Historia ya Morogoro, nne ya kirumi na asili ya boka, nyoka mwenye vichwa saba katika milima ya Uluguru

Leslie Mbena

JF-Expert Member
Nov 24, 2019
207
677
HISTORIA YA MOROGORO, NNE YA KIRUMI NA ASILI YA BOKA, NYOKA MWENYE VICHWA SABA KATIKA MILIMA YA ULUGURU.

Leo 15:15pm 14/06/2020

Wakati wa likizo tukiwa wadogo tulipofunga Shule pale Bungo Primary School, Mimi na ndugu zangu tulikuwa tunakwenda kuwasalimu Bibi na babu kijijini Tawa Matombo,pale kibunduga kwa Mzee Butwa,

Babu na Bibi walifurahi sana na tulipata nafasi ya kufahamu mambo ya mila na utamaduni wetu sisi Waluguru, kijiografia miji ya Matombo na Mgeta ipo nyuma ya milima ya Uluguru, katika miji hiyo ndio asili ya kabila la Waluguru waliopo katika Mkoa wa Morogoro.

Asili ya neno Morogoro ni mluguru, hii ni baada ya Jasusi Mbobezi Henry M Stanley kushindwa kutamka Mluguru na kuongelea kooni na kutoka sauti iliyosikika "Moro-goro" Jasusi Henry M Stanley alipita katika safu za milima ya Uluguru njia ya Kaskazini Mwaka 1874 akiambaa hadi Mashariki ya milima ya Uluguru,

Katikati ya milima ya Uluguru, Henry M Stanley alikutana na jeshi la Simbamweni mtoto wa Kingo Kisebengo, katika mji uliozungushiwa ukuta na kuwa na ngome isiyopenyeka kiurahisi, baada ya kuonekana ni mtu mwema alipokelewa na Mwenyeji wake Chifu Simbamweni,

Jasusi Henry M Stanley aliusifu mji huo uliokuwa chini ya bonde la milima ya Uluguru, akisema mji huo umejengwa kwa mitindo ya kiarabu chini ya bonde la kijani la milima ya Uluguru,yenye misitu minene inayofunikwa na mawingu wakati wote wa Mwaka,

Milima iliyopambwa na mito miwili mikubwa inayokwenda kuzaa mto Ruvu, uliounganishwa na utitiri wa vijito vya maji safi na salama, Jasusi Henry M Stanley katika kitabu chake "How I found Livingstone" chapter 4 na 16 anakiri mandhari ya milima ya Uluguru hajapata kuyaona katika eneo lolote alilowahi kufika katika Afrika Mashariki,

Rejea pia kitabu cha Joseph Thomson:'To The Central Africa Lakes and Back' 1881chapter 1 na 5 kinachoelezea Jeshi kali la Waluguru lilikuwa linavaa majani ya mgomba na magome ya miti,

Thomson akiwa na Baba yake Keith Johnson wakitokea eneo la masai na Ziwa Victoria,wakiingia pwani katika eneo la Waluguru na wakutu Mwaka 1879 anasema hakuwahi kukutana na Waluguru zaidi zao toka kwa Majeshi mengine ya wambuga hadi pale alipokuja kufahamu walikuwepo wengi katika njia aliyopita lakini walivaa majani ya mgomba na kufanana na majani na miti ya porini,

- Historia ya Chief Kingalu,Kiongozi wa Waluguru.

Historia ya Chifu Kingalu inaanzia kwa Chifu Lukwele wa Choma aliyezaliwa mwaka mwaka 1852 na kufariki mwaka 1971, na kuzikwa katika makaburi maarufu wakati huo ya kichangani mjini Morogoro

Chifu Lukwele ndiyo yule askari mwenye historia ya kupigana katika jeshi la Mjerumani dhidi ya Waingereza na washirika wao, kwenye maeneo kadhaa ya Mashariki ya Kati uko uarabuni, Afrika Mashariki, Msumbiji, Malawi na hatimaye Namibia, na kurejea nchini baada ya vita ya kwanza ya Dunia kumalizika katika muongo wa pili wa karne ya 20.

Chifu Lukwele ambaye jina lake halisi ni Salum Bin Msumi, alikuwa ni mmoja kati ya watoto watatu mashuhuri wa Chifu Msumi wa Kibungo, ambaye asili yake kwa baba ni Mluguru na mama ni Mzulu toka Afrika Kusini.

