Milango ya kuelekea kuzimu kutokea duniani

ONTARIO

JF-Expert Member
Oct 16, 2013
1,885
17,018
Salute!

"Nina uhakika wote kuwa tukio lile litakuwa la mwisho kutoka kwenye ubongo wangu. Watu walishangilia nilipoinama kuzoa damu ya mama'ngu sakafuni. Nilishuhudia kwa macho wakichinjwa vibaya. Nilikuwa na miaka 8, sasa nina miaka 96 wala sijasahau hata chembe". Mwanamama Myahudi Abigael aliongea kwa uchungu mbele ya Camera katika video fupi iliyopata views milioni 62 ndani ya masaa 42. "Baba, mama na ndugu wengine walichinjwa mbele yangu, natamani nami ningeungana nao, lakini niliishia kuzoa damu zao sakafuni" Abigael aliendelea.

583c7f93768793010db189ff218620f1.jpg


Kwa ustadi na uweledi wa hali ya juu kuanzia 1941-1945 katika kila wayahudi watatu wawili waliuwawa katika mauaji ya kikakatili zaidi katika uso wa dunia. Wayahudi zaidi ya milioni 6 waliuwawa kinyama.

Mwanaume mmoja aliyetua duniani kwa kishindo alifurahi kuona mifereji inatiririsha damu ya binadamu. Adolf Hitler aliongoza utawala wa Nazi katika kuteketeza vichwa vya Wayahudi milioni 6 ambao yeye aliwaita magugu katikati ya wanadamu.

Mauaji haya ya kutisha ambayo leo yanajulikana kama 'Holocast' yalikuwa ni jawabu tosha la kitendawili kilichomtesa Hitler juu ya nini afanye kuangamiza damu yote ya kiyahudi katika uso wa dunia.

Yote yalianza baada ya kuamrisha kutungwa sheria ya 'Neremberg' ambayo ililenga kusafisha kizazi cha Wajerumani ambapo hakuna Mjerumani aliyeruhusiwa kuoa/kuolewa na Myahudi. Na kwamba Wayahudi wote walitambulika kama wakimbizi katika taifa la Ujerumani.

Pole pole Wayahudi wakaanza kufukuzwa kutoka kwenye miji mikubwa ya Ujerumani, wakaanza kupokonywa nyumba na biashara walizomiliki.

Lakini ilionekana hawa wayahudi walikuwa na uwezo mkubwa sana katika kufikiri na kutatua changamoto, waliweza kutengeneza network kubwa ya media ili kupaza sauti dunia nzima ijue nini Hitler anakusudia kufanya. Hivyo ilikuwa ngumu sana kwa Hitler na Utawala wake kudeal nao kwa njia za kawaida, sasa Hitler akaja na mbinu mbadala ya kuisafisha Ujerumani.

Kazi itakuweka huru kuelekea kuzimu

Kuanzia mwaka 1937 katika mapori manene yaliyopo katika vitongoji vya Poland, utawala wa Nazi ulianza ujenzi wa kambi, hazikuwa kambi za kawaida bali 'kambi za mkusanyiko' (Concentration camps). Kambi nyingi zilijengwa lakini kubwa zilikuwa tano zikiwemo Majdanek, Chelmno, Belzec, Treblinka na kambi maarufu zaidi ya Sobibor.

Miundombinu ndani ya kambi za KIFO

Kambi hizi zilijengwa katikati kabisa ya misitu minene. Kambi zote zilizungushwa na fensi 3 tofauti, uzio wa senyenge za tetenasi, uzio wa ukuta mrefu pamoja na uzio wa umeme. Kambi zilikuwa na ulinzi mzito sana ambapo kulikuwa na minara ya ulinzi 19-25 (watchtowers). Kwa wakati mmoja, kambi 1 ilipaswa kuhifadhi mateka 45,000-50,000, lakini baadae Wanazi walirundika hadi wafungwa 300,000 kwa pamoja.
e435670e8f143bad0b25bf949af4ef02.jpg


Kambi hizi zilijengwa zikiwa na sehemu tatu kubwa;-
■ Sehemu ya mapokezi
Hapa ndipo wafungwa walifikishwa kwa mara ya kwanza. Walikaribishwa kwa shangwe na bashasha na kupewa maelekezo ikiwepo kutengwa katika vikundi kiumri, kiuweledi, kijinsia, nk.

