Millya anatafutwa na polisi athibitishe mtoto wa kigogo anawatuma polisi

Rizwani amesomea sheria na anajuwa jinsi katiba mbovu inavyompa nguvu baba yake.Ndo maana polisi wanadai eti ameshitakiwa kwa kumkashifu mtoto wa Rais.Ina maana sheria inasema kuwa adhabu inaongezeka zaidi kama aliyekashifiwa ni mtoto wa Rais?Lugha iliyotumika ndiyo utajuwa umbumbumbu wetu.Kama ni defamation waweke wazi tu na si kutanguliza maneno kama eti "Kumkashifu mtoto wa Rais" haya yote kwenye chama,halafu eti wanavisema vyama vingine kuwa ni vya kifamilia.Haya hii ni nini sasa?
 
Millya kibaraka wa Lowassa, lakini hii proxy war ya Lowassa na JK si waweke mambo wazi, Lowassa atoe siri aseme tu wazi kwamba JK alihusika Richmond na wananchi na wana ccm watajaji hilo siyo kumalizana kichini chini kutumia hawa vijana wasiokua na msimamo wa maana ya nchi yao akina Malisa, millya, Bashe, Nape n.iki vijana viongozi gani wa kesho wakati ni wanafiki wakubwa kijana unatakiwa ujiamini uchukue risk una maisha marefu zaidi ya hawa wazee na unaweza fanya mengi katika nchi yako hii kutumika kiupofu upofu kwa matakwa ya wezi ni ujinga wakati hawapati kubwa kama wanaowatumikia. wapuuzi wote
 
Hivi kweli kuna haja ya kusherehekea miaka 50 ya uhuru kama wananchi tunatawaliwa kifalme namna hii?
 
Kuna wakati uwa nafiki kuwa Tanzania yawezekana ikawa chini ya Rais kama FDR; Russevelt wa US, uwa nafiki kuwa labda Rais ajijui na ana hali mbaya sana na yamkini hajui yanayoendelea hapa duniani kutokana na ugonjwa aliona kushambulia ubongo hasa ule wa kuanguka mara kwa mara.

Kila nikisia viroja na vihoja hapa home narudi mara zote kusoma sehemu ya historia na siri kuu zinazobaini kuwa mwisho mwa utawala wa FDR hakika hakuwa anajuwa yanayoedelea nchni kwake ingawa system ya US ilificha na kudanganya Umma mara zote na hata mara nyingine kutoa kauli kuwa Rais kasema hivi na vile kumbe hamna kitu na mara nyinge inasema hata kutoa kauli zilizo rekodiwa kana kwamba anahutubia, FDR tayari alikwisha ku-paralise kumbe siku nyingi kabisa kabla ya kufa rasmi!

Sitaki kuamini kuwa rais yupo sawa kwa yote yanayotamkwa na wasaidizi wake yanaonyesha kuwa sasa tunaye FDR ndani ya ofisi, haiwezekani Serikali ikajuwa na chama tawala ikajuwa juu ya watu wanataka kumuhujumu Rais wa nchni lakini pamoja na nguvu zote za Dola hakuna lolote ni jambo jepesi sana la kuongea kirahisi sana na nape na lika malizika na kupita kama upepo wa vuli. Haiwezekanib leo Mawaziri ni Miungu watu na hata wanapofanya makosa hata Umma ukipiga kelele mbaka wakauke koo lakini hamna sauti yoyote ya Rais juu ya kuchukuwa hatua dhidi ya Viongozi wazembe na wasio na uwezo wa kufanya kazi. Hawezi rais akawa mzima kabisa na bado taifa likabaki kuyumba hivi na kuongozwa na genge huku kila mtu akiongea lake na huku wakibishana kila mtu na lake bila hata kuelewana na bado Rais akawa kimia, naogopa sana ni siku nyingi mimi binfasi naona kama kuna tatizo juu ya Rais wetu.

Kama itakuwa ni kama FDR, basi hatuna jinsi Mungu akupe pumzi na upumzike salama tunakupenda lakini tunaimiss sauti yako na ahadi zako kwa TANU na CCM, hasa katika ile chipukizi na paredi uliyocheza Zanzibar wakati mwaka 1977 wakati wa kuzaliwa CCM siamini kama upo sawa na mzima kabisa bado ukawa kimia huku ngawala likizama lakini wewe upo kimia kabisa ndani ya ngalawa.
 
Mbona mwananchi la leo linadai Millya bdo hawajampata lakini wanamsaka..hv ni kweli kwa sasa kuna msuguano kati ya ED VS Jk?
 
Kampeni ya kuhakikisha kwamba raisi wa ccm hatoki kaskazini naona inaendelea, na bila shaka itashika kasi sana siku za hivi karibuni.