Chifu Msumi aliyeitawala kibungo juu na kibungo chini katika milima ya Uluguru rekodi yake ya ndoa na watoto inaonesha kuwa ni mtu wa mitala, na alikuwa na watoto wengi, zaidi ya 30 katika milima ya Uluguru Mkoani Morogoro, Mbambabay Mkoani Ruvuma na jijini Lilongwe nchini Malawi.

Watoto mashuhuri wa Chifu Msumi ni Lukwele (Salum), Sonanga, na Mleke maarufu kama Kingalungalu (waluguru wanatamka ‘Chingalungalu' yaani Kigeugeu) au kwa kifupi Kingalu wa kwanza, ikiwa ni jina lake la kupanga kutokana na tabia yake ya Ugeugeu (aliwahi kumgeuka mkwewe chifu magoma, na kisha baba yake mzazi Chifu Msumi na kupigana nao vita kali kwa nyakati tofauti!akitaka kuongoza safu yote ya milima Uluguru)

- Kutokana na ubabe na nguvu jina la Kingalu hilo likawa jina rasmi la ukoo ambalo litatawala Waluguru.

Kutoka ukoo wa Chifu Msumi tunaweza pia kupata makabila mengine yaliyotika katika koo ya Kiluguru kama Wazaramo, Wakaguru, Wakutu na Wakwere, wote wakifuata mfumojike (kwa Kiingereza ''matrilinear'') yaani ukoo wa mama ndio unaoongoza familia na watoto wote wanahesabiwa kuwa wa ukoo huo.

Katika kupata jina la mtoto anayezaliwa, mtoto wa Kiluguru huitwa jina la ukoo wa baba yake, ambao ndio ukoo wa bibi mzaa baba. yaani, Waluguru wana 'mtala' na ukoo. Mtala ni jina la ukoo wa baba ambalo ndilo analoitwa mtoto.

Kwa mfano, mtoto akiitwa 'Kobero' jina hili ni mtala, si jina la ukoo wake, kwani 'Kobero' ni jina analopewa mtoto ambaye baba yake ni 'Mmande'. Hali kadhalika, mtoto akiitwa 'Mkude' jina hili ni mtala wa ukoo wa 'Wamwenda', lakini si jina la ukoo wa mtoto. Hivyo basi, kwa Waluguru baba hutoa jina na mama hutoa ukoo, jina ni la ukoo wa baba, na ukoo ni wa mama!

- Nne ya Kirumi iliyochorwa na Mjerumani katika kilima kimojawapo cha Mlima wa Uluguru.

Alama ya ushindi baada ya kuupanda Mlima Uluguru sasa inaelekea kufutika katika Mwamba
wa kilele cha Lupanga, ni historia nyingine ya kukumbukwa kwa kila aliyepanda Mlima wa Uluguru na kupiga picha katika eneo hilo ambalo linaonekana vizuri ukiwa chini katikati ya Mji wa Morogoro,

Kilele cha Lupanga kinachotiririsha maji kikiwa na mita 2,150 toka usawa wa bahari ni cha pili kwa ukubwa katika Mlima Uluguru wenye urefu wa Mita 2,630. Tukiwa Scout wenzangu wa kutoka shule za msingi na Sekondari miaka ya 1990 ilituchukuwa saa tisa kufika kileleni,

Ilituchukua saa tatu kushuka, lakini kwa wengi huwachukuwa saa 11.30 hadi 12 kupanda hadi kwenye kilele iko cha Lupanga chenye nne ya kirumi na saa tano na nusu hadi sita kushuka, kushika kilele hicho ni kazi kubwa na hatari zaidi kuliko kuupanda!).

Katika eneo lenye nne ya kirumi (alama IV) uwa kazi zaidi kupanda, kwani muinuko wake baadhi ya maeneo hufika nyuzi tisini, kiasi cha kutegemea mashina ya miti na mizizi kukuwezesha kusonga mbele.

Kihistoria eneo hili lilikuwa chini ya Mamlaka ya Utawala wa Choma (kabla ya Ukoloni kuchukua hatamu) kwenye eneo la Uangalizi wa Mndewa (Sub-Chief) wa Kibwe ambaye ni Sayyid (His Royal Highness) Mwande.

