Elections 2010 Mikoa ya Kuamshwa 2015

Chadema ni chama cha vurugu.
Nawashauli jiungeni na chetu cha CUF kimejaa heshima

CUF na ccm lao moja. Mtwara, lindi, tanga, tabora na ruvuma cuf inajitahidi kukusanya kura, sasa tuone kama wataendelea. full stop
 
Jambo la ajabu ni kuwa mikoa inayosema tutafia CCM ni ile inayonuka umasikini wa kiwango cha juu. Ni wajibu wetu wote kuzinduana maana inaelekea kama ilivyo kwa Rais aliyepo(ambaye ni mwenyekiti wa CCM) kuwa hajui kwa nini nchi hii ni masikini, basi hata hao wanaoikumbatia CCM nao pengine hawajui kwa nini mikoa yao ni masikini. Wanadhani ni mapenzi ya Mungu wao kuwa hivyo na CCM haihusiki. Tuwasaidie kuzinduka.
 
Morogoro inatia aibu. Mie natoka mkoa huo lakini kwa swala la kusinzia ndo tunaongoza. Wanachofanya CCM mikoa yote wanayopata kura nyingi huwa hawapeleki miradi yoyote ya maendeleo. Barabara ya Kidatu - Ifakara - Mahenge mpaka leo hii ni ya vumbi na wakati wa masika ni shughuli pevu. Ukija uchaguzi kura zote kwa CCM. Shame on us!

Wajinga ndiyo waliwao kwa kweli..ukiona sehemu ambazo Chadema ndiyo wameshinda ujue ya kwamba kumeamka... kwa mfano jimbo la Rombo Mramba alikua anatumia gia ya barabara inayojengwa kuunganisha Marangu hadi Kamwanga mpakani mwa Kenya na Tanzania kama mafanikio yake..wananchi wakampiga chini kwa kujua huo ni upuuzi na wala hicho sio kigezo...! Sasa hao wenzangu ambao wanapelekewa tshirt, kofia na kupelekewa show za bure za ubongo wa fleva wanauza haki zao, kwa kweli tunasikitika..inabidi tufanye muamsho wa ukweli! Juhudi zote sasa zielekezwe kule..najua kuna watu wa mikoa hiyo ambao wameamka..nadhani hao hao ndiyo chachu ya mabadiliko..hao hao ndiyo waende vijijini kwao na kuwapiga sindano hao jamaa waamke huko usingizi waone dunia ilipo na inakokwenda.. Wakijua ukweli watalia sana!
 
naona huyu bwana hatupo naye halo! Mungu awe mkombozi wa wananchi wa Tanzania tu?? ebo!
na Wanadamu wote Je?

Kakwambia nani Mungu yupo bize na upuuzi huo?? Wagonjwa waliolazwa mahospitalini wamuombe, wanaoumia na majanga mbali mbali asilia kama sunami, ukame, mafuriko wamuombe, na sisi eti kwa ujinga wetu wa kujitakia eti tumuombe atusaidie...akili hiyo au matope?? Si ndiyo kama ni adhabu utapewa kabisa..?? Tumepewa akili na utashi wa kutumia hiyo ndiyo zawadi tosha kutoka kwa Mungu na sio vinginevyo... Mijitu mingine haijui hata kama ipo!
 
na dodoma jamani inahitaji kuzinduliwa jamani.
tupo tayari kuichangia chadema kupiga operation kadhaa mikoa hii ikiongonzwa na rais wetu wa 2015, dr slaa
 
Ndugu wanajamiiforums nina maoni yafuatayo kuhusu uchaguzi wa 2015:

1) CCM wamechakachua matokeo ktk majimbo ambayo CHADEMA ilishinda km TARIME, KIBAHA, S'WANGA, SEGEREA, K'MBONI, SHY nk. Sasa CHADEMA waende mahakamani.
2) Kuna mikoa inahitaji OPERATION ZINDUKA. Hii ni mikoa ambayo wananchi wake wako nyuma kimaendeleo km vile Morogoro, Singida, Tabora, Ruvuma, Mtwara, Lindi na Kibaha
3) Wananchi wajitokeze kuichangia CHADEMA kwa HALI na MALI.

CHADEMA ni MKOMBOZI WA WANANCHI na TANZANIA
Usisahau DODOMA. Mkoa huu lazima ufanyiwe operation Nyangumi ili CCM wasiwe wanashinda kwa kishindo kama walivyofanya mwaka huu. Inauma sana kwa wananchi maskini kuendelea kuyarudisha madarakani majitu yasiyo na huruma kwa masikini.
 
Izunduliwe vipi? nani wa kuizundua mikoa hiyo? Kuna watu wanatoka mkoa wa Morogoro kule kwenye vijiji vilivyokosa lami, umeme na barabara za uhakika toka uhuru. Wenzao wakikusanyika na kusema waandae mikakati ya kusaidiana ili kupeleka maendeleo vijijini mwao, wanakuwa wa kwanza kukacha vikao. Ndio kwanza wanakataa na kusema wao si wazaliwa wa mikoa hiyo/vijiji hivyo. Vyama vya upinzani pekee haviwezi kuikomboa mikoa kama hii.

