Mikoa 18 kati ya 27 Tanzania ina wagonjwa wa COVID-19

huwa nikiiyona post yako Mkuu ,
Najisikia kucheka kwa majonzi huwa unaongea kwa huzuni iliyokosa faraja.
Nikirudi kwenye avatar yako ndo mbavu sina.
Anyway jikinge mwenyewe full stop sisi wakati wa Dar tumeshazoea hii sijui huko mikoani ambapo km 10 hadi hospital
Kwasasa tumechelewa maana mabus kesho yanawahi tena mikoani yanapeleka huko,baada ya siku2 tena tutaletewa takwimu mikoa itaongezeka.
 
Bams,
Kwahiyo unafikri angechaguliwa Mgombea wa Ukawa ndio nchi isingekiwa na Corona? Corona imeenea nchi nzima na hakuna mtu yeyote mwenye utaalamu wa kuithibiti ninyi kila usiku ujuaji. Kama ni wajuaji si mngeishauri Chadema ikajenga ofisi na kuacha kubeba wagombea toka CCM? Au hilo haukufundishwa na NATO? Ahahahahahahaa!!
 
huwa nikiiyona post yako Mkuu ,
Najisikia kucheka kwa majonzi huwa unaongea kwa huzuni iliyokosa faraja.
Nikirudi kwenye avatar yako ndo mbavu sina.
Anyway jikinge mwenyewe full stop sisi wakati wa Dar tumeshazoea hii sijui huko mikoani ambapo km 10 hadi hospital
Nawaonea huruma na kujionea huruma mm mwenyewe cos elimu bado ni ndogo sana hasa huko mikoani,we jiulize leo watu ndiyo wameanz kuvaa Barakoa dsm? Kweli

Inanisikitisha sana cos nimetembea mikoa kadhaa ya Tz napiga picha WaTz wale,naona nakata tamaa kabisa
 
Tumeuzwa. Nawambia tumeuzwa. Lkn itakua funzo kwa watakao baki. Damu za watakaofariki na waliokwisha kufariki ziende kijijini Chalinze.
 
Kwahiyo unafikri angechaguliwa Mgombea wa Ukawa ndio nchi isingekiwa na Corona? Corona imeenea nchi nzima na hakuna mtu yeyote mwenye utaalamu wa kuithibiti ninyi kila usiku ujuaji. Kama ni wajuaji si mngeishauri Chadema ikajenga ofisi na kuacha kubeba wagombea toka CCM? Au hilo haukufundishwa na NATO? Ahahahahahahaa!!
Interest yangu siyo ya CHADEMA au CCM au chama kingine chochote. Kwangu mimi, siyo muhimu kumpata Rais kupitia chama fulani bali ni muhimu kumpata kiongozi mwenye maono. Mimi siyo mfia chama chochote bali mthamini sana wa uhai na afya za wanadamu wenzangu.

Hatukuzaliwa na chama chochote, na hata kuondoka kwetu, hatutaondoka na chama. Pumzi yako ya uhai haina chama. Wewe na mimi tunaweza kutofautiana katika mengi lakini tunafana kwa kila hali kwenye ubinadamu wetu, na hili ndiyo muhimu kuliko kitu kingine chochote.

Sijawahi kumchukia au kumpenda mtu kwa sababu ya chama chake bali kutokana na matendo yake.

Kuna mengi Makonda alitenda ndivyo sivyo lakini nilifurahishwa naye kwenye tamko lake la watu wavae masks. Hata kama kunaweza kuwa na mapungufu katika utekelezaji wake, lakini amechukua hatua pale uwezo wake unapofikia. Na ndicho tunachotaka. Tunamwomba Rais atumie uwezo wake wote kuwaokoa Watanzania, na ndicho ambacho tumekuwa tukimsihi kila siku.

Mtu mwerevu, akisikia tatizo linakuja, hufanya maandalizi makubwa. Maana ni aheri ujiandae zaidi halafu tatizo likaja katika udogo, kuliko kinyume chake.
 
Sir_Mimi,

Tabia ya Shetani hajawahi kuwaza lililo jema hata Mara moja!Hivo saa zote anawaza yaliyo MABAYA! Kufunga Wapinzani,kuwapoteza na kuona wanakufa ndo furaha yake!
 
Back
Top Bottom