Mikasa/vituko vya lodge

Mikasa/vituko vya lodge

Kama kuna mtu anapata safari ya Ruangwa Mjini kuna hotel inaitwa Green View vyumba 25k(fan) na 30k(ac) hii hotel ipo vizuri saaaana kwenye usafi changamoto ni kubalance maji ya moto na baridi labda na vile Visabuni vya Eva basi lakini kuhusu usafi nawapa kongole, Nimelala apo mwaka jana na mwaka huu pia.
Na ni mwendo wa dk 2 kwenda stendi...pazuri sana,ila kama bajeti yako nzuri unaeza enda Kidia napo ni pazuri sana
 
kuna guest nishawahi ingia nilisikia kelele tu muda mwingi wanazagamuana hadi saa 9 ikaacha ikaanza tena 11 niliwahi sana kwenda stand ile siku na nililala sana kwenye basi sitasahau
Hiyo ilinipata mwaka Jana, nilienda mwanza kwenye rock city marathon, nikalala mtaa wa kirumba maana sio mbali na rock city Moore tunapoanzia mbio. Aisee vyumba vyote vya hiyo guest ilikua ni kelele tupu, nje ukutani ni kelele, kelele kila mahali watu wanapigana mashine. Sikulala Hadi asubuhi
 
Musoma mara,mwaka 2008,siwezi kusahau ile siku tarehe na mwez nimesahau ila siwezi kusahau,nimefika nikitokea Mwanza nilale asubuhi niende zangu dar kupitia sirari kipindi hicho njia ukiwa bukoba unapitia kampala kwa basi,ukiwa mwanza unapitia sirari,daaah nikachukua lodge,hapo hapo kulikuwa na bar,nikatoka enzi hizo balimi tamu balaa nikaanza kupiga balimi zangu ghafla akaja mshkaj akawa anamzingua muhudumu ambae anahusika na upande wa lodge na kaunta ya vinywa daaaah baada ya muda jamaa kaanguka kafa pale pale,cha kushangaza hakuna mlevi wala muhudumu aliostuka wakawa wanasema tu kiburi kimemponza,polisi wakaja wakachukua maiti bila kusema chochote na sisi tuliopo pale,palepale nikapata stor kuwa aliwekewa sumu ya mamba,usiku nimerudi chumbani maji yakawa hayatoki nikatoka kumgongea yule dada muhudumu,kwanza hakuitika ila aliuza nan wewe nikasema mm mpangaji wa chumba flan akauliza unataka nini,nikamwambia maji hakuna,akaniuliza kwahiyo[emoji3] daah nilipokumbuka tukio la yule jamaa aliokufa,nikamjibu hakuna kitu dada nimeuliza tu labda yatarudi na mabomba yapo wazi hivyo yatamwagika[emoji3][emoji16]
 
kuna guest nishawahi ingia nilisikia kelele tu muda mwingi wanazagamuana hadi saa 9 ikaacha ikaanza tena 11 niliwahi sana kwenda stand ile siku na nililala sana kwenye basi sitasahau
Hiyo ilinikuta gesti moja Shinyanga stendi
 
Morogoro nimekutana na Mwalimu tukawa tunaangalia promo ya heineken, nikamnunulia bucket 🪣 mbili mara kaanza kukata mauno na yeye kama wacheza shoo, tumefika chumbani katapikia mashuka yote, nikabeba kibegi changu nikasepa, sijui nini kiliendelea,uzuri huwa naandika majina na no za simu za uongo.
 
Hiyo ilinipata mwaka Jana, nilienda mwanza kwenye rock city marathon, nikalala mtaa wa kirumba maana sio mbali na rock city Moore tunapoanzia mbio. Aisee vyumba vyote vya hiyo guest ilikua ni kelele tupu, nje ukutani ni kelele, kelele kila mahali watu wanapigana mashine. Sikulala Hadi asubuhi
Walikuwa ni washiriki wenzio wa marathoni maana ni njia mpya ya kufanya umalaya na ukahaba. Hakuna lolote la maana huko kwenye hizo marathoni zaidi ya hiyo. Mungu atusaidie kwa kweli.
 
Miaka miwili nilienda vwawa mbozi kuna guest house ipo karibu na shell ya ilasi inaitwa mkulima guest house,chumba chenye choo,tv,maji ya moto ya heater,kitanda 6x6,wali maharage bure,nguo zisizidi 2 unafuliwa na viatu unabrashiwa kwa sh 10,000/=!!kwa kweli nilistaajabu na wengi hawaamini nikiwahidithia!
Vitu vyote hivyo kwa elfu 10000 ?
 
Dodoma ilikuwa kipindi cha kuanza bunge baada ya uchaguzi, lodge mji mzima zimejaa.

Nilikuja pata lodge saa 6 usiku kuingia bafuni nakuta kimba linaelea, shuka zina unyevu nyevu, kumuuliza muhudumu anadai chumba kimetoka kusafishwa, baada ya vurumai nilirudishiwa pesa yangu. Niliishia kulala kwenye gari mpaka kunapambazuka.

Iringa nilikutana na bonge la tangazo marufuku kwa wasiokuwa wanandoa kulala pamoja. Ukienda na mwanamke sharti uwe na cheti cha ndoa. Niligeuza kutafuta sehemu nyingine, kwa baridi ile sikutaka take chances za kulala mwenyewe.

Cha ajabu nilikuja gundua kuwa ile lodge ilikuwa maarufu kwa mashoga maana hawahoji wanaume kulala pamoja lakini wana tatizo na mwanamke na mwanaume.

Iringa huko huko tulikuja gongewa na mapolisi. Wanatafuta wahamiaji haramu, nilikuwa na mwenyeji wangu tuliokutana usiku huo huo tu. Kuhofia wizi begi langu lenye vitambulisho vyote nilimpa mwenzangu ambae alilala lodge nyingine.

Na rangi yangu si rafiki sana kuepusha shaka ya uraia wangu (kwa mujibu wa mapolisi)mbaya zaidi moja ya mapolisi alikuwa anamjua yule dada na shughuli zake.

Polisi kuniuliza jina la mwenzangu nikabwatuka tu Mary na demu akajibu jina lingine muda huo huo (Hata jina lake nilikuwa silijui).

Siku hiyo niliamini mizimu ipo. Nilipoulizwa jina langu nilitaja jina la ukoo, ghafla mkuu wa wale polisi akakurupuka kuwa anamjua mzee wangu (mzee nishazika miaka mingi iliyopita) alijichanganya tu, na hiyo ndio ikawa pona yangu.

Sumbawanga vijijini nililala lodge usiku mzima kulikuwa na kelele za mapaka hasa ukizima taa. Nilikesha mpaka panapambazuka.

Mwanza nilikutana na demu sehemu niliyoenda kula. Walikuwa wanapiga mziki. Tukaimbishana hivyo hivyo kwenye kelele na kuondoka wote. Kufika lodge kumbe demu kiziwi na kidogo mtambo. Alikuwa anaongea kwa nguvu balaa.

Tena topic za ajabu kama vile utanifanya mara ngapi, utanioa, mbona mbupu zako ndefu, hii ikiwa ni saa 7 za usiku tena kwa kelele. Ilibidi saa 11 asubuhi ninyate nikimbie fedheha toka kwa wa vyumba vya jirani waliosikia, kufika mapokezi jamaa ananicheka mpaka kuanguka kumbe alikuwa akisikia ile mikelele.

Stori za lodge zipo nyingi mno nilizokutana nazo. Nimechoka kuandika.
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom