Mikataba ya madini isiyo na maslahi kwa Tanzania, inachangia vurugu | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mikataba ya madini isiyo na maslahi kwa Tanzania, inachangia vurugu

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by BAK, Dec 16, 2008.

 1. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #1
  Dec 16, 2008
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 70,442
  Likes Received: 81,491
  Trophy Points: 280
  Date::12/15/2008
  Mikataba ya madini inachangia vurugu
  Mwananchi

  VURUGU zilizotokea mwishoni mwa wiki iliyopita katika Mgodi wa Dhahabu North Mara, ulioko Nyamongo, mkoani Mara kwa wakazi zaidi ya 400 wa eneo hilo kuuvamia na kuharibu mali; inadhihirisha kuwa kuna matatizo makubwa katika taratibu za uwekezaji.

  Inadaiwa kuwa baada ya wananchi hao kuuvamia mgodi huo, polisi walipokwenda kutuliza ghasi walizidiwa nguvu na mtu mmoja alifariki dunia katika mapambano hayo na kusababisha zaidi ya askari polisi 800 wa kikosi cha operesheni maalumu kupelekwa kwa ajili kulinda usalama.

  Tukio hilo ni la kusikitisha kutokana na uharibifu mkubwa wa mali za mwekezaji uliofanywa na wananchi waliovamia mgodi huo kudai haki zao zilizokiukwa na mwekezaji. Ni kweli kwamba, hatua iliyochukuliwa na wananchi imesababisha hasara kubwa kwa mwekezaji na taifa kwa ujumla, hivyo kuathiri uchumi wa nchi kwa njia moja ama nyingine.

  Hata hivyo, kwa upande mwingine, tukio hilo linadhirisha kwamba, sheria ya madini na mikataba ya uwekezaji katika sekta hiyo ina matatizo makubwa yanayosababisha wananchi kudhulumiwa haki zao; na hasa juu ya fidia ya ardhi yao inayochukuliwa na wawekezaji zinazodaiwa kuwa ni kidogo, hivyo kuamua kuchukua sheria mkononi baada ya kukosa msaada kutoka mamlaka husika.

  Hivyo basi, pamoja na serikali kupeleka askari wengi kulinda usalama katika eneo hilo, inatakiwa kuchukua hatua za haraka kurekebisha kasoro zilizopo katika sekta ya madini, ili kutengeneza mazingira ya ushirikiano mwema baina ya wawekezaji na wananchi.

  Tunasema hayo kwa sababu, asilimia kubwa ya maeneo yote yenye migodi kumekuwepo na mvutano baina wawekezaji na wananchi wanaolalamikia kupunjwa fidia ya mashamba yaliyochukuliwa wakidai kwamba, hailingani na thamani halisi ya ardhi yao.

  Mbali hilo, pia tunaomba uwekwe utaratibu wa kulinda usalama wa wananchi katika maeneo migodi ili kuwaepusha na ajali za kulipukiwa na baruti, kama ilivyotokea jana jioni katika Mgodi wa Dhahabu wa Geita, mkoani Mwanza ambapo watu watatu wamekatwa na baruti ilioangukia kwenye makazi yao walipoishika.
   
 2. K

  Koba JF-Expert Member

  #2
  Dec 16, 2008
  Joined: Jul 3, 2007
  Messages: 6,144
  Likes Received: 494
  Trophy Points: 180
  ...ndio mwanzo huo na sitashangaa wananchi wakianza kuchukua hatua kama hizi,hata kama ni sheria,uwekezaji au sijui upuuzi gani,hii haiingii akilini jamaa kutoka Canada wanakuja kuchukua mabilioni kwenye backyard za watu huku wenyewe hata maji ya kunywa bado wanafuata mile tano kwa ndoo kichwani...si bora kupigana na kufa tuu kuliko hii fedheha!
   
