Milioni 70/- zatumika kumzika Kanumba | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Milioni 70/- zatumika kumzika Kanumba

Discussion in 'Celebrities Forum' started by Pascal Mayalla, Apr 17, 2012.

 1. P

  Pascal Mayalla JF-Expert Member

  #1
  Apr 17, 2012
  Joined: Sep 22, 2008
  Messages: 22,216
  Likes Received: 10,303
  Trophy Points: 280
  Mazishi ya Tanzania top most celeb, Stephen Kanumba, yamegharimu Shilingi za Kitanzania, Milioni 60 kasoro 2!.

  Kwa mujibu wa taarifa ya M/Kiti wa kamati ya mazishi, Mtitu, gharama halisi za mazishi hayo ni Shilingi milioni 58!.

  Kusema ukweli, hizi sii fedha nyingi ukilinganisha na mambo makubwa yaliyofanyika, lakini pia kwa nchi masikini kama Tanzania, na hali halisi ya maisha ya baba yake mzazi Kanumba, Mzee Charles Kanumba anayoishi pale kijijini TBC ilipomtembelea, fedha hizi sii fedha ndogo!.

  Natamani kamati itoe mchanganua wa matumizi hayo ili kuondoa dhana kufa kufaana, tusije kuta service providers za huduma zote pale msibani, ni hao hao wasanii wenyewe, na sio tuu wame imflate gharama halisi ili kuvuta cha juu, bali wanaweza kabisa kuwa wamefanya usanii mpaka kwenye msiba wa msanii mwenzao kwa kujilipa wenyewe fedha pesa ndefu na kutuletea hesabu za kisanii pia!.

  Usikute hata zile suti nyeusi, hesabu ni mumo humo!.
  Usikute hata yale matangazo live hesabu ni mumo humo!
  Usikute zile fulani tuliombiwa zinagawiwa bure lakini watu tukauziwa, hesabu ni mumo humo!.
  Usikute ile line up ndefu ya wasanii ambao wange perform nao hesabu ni mumo humo! etc, etc!

  Hatuna tatizo na huduma zozote kulipiwa malipo halali kwa huduma iliyotakiwa, ila tuna tatizo kama huduma hizo zilitolewa at inflated rates, ikiwemo watu baki kuvaa suti msiba wa Kanumba ili hali kuna uwezekano mkubwa Baba mzazi alipata homa ya ghafla kwa kuogopa atavaa nini mbele ya kadamnasi ya watu kwenye msiba wa mwanae!

  Ukiondoa hayo, kamati hiyo inastahili kupewa sifa kwa kufanikisha mazishi ya huyu Tz. No. 1 Celeb, Stephen Kanumba "The Great", ambayo yamechukua nafasi ya pili kwa umaarufu ukiondoa msiba wa Baba wa Taifa.

  Wito: Kuvunjwa kwa Kamati kusiwe ndio mwisho wa usaidizi wao kwa mpendwa wao, wajipange kusaidiana na wazazi kuanzisha "Kanumba The Great Memorial Foundation" ili fedha zinazotokana na kazi zake, ziingie kwenye hiyo foundation ili angalau wazazi wa Kanumba wote wawili, waishi maisha yanayo reflect hazina ya utajiri mtoto wao aliyoiacha humu duniani, vinginevyo ni ma distributor (wadosi) ndio watakaofaidika na jasho la Kanumba, huku Mzee Charles Kanumba akiendelea kuishi maisha ya mwanakijiji wa kawaida wa Tanzania kule kijijini!.

  Hongereni Kamati!

  Rip SK The Great!.

  Pasco!.
   
 2. MadameX

  MadameX JF-Expert Member

  #2
  Apr 17, 2012
  Joined: Dec 27, 2009
  Messages: 7,846
  Likes Received: 52
  Trophy Points: 145
  Gharama zote hizo ili iweje...ndio harudi
   
 3. KirilOriginal

  KirilOriginal JF-Expert Member

  #3
  Apr 17, 2012
  Joined: Feb 13, 2012
  Messages: 1,768
  Likes Received: 226
  Trophy Points: 160
  Je aliwahi kusaidia yatima yupi? Skuli ipi? Maendeleo wapi?
   
