Milima ya Uluguru ikiteketea kwa moto leo, NEMC wamelala usingizi!!!!!!!

proisra

JF-Expert Member
Jun 14, 2012
214
158
Baraza la mazingira Tanzania (NEMC) lipo likizo. Wadau wa Mazingira Morogoro hawapo tayari kuingilia kati mambo haya. Maji Morogoro hayapatikani kwa muda mrefu kwa uharibifu wa mazingira unaoendelea, na hasa uchomaji misitu na milima ya Uluguru.

Pichani, moto ukiendelea kuchoma milima ya Uluguru leo asubuhi. Picha hii imechukuliwa karibu na kituo cha Njia pandaya DSM, Bigwa- Morogoro.
 
Attachments

  • DSC01356.JPG
    DSC01356.JPG
    635.3 KB · Views: 106
  • DSC01357.JPG
    DSC01357.JPG
    674 KB · Views: 100
Nilivyokuwa Serengeti mwezi April nilikutana nao huo moto wa haja pale karibu na campsite ya Pimbi, na ikanikera sana na nikabishana sana na yule game guide alipokuja ile jioni kupiga doria, yeye alisema hiyo ni therapy ati kwa wanyama na viumbe hai walio undersoil na oversoil halafu ati pia inatumika ku speed up ecosystem process ya kuandaa chakula ya wanyama tayari kwa next season!!!! mmmmhhh!!:blabla:. Alinichanganya sana kwa kweli.
 
Baraza la mazingira Tanzania (NEMC) lipo likizo. Wadau waMazingira Morogoro hawapo tayari kuingilia kati mambo haya. Maji Morogorohayapatikani kwa muda mrefu kwa uharibifu wa mazingira unaoendelea, na hasauchomaji misitu na milima ya Uluguru.

Pichani, moto ukiendelea kuchoma milimaya Uluguru leo asubuhi. Picha hii imechukuliwa karibu na kituo cha Njia pandaya DSM, Bigwa- Morogoro.
Morogoro hakuna utashi wa watu kuzima moto,nadhani hawajui kuwa kuzima moto ni LAZIMA kwa mujibu wa sheria ni wakati sasa wa kuwalazimisha watu kwenda kuzima moto ili waone uchungu siku nyingine ikitokea hivi waone uchungu na kuwatafuta wanaochoma moto kwa udi na uvumba.
 
Nilivyokuwa Serengeti mwezi April nilikutana nao huo moto wa haja pale karibu na campsite ya Pimbi, na ikanikera sana na nikabishana sana na yule game guide alipokuja ile jioni kupiga doria, yeye alisema hiyo ni therapy ati kwa wanyama na viumbe hai walio undersoil na oversoil halafu ati pia inatumika ku speed up ecosystem process ya kuandaa chakula ya wanyama tayari kwa next season!!!! mmmmhhh!!:blabla:. Alinichanganya sana kwa kweli.

Moto unaochomwa kwenye mbuga za wanyama unawashwa kuteketeza nyasi kavu ili kupisha kuchipua kwa nyasi laini kwa malisho ya wanyama wanaokula nyasi. Usipochoma moto nyasi kavu kwenye mbuga utapoteza idadi kubwa sana ya wanyama kwani wengi hawawezi kula nyasi kavu.
 
Nachukia sana uharibifu wa mazingira, kwa hali inavyoenda tutakua na crisis nyingi huko mbeleni, "ukiacha hizi zilizoanza kuji-unfold", tunacrisis kwenye mazingira (mother nature) ambazo impact zake nadhani tunazielewa.

Lakini hebu tujiulize kidogo, hawa ndugu zetu wanaochoma misitu,kama hapo pichani,tunajua wengi wanafanya hivyo kwa sababu ya shughuli za uchumi (kuchoma mkaa na kilimo) ili nao waweze kudumu katika hii kasi ya maisha.
Hivi unadhani wanapenda kuchoma hiyo misitu? Wana option nyingine zaidi ya hiyo? Hivi kama kuna mtu humu barazan amewahi kuchoma mkaa atakua shuhuda mzuri jinsi hiyo shughuli ilivyokua pevu( mbombo ngafu).

Siamini kama kuna mtu anapenda kuchoma mkaa na kuharibu mazingira, but what option do they have? Anafamilia inamtegemea, watoto wanahitaji kula, kuvaa na kwenda shule,bado bills nyingine na kodi uchwara kibao zinamngoja.

Jamii na serikali yake zimempa option zipi ili asichome mkaa? After all kwake yeye hayo mapori ni ya asili,hakuna serikali wala mwanamazingira aliyeyapanda, atayakata tu na kufanya kuni na mkaa ili apate eneo la shamba ili familia yake isilale njaa.

Kadri tunavyojitahidi kuwaelimisha watu wasiharibu mazingira lazima tuwapelekee na njia mbadala or else tutakua tunatwanga maji kwenye kinu.
 
Morogoro hakuna utashi wa watu kuzima moto,nadhani hawajui kuwa kuzima moto ni LAZIMA kwa mujibu wa sheria ni wakati sasa wa kuwalazimisha watu kwenda kuzima moto ili waone uchungu siku nyingine ikitokea hivi waone uchungu na kuwatafuta wanaochoma moto kwa udi na uvumba.
Mkuu'wewe ukifatwa ukazime moto kwa lazima utaenda?
Especially kwa serikali hii?
 
.........Haya mambo ya ukiukwaji wa utunzaji wa mazingira yapo katika sehemu mbalimbali za nchi hii............ watu wamekata miti na kusababisha kupotea kwa uoto wa asili..... hata miti ya kuwekea mizinga ya kuvuna asali sasa ni issue watu wanakata miti hovyo wanaangamiza misitu iliyowekwa na mwenyezi Mungu, wamapoteza kabisa uoto wa asili . watu wa NEMC kweili wamelala usingizi
 
Mkuu'wewe ukifatwa ukazime moto kwa lazima utaenda?
Especially kwa serikali hii?

Ni sheria inatamka hivyo,siyo mimi,jiulize kama Mlima Kilimanjaro inawezekana ni kwa vipi kimlima cha uluguru ishindikane nakuhakikishia mimi ni mmoja wa wahanga wa kuzima moto kwa lazima Mlima Kilimanjaro watekelezaji wa sheria Morogoro wamelala fofofo wakiamka itawezekana ni kiasi cha Mkuu wa Mkoa kutoa amri tu kwa kufuata sheria inawezekana.
 
Back
Top Bottom