BAK
JF-Expert Member
- Feb 11, 2007
- 124,789
- 288,022
Date::12/15/2008
Mikataba ya madini inachangia vurugu
Mwananchi
VURUGU zilizotokea mwishoni mwa wiki iliyopita katika Mgodi wa Dhahabu North Mara, ulioko Nyamongo, mkoani Mara kwa wakazi zaidi ya 400 wa eneo hilo kuuvamia na kuharibu mali; inadhihirisha kuwa kuna matatizo makubwa katika taratibu za uwekezaji.
Inadaiwa kuwa baada ya wananchi hao kuuvamia mgodi huo, polisi walipokwenda kutuliza ghasi walizidiwa nguvu na mtu mmoja alifariki dunia katika mapambano hayo na kusababisha zaidi ya askari polisi 800 wa kikosi cha operesheni maalumu kupelekwa kwa ajili kulinda usalama.
Tukio hilo ni la kusikitisha kutokana na uharibifu mkubwa wa mali za mwekezaji uliofanywa na wananchi waliovamia mgodi huo kudai haki zao zilizokiukwa na mwekezaji. Ni kweli kwamba, hatua iliyochukuliwa na wananchi imesababisha hasara kubwa kwa mwekezaji na taifa kwa ujumla, hivyo kuathiri uchumi wa nchi kwa njia moja ama nyingine.
Hata hivyo, kwa upande mwingine, tukio hilo linadhirisha kwamba, sheria ya madini na mikataba ya uwekezaji katika sekta hiyo ina matatizo makubwa yanayosababisha wananchi kudhulumiwa haki zao; na hasa juu ya fidia ya ardhi yao inayochukuliwa na wawekezaji zinazodaiwa kuwa ni kidogo, hivyo kuamua kuchukua sheria mkononi baada ya kukosa msaada kutoka mamlaka husika.
Hivyo basi, pamoja na serikali kupeleka askari wengi kulinda usalama katika eneo hilo, inatakiwa kuchukua hatua za haraka kurekebisha kasoro zilizopo katika sekta ya madini, ili kutengeneza mazingira ya ushirikiano mwema baina ya wawekezaji na wananchi.
Tunasema hayo kwa sababu, asilimia kubwa ya maeneo yote yenye migodi kumekuwepo na mvutano baina wawekezaji na wananchi wanaolalamikia kupunjwa fidia ya mashamba yaliyochukuliwa wakidai kwamba, hailingani na thamani halisi ya ardhi yao.
Mbali hilo, pia tunaomba uwekwe utaratibu wa kulinda usalama wa wananchi katika maeneo migodi ili kuwaepusha na ajali za kulipukiwa na baruti, kama ilivyotokea jana jioni katika Mgodi wa Dhahabu wa Geita, mkoani Mwanza ambapo watu watatu wamekatwa na baruti ilioangukia kwenye makazi yao walipoishika.