Milioni 70/- zatumika kumzika Kanumba

Milliom 58 kwa mazishi yale mbona naona kama ni sawa. Tatizo leti Wabongo hatuaminiani kabisa. Kamati imefanya vyema. Tuwashukuru kwa kazi nzuri.
SAMAHANI KUSEMA HILI, BUT AM SURE WEWE NI MMOJA WAO! WALLAH WEW UTAKUWA NI MMOJA KATI YA YALE MABUNDI YALIKUWA FRONT LINE KUONA MWENZAO KAENDA! Nasema hivi malipo ni hapahapa nyie ndio mtakufa na maiti zenu ziliwe na tumbusi! fullu stop!
 
Je aliwahi kusaidia yatima yupi? Skuli ipi? Maendeleo wapi?


Matajiuliza maswali mengi sana mwaka huu lakini Kanumba kama Kanumba ndio alikuwa sasa ameaza kuelekea katika kilele cha mafanikio yake..
Wewe umewahi kusaidia wapi?
 
Huwezi kuwalaumu ndugu wa marehemu kwa sababu waliambiwa wakae pending ili watu wafanye mambo,khaaaa,hata mdogo wa marehemu mwenyewe hakuhusishwa,kama kweli walikuwa na nia nzuri kwa nini hawakutumia number ya mama yake mzazi kwa ajili ya kutuma m-pesa au mdogo wake kanumba.....,ni wezi wote na walitaka kujipublish kuwa wako juu huku wanaiba hela za marehemu.washindwe na walegeee.
 
uzuri, na wao kuna siku watawekewa kamati....
What do you expect from the Tanzanians?
Wamecheka, wamekula, wamefanya kazi na Kanumba na siku ya mwisho ndio hivyo....
Wameshindwa hata kumwonea huruma ndugu yao.....
Jamani, kufa kufaana....
That was the best time to make money!
 
The burial of the local film icon steven kanumba who died this month cost 70 m
a
total of 90 m in actial cash contributions and in for of pledges had been recorded by burial commitee,out of that 53,252,000 was collected and pledges in form of materials ammounted 18,400,000/=

burial commitee chairman mr mtitu told reporters yest a total of 15.5 m in form of pledges including 10m by the gov ,which it plans to hand over to beareaved fammilly was yet collected

accordin to chairman 40m has already given to kanumba's mother
we thank god everything went well frm the day when kanumba passed away to his burial
we thank govt of tanzania and all tanzanian for their valuable support to this commitee

he also refuted claims that his committee had chopped some mny frm contributions saying that the team member had to meet initial exp frm their own pockets...shame mtitu
loh!!

Haya kazi kweny wakubwa na nyie wana familia za wasanii mtakaofiwa muwemakini na hizi vijikamati dnt trust them hata siku moja jiulizeni kwa nini walipinga ndugu hata mmoja wa kanumba kuwepo kwenye kamati kuna nini kipya walichokuwa waanafikiri kukifanya ...msiwe kama misukule ama ni zile sui nyeusi ziliwasumbua mkaamua kuwaachia kusimamia huu msiba???
Tunaomba msipige kelele za kuibiwa wakati ni ninyi wenyewe mlikubali kuongozwa na kamati teule ya chama
 
Soma na hii kutoka nipashe..tuamini ipi sasa!!!
[h=2]utajiri wa steven kanumba watajwa[/h]


na renatha msungu



18th april 2012


email.png

b-pepe



printer.png

chapa



comment_bubble.png

maoni




headline_bullet.jpg
ni magari matatu, viwanja kadhaa
headline_bullet.jpg
mazishi yagharinu mil.52/-



kamati kuu ya mazishi ya aliyekuwa msanii mashuhuri wa filamu nchini, marehemu steven kanumba, imedai msanii huyo amefariki dunia akiwa maskini, kinyume kabisa cha umaarufu mkubwa aliokuwa nao wakati wa uhai wake.

Mwenyekiti wa kamati hiyo, mtitu gabriel, alisema hayo wakati akitoa ufafanuzi kuhusu makusanyo na matumizi ya fedha zilizotumika katika maombolezo, kuaga na mazishi ya kanumba, aliyefariki dunia aprili 7, mwaka huu na kuzikwa aprili 10, mwaka huu.

Mbali na mtitu kutoa ufafanuzi kuhusiana na fedha zilizokusanywa pamoja na matumizi yake, alikanusha taarifa za uvumi kuwa msanii huyo ameacha mali zenye thamani ya sh. Milioni 700.

"hizi taarifa hazina ukweli ndani yake, ninachojua kanumba amefariki akiwa na jina kubwa katika sanaa, lakini ni mtu mwenye pesa ya kawaida," alisema mtitu.