Nilipata bahati ya kupitia nyaraka za utawala wa Choma (Royal Achieves) sikupata chochote juu ya maana ya alama hii (IV), japo ninavyofahamu iliwekwa na Wajerumani miaka takriban 100 iliyopita wakati vita ya Dunia ikianza kunguruma,lakini niligundua ilimaanisha ushindi wa kupanda Mlima Uluguru na kufikia kilele iko cha Lupanga.

-Boka, nyoka mwenye vichwa saba, anayepatikana katika milima ya Uluguru.

Nikiwa likizo moja kijijini Tawa, Matombo miaka ya 1990 tuliamka asubuhi na kukuta mto Mmanga umejaa mara mbili zaidi ukiharibu kingo za ukuta, nyumba za watu, mashamba, ukichukua mbuzi, kondoo, kuku na kila kilichoonekana mali ya wanakijiji pembeni ya mto Mmanga uliokuwa ukitiririsha maji yake kuelekea mto Mfizigo ambao ulipeleka maji katika mto Ruvu uliokwenda kuingia baharini,

Tulipouliza waliokaribu na mto walikiri kusikia miluzi, makofi na vigelegele usiku wa manane huku kishindo kikubwa cha mtiririko wa maji kikisikika katika mto Mmanga, baadae wazee wa mila walikiri kupita kwa nyoka aina ya boka mwenye vichwa saba, akimeremeta na kung'aa mithili ya nyota za angani, akiwa safarini kuelekea baharini.

Wazee walitueleza makazi ya nyoka huyo ambayo uwa ni Mlimani na karibu ya vyanzo vya mito mikubwa,mahali anapokaa uwa panabarikiwa sana mafuta, na ithibitisho wa hilo alipita kwe mto usiku basi asubuhi utakutana na harufu ya petrol na mafuta ya taa, ikieleza mahali alipotoka ameacha hazina hiyo ya mafuta.

Kwa watu wanaokaa maeneo hayo mfano kabila la walugulu wanalifaham hilo, Nyoka huyo uwa na maisha ya kuhama kutoka eneo moja kwenda eneo lingine na katika safari zake inasadikika anatoka milimani na kuelekea baharini kupitia katika maporomoko ya maji na vijito vidogovido.

Kipindi cha masika au mvua kubwa ndio mida anaotumia kwa kipindi cha miaka kumi ndipo hayo yanatokea, katika maeneo hayo karibu na vijiji jirani kuna matokeo ya watoto kuumwa kipindi tuu nyoka huyu anapofanya safari zake,

Mwaka 1984 nyoka huyo alionekana akiondoka kuelekea baharini kwa njia ya moshi baada ya kutiririka na maji yaliyokwenda kutuwama katika bwawa la Mindu,na katika miaka ya tisini ikiwa kina cha maji kimepungua na nguvu ya maji kuwa ndogo alionekana maeneo ya kilima cha Lupanga akichukuliwa na mnyororo mkubwa kuelekea baharini,

Nimalizie kwa kusema ni furaha yangu leo nimeiandika historia ya Morogoro nikielekea kuchukua form ya Ubunge,Morogoro Mjini,kwetu Uluguruni, ukiwa Kiongozi ni lazima ujue historia ya Morogoro ili uweze kujua ilipotoka Morogoro na inapotakiwa kuipeleka Morogoro,

Kama Mbunge wa Morogoro inakulazimu kujua mambo mengi mno, pengine kwa viongozi wa kawaida (wa kiserikali au kisiasa) hadi wanakufa wengi hawajayajua na kushindwa kuipeleka mbele Morogoro iliyokuwa Mji toka Mwaka 1928 lakini hadi leo 2020 Morogoro bado ni Mji ule ule,

Morogoro ilikuwa Halmashauri Mwaka 1928 kabla ya Dar es Salaam, mpaka leo Morogoro ilitakiwa iwe imeshatoka kwenye Uhalmashauri na kuwa Jiji,

Wazambia, Wamalawi, Wazimbabwe, Wamsumbiji, Wakongo, Waburundi, Warwanda, Waganda, Wakenya wanapita hapo Morogoro wanakuja Kariakoo kununua viatu, nguo, mikoba, na bidhaa nyingine, Je Morogoro mmeshindea kutengeneza hub iwe kama Kariakoo ndogo mkichukua vitu vyote vya Kariakoo vipatikane hapo!?