■ Sehemu ya utawala
Hapa ndipo palikuwa na ofisi pamoja na makazi ya askari na viongozi wa kijeshi. Kulikuwa na anasa nyingi ikiwemo Kulewa, unyanyasaji wa kingono nk.

■ Sehemu ya maangamizi (extermination section).
Huku ndipo yalikuwepo makazi ya mateka, kulikuwa na kumbi kubwa nyingi ambazo zilikuwa na madirisha madogo sana kwa juu kabisa na milango ya chuma, sakafu ya kokoto kubwa kubwa.
915ec4dd93f4a44291d794739734807b.jpg

Gas chambers
Kulikuwa na sehemu za kificho ambapo kulitengenezwa vyumba vidogo mithili ya mabafu ambapo ilikuwa special kwajili ya kunyonya gesi ya oxygen, (mateka wasingeweza kujua hatma yao), kulikuwa na mifereji ya kifo (death trenches) ambazo zilitumika kama machinjio. Ndani humo kulikuwa na vyumba vya mateso makali na majiko yenye masufuria makubwa sawa na matenki ya ujazo wa lita 100,000.
4ce4255319adc45b2f4f5e16e110aebf.jpg


Maisha ndani ya kambi za kifo.

Wayahudi walisafirishwa hadi kambini kwa usafiri wa treni, waliwekwa ndani ya mabehewa ya mizigo kutoka nchi mbalimbali kama Czechoslavakia, Ujerumani, Austria, Uholanzi na Poland.
e6efd202d7ba4a39c3907e09144ed7c4.jpg


Baada ya kufika kambini walipelekwa mapokezi, kisha kukaribishwa kwa furaha kabisa na kupewa maagizo ya kuandikia ndugu zao barua kuwaambia kuwa wamewasili salama (Barua hizi zilitumika kama ramani kuwatambua na kuwakamata wayahudi wengine).
269c054d3ada6f454c7a06030686b9bf.jpg


Wanawake na wanaume walitengwa, na watoto waliruhusiwa kujichanganya na mama zao.

Mateka wote walipewa taarifa kuwa safari yao itaendelea keshowe, lakini lazima wapate kuoga na kukabidhi nguo zao ili zipulizwe dawa ya kuuwa wadudu (disinfectants). Maji ya kuoga yote yaliwekwa sumu kali yenye kuwasha na kusababisha maumivu ya ngozi, na nguo zilipulizwa sumu ya vipele na vidonda.

Vyakula viliwekwa sumu isiyouwa bali inayosababisha maumivu, michubuko na uvimbe kwenye mdomo na ulimi. Midomo ya Wayahudi ilibabuka mno, hivyo wasingeweza kuzungumza wenyewe kwa wenyewe.

Mapigo na mateso ndani ya kambi yalianza baada ya siku 2 tangu kuwasili. Siku ya 4 na kuendelea Wayahudi makundi kwa makundi waliinguzwa ndani ya gas chambers, watu 500 kwa pamoja wangeingizwa kwenye vyumba vidogo na kunyimwa oxygen kwa kuingiziwa Carbon monoxide hadi kufa.
6d541dcf8e6f1f0d9803eafdb8f273cc.jpg


Wengine waliingizwa kwenye mifereji ya mauwaji kisha kuchinjwa shingoni kama kuku. Damu ilitiririka hadi kilomita 1 kuelekea kwenye mashimo yaliyejengwa kama matenki ya chuma. Damu hizi ndiyo ilitumika kufua umeme asilia ambao ulitumika katika makazi ya askari wa Nazi kambini. Mashimo haya waliitwa 'ziwa tamu'.

Baadhi ya mateka waliuwawa kwa vipigo vikali ndani ya vyumba vya mateso, ambapo wangekatwa pole pole kuanzia vidole, viganja, mikono, miguu, shingo hadi kifo. Hili ni lile kundi la mateka watata na wasumbufu zaidi.
c02fa29614382f9c0ed86372e5f65d95.jpg


Kuna Wayahudi wengine walitupwa kwenye vyumba vya barafu, hivyo wangepigwa baridi, wagande hadi kufa.
f1b8e55506a21c5961d66e760d4e7417.jpg


Kuna wengine walitumbukizwa kwenye masufuria ya maji yaliyotokota na kuachwa wachemke hadi kufa.