Alisema kinachozungumzwa na watu hakina ukweli.

Mjumbe wa kamati hiyo, william mtitu, alisema mali zilizoachwa na marehemu kanumba ni magari matatu na, viwanja ambavyo hata hivyo, hakutaja idadi yake wala mahali viliko.

Kuhusu nyumba aliyokuwa akiishi eneo la sinza, alisema kuwa ilikuwa ni ya kupanga.

Pia alisema alikuwa akimiliki kampuni inayohusika na uandaaji na utayarishaji wa filamu ijulikanayo kwa jina la "kanumba the great" jijini dar es salaam.

Kampuni hiyo ambayo inamiliki studio, inaelezwa ina mchango mkubwa wa kuinua vipaji vya wasanii chipukizi, akiwamo wema sepetu na elizabeth michael, maarufu kama ‘lulu'.

Hata hivyo, alikataa kueleza kiasi cha fedha alizoacha kanumba na akaunti zake za benki kwa maelezo kwamba suala hilo ni la familia.

Awali, gabriel mtitu alisema wao kama kamati, walipokutana siku ya msiba wa nyota huyo wa filamu, kulikuwa hakuna kianzio chochote cha kufanikisha msiba.

Badala yake, alisema walifanya bidii ya kukusanya fedha ambazo zilitumika wakati wa msiba.

Mtitu alitaja makusanyo ya michango pamoja na matumizi ya fedha zilizotumika katika maombolezo hadi mazishi ya msanii huyo.

Alisema makusanyo ya michango yote ilikuwa ni sh. 53,252,000 na kwamba, kati ya fedha hizo, zilizotumika ni sh. 52,102,000.

Mtitu alisema fedha zilizotolewa ahadi ni sh. 15,500,000, wakati ahadi ya vifaa ilikuwa ni sh. 18,400,000. Alisema ahadi zilizolipwa ni sh. 2,850,000.

Mtitu alisema gharama zote za maombolezo hadi mazishi zikiwemo taslimu na ahadi ni sh. 70,502,000.

"salio ni sh. 4,000,000 ambazo zimekabidhiwa na zitaendelea kukabidhiwa kwa mama wa marehemu kadri ya marejesho ya ahadi yatakavyokuwa," alisema mtitu.

Alisema wao kama kamati wamekamilisha rasmi shughuli za msiba huo, na kuiachia familia iendelee na taratibu nyingine.

Mtitu alisema ili kuhakikisha wanamuenzi marehemu kanumba, wanatarajia kuanzisha tuzo ya steven ambayo itatoa changamoto kwa wasanii kuiga mfano wa utendaji wake wa kazi.

"tuna mikakati ya kuanzisha tuzo ya steven ambayo itatoa changamoto kwa wasanii kujituma ili waweze kufikia kiwango alichofikia katika uigizaji wake," alisema mtitu.

Akizungumzia malalamiko ya baadhi ya watu kutopewa nafasi ya kuuaga mwili wa marehemu, alisema ilishindikana kutokana na matarajio ya watu waliofika katika mazishi yake yalikuwa kinyume cha makadirio yao.

"hatukutarajia idadi kubwa ya waombolezaji kujitokeza kiasi kile. Baada ya viongozi wa serikali kuondoka, kulitokea msongomano uliopelekea kamati kuzuiwa watu kuaga," alisema mtitu.
 
Kufa kufaana na afae dhambini vitu au mali zake zitaliwa dhambini, watu wamepiga hela na kupata za kunywea mvinyo na kuchakachulia mashee.
 
me wala sioni cha kushangaza hapo mana shopping ya wema tu dubai alitumia hiyohiyo amount, pili tanzania ni nchi maskin nadhan wangeweza kuwanunulia wamama magodoro katik hospial mbalimbali angalau wajifungulie hapo kuliko chini.................................maoni yangu tu.
 

Wednesday

Imeandikwa na Anastazia Anyimike; Tarehe: 17th April 2012 @ 23:44



kanumba6.jpg




KAMATI ya mazishi ya aliyekuwa msanii maarufu nchini, Steven Kanumba, imesema imetumia Sh milioni 70 kugharimia maziko yaliyofanyika Aprili 10.

Kanumba alifariki dunia usiku wa kuamkia Aprili 7 na kuzikwa siku tatu baadaye kwenye makaburi ya Kinondoni na maelfu ya wananchi wa Dar es Salaam na mikoa jirani.