Viongozi wa Morogoro walipaswa waitangaze vilivyo kwamba Morogoro ni Kariakoo ndogo na hakuna sababu ya kupita Morogoro kwenda Dar es Salaam kilomita 200 wakati vitu vyote vinapatikana Morogoro,

Mkiweza kuwapata awa Wazambia, Wamalawi, Wazimbabwe, Wamsumbiji, Wakongo, Waburundi, Warwanda, Waganda, Wakenya wanaopita hapo Morogoro kuja Kariakoo kununua viatu, nguo, mikoba, na bidhaa nyingine,

Mtakuwa mmepata dola, hivyo biashara ya fedha ya kigeni itashamiri Morogoro kubadili dola kuwa shilingi na shilingi kuwa dola, hakuna biashara hapa Kariakoo inayowatajirisha watu haraka kama biashara hiyo ya dola,

Mkiweza kuwapata awa Wazambia,Wamalawi,Wazimbabwe,Wamsumbiji,Wakongo,Waburundi,Warwanda,Waganda,Wakenya wanaopita hapo Morogoro kuja Kariakoo kununua viatu,nguo,mikoba,na bidhaa nyingine,

Mtakuwa mmeleta mzunguko wa fedha hapo Morogoro naamini hakuna kijana atakayekosa kazi,Miaka ya nyuma Morogoro ilipata kuwa hub ya kikazi na kibiashara, People were flocking from all over East Africa coming to Morogoro,

Hii ilisababishwa na Uwepo wa kivutio cha muziki bora katika East Afrika,mziki ulioongozwa na Mbaraka Mwishehe na bendi maarufu kabisa za Cuban Marimba na Morogoro Jazz,

Hii ni changamoto kwa kila kiongozi katika Mkoa wa Morogoro (japo una hiyari ya kuyafanyia kazi au kuyaacha kutegemea na Utamaduni, Jiografia, Mazingira, Wakati, na mipaka ya Kiuchumi).
Kila jambo hufunzwa na falsafa yake, mathalani italeta Maendeleo na tija kwa Taifa la Tanzania.

Nikiishia hapa,Mimi ni
Msemakweli Chakubanga,
Dar es Salaam.
0755078854

-Bachelor of Business Administration in International Business.
-Master's in Leadership and Management.

-Research; Assessing Effects of Micro-Financing on Poverty Reduction.
 
Tutakutana kuchukua fomu ya ubunge...
Nimeipenda historia ya mji kasoro meli bahari Mindu tayari umeitaja.
Na ukanda wa bwawa hilo pana dhahabu maridhawa kabisa.

Umesema kweli Morogoro ni mji au jimbo lililokosa uwakilishi kwa miaka mingi saana, ni moja ya mji uliokuwa mashuhuri sana enzi na enzi kabla ya mikoa mingine lakini ndio mkoa uliosahahaulika na kuachwa nyuma.

Ni heri uwe mbunge wewe au mimi tulete mabadiriko tarajiwa.
 
Mkuu nimekupata Sana Sasa hayo makaburi uliyoyataja ya kichangani ni yapi? Yako sehemu gani pale morogoro? Maana Kuna makaburi yapo njia ya kuendea shule ya sec kigurunyembe Kama unatokea ofisi za manispaa na nyuma ya shihata zamani je ndio makaburi hayo unayoyazungumzia ya kichangani?
 
Aisee
Nashukuru kwa kunijuza kuhusu hostoria ya Morogoro
Kiukweli Morogoro inarudi nyuma sana kwa sasa> Yaani ile Moro ya miaka ya tisini sio ya sasa. Moro ya kipindi kile unakutana na mifereji ya maji safi inatiririka mitaani unaweza hata kunywa. Hii ya sasa ni vumbi tu limejaa.
Nimemiss ile Morogoro ya viwanda haswa
 
Kuhusu iv ya kirumi ingaliko hata Leo halafu hivi kule mlimani kuna watu wanaishi mkuu?
 
Kwa wasiojua Nyerere alikuwa mbunge wa kwanza wa Morogoro wengine Ni Shamim Khan Abood Mzeru nk
 
Mkuu nimekupata Sana Sasa hayo makaburi uliyoyataja ya kichangani ni yapi? Yako sehemu gani pale morogoro? Maana Kuna makaburi yapo njia ya kuendea shule ya sec kigurunyembe Kama unatokea ofisi za manispaa na nyuma ya shihata zamani je ndio makaburi hayo unayoyazungumzia ya kichangani?
Hapana mkuu hayo ya nyuma Shihata ni ya Sultani Kingo Kisebengo.
 
