Mikakati thabiti ya siasa UKAWA

Mikakati thabiti ya siasa UKAWA

Siasa za kinafiki nazichukia sana. Sizipendi kuziona,kuzishiriki,kuzisikia wala kuzinusa. Hukasirishwa nazo sana. Eti leo Dr. Slaa amekuwa kipenzi cha CCM. Eti leo Dr. Slaa wa CHADEMA anaonewa huruma na wanaCCM na hata viongozi waandamizi. Tangu lini mambo haya? Si huyu aliyekataliwa chamani,kwa hila, mwaka 1995 kule Karatu na ukawa ndiyo mwanzo wa yeye kuhama CCM na kujiunga CHADEMA?

Ni Dr. Slaa huyuhuyu alikuwa akiitwa majina mbalimbali ya kukereketa na kufukuta masikion mwa watanzania. Dr. Slaa, ashakum si matusi, ameitwa Padre Mzinifu na hata Babu Slaa. Aliitwa hivi kumpotezea maboya na kumtweza mbele ya watanzania. Dr. Slaa wa CHADEMA aliandikwa,kutangazwa na kusemwa kama asiyefaa. Leo,walewale wapondaji wanamsifu Dr. Slaa na kumuonea huruma kuwa amepokwa nafasi ya kugombea Urais. Unafiki.

Makada wa CCM,wale wenye uelewa finyu wa mambo ya kisiasa, wanaona kuwa kwakufanya hivyo watawavuruga CHADEMA. Vipi kuhusu patashika-nguo kuchanika ndani ya CCM? Muda huu tuutumie kujipanga dhidi ya UKAWA na mchezaji wao mpya Lowassa. Ya Dr. Slaa yatatudumaza na kutukwamisha. Dr. Slaa bado yuko CHADEMA na mwenye ari kubwa. Wabobezi tunajua.

Mchezo anaoucheza Dr. Slaa na CHADEMA ni kama ule wa kwenye filamu maarufu ya kikorea ya Jumong. Jumong alipotea na kujipoteza mara kadhaa kuhadaa mahasimu wake. Alipojitokeza kwa surprise, mahasimu wake waliipata habari yao. Makada wenzangu, Dr. Slaa hatuhusu. Tuendelee kuzichanga vyema karata zetu kwa mpambano wa Oktoba 25 mwaka huu.

Siasa za kinafiki hazina rafiki na hatufiki!

Mzee Tupatupa wa Lumumba, Dar es Salaam

Leo ndio nimekufahamu vema; chadema mkubwa wewe!!
 
Hilo swali ligeuzie kwako kisha jiiulize tangu lini fisadi Lowassa amekuwa kipenzi cha Chadema.
Toka alipoamua kuachana na kundi la wezi waua albino, mafisadi, wahujumu uchumi, wazee wa ESCROW, wazee wa RICHMOND, wazee wa EPA. Need i say more?
 
Mtani wangu Chikawe ameponzwa na Polisi wake. Teh teh

Mzee Tupatupa

Mzee wangu unanidanganya bintiyo,najua A-Z,hiyo ni kule kwa Mkullu siyo Polisi...........

Kama ilivyokuwa URAIS wa KWANGU NA FAMILIA YANGU,SINA UBIYA NA MTU ,ndicho kinachoendelea na HUKU WENYEKITI WANGU NI WA KWANGU NA FAMILIYA YANGU HAUNA UBIYA NA MTU...

Umenisikitisha Mzee wangu,umeamua kunidanganya,najua NACHINGWEA NA CHIKAWE ni PAKA NA MKIA wake............:disapointed::disapointed::disapointed::disapointed:
 
Naona umeamua kuitukana Chadema rasmi,, Kama unampenda sana Slaa nenda kanywe nae chai... Slaa angekuwa anakubalika asingeshindwa uchaguzi mwaka 2010

Tatizo hata post yangu hujaielewa.

1.Ungeenda kuisoma post ya Mussa Allan halafu ukaja jibu post yangu.

Umekurupuka kurupu!!!!!!!!!!!

