Mag3
Platinum Member
- May 31, 2008
- 13,064
- 22,756
Baada ya kuapishwa tarehe 4/11/2015, cha kwanza alichowaahidi viongozi wakuu wastaafu ni kuendelea kuishi kwa amani na kuwataka walale usingizi mwororo bila kujali kelele za aliowaita wapinzani wakorofi.
Hiyo ilikuwa ni kabla ya sakata la madini na juzi tena kawahakikishia kutokuwa na hofu kwa waliyoyatenda na kwamba hataruhusu heshima yao waliyoijenga wakiwa madarakani kuharibiwa na wananchi wakorofi.
Na kweli imetokea. Wananchi wamepigwa marufuku kuyataja majina mawili Mkapa na Kikwete na kuwahusisha na mikataba yoyote ile inayolalamikiwa kama huu wa madini na badala yake walioagizwa kusign mikataba ndio washughulikiwe.
Na kweli imetokea. Waziri wake Mwakyembe tayari kafungia gazeti moja kwa miaka miwili kwa kosa tu la kuchapisha picha za Mkapa na Kikwete kwenye kurasa zinazoongelea mikataba hiyo iliyoitia taifa hasara.
Si hivyo tu. Adui wa taifa hili kwa sasa ni wale waliokuwa wanalalamikia hii mikataba kwamba ni ya hovyo na ya kifisadi. Anayeongoza kwa hili ni Mh. Tundu Lissu aliyeanza kupigia kelele hii mikataba toka miaka ya 1990s.
Je nini hasa ni lengo la Rais John Pombe Magufuli? Hata kwa akili kidogo ilitegemewa kwamba wahusika wangeshughulikiwa bila kujali nafasi zao katika jamii kwa kulisababishia taifa hasara ya mabilioni kwa miaka mingi.
Ilitegemewa kwamba ili kufanikisha hili hatua zingechukuliwa kuhakikisha hakuna mhusika anayekwepa kuwajibishwa kwa sababu tu kuna mwanya unaoweza kutumika kuzuia wengine wao kushughulikiwa kisheria.
Bila kumung'unya maneno au kupepesa macho, wahusika wakuu wa sakata hili na mengine mengi ni CCM na serikali yake. Hakuna namna mwanachama au kiongozi wa CCM anapona kwenye hili na hasa viongozi wake wakuu.
Je nini kinachowalinda hawa wasaliti wakuu wa taifa? Magufuli anajua, mimi najua na Mtanzania yeyote anajua...kikwazo ama kisiki ni sheria mama, Katiba, ambayo inacho kipengelele kinachowalinda wezi wakuu wa taifa letu.
Katiba inamlinda Mkapa, katiba inamlinda Kikwete na Katiba inamlinda na itaendelea kumlinda Rais, Jemadari Mkuu na Mtendaji Mkuu wa serikali ya Jamhuri ya Tanzania. Mpaka tutakapoking'oa kisiki kinachowalinda hatutafanikiwa.
Rais John Pombe Magufuli, kama wewe ni jasiri na una nia thabiti ya kupigana hii vita, kwa nini unasita kutumia silaha pekee ya maangamizi, silaha inayopatikana ndani Rasimu ya Katiba ya Jaji Warioba kama itapitishwa?
Je unawalinda watangulizi wako au unajilinda wewe siku za usoni? Ili kuondoa utata huu moja, kwa niaba ya CCM waombe radhi Watanzania na pili, malizia mchakato wa Katiba mpya bila kuchelewa.