Millya anatafutwa na polisi athibitishe mtoto wa kigogo anawatuma polisi

iron finger

JF-Expert Member
Sep 27, 2011
358
220
Mwenyekiti UVCCM amekamatwa na polisi baada ya kile kinachodaiwa kumsema riz wakati wa kuzindua mashina ya chama wiki iliyopita huko Arusha,Millya alimtaka riz aache kuingilia uvccm. Tukio hilo limetokea mchana huu huko mjini Arusha.
 
mwenyekiti uvccm amekamatwa na polisi baada ya kile kinachodaiwa kumsema riz wakati wa kuzindua mashina ya chama wiki iliyopita huko Arusha,Millya alimtaka riz aache kuingilia uvccm.tukio hilo limetokea mchana huu huko mjini Arusha.

Siwaamini hawa magamba wanaweza wakawa wanatuzuga.
 
Ha, kumbe panzi wanaanza kutafunana!!! Hiyo ni kawaida katika maisha yao na wanaendelea kuishi tu kama panzi.
 
Mkuu kosa ambalo limeandikwa kwenye kitabu cha kukamatwa ni nini ? Sidhani kama wanaweza wakasema upo chini ya ulinzi kwa kumtaja mtu.., kwahiyo ni sababu gani waliyotoa?
 
Wanawazingua wakuu hao wana lao jambo wanacheza nalo .Wanataka kuonyesha kitu ili wahalalishe kuwakaata watu wa Chadema .Kaeni macho .
 
Mkuu kosa ambalo limeandikwa kwenye kitabu cha kukamatwa ni nini ? Sidhani kama wanaweza wakasema upo chini ya ulinzi kwa kumtaja mtu.., kwahiyo ni sababu gani waliyotoa?

Mpashaji wangu kaniambia sababu kubwa ambayo polisi wamemkamata Millya ni yale maneno aliyotoa wakati wa uzinduzi wa mashina kwamba riz hapaswi kuingilia siasa za vijana na pia watanzania hawakumchagua riz awe rais wamemchagua baba yake.

Lakini la ndani zaidu kuna harusi ya kada mmoja wa ccm ambayo ilifanyika huko moshi baada ya harusi kulikuwa na kikao kisicho tambulika kisheria ambacho kiliongozwa na mkit uvccm ndugu benno yaliyoelezwa humu yalimkashifu sana riz na baba yake nafkiri nayo ni sababu!
 
safi laana ya mzee ndesamburo inafanya kazi!jana tumesikia ya nape!

Umesahau laana ya Mwalim Nyerere...Simba akionja damu ya mtu basi kwamwe hatoacha tabia hiyo! walivurugana vibaya sana 2005 na hii sasa ni trela ya movie part 11 ya kuelekea 2015, Movie lenyewe badooooo halijaanza ila ngojeni kidogoi
 
mwenyekiti uvccm amekamatwa na polisi baada ya kile kinachodaiwa kumsema riz wakati wa kuzindua mashina ya chama wiki iliyopita huko Arusha,Millya alimtaka riz aache kuingilia uvccm.tukio hilo limetokea mchana huu huko mjini Arusha.

Kwani Ridhiwani ni nani nchi hii? Hii nchi ni ya ajabu sana, unajua ukifikria sana unatamani hata kulia,tunaipeleka wapi hii nchi? Huyu Ridhiwania akitoa taarifa tu polisi wanachukua hatua,akitoa mtu mmoja maskini kule Maneremango hakuna hata wakusumbuka na taarifa hizo...Nadhani watanzania tuna kitu tunapaswa kufanya kurudisha heshima ya nchi hii,tunadharaulika sana jamani......
 
Haswa mkuu umenena...nchi imepoteza dira kwa kweli..ni aibu nchi kuendeshwa kwa maslahi ya wachache wengi wakikandamizwa..Viongozi wanafanya kazi kana kwamba hawatoki miongoni mwetu na hao wana usalama ni kama wote hawana reasoning power..wakiambiwa lolote na hao viongozi wao ni kutekeleza tu tena wakati mwingine kinyama..mwisho wa haya ni mbaya sana..

Kwani Ridhiwani ni nani nchi hii? Hii nchi ni ya ajabu sana,unajua ukifikria sana unatamani hata kulia,tunaipeleka wapi hii nchi? Huyu Ridhiwania akitoa taarifa tu polisi wanachukua hatua,akitoa mtu mmoja maskini kule Maneremango hakuna hata wakusumbuka na taarifa hizo...Nadhani watanzania tuna kitu tunapaswa kufanya kurudisha heshima ya nchi hii,tunadharaulika sana jamani......
 
Back
Top Bottom