Mwenyekiti wa Kamati hiyo, Mtitu Gabriel alisema jana kwamba kamati hiyo iliyoratibu mazishi ya msanii huyo tangu Aprili 7, ilikusanya michango na ahadi za takribani Sh milioni 90 huku gharama za mazishi hadi maziko vikigharimu Sh 70,502,000.

Akitoa mchanganuo huo, Mtitu alisema Kamati yake ilitumia Sh 52,102,000 na ahadi za malipo ya vifaa ambazo ni Sh 18,400,000 na zilitumika kwa vifaa mbalimbali zikiwamo taa, jukwaa, viti na maturubai.

Alisema Sh milioni nne zilizobaki kutokana na zilizokusanywa zilikabidhiwa kwa mama mzazi wa Kanumba, Flora Mtegoa na Kamati haijatimiziwa ahadi ya Sh milioni 15.5.

Alipoulizwa kama Kanumba ameacha mali ya Sh milioni 700, Mtitu alisema pamoja na msanii huyo kuwa na jina kubwa, lakini alikuwa masikini na si tajiri kama ilivyokuwa inafikiriwa.

"Pamoja na jina la Kanumba kuwa kubwa, hakuwa na fedha, na ndiyo maana baada ya kutoka kuhifadhi mwili wake Muhimbili, tulijikusanya na kujipanga kuhakikisha tunampumzisha kwenye nyumba ya milele kwa heshima ya hali ya juu na hili tumelifanikisha," alisema Mwenyekiti huyo.

Pamoja na kukanusha ‘kuchakachua' fedha zilizokusanywa, Mtitu alisema Kamati yake ilianza ikiwa haina hata Sh 100 na kulazimika wanakamati kubeba gharama za awali.

"Tulitambua mchango mkubwa wa Kanumba enzi za uhai wake, tuliona iko haja ya kufanya yote haya, tulianza tukiwa hatuna hata Sh 100, ingawa baadaye Kamati ilichangia gharama za awali ambazo zilipatikana miongoni mwa wajumbe wenyewe," alieleza.

Akizungumzia kushindwa kutoa nafasi kwa wananchi kuaga mwili wa Kanumba, Mtitu alisema Kamati ilikadiria kuwa watu wapatao 40,000 wangehudhuria kutokana na idadi ya watu ambao walikuwa wakifika msibani, lakini wingi wa watu na ufinyu wa muda siku hiyo ndivyo vilifanya utaratibu ukatizwe.

"Wakati wa mazishi tulikuwa tunahudumia waombolezaji 3,000 mpaka 4,000 kwa siku, hivyo tukaweka makadirio ya watu 40,000 siku ya maziko, lakini watu waliojitokeza walikuwa wengi na ikawa vigumu kutoa nafasi kwa wote kuaga, hasa kutokana na wingi na mazingira yalivyokuwa na muda pia," alifafanua.

Kamati iliyoratibu shughuli zote za mazishi iliundwa na wadau wa filamu, wasanii, wafanyabiashara, ndugu na marafiki wa Kanumba, aliyekuwa mwigizaji nyota wa filamu nchini na aliyevuma pia katika nchi mbalimbali barani Afrika.

Kifo chake kilikuwa cha utata baada ya kudaiwa kuwa na ugomvi na mwigizaji wa kike, Elizabeth Michael ‘Lulu', ambaye inadaiwa alikuwa mpenzi wake.

Lulu tayari amefikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, Dar es Salaam kwa tuhuma za mauaji ya msanii huyo.

Katika hatua nyingine, Gabriel alisema katika kumuenzi Kanumba, wanafikiria kuandaa Tuzo za kutambua kazi za sanaa ya maonesho na filamu, ambazo wataziita kwa jina la Tuzo za Steven Kanumba.












 
ile kamati imeiba pesa nyingi sana...zile guni 32 z chele zilizotolewa ziko wapi? badala yake mke wa luge akawa anahudumia chakula.....na kisha kulipwa......
 
Hapo ni kiasi gani kimechakachuliwa na hiyo Kamati? Serikali inawaamini kina Ruge, ndio hao wameweka hizo baadhi ya fedha Mifukoni badala ya kuupa mama Kanumba?

Inasikitisha sana, sasa hivi kila kitu lazima shibe ipatikane kwangu kwanza kabla ya kitu chochote kitendeke...

Labda tuyafuate ya CHINA, kula rusha - una - nyongwa, iba pesa - unayongwa, iba kura za uchaguzi - unanyongwa.
 
Mh, watu 4000 kwa siku ni wengi sana,

Poleni kwa kazi ngumu!
Pesa ni shetani, halfu wa TZ hatuaminiani hata robo!
 
Back
Top Bottom