Milipuko 2 yatokea mjini Jos, Nigeria

Milipuko 2 yatokea mjini Jos, Nigeria

MK254

JF-Expert Member
Joined
May 11, 2013
Posts
33,573
Reaction score
53,604
Mara nyingi milipuko ikitokea hapa Kenya, mnakurupuka eti tuondoe majeshi Somalia na kutoroka. Sasa jameni muwape ushauri Wanigeria cha kufanya. Dunia haiwezi ongozwo na uoga, bali ujasiri na kuwaonyesha maharamia kwamba hawana nafasi ndani ya jamii.

===================================================

Milipuko miwili mikubwa imetokea nchini Nigeria katika mji wa Jos.

Milipuko hiyo imetokea katika soko ambalo lina shughuli nyingi na ambalo lilikuwa na msongamano wa watu eneo la Kati mwa Nigeria.
Mwandishi wa BBC Ishaq Khalid aliye mjini humo anasema kuwa kuna hofu ya watu wengi kujeruhiwa hasa kwa kuwa soko hilo lilikuwa na idadi kubwa ya watu.
Haijulikani kilichosababisha milipuko hiyo mjini Jos, mji ambao umeshuhudia mashambulizi makali kati ya wakristo na waisilamu.
Kundi la Boko Haram, pia limekuwa likifanya mashambulizi katika mji huo.

Milipuko 2 yatokea mjini Jos, Nigeria - BBC Swahili - Habari
 
NO ONE WISH TO KILL OR DIE BUT.

What i want to say in summary about BOKO HARAM is that.
BOKO HARAM was started 2002 in a village of Kannama in Yobu State before the administration of chief Olusegun Obasanjo landed offensive attack against them. Their unusual life style of living in the bush and excluding themselves from the 'sin' of this world.
This was a souce of concern Obanjo administration hence the offensive agaist them.they move from Kannama to Bama and Maiduguri in Borno State. At kannama they were not violet.
The gorvervement was just not comfortable with their belief the society is consumed or filled with so many ill and atrocities, and that they cannot live in this present day society ,so they went to the sahara desert of kannama in the bush and started living there.
The gorverment become suspicious and decide to dispatch them using force.with that period the sect under the leadership of late mohammed yusuf were peaceful in their conduct.
 
Boko haram hao...
Ndio hapo sasa, Nigeria lazima wapigane nao hadi afe wa mwisho, suluhisho sio kuwaachia nchi maana sera zao ni za kiajabu ajabu. Hiyo ndio taswira hata Somalia, Alshabaab pindi watakapoachiwa nchi basi hata sisimizi hatapata pa kuishi. Jamaa kwa muda kidogo tu walitawala hata bahari hindi.
 
Ndio hapo sasa, Nigeria lazima wapigane nao hadi afe wa mwisho, suluhisho sio kuwaachia nchi maana sera zao ni za kiajabu ajabu. Hiyo ndio taswira hata Somalia, Alshabaab pindi watakapoachiwa nchi basi hata sisimizi hatapata pa kuishi. Jamaa kwa muda kidogo tu walitawala hata bahari hindi.

maneno yako yakwamba hata sisimizi hatapata pa kuishi. Ni sawa na kusema sheria aliokuamrisha mwenyezimungu uitumie ndio unayoipinga.

Na ukiipinga sheria yake basi umempinga na mola wako.
 
maneno yako yakwamba hata sisimizi hatapata pa kuishi. Ni sawa na kusema sheria aliokuamrisha mwenyezimungu uitumie ndio unayoipinga.

Na ukiipinga sheria yake basi umempinga na mola wako.
Sheria ya Mungu hailazimishiwi watu, bali ni kwa kauli ya mtu kwa akili zake mwenyewe na hekima alizopewa na Mungu kuifuata. Sielewi ni sheria zipi hizo zinahusu kuwateka watoto na kuwabaka msituni.
 
Kuna watu wanakurupuka hata walichokisoma hawajakielewa.
 
Takriban watu 46 wameaga dunia na wengine
wengi kujeruhiwa baada ya milipuko miwili
mikubwa kutokea nchini Nigeria katika mji wa
Jos.Milipuko hiyo imetokea katika soko lenye
shughuli nyingi .
Mwandishi wa BBC aliyeko huko anasema
kuwa amehesabu miili 40 ikipelekwakatika
chumba cha kuhifadhia maiti katika hospitali
moja iliyoko JOS.
Mwandishi wa BBC Ishaq Khalid aliye mjini
humo anasema kuwa kuna hofu ya watu wengi
kujeruhiwa hasa kwa kuwa soko hilo lilikuwa
na idadi kubwa ya watu.
Aidha anaarifu kuwa taharuki ietanda katika
eneo hilo baada ya vijana waliopandwa na
hasira kufunga mabarabara ya kuingia na
kutoka mjini humo na kuzua hofu ya
makabiliano.
Mji wa Jos itakumbukwa iliwahi kushuhudia
mapigano mabaya zaidi baina ya makundi ya
vijana Waislamu na wale Wakristu
iliyosababisha maafa mengi.
Mabomu hayo yanasemekana kuwa yalikuwa
yametegwa moja katika lori na lingine katika
gari la uchukuzi wa abiria na yakalipuka kwa
mpigo moja katika soko la lingine karibu na
hospitali.
Hakuna aliyekiri kutekeleza mashambulizi
hayo ijapokuwa jimbo hilo limewahi
kushambuliwa na kundi la Boko Haram zaidi
ya miaka miwili iliyopita.


