
 18. BPM

  BPM JF-Expert Member

  #18
  Feb 9, 2012
  Joined: Mar 10, 2011
  Messages: 2,766
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 135
  hahitaji kutumia nguvu wala ninini.. mwambie akae chini atulizane hahitaji kufanya papara kwani afanyalo mwenza wake ni makusudi na anaelewa afanyalo .. yeye akae chini atulizane japo hata kwa week chache zijazo . kwani mwenza yawezekana ana jambo ambalo anataka kulifanya au amedhamiria kulifanya , maana ndoa bado mbich sana na haijaweza walau kufika miez 6 , asikurupuke atulie asome mchezo
   
 19. J

  Jrafiki Member

  #19
  Feb 9, 2012
  Joined: Dec 23, 2011
  Messages: 75
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Sina uhakika sana kama mimba kwa asilimia kubwa huchangia matatizo kama hayo ila kinachoonekana hapo ni kwamba MIFUMO YA MISINGI YA KIMAPENZI INA ULAKINI.Kuna elements nyingi sana za kuchukuliana rahisi rahisi baina yao.Hili ni tatizo ambalo si tu hujitokeza pale ujauzito unapokuwepo ila hata ktk mambo mbalimbali ya maisha yenu.Wanaume wengi hukosea hapo wanapoanzisha mahusiano mwishowe hupelekea matatizo mengi(ie dharau,kujisahau,kujiamini kupitiliza na kusikokua na msingi) kufumuka toka kwa mwanamke.Kwa lugha nyepesi mahusiano haya nayaita 'legelege'.Ukianzisha mahusiano ya namna hii matatizo ya kimapenzi utakuwa ukitembea nayo kila uendako.
  Kitu cha kufanya kwa huyo rafikiyo.
  Aangalie upya ujenzi wa misingi ya mahusiano yake na yeye anatakaje,ataisimamiaje na atafanikiwaje kuepuka na matatizo YASIYO YA LAZIMA.Its difficult kumshauri afanye a,b,c...kwa sababu am don't know charachers zake and his geniun.The way unavyoplan,the way unavyosimamia what you planned ndivyo outcome itakavyokuwa.
   
 20. Fixed Point

  Fixed Point JF Bronze Member

  #20
  Feb 9, 2012
  Joined: Sep 30, 2009
  Messages: 11,321
  Likes Received: 89
  Trophy Points: 145
  sikubaliani na hili!
  ni uamuzi tu, nataka kufanya hili, sitaki hili............. siyo MIMBA, tunazisingizia jamani!
   
Loading...