 3. jmushi1

  jmushi1 JF-Expert Member

  #3
  Dec 16, 2008
  Joined: Nov 2, 2007
  Messages: 17,552
  Likes Received: 1,898
  Trophy Points: 280
  Umasikini hauzungumziwi..Ni vurugu tu...Hii ina maana kuwa viongozi wetu hawaamini kabisa kuwa wananchi wana haki inapokuja kwenye rasilimali zao na ndio maana ni wazi kabisa wamekuwa wakiwatetea wawekezaji hata ikibidi kwa kutumia excess power za nguvu ya dola...Wameshakula ten pasenti shida ikwapi.
   
 4. Zero

  Zero JF-Expert Member

  #4
  Dec 16, 2008
  Joined: Mar 8, 2008
  Messages: 301
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  Naomba nitoe mtizamo tofauti kwenye hili lilotokea juzi huko North Mara. Hizi hazikuwa vurugu za wananchi kudai haki zao. Hizi hazikuwa vurugu za wananchi kudai fidia kwa ardhi yao iliyochukuliwa na mgodi. Bali zilikuwa ni vurugu baada ya wananchi kuvamia "pit" baada ya kusikia kwamba mwamba uliolipuliwa ulikuwa na "high grade ore". Hii tabia sio mpya kwa maeneo ya mgodi wa North Mara, but this was too much. Ikumbukwe kwamba kwa maeneo mengi ya wilaya ya Tarime huu ni msimu wa vijana kufanyiwa jando. Baada ya jando jamii hufanya sherehe kubwa kuwapongeza wale waliotoka jandoni. Hivyo kila mmoja anakuwa anatafuta namna ya kufanya shughuli yake iwe kubwa.

  Mwekezaji alikuwa na haki ya kujilinda hapa. Mkumbuke kwamba nyie ndio kesho mnalalamika mkisikia mwekezaji anasema kapata hasara. Atapataje faida kama yeye analipua miamba halafu wananchi wanavamia na kuchukua "high grade ore" yote?
   
 5. Ngongo

  Ngongo JF-Expert Member

  #5
  Dec 16, 2008
  Joined: Sep 20, 2008
  Messages: 12,155
  Likes Received: 3,632
  Trophy Points: 280

  Mkuu Zero heshima mbele
  Sikubaliani kabisa na mtazamo wako kuhusu uvamizi mgodi huko North Mara,wananchi wamechoka kuona madini yao yakitoroshwa kwa kisingizio cha uwekezaji.
  Mkuu Zero lazima tukubaliane bila kutafuna maneno kwamba ardhi yenye madini ya dhahabu ilipaswa kuwanuafaisha wananchi au vijiji vinavyozunguka mgodi na taifa kwa ujumla lakini hali imekuwa tofauti na katika hili hakuna mtanzania aliyesikitika binafsi naona hii move ni mwanzo mzuri kwa taifa na wananchi kuanza kutambua jinsi wawekezaji wanavyohamisha rasilimali bila ya wananchi na taifa kufaidika.Mkuu Zero hukiangalia Afrika kusini na Botswana rasilimali ya madini imeweza kuondoa umasikini uliokithiri,tazama barabara,hosipital,shule na nk viko katika hali nzuri nasi hivyo tu madini yao pia yameweza kusaidia kuinua sekta nyingine hali ambayo hapa kwetu Tanzania haipo.Mikataba ya madini imewanufaisha baadhi ya wanasiasa na watendaji wakuu serekalini na kuliacha taifa katika hali ya kutonufaika kabisa.Tanzania sasa ni nchi ya tatu Afrika kwa uzalishaji wa dhahabu lakini mchango wake katika pato la taifa ni chini ya 3%,niliwahi kusikia eti Tanzania Brewaries {TBL} inalipa kodi kubwa kuliko migodi yote ya dhahabu !.Natoa wito kwa wananchi wote walioko karibu na maeneo ya migodi kuongeza preassure kwa wawekezaji wababaishaji ili taifa liweze kunufaika na rasilimali zake.
   