HISTORIA YA MOROGORO, NNE YA KIRUMI NA ASILI YA BOKA, NYOKA MWENYE VICHWA SABA KATIKA MILIMA YA ULUGURU.

Leo 15:15pm 14/06/2020

Wakati wa likizo tukiwa wadogo tulipofunga Shule pale Bungo Primary School, Mimi na ndugu zangu tulikuwa tunakwenda kuwasalimu Bibi na babu kijijini Tawa Matombo,pale kibunduga kwa Mzee Butwa,

Babu na Bibi walifurahi sana na tulipata nafasi ya kufahamu mambo ya mila na utamaduni wetu sisi Waluguru, kijiografia miji ya Matombo na Mgeta ipo nyuma ya milima ya Uluguru, katika miji hiyo ndio asili ya kabila la Waluguru waliopo katika Mkoa wa Morogoro.

Asili ya neno Morogoro ni mluguru, hii ni baada ya Jasusi Mbobezi Henry M Stanley kushindwa kutamka Mluguru na kuongelea kooni na kutoka sauti iliyosikika "Moro-goro" Jasusi Henry M Stanley alipita katika safu za milima ya Uluguru njia ya Kaskazini Mwaka 1874 akiambaa hadi Mashariki ya milima ya Uluguru,

Katikati ya milima ya Uluguru, Henry M Stanley alikutana na jeshi la Simbamweni mtoto wa Kingo Kisebengo, katika mji uliozungushiwa ukuta na kuwa na ngome isiyopenyeka kiurahisi, baada ya kuonekana ni mtu mwema alipokelewa na Mwenyeji wake Chifu Simbamweni,

Jasusi Henry M Stanley aliusifu mji huo uliokuwa chini ya bonde la milima ya Uluguru, akisema mji huo umejengwa kwa mitindo ya kiarabu chini ya bonde la kijani la milima ya Uluguru,yenye misitu minene inayofunikwa na mawingu wakati wote wa Mwaka,

Milima iliyopambwa na mito miwili mikubwa inayokwenda kuzaa mto Ruvu, uliounganishwa na utitiri wa vijito vya maji safi na salama, Jasusi Henry M Stanley katika kitabu chake "How I found Livingstone" chapter 4 na 16 anakiri mandhari ya milima ya Uluguru hajapata kuyaona katika eneo lolote alilowahi kufika katika Afrika Mashariki,

Rejea pia kitabu cha Joseph Thomson:'To The Central Africa Lakes and Back' 1881chapter 1 na 5 kinachoelezea Jeshi kali la Waluguru lilikuwa linavaa majani ya mgomba na magome ya miti,

Thomson akiwa na Baba yake Keith Johnson wakitokea eneo la masai na Ziwa Victoria,wakiingia pwani katika eneo la Waluguru na wakutu Mwaka 1879 anasema hakuwahi kukutana na Waluguru zaidi zao toka kwa Majeshi mengine ya wambuga hadi pale alipokuja kufahamu walikuwepo wengi katika njia aliyopita lakini walivaa majani ya mgomba na kufanana na majani na miti ya porini,

- Historia ya Chief Kingalu,Kiongozi wa Waluguru.

Historia ya Chifu Kingalu inaanzia kwa Chifu Lukwele wa Choma aliyezaliwa mwaka mwaka 1852 na kufariki mwaka 1971, na kuzikwa katika makaburi maarufu wakati huo ya kichangani mjini Morogoro

Chifu Lukwele ndiyo yule askari mwenye historia ya kupigana katika jeshi la Mjerumani dhidi ya Waingereza na washirika wao, kwenye maeneo kadhaa ya Mashariki ya Kati uko uarabuni, Afrika Mashariki, Msumbiji, Malawi na hatimaye Namibia, na kurejea nchini baada ya vita ya kwanza ya Dunia kumalizika katika muongo wa pili wa karne ya 20.

Chifu Lukwele ambaye jina lake halisi ni Salum Bin Msumi, alikuwa ni mmoja kati ya watoto watatu mashuhuri wa Chifu Msumi wa Kibungo, ambaye asili yake kwa baba ni Mluguru na mama ni Mzulu toka Afrika Kusini.

