Milipuko Mikubwa yarindima Kibamba...

Mbagala, Gongolamboto, Kibamba...

Nasubiria Lugalo....
 
Wakuu sasa nitoke au niendelee kusubiria?.....hali ikoje? Ni transforma au mabomu? Tupeni updates bana.......
 
Ningependa kuamini kuwa serikali inaposema haina pesa ya kuongeza mishahara haimaanishi wizara nyingine hazipati fungu la kutosha

Hata hivyo napoweza kukubaliana na wewe ni kwamba serikali ya CCM imejaa wezi hivyo kwa wizara ya ulinzi sitashangaa kama hapo pana hujuma kupita hata za Tanesco. Kama ulivyosema hata haya mabomu yanayolipuka mara kwa mara inawezekana mitumba ama tulipewa(dump) bure ila yashaandikiwa risiti za manunuzi, Bongo Dar Es Salaama, kaa chonjo!
 
Mkuu natambua kuwa mgomo wa walimu umetuathiri wengi ila kwa sasa umeisha na Hussein Mwinyi yuko pale kwa Drs (Afya). ulinzi na JWTZ yupo Shamsi Vuai Nahodha
 
Wakuu kiukweli ni mlipuko mmoja tu umetokea na ni wa transfoma ndio maana umeme nao umekatika......lakini kwa sababu hili ni jukwaa la siasa tunaweza kusema ni milipuko 5 au 6 ili tupate sababu ya kuwalaumu . ....
 
duh..utakuwa unaishi Mtukula kagera wewe.

Mtoa mada anaandika kana kwamba JF ni ya watu wa Dsm tu. Ukitoa taarifa lazima iwe complete. Hata kama ni mtu wa Mutukula, Mulongo, Bugarama, n.k. waelewe location ya tukio.

Any way hali ikoje sasa??
 
Wakuu kiukweli ni mlipuko mmoja tu umetokea na ni wa transfoma ndio maana umeme nao umekatika......lakini kwa sababu hili ni jukwaa la siasa tunaweza kusema ni milipuko 5 au 6 ili tupate sababu ya kuwalaumu . ....

na hii ni tatizo kubwa sana......watoaji wa mada hu-mislead watu......na watu nao hukurupuka kama kuku waangaliavyo mwewe...."kwa jicho moja" na kuanza kuchangia UPOTOFU lwa mapovu ya kutosha
Habari sahihi ikija kinyume chake ni aibu kwa JF
 
Mungu wangu! Sie tunaekaa karibu na huko, ngoja nihamishe watoto mapemaaaaa.
 
Bitabo asante sana. Nilipitiwa mkuu mwenzangu si unajua tena ukiwa na jazba na usongo kidogo.
 
na hii ni tatizo kubwa sana......watoaji wa mada hu-mislead watu......na watu nao hukurupuka kama kuku waangaliavyo mwewe...."kwa jicho moja" na kuanza kuchangia UPOTOFU lwa mapovu ya kutosha
Habari sahihi ikija kinyume chake ni aibu kwa JF
MODS nao wanabeba sehemu ya lawama maana zinawekwa habari za kupotosha kwa makusudi wanakaa kimya wapotoshaji wangekuwa wanalimwa ban bila mzaha mtu angejishauri mara mbili kabla ya kupost kitu, mods acheni mzaha!
 
Mtoa mada anaandika kana kwamba JF ni ya watu wa Dsm tu. Ukitoa taarifa lazima iwe complete. Hata kama ni mtu wa Mutukula, Mulongo, Bugarama, n.k. waelewe location ya tukio.

Any way hali ikoje sasa??

sio huko tu mkuu pia tokyo, seoul,washington, manilla,dominica republic, laos, iran.,soweto, durban na kwengineko JF ni international mkuu
 
Nawahakikishia nimesikia milipuko minne mimi naishi maeneo ya Gogoni karibu na makazi ya mzee Kawawa.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…