Wayahudi wengine waliingizwa kwenye kumbi kubwa na kufungiwa humo bila mafanikio ya kutoka na kuachwa bila huduma yoyote kwa siku 8. Wengi walikufa kwa kukosa hewa, joto kati, baridi, njaa na kiu.
65dd1ee4701cfb74a7892ce9d74b55a8.jpg


Kuna wayahudi waliuwawa kwa sumu ya maumivu ya tumbo.
0ae0f7aa07779f444c55c07de737ae4b.jpg


Wengine hawa walemavu na wanawake walitumika kama shabaha katika mafunzo ya wanajeshi ya kupiga risasi.

Baadhi ya wafungwa walifukiwa wazima kwenye mashimo makubwa. Ili kuficha ushahidi miili yote ilifukiwa mashimoni na mingine kuchomwa moto hadi majivu (cremation).
8b3f8a6aad551a7ca49264122e59e9ab.jpg


Kila baada ya wiki 2 waliletwa wafungwa wengine ambao wangeuwawa kwa staili kama hizo.

Kidume LEON: Escape from the Sobibor.

Kukikuwa na majaribio mengi sana ya kutoroka kutoka kambi za vifo, hakuna hata jaribio moja lililofanikiwa. Waliojaribu kutoroka ndio wale waliouwawa vifo vya kikatili zaidi kama kuchomwa moto wakiwa wazima, kuchemshwa kama supu na kukatwakatwa vipande.

Mwaka 1943 msimu wa kiangazi (summer), mateka wengi walifikishwa katika kambi 1 maarufu ya Sobibor. Hili kundi lilikuwa alikuwemo Leteni wa Kirusi mwenye damu ya Kiyahudi Leon. Jamaa alikuwa genius sana mwenye uwezo mkubwa sana katika maswala ya kivita.

6007911a898b120fe694c188328c9692.jpg


Siku ya kuwasili pale mapokezi aliweza kwa asilimia 100 kujifanya kichaa, hivyo hakuna Mnazi aliyemtilia shaka wala hakuna mlinzi aliyemshtukia.

Akiwa kambini alifanya vikao vya siri sana na mateka wenzie, akateuwa viongozi na kikosi kazi. Aliwashawishi mateka wenzie chini chini kwa maneno haya "Hakuna kushindwa, tupo hapa kwajili ya kufa, kifo ni lazima lakini si kufa kama mzoga mikononi mwa mjerumani".

Jamaa alikuwa vizuri kwenye kuchora ramani za utekaji na uvamizi. Aliwateua mateka watatu na kuwapa jukumu la kulegeza mlango wa ukumbi ambapo yeye na makamanda wake wengine waliishi. Mpango wa kulegeza mlango ulifanikiwa ndani ya siku moja kwa kuvunja kwa siri kuta za pembeni kwa vyuma vidogo vidogo.

Jembe Leon akasuka ramani ya kuwateka walinzi wa kuwapora silaha.

Usiku wa mashambulizi, Leone akiwa front line pamoja na mateka wachache waliweza kuvamia minara ya walinzi 23 yote na kuwateka walinzi watatu waliokuwa katika kila mnara, wakawauwa na kuwapora silaha. Jumla ya Walinzi Wanazi 44 waliuwawa na mapambano yakaanza. Kumbi zote za kulala mateka zikafunguliwa na mateka wakaamriwa wafanye kila wawezalo kutoroka kambini.

Baada ya Utawala kugundua wakaamuru askari washambulie, kina Leone walipambana sana sana, mateka wengi waliuwawa wakijaribu kutoroka.

Bwana Leone hakurudi nyuma, alipambana sana hadi kupigwa risasi mkono wake wa kulia hakurudi nyuma, alizidi kupambana kiume, alitumia mkono wake wa kushoto mpaka risasi zilipomuishia. Akapiga magoti, akaweka mikono mfukoni kisha akasema "Nimefurahi sana kuja huku, naomba mnionyeshe njia ya kuelekea kuzimu". Hapo alitandikwa risasi 17 hadi kifo.

Wayahudi waliuwawa sana. Lakini zaidi ya 300 walifanikiwa kutoroka wakiwa hai.

Baada ya uvamizi wa Escape from Sobibor

Hitler akiwa na hasira sana aliamrisha kambi ya sobibor iwe vumbi mara moja. Ndani ya muda mfupi sobibor iliteketezwa yote na eneo lote likalimwa na kupandwa mazao ya chakula kisha shamba likatelekezwa.

