Millya 'amchana' Ridhiwani Kikwete

Godlisten Masawe

JF-Expert Member
Jul 20, 2011
738
281
RIDHIWANI Kikwete mtoto wa Rais Jakaya Kikwete ametajwa kuingilia na kuamua kuendesha siasa za Mkoa wa Arusha kwa kutumia ‘rimote Control' akiwa jijini Dar es Salaam.

Katika mkutano wa leo uliofanyika katikati ya Jiji la Arusha na kuhudhuriwa na vijana wengi, Ridhiwani ametajwa kuwashika baadhi ya viongozi wa UVCCM wilaya ya Arusha na kuwaweka kwenye himaya yake.

Akizungumza baada ya kuhitimisha kazi ya ufunguzi wa mashina ya CCM zaidi ya 100 katika maeneo mablimbali ya jimbo la Arusha, Mwenyekiti wa UVCCM Mkoa wa Arusha James Millya alimrushia kombora hilo Ridhiwani mbele ya halaiki ya watu mjini hapa.

Huku akionyesha kuzungumza kwa hasira Millya aliyeshiriki zoezi hilo akiwa na baadhi ya viongozi wa Umoja huo wa kitaifa, akiwamo Beno Malisa Makamu Mwenyekiti alisema, wanachama wa CCM mkoa wa Arusha na maeneo mengine nchini walimchagua baba yake Ridhiwani kuwa kiongozi wao na si mtoto wake.

"Huyu mtoto anataka kuongoza siasa za Arusha akiwa Dar es Salaam, hivi mbona sisi hatuingilii siasa za Bagamoyo, sasa tumtaka abakie na Bagamoyo yake na atuachie Arusha yetu. Anajifanya anajua sana, tunachojua sisi tumemchagua baba yake kuwa kiongozi wa taifa haiwezekani na mtoto wake aongoze Arusha," alisema Milya huku akishangiliwa na ummati mkubwa wa watu.

Naye Malisa akizungumza katika mkutano huo wa hadhara alisema, yeye binafsi ameshuhudia jinsi viongozi wa uuma waliochaguliwa kuwatumikia wananchi wakijitahidi kuzuia kazi ya kufungua mashina ya CCM.

"Tumewajua wote waliopambana ili kutuzuia tusiimarishe Chama chetu, jamani hivi haya mambo ya urais wa 2015 yanatoka wapi wakati sisi tupo kwenye kuimarisha Chama. Mimi ni shahidi leo wametutumia mpaka sms kututishia tusifanye hii kazi, jamani viongozi wanaacha kufanya kazi ya kuhakikisha vijana wanaonbdokana na ukali wa maisha wanahangaika kuzuia kazi ya kufungua mashina.

Malisa alikwenda mbali zaidi na kusema kuwa muda wa kufanya mambo kwa kutumia busara sasa umepitiwa na wakati.

Baadhi ya viongozi wa UVCCM waliokuwa katika shughuli hiyo ya kuzindua mashina ni pamoja na Mbunge wa Vijana Catherine Magige, Mwenyekiti wa UVCCM Mkoa wa Kilimanjaro Godling Moshi, Mwenyekiti wa UVCCM Mkoa wa Morogoro, wajumbve wa Kamati ya Utekelezaji mkoa wa Arusha, na viongozi wengine.

Utata wa kufunguliwa kwa mashina hayo uliibuka jana baada ya kambi ya Mwenyekiti wa UVCCM wilaya ya Arusha God Mwalusamba kutangaza kuwa haikuwa na taarifa ya ziara hiyo ya uzinduzi wa mashina.

Tangu kufanyika kwa uchaguzi mkuu mwaka 2010 Mwalumba alikuwa kambi ya Dk. Batilda Burian lakini mara baada ya kumalizika kwa uchaguzi huo alihamia kambi ya Mary Chatanda Katibu wa CCM Mkao wa Arusha.
 

The Hunter

JF-Expert Member
Dec 25, 2010
1,049
302
Tutarajie mengi, maana siri ya huu mkimbizano nyie ndo mnaujua! CDM tutadumu na tutawakumbusha siku moja vijana wenzetu mlipotoka kuingia CCM.
 
  • Thanks
Reactions: Ame

Feedback

JF-Expert Member
Mar 14, 2011
7,990
4,502
Baada ya vita vya panzi kazi inayobaki huwa ni kubaka tu na kutia kapuni.
 

Mzee wa Rula

JF-Expert Member
Oct 6, 2010
8,177
3,326
Inaonekana Ridhiwan ana influence kubwa sana mpaka kufikia Milya kulalamika namna hiyo! Naona wamewekeza nguvu nyingi katika jiji la Arusha labda mavuno yanaweza kuwa mazuri 2015.
 

Gwallo

JF-Expert Member
Oct 15, 2010
3,088
3,459
Waongeze juhudi na maarifa katika mapambano yao, Arusha imeshawatoka haitarudi mikononi mwa walaghai. Hii move itatoka na mtu tusubiri tuone!!!!!!!!!!
 

Kituko

JF-Expert Member
Jan 12, 2009
9,559
9,251
vita ya Lowassa dhidi ya JK na wenzie ndio imeanza rasmi, ndani ya miaka minne, tutarajie chama kipya kitachotokana na UVCCM
 

ipogolo

JF-Expert Member
Aug 15, 2011
6,241
5,915
Labda kwa wanaoujua wadhifa wa Ridhiwan ndani ya UVCCM watusaidie kutujuza.
 

MASEBUNA

JF-Expert Member
Oct 9, 2011
243
54
Kuna Tread ilikuwa huku ikisema UVCCCM ni Janga la taifa, nikiisoma picha ya kuelekea 2015 sipati picha.
 

Shine

JF-Expert Member
Feb 5, 2011
11,483
1,358
Vita vya panzi furaha kwa kunguru, naona ukombozi wa nchi yetu unaonekana kwani wanavyoshindwa kuelewana ndivyo vyama vya upinzani wanapata mwanya wakuchukua majimbo mengi na hata urais na yule nepi aliyesema TZ ni mali ya ccm ataumbuka
 

jigoku

JF-Expert Member
Sep 9, 2011
2,413
730
Bado wakizichapa au wakitekana nyara ndo tutajua kweli wameamua sio kulaghai kwa mitusi na vijembe,wafanye kama walivyotutendea kwa kada wa chadema kule Igunga.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

1 Reactions
Reply
Top Bottom