 4. Judi wa Kishua

  Judi wa Kishua JF-Expert Member

  #4
  Apr 17, 2012
  Joined: Apr 15, 2012
  Messages: 926
  Likes Received: 453
  Trophy Points: 80
  mara milion 58 mara ya kwanza walisema ni milioni 50,wakiendelea kubanwa ukweli utajulikana tu...kuna milion 2.5 zilikuwa chumbani kwa Kanumba zimepotea na wao ndio watu wa kwanza kuingia umo waseme zimeenda wapi...vitu vingi pale watu walijitolea waseme izo pesa ziligharamia nini...we kamati yupo Steve Nyerere,Ruge,JB,Dr Cheni na wahuni wote wa mjini unategemea nini..
   
 5. b

  bebiwilli Member

  #5
  Apr 17, 2012
  Joined: Mar 4, 2011
  Messages: 70
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Wa kulaumiwa ni ndugu wa marehemu kwa nini hawakuwepo kwenye kamati? Hata kama umefiwa na unauchungu lazima ndugu muwe kwenye kamati,Haya yote yasingetokea,kamati yote imejaa wasanii,miwani na misuti mikubwa ili ionekane kwenye camera,
   
 6. Ulukolokwitanga

  Ulukolokwitanga JF-Expert Member

  #6
  Apr 17, 2012
  Joined: Sep 18, 2010
  Messages: 8,203
  Likes Received: 3,188
  Trophy Points: 280
  Hii nchi nzuri bana, kumbe dili moja tu la kuwa katika kamati ya mazishi ya supastaa tayari unapata mtaji wa kufungua kaduka mtaa wa pili?!
   
 7. b

  bebiwilli Member

  #7
  Apr 17, 2012
  Joined: Mar 4, 2011
  Messages: 70
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Yaani mi nilijua walivyotangaza kuomba mchango watatangaza pia kamati imebakia na kiasi fulani na imepelekwa kwa wafiwa,lakini kimya,mama kanumba bora ungeenda kumzika mwanao shinyanga mngekuwa mnafarijiana na baba watoto wako,vishadadu waliokushawishi uzike dar ona wanakuacha peke yako walikusaidia kuzimia2 tena bila aibu wengine walikuwepo kilimanjaro awards wakati juzi2walizimia,nw wamesepa washapata chao hata kaburi hawatakumbuka kulitoa majan,
   
 8. Edson

  Edson JF-Expert Member

  #8
  Apr 17, 2012
  Joined: Mar 7, 2009
  Messages: 9,103
  Likes Received: 523
  Trophy Points: 280
  serikali ilisema itagharimia mazishi...sasa hizi garama za wapi tena?
   
 9. Matola

  Matola JF-Expert Member

  #9
  Apr 17, 2012
  Joined: Oct 18, 2010
  Messages: 32,150
  Likes Received: 7,139
  Trophy Points: 280
  Mtitu aliposema kesho siku ya mazishi ya Kanumba itakuwa ni Show wengi hamkumuelewa, lakini sisi wakazi wa mjini tulimuelewa vyema anamaanisha nini.
  Siku sio nyingi utasikia Twanga Pepeta wamenunuwa vyomba vipya, mkiweza kuifuatilia namba ya Asha Baraka kwa tarehe zile ndio mtashangaa ni M Pesa kiasi gani zilitumwa kwake kama rambirambi za msiba.
   
 10. Tangawizi

  Tangawizi JF-Expert Member

  #10
  Apr 18, 2012
  Joined: Jun 25, 2009
  Messages: 2,477
  Likes Received: 715
  Trophy Points: 280
  Sometime I wish my family could be strong and able to resist the charms of smart people who can steal anything for money!
   
 11. Papizo

  Papizo JF-Expert Member

  #11
  Apr 18, 2012
  Joined: Feb 24, 2008
  Messages: 4,409
  Likes Received: 250
  Trophy Points: 180

  Daaaa sio mchezo aiseee naona mkuu hapo umenena, wakuu mliokuwa ndani huko tunaomba idadi ya MPESA aliyopkea Asha Baraka najuwa dataz hapa JF ndio nyumbani.
   
 12. Papizo

  Papizo JF-Expert Member

  #12
  Apr 18, 2012
  Joined: Feb 24, 2008
  Messages: 4,409
  Likes Received: 250
  Trophy Points: 180
  Nani alisema chumbani kwake kulikuwa na hicho kiasi??
   