Zinahitajika juhudi za kila mmoja wetu. Wasomi wawe na tabia ya kwenda likizo vijijini kuwakwamua kimawazo wananchi wenzao wa huko ambao magazeti na vyombo vya habari ni mambo ambayo hayako katika agenda zao za kila siku.

Kuna mifano mingi tu humu ndani ambayo baadhi ya wasomi waliofika vijijini na kutumia muda kukaa na ndugu zao waliweza kuwapatia mabadiliko ya fikra na kupata mawazo ya kimapinduzi na kuwaondoa hofu kuwa ukichagua upinzani, nchi itaingia kwenye vita.

Sikonge ana mpango wa kwenda kugombea jimboni kwao mwaka 2015. Namshauri ndugu huyu aanze leo kama si jana. Wakikuona, ukawambia, watakusikiliza na kukuamini. Na si lazima uwe na haja ya kugombea tu. Kama kweli tuna hasira na tumeguswa na umbumbumbu wa watu wetu; tuanze sasa. Mie nitakuwa kila likizo lazima nitie timu kijijini walau kwa wiki moja. Nitawapelekea na magazeti mengi pia; kwani ganda la muwa la jana, chungu kaona kivuno.

Then Slaa akipita na jeshi lake mwezi mmoja kabla ya uchaguzi, inakuwa tia maji tia maji tu.

Ila sio siri, Morogoro inatia kichefuchefu.
 
Na TANGA.....toka 1970s hakuna maendeleo lakini kila uchaguzi CCM wanashinda 100

Mkuu umenena, hakuna mkoa maskini kama Tanga japo wana rasilimali nyingi na kilimo cha uhakika kwani hata mto pangani wanaweza tumia. Halafu tena kuna madini rodlite, gold, greenganete, etc. Kama handeni kwa Abdalah Kigoda ni tishio la umaskini, nyumba tembe za nyasi, Barabara zero, yaani hopeless kabisa. Siku chache kabla ya uchaguzi nilikuwa kikazi Handeni, yaani wananchi walikuwa wanalaani sana na kusema watampa ubunge CUF. Nikafikiri ni kweli!!! Matoke ya jana lo, Kigoda tena!!! Ila wanasema Kigoda anatumia t---------li sana, anageuza macho unafikiri umepigia mwingine kumbe yeye!!! Ha ha ha nilicheka!!!

 
Usisahau DODOMA. Mkoa huu lazima ufanyiwe operation Nyangumi ili CCM wasiwe wanashinda kwa kishindo kama walivyofanya mwaka huu. Inauma sana kwa wananchi maskini kuendelea kuyarudisha madarakani majitu yasiyo na huruma kwa masikini.
DODOMA hatuna shida maendeleo hayooooo CCM inatuletea, DODOMA ya 2008 si ya leo na bado, acheni papara mambo mazuri hayataki haraka, mwanza ya 1996 si ya leo, leo mwanza ni jiji na hili limetokea ndani ya serikali ya CCM, mambo kwa awamu, kwani akipewa nchi slaa au chadema ndio mikoa yote itabadilika kwa mara moja, kupanga si kutenda! eti miaka 5 tu inatosha.. wasomi na bado mnadanganyika,
 
Naomba HQ ya hii kampeni iwe SIKONGE.

Tunahitaji sana mabadiliko huku ila watu hawajui waanzie wapi.
 
wajinga ndiyo waliwao kwa kweli..ukiona sehemu ambazo chadema ndiyo wameshinda ujue ya kwamba kumeamka... Kwa mfano jimbo la rombo mramba alikua anatumia gia ya barabara inayojengwa kuunganisha marangu hadi kamwanga mpakani mwa kenya na tanzania kama mafanikio yake..wananchi wakampiga chini kwa kujua huo ni upuuzi na wala hicho sio kigezo...! Sasa hao wenzangu ambao wanapelekewa tshirt, kofia na kupelekewa show za bure za ubongo wa fleva wanauza haki zao, kwa kweli tunasikitika..inabidi tufanye muamsho wa ukweli! Juhudi zote sasa zielekezwe kule..najua kuna watu wa mikoa hiyo ambao wameamka..nadhani hao hao ndiyo chachu ya mabadiliko..hao hao ndiyo waende vijijini kwao na kuwapiga sindano hao jamaa waamke huko usingizi waone dunia ilipo na inakokwenda.. Wakijua ukweli watalia sana!
lakini mkuu usisahau ile methali inayosema ukimwamsha aliyelala.................! Hawa dawa yao ni viboko tu
 