Chifu Msumi aliyeitawala kibungo juu na kibungo chini katika milima ya Uluguru rekodi yake ya ndoa na watoto inaonesha kuwa ni mtu wa mitala, na alikuwa na watoto wengi, zaidi ya 30 katika milima ya Uluguru Mkoani Morogoro, Mbambabay Mkoani Ruvuma na jijini Lilongwe nchini Malawi.

Watoto mashuhuri wa Chifu Msumi ni Lukwele (Salum), Sonanga, na Mleke maarufu kama Kingalungalu (waluguru wanatamka ‘Chingalungalu' yaani Kigeugeu) au kwa kifupi Kingalu wa kwanza, ikiwa ni jina lake la kupanga kutokana na tabia yake ya Ugeugeu (aliwahi kumgeuka mkwewe chifu magoma, na kisha baba yake mzazi Chifu Msumi na kupigana nao vita kali kwa nyakati tofauti!akitaka kuongoza safu yote ya milima Uluguru)

- Kutokana na ubabe na nguvu jina la Kingalu hilo likawa jina rasmi la ukoo ambalo litatawala Waluguru.

Kutoka ukoo wa Chifu Msumi tunaweza pia kupata makabila mengine yaliyotika katika koo ya Kiluguru kama Wazaramo, Wakaguru, Wakutu na Wakwere, wote wakifuata mfumojike (kwa Kiingereza ''matrilinear'') yaani ukoo wa mama ndio unaoongoza familia na watoto wote wanahesabiwa kuwa wa ukoo huo.

Katika kupata jina la mtoto anayezaliwa, mtoto wa Kiluguru huitwa jina la ukoo wa baba yake, ambao ndio ukoo wa bibi mzaa baba. yaani, Waluguru wana 'mtala' na ukoo. Mtala ni jina la ukoo wa baba ambalo ndilo analoitwa mtoto.

Kwa mfano, mtoto akiitwa 'Kobero' jina hili ni mtala, si jina la ukoo wake, kwani 'Kobero' ni jina analopewa mtoto ambaye baba yake ni 'Mmande'. Hali kadhalika, mtoto akiitwa 'Mkude' jina hili ni mtala wa ukoo wa 'Wamwenda', lakini si jina la ukoo wa mtoto. Hivyo basi, kwa Waluguru baba hutoa jina na mama hutoa ukoo, jina ni la ukoo wa baba, na ukoo ni wa mama!

- Nne ya Kirumi iliyochorwa na Mjerumani katika kilima kimojawapo cha Mlima wa Uluguru.

Alama ya ushindi baada ya kuupanda Mlima Uluguru sasa inaelekea kufutika katika Mwamba
wa kilele cha Lupanga, ni historia nyingine ya kukumbukwa kwa kila aliyepanda Mlima wa Uluguru na kupiga picha katika eneo hilo ambalo linaonekana vizuri ukiwa chini katikati ya Mji wa Morogoro,

Kilele cha Lupanga kinachotiririsha maji kikiwa na mita 2,150 toka usawa wa bahari ni cha pili kwa ukubwa katika Mlima Uluguru wenye urefu wa Mita 2,630. Tukiwa Scout wenzangu wa kutoka shule za msingi na Sekondari miaka ya 1990 ilituchukuwa saa tisa kufika kileleni,

Ilituchukua saa tatu kushuka, lakini kwa wengi huwachukuwa saa 11.30 hadi 12 kupanda hadi kwenye kilele iko cha Lupanga chenye nne ya kirumi na saa tano na nusu hadi sita kushuka, kushika kilele hicho ni kazi kubwa na hatari zaidi kuliko kuupanda!).

Katika eneo lenye nne ya kirumi (alama IV) uwa kazi zaidi kupanda, kwani muinuko wake baadhi ya maeneo hufika nyuzi tisini, kiasi cha kutegemea mashina ya miti na mizizi kukuwezesha kusonga mbele.

Kihistoria eneo hili lilikuwa chini ya Mamlaka ya Utawala wa Choma (kabla ya Ukoloni kuchukua hatamu) kwenye eneo la Uangalizi wa Mndewa (Sub-Chief) wa Kibwe ambaye ni Sayyid (His Royal Highness) Mwande.

