Mikataba ya hovyo; Je, Magufuli anawalinda Mkapa na Kikwete au anajilinda yeye!

Waerevu tunaelewa hakuna atakayechukuliwa hatua katika ile list ya waliotajwa. Hakuna hata mmoja atajitetea bila kuwataja waliokuwa na maamuzi ya mwisho.

Waerevu tunajiuliza inawezekana vipi mtoto anamvua baba yake nguo in public mchana kweupe kisha anawaambia watu wakimchungulia watachukuliwa hatua.

Alikuwa hajui matokeo ya alichokifanya kujipa promo. Sasa anajitahidi wenzake wasimwage mboga.
 
Licha ya kujifanya "hajaribiwi,haendeshwi wala hapangiwi" historia inamwonya.Chiluba alijifanya KUFUKUA makaburi Zambia kwa kumwandama KK,yaliyomkuta atakuwa anayajutia huko aliko.
Huyu naye analijua hilo.
 
Licha ya kujifanya "hajaribiwi,haendeshwi wala hapangiwi" historia inamwonya.Chiluba alijifanya KUFUKUA makaburi Zambia kwa kumwandama KK,yaliyomkuta atakuwa anayajutia huko aliko.
Huyu naye analijua hilo.


Matamko ya Magufuli yanikumbusha hadithi ya Macbeth kwenye Sounds of Fury...

To-morrow, and to-morrow, and to-morrow,
Creeps in this petty pace from day to day,
To the last syllable of recorded time;
And all our yesterdays have lighted fools
The way to dusty death.

Out, out, brief candle!
Life's but a walking shadow, a poor player
That struts and frets his hour upon the stage
And then is heard no more.

It is a tale told by an idiot,
full of sound and fury
Signifying nothing.
 
Anajilinda asije akachimba shimo akaingia mwenyewe kwani atakapomaliza utawala wake 2025 asiweze kushtakiwa kwa uvunjaji wa katiba na mambo au uamuzi wa hovyo atakaokuwa amefanya kwa muda wa miaka kumi! Kamati ya Mruma na Urosso hazina kitu kipya kwani hata kiasi cha mrabaha cha 4% tunayostahili kulipwa kutoka kwenye makenikia hawakutaja?
Kama Barrick walidanganya walipaswa wapelekewe demand note au sheria ichukue mkondo wake kwa nini kufanya negotiation na mtu aliyekuibia na huku dhahabu anaendelea kuchimba na kusafirisha nje! Hivi Watanzania nani katuloga. Hawa Professor uchwara have just taken the whole nation for a ride actually on a wooden bicycle !
 
Mtu wa kawaida anaweza fikiri Magufuli anavyo apa kuwalinda kina JK na Mkapa
basi kweli 'anawapenda na anataka kuwalinda'

Ukweli ni kuwa JK na Mkapa wana mizizi mirefu kwenye CCM

wao wawili wakiamua huyu Magufuli 'aondoke'
anaondoka bila ubishi..na Magufuli anajua hilo

So hadharani anaahidi 'kuwalinda' huku anajua anachowaahidi ni
'kutowagusa' ili na yeye 'wamuache' afanye anavyotaka...

"Ccm ina wenyewe" Cap Komba sio mjinga kuimba hivyo.
 
Kwa jicho la asili inaonekana anawalinda ila kwa jicho la akili yenye werevu ni kwamba ameamua waaibisha, Mwakye anamwangalia na kumcheka sanaaaa, Nyerere alisemaga "mtu mwenye akili anapokufanyisha vitu vya kijinga na ww ukafanya nakufurahia huwa ANAKUDHARAU". Czonje ana akili ndomana hamfurahii 2nduLisyu
 
Ndugu zangu Watanzania kwa ujumla wetu ni muhimu tuelewe ni kwa nini wakati wa uchaguzi viongozi wa CCM wako tayari hata kumwaga damu za Watanzania ili mradi waingie madarakani? Zipo sababu mbili kuu: Mosi, ni kuwa wamefanya makosa makubwa sana hasa katika kugawa rasilimali za Taifa hili bure kwa wazungu wakijua wazi kuwa katiba waliojitungia inawalinda. Pili, ni tamaa iliyopitiliza ya ukwasi na madaraka.
Watu wa aina hii ni nadra kuacha madaraka kwa hiari. Daima watataka kibaraka (puppet) wao achukue nafasi ya uongozi ili waishi kwa usalama. Bila hivyo ukweli ni kwamba watakuwa mashakani. Hapa ndipo dhana ya 'Mkoloni mweusi' inapoanzia. Hatuwezi kuwaondoa hadi yaanzishwe mapambano ya kutumia nguvu. Ndiyo njia pekee ya kuuondoa uovu huu na janga hili la kulindana na si vinginevyo. Tukumbuke kuwa walishatamka hadharani kuwa hawawezi kuondolewa kwa 'vikaratasi'. Zanzibar ni mfano hai.
Hebu fikiria ikiwa mtu wao anafikia hatua ya kutufunga midomo tusiyatamke majina yao kwa ujahili waliotufanyia, na ambao yeye mwenyewe ameufunua, tusemeje, kama huu si zaidi ya ukoloni ni nini hasa!!!
 
Uzuri Jpm alichojitahidi kuonyesha dunia ni kuwa walichokuwa wanakipigia kelele wapinzani ni kweli sisi wanaccm ndo tulihusika kupora mali za taifa hili kwa muda mrefu
 
Uzuri Jpm alichojitahidi kuonyesha dunia ni kuwa walichokuwa wanakipigia kelele wapinzani ni kweli sisi wanaccm ndo tulihusika kupora mali za taifa hili kwa muda mrefu
Ni kama kuitangazia dunia kwamba uko uchi na kweli unapata ujasiri wa kutoka hivyo hivyo ukiwa mtupu. Huku nyuma familia yako nayo inapiga vigelegele unavyopendeza. Anatokea jirani na kukushangaa mtu mzima kukata mitaa ukiwa uchi, loo, unakurupuka na kutaka kumtoa shingo.
 
Back
Top Bottom