Mikail Gobachev anastahili kuwa mtakatifu? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mikail Gobachev anastahili kuwa mtakatifu?

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Tango73, Feb 12, 2012.

 1. Tango73

  Tango73 JF-Expert Member

  #1
  Feb 12, 2012
  Joined: Dec 14, 2008
  Messages: 1,678
  Likes Received: 34
  Trophy Points: 135
  Raisi wa zamani wa Urrusi Mikail Gobachev ansifa zote za kuwa mtakatifu. Ukikumbuka kwa jinsi gani siasa za kikomunisti au ujamaa na kujitegemea zilivyokuwa zinasumbua watu katika nchi zao. Huyu mrusi anstahili kabisaa kuheshimiwa kitakatifu kwa jinsi alivyo waokoa mabilion ya watu waliokuwa wanakandamizwa na siasa za kikomunisti.

  Gobachev alijivua kabisaa umwinyi wa kuimbiwa kwaya na kuheshimiwa kama mungu na watu wake ingawa alikuwa katika nafasi nzuri sana ya kuwa billionea akistahafu. Kwa ujasiri wake, aliungana na Papa Paulo na Raisi wa marekani wakati huo, Ronald Regan kuhakikisha watu wote waliokuwa wanateswa na siasa za uongo na za kikatili za kikomunisti wanaokolewa na kuwa huru.

  Gobachev hakutaka kabisaa kuja kuwa tajili kama walivyo wenzake waliokuwa wakuu wa KGB au Viongozi wa Chama cha kikomunisti cha Urussi-CCCCP. Gobachev aliwajali sana raia zake na watu waliokuwa wanateseka bila wao kujijua ndani ya nchi zao, ndio maana aliuchukia ukomunisti kwa nguvu zake na zakukopa zote.

  Dunia lazima impatie heshima inayostahili mzee Mike' na awe anakumbukwa milele na wanyonge waliokuwa wanfanywa watumwa na wachache ndani ya nchi zao. Mkombozi siku zote hupendwa na kuabudiwa, sasa kwa nini wanadamu tusimuenzi mtu kama Gobachev? Haswa sisi watanzania ni lazima sana kumkumbuka Gobachev. Kukosa ujasili wake alioutumia kukomboa watu waliokuwa wanatwaliwa kimwinyi, hatungekuwa na upinzani kama wa CHADEMA, uhuru wa vyombo vya habari, kumiliki TV na kuona matukio makuu ya kisiasa, soka, usanii na dini duniani.na vile vile tusinge miliki Fliji,kuwa na vyuo vikuu ishirini , kuwa na mainjinia, madaktari na wanasheria wengi kuliko wansiasa..

  Sasa hivi secta ya michezo, usanii na muziki zinalipa sana Tanzania na vijana wetu wanatajilika kila kukicha , hii yote ni kwa sababu ya ujasiri wa Gobachev. Jamani Gobachev anastahili kuwa Mtakatifu. nani alikuja jua kuwa ipo siku wachezaji wa Yanga wangekwenda kaunda kufanya mazoezi huku kila mmoja kapaki gari lake katika parking lot ya yanga?
   
 2. M

  Madodi Senior Member

  #2
  Feb 12, 2012
  Joined: Apr 10, 2011
  Messages: 181
  Likes Received: 19
  Trophy Points: 0
  mmmmhh...nina mashaka na ww? Nijuavyo mm huyu gobachev ni kibaraka wa c.i.a
   
 3. J

  Jasusi JF-Expert Member

  #3
  Feb 12, 2012
  Joined: May 5, 2006
  Messages: 11,484
  Likes Received: 165
  Trophy Points: 160
  Halafu huo utakatifu aupate wapi na wapi? Huo hutolewa na Kanisa Katoliki peke yake.
   