Nilipata bahati ya kupitia nyaraka za utawala wa Choma (Royal Achieves) sikupata chochote juu ya maana ya alama hii (IV), japo ninavyofahamu iliwekwa na Wajerumani miaka takriban 100 iliyopita wakati vita ya Dunia ikianza kunguruma,lakini niligundua ilimaanisha ushindi wa kupanda Mlima Uluguru na kufikia kilele iko cha Lupanga.

-Boka, nyoka mwenye vichwa saba, anayepatikana katika milima ya Uluguru.

Nikiwa likizo moja kijijini Tawa, Matombo miaka ya 1990 tuliamka asubuhi na kukuta mto Mmanga umejaa mara mbili zaidi ukiharibu kingo za ukuta, nyumba za watu, mashamba, ukichukua mbuzi, kondoo, kuku na kila kilichoonekana mali ya wanakijiji pembeni ya mto Mmanga uliokuwa ukitiririsha maji yake kuelekea mto Mfizigo ambao ulipeleka maji katika mto Ruvu uliokwenda kuingia baharini,

Tulipouliza waliokaribu na mto walikiri kusikia miluzi, makofi na vigelegele usiku wa manane huku kishindo kikubwa cha mtiririko wa maji kikisikika katika mto Mmanga, baadae wazee wa mila walikiri kupita kwa nyoka aina ya boka mwenye vichwa saba, akimeremeta na kung'aa mithili ya nyota za angani, akiwa safarini kuelekea baharini.

Wazee walitueleza makazi ya nyoka huyo ambayo uwa ni Mlimani na karibu ya vyanzo vya mito mikubwa,mahali anapokaa uwa panabarikiwa sana mafuta, na ithibitisho wa hilo alipita kwe mto usiku basi asubuhi utakutana na harufu ya petrol na mafuta ya taa, ikieleza mahali alipotoka ameacha hazina hiyo ya mafuta.

Kwa watu wanaokaa maeneo hayo mfano kabila la walugulu wanalifaham hilo, Nyoka huyo uwa na maisha ya kuhama kutoka eneo moja kwenda eneo lingine na katika safari zake inasadikika anatoka milimani na kuelekea baharini kupitia katika maporomoko ya maji na vijito vidogovido.

Kipindi cha masika au mvua kubwa ndio mida anaotumia kwa kipindi cha miaka kumi ndipo hayo yanatokea, katika maeneo hayo karibu na vijiji jirani kuna matokeo ya watoto kuumwa kipindi tuu nyoka huyu anapofanya safari zake,

Mwaka 1984 nyoka huyo alionekana akiondoka kuelekea baharini kwa njia ya moshi baada ya kutiririka na maji yaliyokwenda kutuwama katika bwawa la Mindu,na katika miaka ya tisini ikiwa kina cha maji kimepungua na nguvu ya maji kuwa ndogo alionekana maeneo ya kilima cha Lupanga akichukuliwa na mnyororo mkubwa kuelekea baharini,

Nimalizie kwa kusema ni furaha yangu leo nimeiandika historia ya Morogoro nikielekea kuchukua form ya Ubunge,Morogoro Mjini,kwetu Uluguruni, ukiwa Kiongozi ni lazima ujue historia ya Morogoro ili uweze kujua ilipotoka Morogoro na inapotakiwa kuipeleka Morogoro,

Kama Mbunge wa Morogoro inakulazimu kujua mambo mengi mno, pengine kwa viongozi wa kawaida (wa kiserikali au kisiasa) hadi wanakufa wengi hawajayajua na kushindwa kuipeleka mbele Morogoro iliyokuwa Mji toka Mwaka 1928 lakini hadi leo 2020 Morogoro bado ni Mji ule ule,

Morogoro ilikuwa Halmashauri Mwaka 1928 kabla ya Dar es Salaam, mpaka leo Morogoro ilitakiwa iwe imeshatoka kwenye Uhalmashauri na kuwa Jiji,

Wazambia, Wamalawi, Wazimbabwe, Wamsumbiji, Wakongo, Waburundi, Warwanda, Waganda, Wakenya wanapita hapo Morogoro wanakuja Kariakoo kununua viatu, nguo, mikoba, na bidhaa nyingine, Je Morogoro mmeshindea kutengeneza hub iwe kama Kariakoo ndogo mkichukua vitu vyote vya Kariakoo vipatikane hapo!?

