Mikataba inaumiza watu wengi

Mikataba inaumiza watu wengi

Majimoto

Senior Member
Joined
Nov 22, 2007
Posts
138
Reaction score
148
Angalia wastaafu wengi wanapo ondoka kwenye ajira, wengi wanalipwa mafao ya kutosha kuweza angalau kusogeza siku za kuishi.

Tatizo la hawa wastaafu wanasahau kuwa siku walipoajiriwa waliapa, wengine walitumia vitabu vya dini zao, wengine waliapa kwa kusaini hati ya kiapo cha kukubali kuanza kumtumikia mwajiri mpya, wengine waliapa kwa maneno kuwa wako tayari kuchukua nafasi mpya ya kazi. Viapo vingine vinaishia kusema"Mungu nisaidie"

Ndugu zangu katika ulimwengu wa kiroho kiapo ni kifungo, ni sawasawa kama mkono wako wa kushoto umefungwa pingu na mkono wa kulia wa mwajiri wako. Kifungo hiki kinawapa wakati mgumu sana wastaafu, ndiyo maana utakuta mstaafu anaaga nyumbani anakwenda ofisi ya zamani kusalimia marafiki zake na hali hii huwa inajirudia mara kwa mara hadi mafao yanaisha bila kufanya jambo lolote la maendeleo.

Unapostaafu hakikisha unafanya mambo yafuatayo:
a) Vunja kiapo ulichoapa ulipopata ajira yako.
b) Epuka ajira za muda (mikataba) unapostaafu.
c) Fungua ofisi yako, ofisi ndiyo ifanye mikataba na ofisi yako ya zamani, wewe ukiwa ndiye mtendaji.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom