Mikasa ya ajabu niliyoishuhudia kwa macho yangu

Hahhaha
Halafu watakuwa wanapenda sana tuwabembeleze wakisusa

Usikute wanajisemea ebu ngoja niwatetemeshe kidogo wanibembeleze wanasikia raha sana

uwiii usimtibue tena Lwanda maana amekubali kuendelea
Jf sihami yani tuwabembeleze ma baby zetu tukiingia na humu tuwabembeleze waleta story woiii
JokesLwanda usini mind tuendelee mkuu shusha kama tano za kutupooza leo
 
MKASA WA PILI -Sehemu ya pili 41.

Inaendelea.............

Nilipoingia chumbani nilimkuta yule Malikia,utaratibu ulikuwa ni ule ule wa kusuju,baada ya muda akaanza kunieleza "Leo umenifurahisha sana kijana wangu".

Aliniambia "Hebu niambie unataka nikufanyie nini?".

Nilimwambia "Nahitaji pesa hii unayonipatia unipe uwezo wa kuifanyia maendeleo".

Akasema "Ni hilo tu kijana wangu au kuna lingine?"

Nilimwambia "Ni hilo tu Malikia!".

Aliniambia "Sawa nimekusikia lakini labda nikuombe kitu kimoja".

Nilimtegea sikio kwa makini nione ni kitu gani ambacho alikuwa akitaka kunieleza!.

Aliniambia "Hakikisha unafanya yale yote niliyokueleza wakati tukiwa ziwani na nilikuambia juzi ya kwamba yale yote uliyo yaona huko nilipowatuma kutoa kafara usithubutu kueleza kwa mtu yeyote na hata wale watu uliowaona iwe ni siri yako!".

Alikuwa akiniambia kwa msisitizo mkali sana,na mara zote kauli zake za msisitizo nilikuwa nazitilia uzito sana,vinginevyo nisingekuwa makini nilikuwa nakufa.

Aliendelea kusema "Ikiwa utafanya vinginevyo basi tutakutana ziwani na nitakushughilikia kwa mikono yangu mwenyewe!"

Wakati alipokuwa akiongea ghafla alibadilika sura ikawa ya kutisha sana,yaani sielewi ni fananishe na kitu gani.Kiukweli niliogopa sana mpaka nikataka kujikojolea!.Baada ya kuona ninaogopa aliniambia "Usiogope maana nilitaka unishuhudie namna nilivyo na huu ni mwanzo tu ukifanya vibaya basi nadhani sitakuja kama unavyonifahamu,endelea kufanya vizuri kijana wangu kwani nimekupenda sana!".

Baada ya hayo maagizo yake ghafla alitoweka,ndipo nilinyanyuka pale chini na kukifunga kile chumba na kuelekea chumbani kwangu!,Ndugu zangu achaneni na habari za Shetani kwa maana mimi japo nilikuwa tajiri lakini cha moto nilikiona,kwanza kile kitendo cha kukutana na yule Malikia tu mle chumbani ilikuwa ni hatari sana,hebu fikiria unamuona kiumbe ambaye alikuwa mrefu wa futi 12,pia alikuwa na nywele ambazo zilikuwa zinaanzia kichwani mpaka chini kwenye mazulia ya kile chumba,kuna muda nilikuwa nikiingia kwenye kile chumba namkuta amekaa lakini kiti alicho kalia hakionekani,yote tisa,kumi lilikuwa ni hilo tukio la kubadilika sura yake na kuwa kiumbe aliyekuwa akitisha sana,kama ulikuwa huna roho ya kishetani basi ulikuwa unasahaulika kabisa!.

Baada ya siku kadhaa kupita nilimtafuta yule jamaa aliyekuwa mtaalamu wa majengo nikamwambia tuanze ujenzi wa zile nyumba upesi maana pesa nilikuwa nayo,kuna eneo nilinunua maeneo ya Buhongwa ambalo lilitosha kabisa zile nyumba tatu ambazo zilikuwa apartment.Kiasi cha kwanza nilimpa milioni 50 na kila alipokuwa akifika kwenye hatua kadhaa nilikuwa nikimlipa pesa zake!.Sasa Kuna siku nikiwa natokea hapo site kwenye hizo apartment zangu zilizokuwa zinajengwa nilipitia mjini kuchukua mahitaji ya nyumbani na ndipo kwa mbali nikamuona yule tajiri ambaye nilimuona kwenye lile tukio la kule Buhemba tuliposababisha ile ajali ya yale magari mawili.Kiukweli jamaa alikuwa anaonekana ana pesa nyingi kuliko zangu maana tajiri hata kwa kumuangalia tu ulikuwa unamfahamu,alikuwa na gari moja kali sana kuliko hata ile ya kwangu na nadhani alikuwa kwenye moja ya miradi yake maana alikuwa kasimama mahali fulani akionekana kuongea na watu fulani.

Nilimuuliza dereva wangu "Hivi yule jamaa huwa anaitwa nani?"

