Mikoa 18 kati ya 27 Tanzania ina wagonjwa wa COVID-19

na mzee wenu amewakimbia , nashindwa kuelewa ni mwanaume wa aina gani anakimbia familia wakati wa matatizo,
wanaume wa shoka nchi zingine wamebaki na wananchi wanapambana pamoja

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ilikuwa ujuha kuachia mabasi kutoka Dar kwenda mikoani. Ni ujuha zaidi kutokuchukua hatua sasa. It is never too late to do the right thing.
 
Hivi ukiumwa Corona lazima ufe? wagonjwa wameshasambaa tayari hata ukiifunga Dar isiingiliane na mikoa mingine sioni Kama unafuu wowote

Sent using Jamii Forums mobile app
Mmeshauriwa mara ngapi na kuanzia lini? Halafu bahati ya mwenzio usiilalie mlango wazi, sio kwa sababu yeye alipona basi na wewe lazima upone, una uhakika gani kwamba ukipata huo ugonjwa utapona?
 
Mkoa niliokuwepo wagonjwa waliopatwa na corona waliojiwa wote wakasema walitoka Dar siku za karibuni, tena mmoja alisema alivyokuwa kanisani alikaa na mtu mwenye mafua hivyo aupata alivyokuwa kwenye ibada

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hii Serikali ni kaidi sana. Hii corona itatimba mpaka Chato na Ruangwa ndiyo watie akili
Hivi umeisha bahatika kuwaona hao wagonjwa wa COVID-19 waliopo Tanzania ?
Maambukizi yanaweza kufika hata watu milioni, lakini hatuta kuwa na vifo kama China,Marekani au hata Italy.
Mungu ni fundi angeleta usawa kwenye hili gonjwa, sasa hivi Tanzania population ingekuwa 20,000 au 10,000 tu.
 
Tanzania's Coronavirus April Timeline

1 April: 20
6 April: 24
10 April: 32
14 April: 53
15 April: 83
16 April: 94
17 April: 147
19 April: 170
20 April: 254

"Increasing geometrically".
 
Adjustments.jpg



Sent from my iPhone using Tapatalk
 
Ndiyo maana tunaambiwa tuwe makini sana wakati wa kuchagua viongozi. Upigaji kura kwa ushabiki na kuangalia vyama, adhabu yake ni kubwa.
Familia ya mbowe ilikuwa ya mwanzoni tunkukutwa na Corona na wao wakajikausha hadi walipoumbuliwa na Makonda!!! Kwa hiyo mlifanya chaguo sahihi kumpa kura mbowe uenyekiti wa chadema?
 
Tunaliomba Bunge liazimie kuisimamia na kuishauri serikali ichukue hatua ya kuiweka Dar kwenye uangalizi maalum (Karantini). Tishieni hata kumng'oa kama analeta ubishi, atasalimu amri tu. Au kataeni kupitisha bajeti yoyote kama wanagoma kuchukua hatua stahiki.

Hili jambo la kumtupia Mungu kila tatizo ni kukosa maarifa na Mungu anasema wazi kabisa kwamba tunaangamia kwa kukosa maarifa. Yaani hata kuiweka karantini Dar nako tunaomba kwa Mungu? Afanye nini?
 
Miaka ya 1980 nikiwa Chuo Kikuu nikisomea uongozi tulifundishwa nadharia nyingi za uongozi na kwamba kila nadharia huwa ina mtu anayeiamini au watu wanaoiamini na kuitumia katika uongozi wao. Nadharia mbili kubwa ninazozikumbuka ya kwanza ni ile inayoitwa "Classical or Scientific Management" na ya pili inaitwa "Human Relations School of Thought". Viongozi wanaoamini na kuitumia nadharia ya kwanza ya "Scientific/Classical management" wao kipaumbele ni uchumi, yaani uzalishaji ili kupata kipato hata kwa kuwaburuza na kuwapiga wafanyakazi ilimradi tu wazalishe kingi. Wao habari ya mahitaji ya binadamu haipo.

Kwa viongozi hawa binadamu ni sawa tu na mashine ya kuzalishia mali, yaani ni sawa tu na chombo chochote kisicho na uhai ambacho unaweza kukitumia kuzalishia mali, mfano msumeno, nyundo, jembe, panga, mashine ya kukobolea mahindi au mpunga, n.k. Hapo viongozi hawa hawataki kusikia mfanyakazi anahitaji likizo, kupumzika wala kwenda hata kuhudhuria msiba wa mzazi wake wala likizo ya uzazi hakuna, ni kazi tu. Yaani hapa kazi tu! Kwao utu wa mwanadamu na hadhi yake na uzima wake si kipaumbele.

Viongozi wanaofuata nadharia ya pili ya "Human relations" wao huhimiza watu wafanye kazi lakini wakati huohuo mahitaji ya mwanadamu lazima yazingatiwe, afya ya mwanadamu sharti izingatiwe na haki zake apewe. Viongozi hawa hutanguliza utu na ubinadamu mbele hata kuliko kipato au uchumi. Wao huamini kwamba binadamu mwenye afya njema, anayethaminiwa na mwenye ari ya kufanya kazi ndiye huzalisha zaidi na kufurahia matunda ya kazi yake kwa manufaa ya nchi na ya wanadamu. Hivyo viongozi wa mrengo huu hutenga muda wa kusikiliza na kushughulikia matatizo ya binadamu.Kwa viongozi hawa utu, hadhi na mahitaji ya binadamu ni kipaumbele cha kwanza.

Kwa mujibu wa wataalamu hawa wa uongozi, wanashauri kwamba tunapochagua watu wa kutuongoza sharti tujue mtu huyo anaamini katika nadharia ipi ya uongozi? Je, anaamini katika nadharia ya kwanza ya kuwaona binadamu ni sawa tu na vitu vingine kama mashine tu au anaamini kwamba binadamu ni kiumbe tofauti na ana thamani tofauti na vitu vingine na hivyo anatakiwa kusikilizwa, kuhudumiwa na kupewa wajibu na haki stahiki zikiwemo za kulindwa utu na uhai wake.

maswali ni je, huwa tuna muda wa kuwajua na kuwapima viongozi wetu kabla ya kuwachagua watuongoze? Je, vyombo vya kuwachuja wagombea wa uongozi husika hutuletea wagombea sahihi? Vyombo hivyo vina weledi wa kutambua wagombea wanaokidhi mahitaji yetu? Je, huwa tunachagua chama au mtu? Je, hata kama mtu ni sahihi mifumo inamwezesha kuwa kiongozi bora?

Kwa ujumla tuna safari ndefu katika uongozi. Mara nyingi tunacheza bahati nasibu tu. Mwisho ndipo majuto hutukuta na tukawa hatuna namna ya kufanya zaidi ya kusubiri huruma za Mungu wakati huo tukiwa hatustahili kuhurumiwa maana wenyewe tunakuwa sehemu na chanzo cha tatizo.
 
Back
Top Bottom