Mikopo inaumiza watumishi chanzo cha rushwa na matumizi mabaya ya ofisi

ndege JOHN

JF-Expert Member
Aug 5, 2015
19,579
44,825
Hata ingekuwa ni wewe una shida umekwama labda ada au kodi kama unadhaminika lazima ungekopa ikizingatiwa USA NA CHINA pia wanakopa. Shida inaanza pale unategemea upate activities za serikali ulipwe posho upunguze madeni kumbe ni uongo hesabu zinagoma aidha unaitumia au inaibuka dharura nyingine hivyo unabakia kuwa mtumwa wa madeni.

Kuna staff alikuwa anamcheka mwenzake anavyoenda kaushadamu siku moja huyu mwenzake kama bahati akaiokota salaryslip ya huyo staff aisee ni zaidi ya comedy Faidika, bayport, ABC, nmb kote jamaa yupo sasa hapo utabakiwa na nini hata kama take home ingekuwa 1.5 m kumbe alikuwa anamcheka mwenzake kama kufanyia bullying tu..bado kuna ada,misiba,sherehe,mizinga kama ndo mtu wa kumwagilia pombe chini ya pua ni hatari.

Haya itokee mchoro na deal unashirikishwa utashindwa kweli kujilipua.Ndo maana wale waliokamatwa na mashine fake za POS sio kwamba wanapenda sana ila mtu anafikiria anaona hii ndo kamba yake halafu unakuta hata hayo mabillion yanayotajwa kuibiwa halmashauri sio za staff wadogowadogo nyingi huwa zinaenda juu unaweza kuta hao wakata risiti wanahusika lakini labda kaambulia million 3 tu kwenye hayo mabillion.

Siungi mkono ubadhirifu lakini chanzo kinajulikana ni mishahara kiduchu sana ya ofisi nyingi.ni taasisi chache ndo wanaolipana vizuri na kukopeshana hela ya maana mfano NHIF ambayo hata ukisema ujenge unamaliza kujenga ila nyingi ya ofisi za umma ni majanga full stress ndo ajira inakuwa kama Ndoa kwamba KATAA AJIRA NI UTAPELI
 
Ila kuna miamba huko aisee sijui haigopi hela za moto..mimi aisee Mungu anisaidie nisidokoe hela isiyo halali yangu maana najua takukuru sitawaweza
Hao jamaa uliowataja sio kabisa yaani .
Rafiki nimekaa ndani sana , ni mwaka huu nimerudi uraiani na kuendelea na kazi ila kuiibia serikali ni rahisi ila pia ukiona huko huru jua hawajaamua kukufuatilia .

Nimejifunza sasa naridhika na kidogo nachopata , napiga kazi kwa moyo ijumaa niko mjini na totoz kula maisha sana .

Ila kuiibia serikali kwasasa sitaki na nimekoma lakini tukatae tukubali hujuma haiwezi kukuacha salama .
 
Mkuu unazidi kunitisha ni kweli wakati mwingine unakuta umeunganishwa kwemye ishu na kama unavojua kazi za kiofisi ni siri Huna budi kukubaliana na wenzako mpitishe jambo ila sasa linapokuja kuwageuka ni aidha uziteme au uhangaishwe sana maelezo kama yote.ndo maana mimi hata ukuu wa kitengo wala uboss siutaki kwa sababu najua for any case utawajibika wewe in charge bora niridhike na hiki cheo tu kwanza in fact uzuri kuna vilifestye ninavyo najua sitafikiria kupewa uongozi hio kwangu mimi ni salama zaidi
 
Hapo ndiyo tunapouvaa mtego bila kujua
Ndiyo maana nimejifunza urafiki kazini hapana maana mnapanga issue vizuri inatick kumbe kuna mchomaji .

Dili likimbumburuka mkuu wa idara unalo kuna mijitu imetoka familia za kimasikini yaani kesi kidogo ishakimbia nchi eti oooh sitaki familia yangu ipate mawazo juu yangu .

Msala unabaki nao pekee yako unasekwa lupango mwenyew wahuni wanakucheua no kuja hata kukupa hi .

Unapambana unayamaliza unatoka lupango yanajazana magetoni kukupa pole , unavunga unarudi kazini kibabe unapiga kazi no urafiki wewe na life lako .

Yanakugeuza role model kwa ajira mpya eti oooh kuwa makini mwenzio yalimkuta yaani ni upuuzi mtupu .

Oya wewe mimi rafiki yangu ni pombe ndiyo nampa siri zangu tu ila hawa masnitch wakunipigia mara oooh blood , mara homie sitaki ushoga wao.
 
Back
Top Bottom