Mikopo CRDB na NMB

Aisee wacha nife maskini kuliko maisha ya kukopa kopa. Una mshahara wa laki 4.2 halafu wachukue Nusu hapo mtu unaishi Dsm na familia mtatoboaje?
Kama unachukua kufanya biashara huwez liona gepu la mkopo.

Mshahara kwako utakua Ni ziada TU katika mizunguko yako ya KILA siku.

Ktk mikopo, akili yako isiwe upande wa kufeli mkuu

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Na mtu anapotaka kuchukua mkopo ni bora aconsider mkopo atakaochukua hata kama ni kiwango kidogo na kama itakuwa ni kwa ajili ya kufanyia biashara basi ahakikishe faida anayopata kwenye hiyo biashara kwa mwezi izidi kiwango cha makato yake:

Mfano amechukua mkopo milioni 7, labda aanzishe biashara ya boda boda. Kwenye mkopo makato yake labda ni laki 2.
Hivyo kama ataanzia na boda boda 3, wiki atapata 50 elfu kwa kila boda boda hivyo inakuwa

50,000 x 3 = 150,000 kwa wiki
150,000 x4 = 600,000
Hivyo makato yake yatakuwa laki 2 lakini yeye anazalisha laki nne zaidi kwa mwezi. Hivyo maumivu ya mkopo hatoyapata kwa vile faida anayopata ni mara mbili zaidi ya mkopo. Kwa mfano kama makato ni kwa miaka 5 = Marudisho yake Bank itakuwa milioni 12.

Hivyo kwenye biashara yake ndani ya mwaka tu atakuwa ametengeneza 600,000 x 12 = 7,200,000 Hivyo hapo ana uwezo wa kupunguza deni ndani ya mwaka au anauwezo wa kuongeza pikipiki nyingine. Hivyo biashara yake itazidi kukuwa.

Na kama ataongeza pikipiki nyingine 3 atakuwa na uwezo wa kulipa deni lote Bank ndani ya miaka 2 kwa maana atakuwa na pikipiki 6 ambapo kwa mwezi atakuwa na 1,200,000 x 12 = 14,400,000.

Kwa mtizamo wangu atakuwa na uwezo wa kumaliza deni lote ndani ya miaka 2 kwa vile atakuwa tayari kwenye makato yake ya mkopo atakuwa ameshakatwa 4,800,000 hivyo anao uwezo wa kumalizia 7,200,000 iliyobaki. [emoji120][emoji120][emoji120] Huu ni mtizamo wangu binafsi

[emoji2398]ᵃʳᵉᵉᵐ [emoji769][/b]
 
Nilipobisha ni sababu kwanza makato hayapungui huu ni mwaka wa pili, makato ni constant na benki ni hiyohiyo crdb!

Ndio maana nikasema ulichosema SIO KWELI.
 
Nilipobisha ni sababu kwanza makato hayapungui huu ni mwaka wa pili, makato ni constant na benki ni hiyohiyo crdb!

Ndio maana nikasema ulichosema SIO KWELI.
Hukunielewa, makato hayapungui hadi unamaliza mkopo, kinachopungua ni riba. makato yakipungua mkopo hauwezi kuisha
 
OK

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Yeap I respect JF

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Yaani broo umefafanua vizuri mno. Nakupa big up sana

Sent using Jamii Forums mobile app
 

Hesabu za darasani na za mazingira halisi ziko tofauti apo umeassume other factor remain constant kama Service za pikipiki, pikipiki kuibiwa, ajali, uchakavu wa pikipiki itafikia mahala utaiuza ata kwa laki 8 izi factor zote wewe hauja ziweka apo.

Njo kwenye reality sasa unazan utapata madereva wote wahaminifu walete izo pesa kwa wakati?
Ulicho ongea ni kweli kwenye
Kudetermine credit worthness of borrower tunaangalia kitu kinaitwa

Repayment Capacity(RC)
Net profit of bzns( NB)
borrower living expenses (BL)

RC=NB-BL

Baada ya hesabu hii hapa tunalinganisha sasa rejesho la mteja kila mwezi labda alibidi arudishe 120k@week
Tunapima sasa kwa mfano wako wa pikipiki (3) uyu mtu anazalisha 150k each week je anategemea biashara hii pia kwa matumizi mengine? Jibu kama ni ndio tunaangalia kila week anatoa pesa kiasi gani katika faida ya biashara mfano anatoa 10k ya services ndogo pikipiki zote, anategemea pesa ya kula hapa hapa kwenye hii biashara kama elfu 40 anatoa kila week kwaiyo jumla ya matumizi yake ni 50k so

RC=150k-(pesa ya kula + ela ya service za pikipiki)
=150k-(40k+10k)
=150k-50k
=100k
Kwaiyo unaona uwezo wa mteja kurudisha mkopo kila week ni 100k ila kumbuka anataka mkopo mkubwa ambao ataitaji rejesho la 120k hivyo hapa Credit officer ana option 2
Either kumsgauri mteja achukue mkopo wenye kato la chini (yaani apunguze kiwango cha mkopo) au anacancel mchakato mzima kwa kutompa mkopo mteja sababu ni

Mteja atakua hana uwezi wa kurejesha pesa kila week.
Rejesho la taasisi ni 120k
Uwezo wa mteja ni 100k

Inamaana kuna uhaba wa 20k kila week hivyo mkopo unaweza usilipike kikamilifu.
Afisa mikopo wengi hawazingatii hii kanuni kwakua wao wanacho jali ni kufikisha target na ndio maana muda mwingi wanapata wakopaji wabaya na sugu wa kulipa madeni


Sent from my iPhone using JamiiForums
 
Mh ! Naaam
Sent using Jamii Forums mobile app
 
Huu uzi Ni mzuri kuliko ule wa rikiboi una nondo zote ambazo hazifundishwi ofisini muajiriwa mpya anapaswa ajue
 
Sawa kwa mtazamo wako. Lakini kwasasa watu wanafanya biashara ki mikataba.

[emoji2398]ᵃʳᵉᵉᵐ [emoji769]
 
Elimu nzuli sana
Congratulations bloo
Sent using Jamii Forums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…