 6. Gelange Vidunda

  Gelange Vidunda JF-Expert Member

  #6
  Dec 16, 2008
  Joined: Aug 18, 2008
  Messages: 312
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  Nilikuwa naangalia TV jana usiku na mwanakijiji mmoja wa jirani na huo mgodi alisema wao waliambiwa kuwa huu mgodi ukija utanufaisha wanavijiji wote jirani na huo mgodi. Alisema tatizo ni kwamba kila kitu kipo ndani ya eneo la mgodi - wakitaka kusafiri basi lazima waingie eneo la mgodi manake barabara na vituo vinaishia humo; wakitaka maji ya kunywa na matumizi mengine basi lazima waingie eneo hilo kwani visima na mabomba yamo ndani ya eneo hilo; wakitaka mahitaji mengine kama vyakula na maduka n.k. vyote vimo ndani ya maeneo ya mgodi, na ili kuvipata wananyanyaswa ile mbaya na masheria ya hapo mgodini.

  Now, what did Bob Marley say? "A hungry man is an angry man" What else did he say? "You can fool people sometimes but you can't fool them all the time"

  People, this is a case of an angry man who has been fooled once too many times! Hata kama raisi alisema kwamba lazima uliwe ili nawe ule, but damn!, tumeshaliwa vya kutosha.............tena bila Vaseline au KY!!!! (Sometimes I wonder yeye alitafsiri vipi kuliwa....???)
   
 7. Mpita Njia

  Mpita Njia JF-Expert Member

  #7
  Dec 16, 2008
  Joined: Mar 3, 2008
  Messages: 7,012
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 145
  Mkuu Zero, kama wananchi ingekuwa wameoatiwa haki zao zote zinazostahili, wasingethubutu kuvamia mali ya mtu mwingine. Wanafanya hivyo wakiamini kuwa wanadhulumiwa-pamoja na tamaa yao ya kupata mali haraka haraka
   
 8. Zero

  Zero JF-Expert Member

  #8
  Dec 16, 2008
  Joined: Mar 8, 2008
  Messages: 301
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  Najua mmesoma between the lines na mmeelewa hoja yangu. The problem is mmeshakuwa na mentality ya kupingana na the so called foreign investors. I share the same mentality. I feel like they are screwing us. But my argument over the North Mara incident is, this was not related to compensation or anything of similar nature. It was pure greed from the Nyangoto villagers. Hawakuvamia mgodi kwasababu eti wanaona hawafaidiki na mgodi. Walivamia pale kama wezi. Na hoja yangu ni kwamba, huyu mwekezaji ana kila haki ya kujilinda against such intrusion. Tuache hii mentality ya kufikiria wawekezaji watatufanyia kila siku. Tuilaumu serikali yetu kwa kutowabana hawa wawekezaji kwenye mikataba.

  Kwa wale wanaojua Corporate Social Responsibility, ni kwamba hawa investors wanajaribu kwa uwezo flani. Jamii ina kila haki ya kuendelea kudai kama inaona haifaidiki sana na hii CSR. Lakini sio suala la jamii kuvamia mali za mwekezaji kwa kisingizio kwamba hawafaidiki na CSR. Jamii inapaswa kuivamia serikali na kuibana kwa kuingia mikataba mibovu na sio mwekezaji ambaye hana makosa. Chukua mifano ya mashirika ya umma, halafu utoe mfano ni shirika gani la umma limewahi kufanya CSR. Hakuna! Leo wawekezaji wakiondoka na serikali ikaachiwa miradi yote mikubwa itaweza CSR?
   
 9. Zero

  Zero JF-Expert Member

  #9
  Dec 16, 2008
  Joined: Mar 8, 2008
  Messages: 301
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  This is total crap. I have been to Nyamongo and Nyangoto. Sio kweli kwamba huduma ziko ndani ya mgodi. Nyamongo ni kamji kanakojitegemea kabisa. Mabasi kutoka Tarime mjini yafikia Nyamongo. Ni mji uko nje ya mgodi. Kwa taarifa yako kuna mpaka bar ya mtu binafsi iko nje ya gate la mgodi. Huyo mwananchi alikuwa anakuza mambo tu. Nadhani kwa wale waliofika maeneo haya wanajua ninachokiongea hapa.
   
 10. Masanja

  Masanja JF-Expert Member

  #10
  Dec 16, 2008
  Joined: Aug 1, 2007
  Messages: 3,595
  Likes Received: 3,758
  Trophy Points: 280
  Zero I think you have argument here which merits critical thinking.