Nakuelimisha maana ya badniko langu;

1.Mussa Allan ni Team Lowassa kindakindaki,akili na mwili vyote viko kwa Lowassa,nimemtaadharisha tu kwamba kama anampenda hivyo na anautaka ukuu wa wilaya basi ni lazima ahakikishe CDM inapata madiwani na wabunge mkoani kwake ili afanye kazi kwa AMANI...Upo?

Usirukie gari kwa nyuma utadondoka.........
 
Pamoja na yote hayo hawatakiwi kutuchanganya sasa hivi

Tatizo lililopo ni Josephine ambae alikuwa amejiandaa kuishangaza dunia.angalau Tanzania kungekuwepo ajabu la dunia kwa kimada kuwa first lady?!!!
 
Wadau amani iwe nanyi
Chadema ni noma wamefunika mbaya kila kona chadema lowassa, kwa vile ni wabunifu wamebuni tena nini kifanyike wakakubaliana kwa pamoja Dr slaa ajifanye kama hataki ujio wa lowasa magazeti,TV na wananchi wahemke kwa wiki kadhaa baada ya hapo ajitokeze hadharani akanushe na kutangaza lowassa na ukawa ukawa na mshikamano mpaka kieleweke
 
wacha ccm icheze ngoma ya Chadema bila kujua apigae ngoma
 
Wadau amani iwe nanyi
Chadema ni noma wamefunika mbaya kila kona chadema lowassa, kwa vile ni wabunifu wamebuni tena nini kifanyike wakakubaliana kwa pamoja Dr slaa ajifanye kama hataki ujio wa lowasa magazeti,TV na wananchi wahemke kwa wiki kadhaa baada ya hapo ajitokeze hadharani akanushe na kutangaza lowassa na ukawa ukawa na mshikamano mpaka kieleweke

Mkuu huo ndio ukweli kabisa kwani vyombo vyote vya habari ni kuipigia promo cdm na ukawa,maccm yanatoa mapovu bila kujijua kuwa yanatumika kama remote
 
Haka kamchezo kama ni kweli kameishika lumumba pabaya duh!
 
Hakika mtoa uzi umenena yan bnafs nlishaliona hlo na kuna mtu nlimwmbia hvyo akakubal. Mm nliwaza haitawezekana Dr na Mbowe wakoxane kisa mtu from ccm never aisee so nkajua tu hii ni sehem ya mbinu ya kuzima na kufifisha nyota ya JPM ktk kipnd hk na kiukwel imefanikiwa.
 
Kamamda game is over endelea na drama zako.
 
Iyo ndo chadema bhanaa!!!! ooooo !!!wamechukua fisadi me nashangaa ccm kura za maoni rushwa ,kejeli,ngumi na ubabe umetawala ,,,,,,chadema wao wanapeta tu ccm jiandaeni mtaipata mwaka uuu ????
 
tukutane kwenye upigaji wa kura sasa
 
Huku Lowasa akipewa jukumu la kuipeperusha bendera ya Urais kupitia Ukawa 2015. Upande wa pili,
inahitaji akili ya ziada sana kuweza kugundua striking moves za Ukawa. Hapa wamekuja na Mkakati wa kumpumzisha Dr Slaa kimkakati ili awe strike move kwenye hatua za mwisho kabisa za Ushindi.
Wadau wa Soka mnajua umuhimu wa Striker mkali anayetokea bench kwenye dakika za majeruhi za fainali muhimu.
"Ukawa hauongozwi kwa siri, bali kwa mikakati" najaribu kumuelewa Mbowe kinamna hii.
Nawasirisha kwa mjadala.
 
JK amenichekesha sana leo,,eti dunia nzima inajua Tanzania tunapata maendeleo wakati sisi wenyewe watanzania hayo maendeleo hatuyaoni.
 
JK amenichekesha sana leo,,eti dunia nzima inajua Tanzania tunapata maendeleo wakati sisi wenyewe watanzania hayo maendeleo hatuyaoni.

tumsamehe tu,yawezekana ni kweli kiasi flani coz viongozi wa Tanzania wamepata maendeleo,simhukumu Jk kwani hajaangalia mtanzania wa kawaida
 
Back
Top Bottom