Milo mitatu kwa siku ni kwa masikini

Jamaa ni muongo sana.
Wenzetu wenye nazo;
1.Asubuhi kifungua kinywa wengine wanaita starter

2. Saa 4 chai/,kahawa

3. Saa 6 hadi 7 lanchi

4. Saa 4 kahawa/juisi nk

5. Usiku ndio...nini vile?

Wenye nazo hawaishi kutafuna kutwa.

Acha Janabi awatie moyo sijui ni siasa?
Meetings zao ni kwenye restaurants na hotels na huko wakifika lazma waagize kahawa na desserts

Bado hujarudi kwa matajiri wetu wa mikoani, hao ni mwendo wa ugali, nyama choma, samaki, soup, bear etc
 
Mimi nilianza kula mara Moja Kwa siku zaidi ya miaka 2 sasa, Kwa kweli inasaidia sana kiafya, uzito ulipungua vizuri sana, usingizi safi na stress naona zimeenda chini sana, nilibadilisha kidogo aina ya chakula ninachokula na kiasi nilipunguza sana,nilikata wanga kama ugali na wali Kwa kiasi kikubwa na kuongeza mbogamboga, matunda, samaki na nyama, mazoezi nayo niliongeza kidogo, Niko fit kweli kweli sasa and I look and feel good ila beer ilinishinda kuacha, jaribuni ni kitu kizuri sana
 
Mimi sina ratiba ya kula kama mbwa , pale ninapohisi njaa huwa ndio nakula , yani mwili ukihitaji nakula ,kama sina njaa sina sababu ya kula.
Kwa hiyo min huwa hupati hamu ya kula kitu flani. Mfano umemiss mahindi au mtindi wa Asas 😁
 
No kwangu mlo naufanyia meditation ili kuleta balance,kimwili , hamu au tamaa nivitu nmeshavuka kuvipambania nisiwe navyo mkuu .
Inabidi unipe madini zaidi kuhusu hicho kitu maana sikuwahi kufikiria kama chakula kinaweza kuhusishwa na meditation
 
Acha kajua kazame niende rodi....naanza kwenye mishkaki ya 200 kama mi 5 hivi nikitoka juisi ya mua, halafu nizame kwa ombi nipige supu ya pweza baadae nizame kwa dada zai nichukue chapati 4 niende nazo home,.nikirudi napiga menu ya usiku baadae ukishapata mmea natoa chapati zangu namalizia na chai ya saa 5 usiku
 
Inabidi unipe madini zaidi kuhusu hicho kitu maana sikuwahi kufikiria kama chakula kinaweza kuhusishwa na meditation
Kina uhusiano mkubwa , ili ufanikiwe lazima mwili uwe kwenye balance yake, na ili kupata balance vipo vyakula vya kuzingatia , wewe angalia tu jamii zinazopendelea kula nyama sna jinsi walivyo aggressive na kukosa utulivu !

Pia ni vizuri kula kwa kiasi na mapema hasa dina , kabla ya giza kubwa , pia ni vizuri kula kwa uzingativu , sio unakula huku unawaza madeni ya vikoba , pia ni vizuri kula angalau mara moja vyakula vinavyo mea chini ya udogo hasa viazi ,magimbi na nk .

Jinsi ulivyo unajengwa na asili ya vyakula unavyokula na ulipo tokea .
 
Shukrani mkuu ila mengine hapo yanahitaji commitment sio ya mchezo. Hongera kwa kuweza
 
Mbona wenzetu wazungu wanakula milo minne na asilimia kubwa wana afya nzuri zaidi kutuliko sisi?!
Wengi sasa kuishi miaka 90 hadi 100 ni kitu cha kawaida.
Acheni kuwafariji watu.
Serikali iache kukwepa majukumu ya kupunguza ukali wa maisha ili raia wapate kula milo mitatu au zaidi.
Janabi sijui ana agenda gani
 
Kula kwa kiasi kikubwa hutegemea na kazi ya mtu anayofanya
watu wanaokalia kiti cha kuzunguka wasijilinganishe na wanaolima kwa jembe la mkono nk nk nk
Wanaolima kwa jembe la mkono na kazi nyingine ngumu hata wakila milo minne kwa siku ni haki yao na wala haitawapa madhara yoyote!
 
Mbona wenzetu wazungu wanakula milo minne na asilimia kubwa wana afya nzuri zaidi kutuliko sisi?!
Wengi sasa kuishi miaka 90 hadi 100 ni kitu cha kawaida.
Acheni kuwafariji watu.
Serikali iache kukwepa majukumu ya kupunguza ukali wa maisha ili raia wapate kula milo mitatu au zaidi.
Nadhan mtoa hoja kaeleza vuzuri sana namna anavyoona inafaa mtu kujiwekea ratiba za milo.

Kaeleza umuhimu wa kula milo miwili badala ya mitatu na maana yake.

Sasa wewe ulitakiwa uje na maelezo yaliyojitosheleza kutetea hoja ya milo mitatu na faida zake.

Kuna mwingine atakuja na minne ama mitano nk nk.

Nadhani mtu ale kutokana na mahitaji ya mwili kwa namna ya kaz anazozifanya, kuliko kujikaririsha ratiba za vyakula ambapo vikiliwa hurundikana tu mwilini na kusababishia watu wengi madhara ya kiafya.

Suala la kipato ama umasikini tusiliweke kwenye mjadala huu.
 
Back
Top Bottom