Lakini kwakuwa hawa wawili wanaounda utatu hawakukutana barabarani, sidhani kama baba riz atakuwa amehusika katika kukamatwa kwa milya.

Sidhani kama baba riz anaweza kumtikisa mtoto wa lowasa. Mi nadhani kuna kitu kinatengenezwa hapa kuwapumbaza watu, tuwe makini sana na hizi sarakasi za ccm kaskazini mwa nchi!!

Rais kutoka Bara? Zanzibar inaelekea kupigwa tatu bila . Maumivu ya kichwa huanza polepole!
 
wakigombana chukua nafasi kufungua matawi mpaka vijijini wakipatana mtakutana kwenye uchaguzi
 
Mwenyekiti UVCCM amekamatwa na polisi baada ya kile kinachodaiwa kumsema riz wakati wa kuzindua mashina ya chama wiki iliyopita huko Arusha,Millya alimtaka riz aache kuingilia uvccm. Tukio hilo limetokea mchana huu huko mjini Arusha.


Kwanini wa simuachie ccm mnang'ang'ania nini tuone kama anaweza kuendesha peke yake
 
Rizwani amesomea sheria na anajuwa jinsi katiba mbovu inavyompa nguvu baba yake.Ndo maana polisi wanadai eti ameshitakiwa kwa kumkashifu mtoto wa Rais.Ina maana sheria inasema kuwa adhabu inaongezeka zaidi kama aliyekashifiwa ni mtoto wa Rais?Lugha iliyotumika ndiyo utajuwa umbumbumbu wetu.Kama ni defamation waweke wazi tu na si kutanguliza maneno kama eti "Kumkashifu mtoto wa Rais" haya yote kwenye chama,halafu eti wanavisema vyama vingine kuwa ni vya kifamilia.Haya hii ni nini sasa?

Mkuu, sikutegemea a PREMIUM JF Member kama wewe utachukuliwa na hili bandwagon la uzushi na kulitolea hukumu kwa uhakika namna hii.

Labda nikuulize, je umeiona hiyo charge sheet inavyosomeka?...
Mkuu JF ya sasa ni tofauti sana na JF ya miaka ya nyuma, wakurupukaji wamekua wengi mno...na hakuna filters!

Ukisoma humuhumu kuna mtu kakutana na Millya akiwa hana wasiwasi, Mwananchi gazeti linasema bado anatafutwa...
 
Wanawazingua wakuu hao wana lao jambo wanacheza nalo .Wanataka kuonyesha kitu ili wahalalishe kuwakaata watu wa Chadema .Kaeni macho .
...Kweli kabisa. Sitarajii kwa kutaja jina tu Rizwani basi polisi wakamate mtu kuna kitu kimejificha hapa. Wanataka kugeuza Tanzania nchi ya kifalme mpaka wajuu wa mfalme nao waabudiwe?
 
sasa imefika tanzannia kuwa nchi ya kifalme maana watoto wa viongozi wa juu wanaheshimika hata kuliko wabunge.polisi tendeni haki na sio kukurupuka
 
Nilishasema this is another movie tusubiri itakuwa na series ngapi dah...kwel tanzania......
 
Wamesema jamaa amekamatwa coz alisema kunamto2 mmoja wa kigogo aliwa2mia mapolice ili wacfungue mashina huko Atown
Ndo mana police wanamind na wakaanza kumsaka ili azbitishe kaul yake
Source.magazet ya leo asb
 
Mkuu, sikutegemea a PREMIUM JF Member kama wewe utachukuliwa na hili bandwagon la uzushi na kulitolea hukumu kwa uhakika namna hii.

Labda nikuulize, je umeiona hiyo charge sheet inavyosomeka?...
Mkuu JF ya sasa ni tofauti sana na JF ya miaka ya nyuma, wakurupukaji wamekua wengi mno...na hakuna filters!

Ukisoma humuhumu kuna mtu kakutana na Millya akiwa hana wasiwasi, Mwananchi gazeti linasema bado anatafutwa...

Mkuu ukisema hivyo unakua unakata tamaa, jambo la msingi tujitahidi kuwaelimisha waweze kuacha kudandia, na kwa kweli kwa sasa ushabiki unatawala sana badala ya umakini na hoja zenye ukweli. Taarifa ya kwanza ilisema Millya amekamatwa, bvila kutafakari wengi wakaanza kuhukumu, leo Millya hajakamatwa na sasa imeendelea hoja ya sababu za kukamatwa, nayo inaendelea bila kuangalia tatizo hasa nini! Polisi wanaweza kuzuga sababu na baadae mkashangaa tatizo ni tofauti kabisa. JF bado ina watu makini na itaendelea kuwa makini, tusikate tamaa tupambane kueleza ukweli na tujitahidi kupunguza unazi, itazidi kutupa heshima tuloijenga miaka mingi.
 
Back
Top Bottom