Mikataba wa bajaji, pikipiki na guta

baba aura

JF-Expert Member
Aug 5, 2023
231
353
Habari wakuu,hebu wale wazoefu wa kuchukua vyombo vya moto hivyo kwenye heading mtujuze machimbo bora

Maana sehemu zingine mikataba yao inatunyonya saana mpaka jasho zinavuja pia tujuzane changamoto zake
 
Chimbo rahisi la bajaji ni:-

1. Ununue bajaji used-nzuri iifanyie matengenezo madogo madogo upige kazi. Kama dereva ni wewe mwenyewe itakulipa vizuri sana. Mimi nimelifanya hili. Nilinunua bajaji kwa bei ya 1.5 m na inafanya vizuri baada ya kurekebisha vitu kadhaa.

2. Chimbo lingine ni kununua bajaji mpya ambayo kwa sasa ni zaidi ya milioni 9.

3. Chimbo la tatu ni kukopa benki. Rejesho lao ninadhani si zaidi ya 15k kwa siku.

4. Chimbo la nne ni kukopa Halmashauri. Mikopo yake haina riba. NB: Kwa sasa serikali inataka kuhamishia mikopo hii ifanyike chini ya benki. Sijajua kama itabadilika masharti au laah!

5. Chimbo lingine ni kukopa kwenye makampuni ambapo riba ni 40% (riba umiza).
 
Back
Top Bottom