Dereva wangu aliniambia "Bosi yaani............humfahamu?".

Dereva aliendelea kuniambia "Inaonekana hujakulia Mwanza bosi,mbona huyo ni tajiri mkubwa tu anayefahamika hapa mjini!".

Sasa nikakumbuka kwamba wakati nikiwa bado nasoma nilikuwa nikimsikia huyo tajiri lakini sikuwahi kumuona,hata tulivyoenda kufanya lile tukio nilikuwa simfahamu bado,kilichofanya nikamfahamu ni siku hiyo nilipomuona hapo mjini nikamuuliza dereva akanitajia jina lake ndipo nikamfahamu.Miaka ya nyuma wakati tunasoma nilikuwaga tu namsikia huyo jamaa maana alikuwa ni miongoni mwa matajiri wa Mwanza waliyokuwa wakizungumzwa sana kwasababu ya utajiri wao,kwahiyo kuanzia hapo ndiyo nikaelewa sasa.Sikutaka kabisa mtu yeyote afahamu kilichokuwa kinaendelea na tokea hapo ndiyo nikawa namfahamu huyo tajiri naye utajiri wake ulikuwa wa kishirikina!.

Basi tuliondoka zetu kuelekea nyumbani,tulipofika nyumbani niliona sasa ulikuwa muda muafaka wa kuanza kuwasiliana scolastica ili nianze kumpanga kwa mashambulizi!.Nilichukua simu yangu nikampigia Scolastica na kiukweli tuliongea sana na kumbe alikuwa amenielewa toka siku ile ya kwanza!.

Scolastica aliniambia "Basi nimekuelewa nitafanya hivyo".

Sasa nilipanga kwanza nimshughulikie yule mwanamke wa bosi wake wa zamani dereva wangu dada,kwasababu nilijua ningeanza na Scolastica angeenda kumwambia halafu angeniona nataka kuwazunguka.Hawa wanawake sikuwa na haraka ya kuwatengenezea dawa ili wanikubali maana walinipenda wao wenyewe,kwao nilitumia fedha tu kuwanasa.Sasa Kwakuwa nilikuwa nina muda mrefu sijapiga bakora za kim-kakati,nilimpigia simu yule mwanamke wa bosi wake wa zamani dereva wangu,nilimwambia ajitahidi aje pale nyumbani kwangu,nilitaka aje alale kabisa ili niweze kumshughulikia vizuri!.

Aliniambia "Mmh! ngoja niangalie kama itawezekana kulala maana nitaangalia ratiba ya mume wangu kwanza,kama hatokuja kwangu basi nitakuja".

Kweli,usiku huo alinipigia simu akaniambia nimwambie dereva wangu amfuate,aliniambia kwamba angemkuta jirani na kwake akimsubiri.Usiku huo nilienjoy sana maana nilimkarabati sana yule mwanamke mpaka asubuhi,siku iliyofuata sikuwa na presha maana sasa nilifahamu aliyekuwa akifuatia ni Scolastica.

Sasa nakumbuka baada ya siku kadhaa kupita yule binti mtoto wa shangazi naye alikuwa amemaliza mitihani yake,hivyo alikuwa tu hapo nyumbani kwangu.
Kuna siku nikiwa kule site Buhongwa ambako ujenzi wa zile apartments zangu ukiwa unaendelea kuna sauti niliisikia ikiniambia "Mbona unatuudhi?,kwanini unatuudhi?".

Sasa nilitoka haraka hilo eneo lililokuwa na watu wengi wakiendelea na ujenzi nikasogea eneo la mbali kidogo lisilokuwa na watu nikawa nauliza "kuna nini wakubwa zangu?".

Ile sauti iliniambia "Binti uliyemuacha nyumbani kafanya nini?".

Kiukweli ile kauli ilinifanya nikaishiwa nguvu ghafla maana nilijua tayari yule binti atakuwa kaharibu!,nilimwambia fasta dereva aniwahishe nyumbani maana kuna shughuli inapaswa nikaifanye.Ile nimefika tu nyumbani nikakuta yule binti ametoa lile zulia kule kwenye chumba siri akiwa anaendelea kukifagia kile chumba,nilikasirika sana lakini sikutaka kumwonyesha!.

Nilimuuliza"Wewe huku unatafuta nini?".

Aliniambia "Nimeamua nifanye usafi nyumba nzima kaka,hivyo nikaona nifagie na hiki chumba chako cha sala".

Yaani alikuwa anaongea bila hata kuonyesha wasiwasi yule binamu yangu!.

Nilimuuliza "Funguo umetoa wapi?"

Akaniambia "Niliingia chumbani kwako nikazikuta pale mezani hivyo nikajaribu kufungua zikafungua nikajua ndizo".

Akaniuliza "Kwani kuna ubaya kaka kufanya usafi huku".