Mataifa makubwa duniani yakapata siri ya kambi za mauwaji za Wanazi lakini bado hawakuweza kung'amua locations ya kambi hizi.

June 1944, Marekani, Uingereza, Canada na Vikosi huru vya Ufaransa vilivamia maeneo yote yaliyotekwa na Ujerumani. Leo hii uvamizi huu unajulikana kama 'D-Day invasion'

aa22ee712e156f1e2901e13c78ffcec2.jpg


Ndani ya siku chache Ujerumani alitandikwa vibaya mno, Hitler akaamua amuuzie kesi Kamanda wake Gerd Rund aongoze vita hiyo, kisha yeye akaingia mafichoni kwenye handaki la siri.

Hadi July 1944 Ujerumani alikuwa nyang'anyang'a, alikuwa tayari kapokonywa eneo lote la ulaya aliloliteka awali. Kambi ya kwanza ya mauwaji ilipatikana, japo mateka wote walikuwa wametoroshwa kuelekea magharibi zaidi ili kupoteza ushahidi lakini chembe za mifupa ya wayahudi ilipatikana.

Aug 1944 kambi kubwa zaidi ya mauwaji ilipatikana, Wayahudi 8203 walikutwa wakiwa hai, wengi walikuwa ni watoto wadogo.
d344703afc765f12904de11428523bcf.jpg


Wasovieti walivyozidi kuelekea Magharibi waligundua kambi za mauwaji zaidi ya 112. Waandishi wa habari walirecord matukio yote kama mateka walivyosimulia, documentary ilirushwa kwenye masinema mengi ya Ulaya. Mauwaji haya yaliliza dunia nzima.
5cce901d3a51ed368cdb08a5de6bced8.jpg


Keshowe asubuhi jembe Churchill-waziri mkuu wa Uingereza akatangaza kipaumbele chake namba moja ni kichwa cha Hitler. Hitler akawa adui namba 1 wa dunia nzima.

Kufika April 1945 Ujerumani ilitandikwa chakari hadi majeshi wakaamua kusurrender. Na Hitler ikasemekana aliamuwa kujiuwa yeye pamoja na mkewe. (lakini nina recommend usome uzi wangu wa nyuma wa 'Mein Kampf' ).
da34965f88cbdfb4603746f8fc080342.jpg
mabaki ya miili ya mateka wa holocaust.
 
Najua swali la kwanza mtu smart atauliza ni "Kwanini Hitler aliwachukia mno Wayahudi?".

Sababu;-

■Ushawishi wa Wayahudi na Wakomunisti.
Hitler akiwa mtoto hadi anakuwa mtu mzima kulishamiri Ukomunisti wa hali ya juu ambao kwa namna moja uliwafanya Wajerumani wawe daraja la chini, wawe maskini na kukosa ushawishi duniani. Wayahudi walikuwa mashabiki wakubwa sana wa Ukomunisti ambao pia uliwafanya wawe na nguvu sana katika nyanja tofauti tofauti.

■Mdororo mkubwa wa uchumi.
Baada ya kutokea Global economic depression Ujerumani walibaki kuwa mafukara sana lakini wayahudi hawakukumbwa na mdororo huo kwasababu wao ndio walikuwa wamiliki wa biashara, vitega uchumi, na makampuni makubwa. Hitler aliona kama Wayahudi wanawanyanyasa kiuchumi.

■Kushindwa WW1.
Hitler aliamini fika kuwa anguko la Ujerumani ktk WW1 lilisababishwa na Wayahudi ambao walilidhoofisha taifa kuanzia ndani (poisoning from inside). Aliamini Wayahudi waliwasaliti vitani.

■Athari ya kitabu cha fasihi andishi.
Hitler hakuwa mtu mwenye elimu kubwa sana, lakini akiwa shule alipata bahati ya kusoma kitabu kilichopinga itikadi za Wayahudi na Waarabu (Anti-semitic literature).
Kitabu hicho kilieleza kuwa wayahudi ndio chanzo kikuu cha balaa zinaikumba Ujerumani, na kwamba Wayahudi ni wanafiki, wasaliti, si waaminifu na hawana uhalali wa kuwa raia wa Ujerumani.

■Maisha ya utotoni ya Hitler.
Inasemekana kiuhalisia Hitler mwenyewe ni Myahudi, kitu ambacho mama'ke hakumwambia utotoni. Chuki ilianza alipishuhudia daktari wa kiyahudi ameshindwa kumtibu mamake kansa ya ziwa hivyo kumsababishia kifo.
Pia Hitler anakumbuka mamake akiteswa sana wakati anafanya kazi za ndani katika familia moja ya matajiri wa Kuyahudi.

■Matatizo ya ubongo.
Kabla Hitler hajawa Chancellor wa Ujerumani aliingia jeshini kupambana WW1 ambapo alipata jeraha kubwa la kichwani. Aliacha jeshi kwa matatizo ya Ubongo kuwa makubwa. Watu wa saikolojia wanasema hata baada ya kupona Hitler alitokwa na mshipa wa utu, hakuona shida kuchinja na kutiririsha damu ya binadamu.

■Kutakatisha kizazi cha Wajerumani.
Hitler aliamini Ulaya ni ya watu weupe tu na Ujerumani ni ya Wajerumani tu, wengine wote hasa Wayahudi ni Magugu na mende. Hivyo alidhamiria kuisafisha ujerumani ibaki na Wajerumani tupu kwa kuwauwa Wayahudi wote.

■Tetesi kuhusu wayahudi.
Katika kitabu cha siri cha wayahudi kilichoitwa 'Itifaki za mababu wa Sayuni' kilidadavua jinsi ambavyo wayahudi walipanga kuongoza na kuitawala dunia katika nyanja za uchumi, biashara na fedha. Hitler aliamini Ujerumani Chini yake ndiyo ilipasa kuitawala dunia na si vinginevyo.

■Maswala ya kisiasa na utaifa.
Hitler aliamini wapinzani wake wengi wa kisiasa waliwatumia Wayahudi kumdhoofisha na kwamba Wayahudi wengi hawakushikamana na matakwa ya kisiasa ya Wanazi.
 
Holocaust didn't happen.Hitler couldn't gather so many Jews(more than six million,because 6m is a number of those killed,not captured) just in Europe in a short time.He didn't have the means.

Holocaust is meant to put Jews in a sympathetic position through the eyes of the world.
In other words holocaust was consipered in order to allow their brutal occupation of Palestine.
 
Holocaust didn't happen.Hitler couldn't gather so many Jews(more than six million,because 6m is a number of those killed,not captured) just in Europe in a short time.He didn't have the means.

Holocaust is meant to put Jews in a sympathetic position through the eyes of the world.
In other words holocaust was consipered in order to allow their brutal occupation of Palestine.
Wanazuoni, taasisi za haki za binadamu, wapelelezi kutoka marekani na hata viongozi wa Nazi wote wamekuwa na mashaka juu ya idadi sahihi ya Wayahudi waliouwawa kwenye holocaust. Wengi wakidai watu milioni 6 ni wachache sana.

Kiusahihi majina ya wayahudi waliothibitishwa kuuwawa kwenye holocaust wanafika mil 4.3, achilia mbali ambao hawajagundulika hadi leo.

Ushahidi wa miundombinu katika concentration camps unaonesha wazi kwamba kuna uwezekano mkubwa kuwa waNazi waliwauwa kimkakati zaidi ya watu milioni 6.
 
Mashahidi wa Yehova ni kina nani hao?
Mkuu kisu cha ngariba hawa mashahidi wa Yehova ni dhehebu la Wakristo ambao wana msimamo mkali sana wa kidini.

Katika utawala wa Hitler waligoma katu katu kuingia jeshini wakiamini Mungu wao si wa vita, hawakukubaliana na matakwa ya Hitler na walidai Hitler ni wakala wa shetani. Kuna kiongozu wa hili dhehebu aliwahi kusema Mungu wao atamchoma Hitler moto wa kipekee.

Hitler akaona hawa nao ni magugu. Zaidi ya mashahidi 20,000 waliuwawa.
 
Huwa nafikiria kwa jinsi Waisrael kwa sasa walivyotapakaa katika nchi mbalimbali haswa huko Ulaya na wengine wakiwa na nafasi kubwa kama wataalamu ndani ya majeshi ya nchi hizo ikiwepo Ujerumani..Ni kweli wameamua kusamehe na kusahau walichofanyiwa na Hitler ama nao wanatengeneza kambi za vifo kwa ajili ya Wajerumani?
 
Na si inasemekana kuwa Hitler alikimbilia Argentina? Baada ya kutafutwa sana baadae mossad walifanikiwa kumkamata
 
Back
Top Bottom