 13. Judi wa Kishua

  Judi wa Kishua JF-Expert Member

  #13
  Apr 18, 2012
  Joined: Apr 15, 2012
  Messages: 926
  Likes Received: 453
  Trophy Points: 80
  mdogo wake,na wanamtisha asilipeleke suali ili kwenye media eti wanalishughulikia wenyewe....soon hii suala mtalisikia tu maana dunia haina siri.....ile lexus kuna shemeji yake kamuoa dada yake ndio anatembelea sasa ivi,japo naskia walimpigia kelele ameriludisha.
   
 14. i

  iMind JF-Expert Member

  #14
  Apr 18, 2012
  Joined: Mar 27, 2011
  Messages: 1,861
  Likes Received: 317
  Trophy Points: 180
  Milliom 58 kwa mazishi yale mbona naona kama ni sawa. Tatizo leti Wabongo hatuaminiani kabisa. Kamati imefanya vyema. Tuwashukuru kwa kazi nzuri.
   
 15. mgodi

  mgodi JF-Expert Member

  #15
  Apr 18, 2012
  Joined: Nov 5, 2010
  Messages: 1,902
  Likes Received: 454
  Trophy Points: 180
  Mkuu, kule kuzimia kila msanii alikuwa na cha juu, haikuwa bure bure.
   
 16. Kimbunga

  Kimbunga Platinum Member

  #16
  Apr 18, 2012
  Joined: Oct 4, 2007
  Messages: 12,749
  Likes Received: 1,522
  Trophy Points: 280
  Mkuu pesa zimetafunwa. Nilitembelea pale kwa Mama siku ya Jumapili nikakuta malalamiko kibao. Tukaambiwa Dotinata ndiye alikuwa mpishi kwenye shughuli kukawa na mengi kwamba mbona watu hawakula. Kwamba familia haikushirikishwa kwenye kamati na mambo kibao yanayoonyesha kwamba kuna kutafunwa kwa pesa.

  Hivi serikali si ilisikika ikisema itasimamia mazishi? Hizo million 70 ni pamoja na za serikali au?
   
 17. Kimbunga

  Kimbunga Platinum Member

  #17
  Apr 18, 2012
  Joined: Oct 4, 2007
  Messages: 12,749
  Likes Received: 1,522
  Trophy Points: 280
  Mkuu hiyo pesa ni nyingi mno ukizingatia umasikini wa familia zetu za kibongo. Wabongo kwa mabao nani amuamini mwenzake. Huoni siku hizi kwenye vikao vya harusi mtunza fedha ni bwana/bibi harusi mwenyewe. Sasa hii kamati haikushirikisha wanandugu.

  Nilisikia baadhi ya ndugu wakilalamika kwamba waliposikia michango walidhani mama K atatoka lakini akaishia kuambulia million 3 za mabaki.
   
 18. t

  thandiswa Member

  #18
  Apr 18, 2012
  Joined: Apr 10, 2012
  Messages: 86
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Dhambi hatuogopi hata hela za michango ya marehemu jamani? wanajua wazi wazazi wa the Great ni watu wazima leo wanawfanyia hivi,mi nachojua Mungu hulipa hapa hapa duniani si tuwe wasikilizaji. Mama K aendeleze miradi ya mtoto wake na Mungu atamsaidia na ataendelea kula jasho na matunda ya kipenzi chake. hao waliokula laana iko juu yao. si mtitu wala jb wa maana hapo wote wizi mtupu
   
 19. K

  Kiduku JF-Expert Member

  #19
  Apr 18, 2012
  Joined: Sep 29, 2010
  Messages: 481
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  afe mwingine na kamati iwe ile ile
   
 20. cacico

  cacico JF-Expert Member

  #20
  Apr 18, 2012
  Joined: Mar 27, 2012
  Messages: 8,392
  Likes Received: 125
  Trophy Points: 160
  MUNGU MUUMBA anisamehe kama natenda dhambi! but ile kamati imechakachua fedha ya kutosha tu! ni wachakachuaji vibaya mno, yaani wote wale ni wasanii tu, magunia 32 ya mchele for crying out loud yamekwenda wapi? na chakula kilikuwa kinapikwa palepale! haya serikali iligharamia mazishi for 80% sasa hayo mamilioni yamekwenda wapi??? jamani nilitamani kanumba aamke japo kwa dk 10 aone jinsi wenzake waliofurahia kufa kwake! beliv me not, wakina jb wanatamani mwingine tena afe wapate tena pa kuponea! but who, na STAR ALIKUWA PEKE YAKE??? RIP KANUMBA, U WERE MO THAN THE WORD GREAT!
   
Loading...