Jimbo la Platue liko mpakani kati ya
waislamu wanaoishi Kaskazini mwa Nigeria
na Wakrstu ambao wanaishi Kusini .
Jimbo hili limewahi kushudia mapigano baina
ya wakulima wakristu wa tabaka la Berom na
waislamu wafugaji wa kuhamhama wa tabaka
la Fulani.
Mnamo mwezi Machi mwaka uliopita kituo
cha basi kilishambuliwa kwa bomu na awali
mwaka wa 2012, Boko Haram walifanya
shambulio baya zaidi lililowaua zaidi ya watu
150 katika msururu wa milipuko.
Kundi hilo bado linawazuilia wasichana zaidi
ya 200 wa shule, lililowateka kutoka kijiji
kimoja kaskazini mashariki mwa Nigeria
mwezi mmoja uliopita.
Nchi kadhaa zikiwemo Uingereza, Ufaransa na
Marekani wameahidi kutuma wanajeshi
kusaidia kuwakomboa wasichana hao.
Nao viongozi wa Afrika wanaokutana mjini
Paris wametangaza 'vita' dhidi ya Boko
Haram na kuahidi kushirikiana ki-intelijensia
na kijeshi, kupambana na Boko Haram.



bbc.
 
Kenya na Nigeria wanateswa na magaidi kwa sasa Mungu wape nguvu ndugu zetu hawa wasiokuwa na hatia
 
Inanibidi nifikiri mara mbili juu ya nchi ya Nigeria,vipi wanapokuwa watawala wanajeshi haya mambo ya mabomu hayapo na kama inatokea ni mara chache pia anapokuwapo mtawala ambaye anatokea kaskazini hali ni shwari Je nini siri ya serikali kushindwa kudhibiti hali hii? Au tuamini kuna viongozi wanaopenda uongozi huu uanguke? Je ni kwa maslahi ya nani.
 
Takriban watu 46 wameaga dunia na wengine wengi kujeruhiwa baada ya milipuko miwili mikubwa kutokea nchini Nigeria katika mji wa Jos.Milipuko hiyo imetokea katika soko lenye shughuli nyingi .
Mwandishi wa BBC aliyeko huko anasema kuwa amehesabu miili 40 ikipelekwakatika chumba cha kuhifadhia maiti katika hospitali moja iliyoko JOS.
[h=2]Taarifa zinazohusiana[/h]



Mwandishi wa BBC Ishaq Khalid aliye mjini humo anasema kuwa kuna hofu ya watu wengi kujeruhiwa hasa kwa kuwa soko hilo lilikuwa na idadi kubwa ya watu.
Aidha anaarifu kuwa taharuki ietanda katika eneo hilo baada ya vijana waliopandwa na hasira kufunga mabarabara ya kuingia na kutoka mjini humo na kuzua hofu ya makabiliano.
Mji wa Jos itakumbukwa iliwahi kushuhudia mapigano mabaya zaidi baina ya makundi ya vijana Waislamu na wale Wakristu iliyosababisha maafa mengi.
Mabomu hayo yanasemekana kuwa yalikuwa yametegwa moja katika lori na lingine katika gari la uchukuzi wa abiria na yakalipuka kwa mpigo moja katika soko la lingine karibu na hospitali.
Hakuna aliyekiri kutekeleza mashambulizi hayo ijapokuwa jimbo hilo limewahi kushambuliwa na kundi la Boko Haram zaidi ya miaka miwili iliyopita.
Watu 46 wauawa katika mlipuko Nigeria - BBC Swahili - Habari
 
Naona Lucifer amekasilika sasa, naona anahitaji damu nyingi
 
Mwenye kuiweza vita na magaidi/jihadist/extremist ni mmarekani tuu!
 


​
OK, apparently the bomb explosion that occurred this afternoon at the densely populated Terminus Market near Murtala Mohammed way in Jos is more serious than we thought. The twin explosion, which occurred 30 minutes apart, reportedly killed at least 200 people according to eye-witnesses, making it deadlier than the Nyanya blast.


The bomb was planted in two cars, a Peugeot J5 van and a Toyota Sienna SUV with a Gombe state license plate number. Eye-witnesses said the car had been parked near the busy market since early this morning and had even drawn the curiosity of people in the area who allegedly alerted the police. It exploded many hours later. See a pic of some bodies being removed from the scene after the cut




Read more »
 
Kumekucha naona... Nguzo kuu Ya Uislam inafanya kazi.... Boko Haramz.....
 
Daah,poleni ndugu zetu nigerians,juzi kenya leo nigeria,Mungu atunusuru
 
Haya mambo yanatekelezwa kutokea ndani ya serikali ya Nigeria hivyo ni vigumu kudhibitiwa kirahisi.!
 
Kumekucha naona... Nguzo kuu Ya Uislam inafanya kazi.... Boko Haramz.....


Jizuie ndugu yangu kushabikia chuki hizo...hata hao boko haram walianza kama wewe hivyo, usije kuta na wewe ukawaleta hapa kwetu!
 
Back
Top Bottom