Na special campaigns inabidi zianze immediately, sasa hivi. Kwanza kwa viongozi wa chama kuingia mitaani mijini na vijijini kuwaweka wananchi sawa juu ya nini wanatakiwa kupata toka kwa viongozi waliopewa dhamana. Kwa muda mrefu sasa CCM imekuwa ikifaidi mtaji unaotokana na ujinga wa watanzania walio wengi. Ndiyo maana inazidi kuupalilia ujinga kwa kuendesha mipango ya elimu zisizo na tija ili watu wengi waendelee kuwa wajinga, wanaoamini kuwa kusema CCM ndiyo kama umesema Tanzania. Wanaoamini Nyerere bado ni Raisi wetu na wanaoamini kuwa bila CCm Tanzania itakuwa na vita. Lazina CCM waelewe hata hivyo kuwa ujinga si kilema cha kudumu. watu wakielimishwa wanatoka katika lindi la ujinga na ndio hicho inabidi kifanyike. Hadi sasa dalili ni njema maana hali ya 2005 na sasa ni tofauti, watu wameanza kuelewa japo juhudi zaidi inahitajika. Pamoja na viongozi kuendesha kampeni kuanzia leo hadi uchaguzi wa 2015, sisi sote wapenda maendeleo na neema kwa Tanzania inabidi tuingie mitaani pale tulipo kwa mtu mmoja-mmoja au hata vikundi kueneza ujumbe wa sababu za mabadiliko, huku tukiwakumbusha wananchi kufuatilia utekelezaji wa ahadi zote zilizotolewa na CCM wakati wa kampeni ili wakati wa kampeni zijazo CCM ikisema tumetimiza ahadi ZETU ZOTE asilimia 100 tuwe na 'data' za kuhoji vinginevyo.

Napenda kuwasilisha wadau!!

Naunga mkono hoja yako Mkuu! Ninaomba wazalendo wenzangu tufuatilie kwa makini matukio mtaani/sehemu tunazoishi ili kuwawajibisha watakao kuwa madarakani. Kwa mfano, kuhakikisha fedha zinazotolewa (kama vile za mfuko wa jimbo, shule na zahanati) zinatumika ipasavyo. Tukifanya hivi hizo pesa walizotumia kuiba/kuchakachua kura hawatapata nafasi ya kujirudishia kwa kupora fedha zinazotakiwa kwenda kwa walengwa.
 
Bovidae hapo umelonga. Ushauri wako nauunga mkono asilimia 100! Lazima tuwe waelimishaji umma kuhusu wajibu wa serikali itakayoundwa katika kutimiza ahadi zote walizotoa wakati wa kampeni.
Good idea. Bravo.
 
Tuanzeni na kuwaelimisha watu wadai kutimiziwa ahadi walizoahidi wagombea wa CCM ambazo tuna uhakika hawatazitimiza hata kwa viboko. Hapo ndpipo tutarudi 2015 kuwakumbusha na kuchukua kura zetu kiulaini. CCM hawawezi kutimiza zile ahadi za kufikirika za JK. Jamaa alikuwa anatamka chochote kilichokuwa kinakuja mbele yake. TUNAUHAKIKA HAKUNA MAENDELEO YOYOTE YATAKAYOLETWA NA CCM KATIKA KIPINDI HIKI CHA MIAKA MITANO.
 
Ndugu wanajamiiforums nina maoni yafuatayo kuhusu uchaguzi wa 2015:

1) CCM wamechakachua matokeo ktk majimbo ambayo CHADEMA ilishinda km TARIME, KIBAHA, S'WANGA, SEGEREA, K'MBONI, SHY nk. Sasa CHADEMA waende mahakamani.
2) Kuna mikoa inahitaji OPERATION ZINDUKA. Hii ni mikoa ambayo wananchi wake wako nyuma kimaendeleo km vile Morogoro, Singida, Tabora, Ruvuma, Mtwara, Lindi na Kibaha
3) Wananchi wajitokeze kuichangia CHADEMA kwa HALI na MALI.

CHADEMA ni MKOMBOZI WA WANANCHI na TANZANIA
SASA WEWE NDIO UMEDATA KWELI YAANI MKOMBOZI GANI HUWA ANAHITAJI KUCHANGIWA ILI AKUKOMBOE? SAWA SAWA NA MTU ANAKUJIA UKIWA MSIBANI,MSIBA NI WA BABA YAKO HALAFU ANAKWAMBIA NISAIDIE ELFU KUMI HAPO ILI NITOE MCHANGO WA MSIBA KAMA WEWE UTAMFANYAJE?UKIKUBALI KUWA WATANZANIA NI MASIKINI HIZO MALI ZA KUICHANGIA CHAFYOKO ZITATOKA WAPI? MSHAURINI SLAA AENDE AKAOMBE MSAMAHA ARUDI KUCHUNGA KONDOO WA................ UTAKUWA UMEELEWA.:yield:
 
Back
Top Bottom