Viongozi wa Morogoro walipaswa waitangaze vilivyo kwamba Morogoro ni Kariakoo ndogo na hakuna sababu ya kupita Morogoro kwenda Dar es Salaam kilomita 200 wakati vitu vyote vinapatikana Morogoro,

Mkiweza kuwapata awa Wazambia, Wamalawi, Wazimbabwe, Wamsumbiji, Wakongo, Waburundi, Warwanda, Waganda, Wakenya wanaopita hapo Morogoro kuja Kariakoo kununua viatu, nguo, mikoba, na bidhaa nyingine,

Mtakuwa mmepata dola, hivyo biashara ya fedha ya kigeni itashamiri Morogoro kubadili dola kuwa shilingi na shilingi kuwa dola, hakuna biashara hapa Kariakoo inayowatajirisha watu haraka kama biashara hiyo ya dola,

Mkiweza kuwapata awa Wazambia,Wamalawi,Wazimbabwe,Wamsumbiji,Wakongo,Waburundi,Warwanda,Waganda,Wakenya wanaopita hapo Morogoro kuja Kariakoo kununua viatu,nguo,mikoba,na bidhaa nyingine,

Mtakuwa mmeleta mzunguko wa fedha hapo Morogoro naamini hakuna kijana atakayekosa kazi,Miaka ya nyuma Morogoro ilipata kuwa hub ya kikazi na kibiashara, People were flocking from all over East Africa coming to Morogoro,

Hii ilisababishwa na Uwepo wa kivutio cha muziki bora katika East Afrika,mziki ulioongozwa na Mbaraka Mwishehe na bendi maarufu kabisa za Cuban Marimba na Morogoro Jazz,

Hii ni changamoto kwa kila kiongozi katika Mkoa wa Morogoro (japo una hiyari ya kuyafanyia kazi au kuyaacha kutegemea na Utamaduni, Jiografia, Mazingira, Wakati, na mipaka ya Kiuchumi).
Kila jambo hufunzwa na falsafa yake, mathalani italeta Maendeleo na tija kwa Taifa la Tanzania.

Nikiishia hapa,Mimi ni
Msemakweli Chakubanga,
Dar es Salaam.
0755078854

-Bachelor of Business Administration in International Business.
-Master's in Leadership and Management.

-Research; Assessing Effects of Micro-Financing on Poverty Reduction.

Mkuu hawa wakenya wanaokwenda kununua vitu kariakoo kupitia Morogoro wanatokea au kwenda wapi?

Hawa wacongo, warundi, wanyarwanda na waganda si wanaweza kabwa makoo na wengine huko huko Kagera kabla ya kufika Moro mkuu wakaishia huko huko?

Vipi hawa wa Malawi na Zambia wakikabwa makoo tokea pande za Mbeya?

Mkuu wote hao si watashindwa kupumua kama bwana George Floyd huko huko na kabla mno ya kufika Moro?

Kwa sera zako hizi unaziona vipi Kagera na Mbeya wakiamua kuzi adopt?

Hii nchi ni yetu sote maendeleo hayana chama wala ukanda.

Vita ni vita Mura!
 
Hapana mkuu hayo ya nyuma Shihata ni ya Sultani Kingo Kisebengo.
Asante sana sana mkuu je haya ya kichangani yako sehemu gani na je hayo ya Sultani Kingo Yana uhusiano na hayo ya shihata?
 
Makaburi ya kichangani yapo huko huko mtaa wa kichangani,hapo zamani kichangani ilitegemewa kuwa kama Kinondoni,kwa maana studio za Cuban malimba na Moro Jazz zilikuwa hapo na wanamuziki maarufu walikuwa wanakuja hapo kurekosi
 
Kwa wasiojua Nyerere alikuwa mbunge wa kwanza wa Morogoro wengine Ni Shamim Khan Abood Mzeru nk
List ya Wabunge wa Morogoro Shamim Khan 1990,Luteni Kanali Mazora1995,Eng Oscar Thobias Mloka 2000,Daktari Omar Mzeru 2005,Abood 2010.
 
Morogoro Oops!!!
Sasa Hivi Mambo Yapoje
Chief Kingo Ama Ndiyo Maana Kuna Kingolwira Kuenzi Jina Lake
 
Back
Top Bottom