Kwakuwa sikutaka kitu chochote kifahamike nilimjibu "Hakuna ubaya ila mara nyingi huwa sipendi watu waingie ingie chumba ambacho huwa nafanyia Ibada ila hakuna ubaya tena ni vizuri umekifanyia usafi maana toka nimehamia hapa sijawahi kufanya usafi,ok sawa wewe endelea na usafi!".

Niliondoka zangu kuelekea chumbani kwangu na kuanza kulia sana maana nilifahamu kaharibu kila kitu na nikajua adhabu nikayoenda kukutana nayo haikuwa ya kitoto!,Kitu ambacho aliharibu yule binti kwanza kabisa ni kuingia kwenye kile chumba cha siri ambako hakupaswa kukanyaga mtu yeyote tofauti na mimi,ingawa zana za kazi hakuweza kuziona kwasababu nilikuwaga nazihifadhi kimazingara,hivyo mtu yeyote asingweza kuviona vile vifaa ya kazi kama alikuwa si muhusika.Kitu kingine alichokosea yule binti ni kuingia chumbani kwangu nilipolala maana hakupaswa mtu yeyote kuingia ila mimi tu!,wanawake zangu wote hapo kabla nilikuwa ninawaingiza kwenye vile vyumba vingine kwa ajili ya bakora.Kwa upande wangu nilijilaumu sana kuondoka siku hiyo bila kufunga chumba changu na kosa lingine nililolifanya ni kutokuweza kumfunga yule binti kimazingara ili asikifikirie kile chumba,kiukweli nilijisahau sana maana sasa nilikuwa nishazoea!,yale mazoea ya kuondoka bila kufunga chumba changu ndiyo yalinigharimu.

Basi alipomaliza kufanya usafi nilimwambia anipe funguo na akiwa anahitaji kufanya usafi awe ananiambia!,mpaka wakati huo hakuwa hakifahamu chochote!,niliingia ndani ya kile chumba na nikarudishia lile zulia vizuri na kila kitu kilikaa sawa.Nilimwagiza dereva ampelekee yule jamaa pesa fulani ambayo ilipaswa nimpe.

Nikamwambia "Akikuuliza mwambie nimepumzika maana kichwa kinauma sana!".

Dereva alisema "Sawa bosi".

Usiku wa siku hiyo niliuona mchungu sana kwakweli,ilipofika mida ya saa 6 usiku kama kawaida nilisikia sauti ya Malikia ikiniita mle chumbani,moja kwa moja sikutaka kupoteza muda.Nilipofungua mlango na kuingia ndani nilimkuta akiwa si yule Malikia niliyemzoea!,safari hii alikuwa akitisha sana,nilitaka kukimbia lakini sikuweza na sikuwa na namna ilibidi nianguke chini na kusujudu,nilianza kulia kwa uchungu nikimuomba msamaha!.

Aliniambia "Nilishakuonya mara ngapi kuhusu hiki chumba kijana wangu?".

Nilimwambia huku nikilia "Nimekukosea sana Malikia nisamehe na niambie chochote nitafanya ila usiniue tafadhali".

Aliniambia "Hebu niangalie".

Nikamuangalia nikakuta karudi katika hali yake ya kawaida!.

Akaniambia "Simama".

Alianza kuniambia "Nakuonya kwa mara ya mwisho kijana wangu na likijirudia hili la leo basi lazima ulipe wewe mwenyewe".

Ndipo akaniambia "Ninamuhitaji huyo binti na hakikisha haipiti wiki niwe nishampata,bila shaka umenielewa!".

Nikamwambia "Ndiyo,nimekuelewa Malikia".

Baada ya hayo mazungumzo ghafla akatoweka mle chumbani.Nilirudi chumbani na kuanza kulia sana kama mtoto mdogo maana nilijua huyo mtoto wa shangazi hakuwa na muda mrefu alikuwa anakufa!.Na aliniambia nihakikishe haipiti wiki niwe nimempatia.

Itaendelea.............
 
nafwatilia huu uzi kwa makini.. yan mpka niupate ushuda wa jinsigani Yesu alivyobadilisha maisha yako..
 
Attachments

  • Screenshot_20210304-191756.jpg
    Screenshot_20210304-191756.jpg
    45.1 KB · Views: 108
Mkuu bwana sasa huyo mwanae anakujua kama wewe ndio unatumia hii I'd
Daah acha ibaki moyoni mwangu mkuu kwani nakumbuka niliwahi kumsimulia jamaa fulani aisee nilikumbwa na matukio ya ajabu ajabu, pia kuna dogo ambaye yeye alivyoondoka tuu ktk yale mazingira ya nyumba ile alitutumia sms iliyokua ikisema" hapo msiishi kiboya huyo mzee mchawi atawatoa musukule lakini tulichukulia kawaida.

Ila huo muziki uliotukuka si mchezo halafu dzaini kama alitupumbaza yaani tusifikiri chochote kile, mkuu ile oysterbay na masaki wanaoishi kule si watu wa mchezo mchezo wanafuga misukule si kitoto.
 
Shusha nondo mkuu
Nipo na porpcon mdogo mdogo
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom