Mikopo eeehhh noumer,tafadhali chukua hatua(muombaji kawachia bank vumbi..)

Iceberg9

JF-Expert Member
Nov 6, 2012
24,878
47,725
Kwa Hali ya kushangaza bank hizi mbili zajikuta wanapigania kupiga mnada nyumba iliyokuwa as collateral security kwa mteja wao aliyekuwa amechukua mkopo huku mteja huyo akiziacha bank hizo kwenye mataa na vumbii nyuma
1460752316624.jpg
 
Jamaa kaweka nyumba ya urithi rehani familia haijuwi wamekuta bandiko nyumba inauzwa, ama case ipo mahakamani hapo ndo watu wanapo anza kuumwa degedege
Hivi inakuaje bank wanampa mkopo mtu kwa hati ambayo sio jina lake? unakuta mtu yupo kwenye mirathi lakini sio msimamizi wa mirathi anaenda bank anakopa bila hata barua ya wanafamilia. Hizi bank zetu zinasababisha sana migogoro kwenye familia.
 
Watu wanafanyaga fojali wa hizi hati mkuu, mfano mzuri ni huyu jamaa amewezaje kuweka rehani hii nyumba kwa bank zote mbili,hati ya nyumba hiyo hiyo bank zote walipewa na muombaji mkopo hapo kuna mambo ya fojali watoto wa mjini tena....
 
Hakuna mkuu bank wakifata procedure zote vizuri ni rahisi kutambua, tatizo wameendekeza sana 10% wewe leo ukienda bank lazima utoe kiasi ndo upewe mkopo, rushwa huwa inaharibu uwajibikaji na umakini, mtu anawaza pesa tu.
 
Ni tamaa ya bankers wanaokula cha juu ilhali wanajua wanachokifanya ni kinyume na sheria, wanakula chao likisanuka ndio hivyo tena
 
Hivi bank wakipiga mnada wanauza kw bei karibu na bure kabisa si cha msingi warudishe chao..
 
Watu wanafanyaga fojali wa hizi hati mkuu, mfano mzuri ni huyu jamaa amewezaje kuweka rehani hii nyumba kwa bank zote mbili,hati ya nyumba hiyo hiyo bank zote walipewa na muombaji mkopo hapo kuna mambo ya fojali watoto wa mjini tena....
Inawezekana kama hilo eneo halina hati ya serikali bali mkataba wa mauzo,ambao unaweza ukaandika kwa njia nyingi kwa kumaanisha kitu kile kile.
 
Uzembe wa hizo Bank ndio maana kabahatika kupata hilo jina la MJANJA.
Ila kumbe inawezekana.....Ukawazunguka bank kwa style hii ukapiga mpunga mrefu... Hapo kuna bandiko tatu, kesi ipo mahakamani,bank ya CRDB wanayo hati na nyumba imeshauzwa, NMB wanasema ni mali yao,, bonge la mkanganyiko
 
Ninge mjua huyu mkopaji ninge mpigia saluti, maana ni kama MICHAEL SCOFIELD
 
Ila kumbe inawezekana.....Ukawazunguka bank kwa style hii ukapiga mpunga mrefu... Hapo kuna bandiko tatu, kesi ipo mahakamani,bank ya CRDB wanayo hati na nyumba imeshauzwa, NMB wanasema ni mali yao,, bonge la mkanganyiko
Mwenye hati halali ndio mmiliki halali
 
Back
Top Bottom