  But reality check is people have been fooled for quite sometime. Hivi ndugu Zero unapoongelea Corporate Social Responsibility UNAONGELEA KITU GANI HASWA? Hivi mkuu umeshaangalia retuns za hawa watu kwa mwaka? and you dare say kwamba wana "miradi" inayotunufaisha? Miradi ipi hiyo? Mbona tunakuwa cheap kiasi hiki? this is an insult to our minds! Magunia ya Mchele na dagaa kwa yatima ndo CRS?

  Ndo ule ule usanii wa Vodacom Zain et al..they make millions harafu kesho wanagawa madaftari na magunia ya mchele kwa yatima, walemavu nk..then TV zote na blog ya Michuzi wanaweka kwenye headlines! Mbona tunakuwa wepesi wa kudanganywa jamani? Lakini hapana lazima tufike mahali tuitumie elimu yetu kujikomboa hata namna tunavyofikiria... Tumeshajiwekea standard kwamba tukipewa hata madaftari ya watoto wetu basi huo ndo uwekezaji sahihi! Grrrzz....Talk of Corporate Social Responsibility!

  Ukweli ni kwamba hili swala la uwekezaji fake katika dunia ya tatu ni TIME BOMB, na siyo Tanzania peke yake..kwa sababu wananchi tumedanganywa vya kutosha na hawa goons wanaoitwa wawekezaji.... Kama serikali yetu haiwezi kutusaidia basi inabidi tujisaidie wenyewe...

  Uliza jana SIEMENS amelipa kiasi gani kwa serikali ya US na Germany kwa kuhusika na utoaji rushwa kupata biashara zake...more than Billion Euros! To settle the claim...ila sisi hawa wajinga wanaojiita wawekezaji...wakija nchini kwetu tunawachekea simply because they eat with few elites at the expense of millions. Damn it!

  Kwa Tanzania, hakuna Kampuni inayotekeleza CRS kiukweli niutapeli tuu..Na ofcourse they are not bound. Lakini usifikiri wananchi huko Venezuela, Bolivia, Equador nk..ni wajinga..wanaoona kwamba cheating must come to an end at some point. Reasons ulizotoa ni lame at best. Kwa mtu yeyote anayewajua hawa wawekezaji na strategies zao..anajua kabisa kwamba they are good at spinning stories.
   
 11. K

  Koba JF-Expert Member

  #11
  Dec 16, 2008
  Joined: Jul 3, 2007
  Messages: 6,144
  Likes Received: 494
  Trophy Points: 180
  ....pls dont complicate what is simple,uwekezaji umewapa deal mbovu wananchi kwa ajiri ya 10% za kina karamagi na mafisadi wengine walioongozwa na mkapa,hao wawekezaji wasiolipa kodi na mikataba yao ya mtemi mangungo wanajichotea bilions huku wananchi wakiachiwa makelele ya mitambo,dust na mashimo tuu,na wewe unaleta poor excuse zako hapo eti CSR?najua kisheria kulazimisha fair deal kwa sasa ni kama haiwezekani lakini acha wapate huo moto wa wananchi labda next time itasaidia,miaka 40 ya uhuru lakini kina karamagi bado wanatusafisha tuu...its time sasa kuwapiga kwa viatu viongozi mafisadi wote mitaani labda itasaidia wasiibe/kusign bad deals for 10% kwa kuogopa,sometime umafia na uvunjaji sheria unasaidia kuinyoosha society for good!
   
 12. Zero

  Zero JF-Expert Member

  #12
  Dec 17, 2008
  Joined: Mar 8, 2008
  Messages: 301
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  Unfortunately these are not poor excuses! This is the harsh reality. You like it or not. Your government has screwed you. Don't blame the investors, blame your government. Speaking of CSR, I have done my research on this. Yes, the companies are not doing enough. And we cant force them. Sasa kuvamia mgodi na kuchoma moto three expensive mashines ndio kunasaidia kuboresha maisha ya wananchi? Kuvamia mgodi na wananchi wakauwawa ndio kunasaidia kuboresha maisha ya wananchi? The thing is, hata kile kidogo ambacho mwekezaji ilikuwa akitoe kwenye CSR atashindwa kama kila siku anavamiwa na mashine zake kuharibiwa. Do you have any idea North Mara wanaingia hasara kiasi gani kwa kusimamisha "mill" in just one hour? Sasa take this, they have been forced to suspend their operations mpaka hali itakapokuwa shwari. Hii ni hasara kubwa sana kusimamisha "mill" for a day or two days. Ask those who have worked in mines.
   
 13. C

  Curriculum Specialist JF-Expert Member

  #13
  Dec 17, 2008
  Joined: Oct 8, 2007
  Messages: 2,736
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Kaka wewe kweli ni zero, yaani unafikiri kilichowafanya hao wananchi wavamie mgodi ni kwamba tu wanatafuta pesa za sherehe za jando, I never thought a tanzanian can think low like you! wewe hujui wanatanzania wnatafuta uhuru wa rasilimali zao, hujui kwamba kuna kitu kinaitwa resource colonization africa na Tanzania in particular, amka kaka isaidie hii nchi ina descend kwenye chaos!
   
 14. C

  Curriculum Specialist JF-Expert Member

  #14
  Dec 17, 2008
  Joined: Oct 8, 2007
  Messages: 2,736
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Zero, naomba ujiweke kwenye hiyo nafasi ya mwanakijiji wa north mara au buzwagi, kwamba ardhi yako iliyokuwa na dhahabu kauziwa mwekezaji, na wewe umefidiwa laki tatu ya nyumba yako ya majani na shamba lako laki moja kwani halina hata mazao ya kudumu. Halafu umeondolewa na kwa FFU! unafikiri hali yako itakuwaje? uje hawa ni watu wenye familia zao wanaotegemewa! Halafu wanaojua kabisa kwamba hawa watu wanaoitwa wawekezaji wanasafilisha tons of gold kutoka kwenye mashamba yao na wao wanabakia na umasikini mkubwa! unafikiri hiyo haiwezi kuwa sababu ya wao kurisk maisha yao kwa kuwa wanaona hawana cha kupoteza tena, kama ni kudhalilishwa wamedhalilishwa na kufedheheshwa vya kutosha! I tell you maeneo mengi ya Tanzania yametolewa lessen na utafiti wa madini mbalimbali mpaka ya uranium kwa wawekezaji na wakiyapata watataka kuchimba unafikiri hiyo hamishahamisha ya watu itaiweka tanzania kwenye sehemu gani kwa amani na utulivu!? Sheria zetu za madini na uwekezaji zinaifanya Tanzania iwe potential for conflicts na hatuna miaka mingi tutafikia hapo, nakwambia Zero, hakuna mtu mnyonge dunia bali yule aliyekufa, mitutu ya bunduki haitazuia watanzania kudai haki zao!
   
 15. Zero

  Zero JF-Expert Member

  #15
  Dec 17, 2008
  Joined: Mar 8, 2008
  Messages: 301
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  Nashukukuru na wewe umeelewa kwamba your governement has screwed you. Umekiri kabisa kwamba sheria zetu za madini zinaifanya nchi kuwa potential for conflicts. How is to blame here? Is it the investors or the government? Take it this way, the investors have screwed your government and in turn your government has screwed you. You should blame your government for being screwed. And its now screwing you.

  Mimi nakiri kabisa wananchi hawafaidiki na hii migodi. Hilo nalielewa fika. Ndio maana huko mwanzoni nikagusia issue ya CSR maana kwa upande wa taxes ndio hivyo tena kwamba serikali imeshindwa. Makampuni haya yanajitahidi kufanya CSR, but we feel that they are not doing enough. Lakini kuwavamia hawa wawekezaji wont solve anything. They wont increase their CSR. Sana sana watalalamika kupata hasara kila mwaka. Chukua huu mfano wa North Mara. Kama wenyewe wanaclaim mashine zilichomwa juzi zilikuwa na thamani ya millions of dollars, unatarajia watafanya chochote kwenye CSR next year? Nope, I dont think so.

  Kikubwa hapa ni kubadili sheria husika pamoja na kuing'oa CCM madarakani.
   
Loading...