 4. Inkoskaz

  Inkoskaz JF-Expert Member

  #4
  Feb 12, 2012
  Joined: Nov 6, 2010
  Messages: 6,317
  Likes Received: 437
  Trophy Points: 180
  warusi wengi ni Orthodox
   
 5. Narubongo

  Narubongo JF-Expert Member

  #5
  Feb 12, 2012
  Joined: Nov 3, 2010
  Messages: 1,922
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 135
  utakatifu si zawadi kama Phd za heshima. Process yake ni ndefu sanaaaa na ukitaka kuleta siasa itageuka aibu kwa marehemu. Bado najiuliza mpaka kesho swala la mwl
   
 6. Kimbunga

  Kimbunga Platinum Member

  #6
  Feb 12, 2012
  Joined: Oct 4, 2007
  Messages: 13,010
  Likes Received: 1,816
  Trophy Points: 280
  Mkuu najua Orthodox ni kajisehemu ka Kanisa Katoliki; hivi wao hawana watakatifu kama Kanisa Katoliki la Roma? Labda swali lingine ni je Gorbachev ni makatoliki? Mtoa mada amesema waliungana na Pope John Paul (RIP) na Ronald Regan (RIP); je Regan naye hastahili huo utakatifu?

  Mchakato wa utakatifu ndani ya Kanisa Katoliki ni mgumu lakini ni jambo la wazi kwamba Gorbachev ana nafasi yake katika historia ya hii sayari ya dunia kama walivyo akina Hitler, Stalin, Mao, nk
   
 7. T

  Topical JF-Expert Member

  #7
  Feb 12, 2012
  Joined: Dec 3, 2010
  Messages: 5,176
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 0
  Halafu hao watakatifu ndio wanapata nini mbele ya Mwenyezi Mungu?

  Hakuna mtakatifu, kila mtu anatakiwa ajitahidi kuomba apate huruma za Mwenyezi Mungu

  Otherwise wakatoliki wanadanganyana na utakatifu wao wa kijinga sana
   
 8. Kiranga

  Kiranga JF-Expert Member

  #8
  Feb 12, 2012
  Joined: Jan 29, 2009
  Messages: 34,605
  Likes Received: 6,175
  Trophy Points: 280
  Concept nzima ya utakatifu ni unafiki tu, mkimpa utakatifu leo na kesho kugundua kwamba aliua watu maelfu itakuwaje?
   
 9. Shine

  Shine JF-Expert Member

  #9
  Feb 12, 2012
  Joined: Feb 5, 2011
  Messages: 11,514
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 0
  kha kumbe siyo mkatoliki?
   
 10. Shine

  Shine JF-Expert Member

  #10
  Feb 12, 2012
  Joined: Feb 5, 2011
  Messages: 11,514
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 0
  Nlifikiri unajiuliza suala la jk maana nae angekuwa mkatoliki nae angefaa bila kumsahau el siasa makanisani
   
 11. Kipis

  Kipis JF-Expert Member

  #11
  Feb 12, 2012
  Joined: Jul 23, 2011
  Messages: 493
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Mkuu hawa jamaa mie wananiachaga hoi kweli! Pamoja na kuwa wana madigrii chungu mbovu lakini bure kabisa! Hivi utakatifu wanaufahamu kweli hawa!
   
 12. p

  punainen-red JF-Expert Member

  #12
  Feb 12, 2012
  Joined: Nov 18, 2010
  Messages: 1,735
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 0
  Mkuu, pamoja na kuwa mimi siyo m-roman na hii mada haijaweka wazi kama jamaa ni wa dhehebu hilo au la, lakini nadhani kuua makumi au maelfu hakumfanyi mtu awe au asiwe mtakatifu (mbele za Mungu) Kuna mitume walioua, na kuna watu hadi leo wanaaminishwa kuwa wakijilipua katikati ya makusanyiko makubwa watapokelewa na mungu wao! Jambo muhimu ni sisi kujiuliza tunawezaje kutambua uhalali wa imani ambazo siyo zetu na kwa uhalisi tukisikia lolote kuzihusu mioyo yetu inajikunja kiuadui???
   
 13. Kipis

  Kipis JF-Expert Member

  #13
  Feb 12, 2012
  Joined: Jul 23, 2011
  Messages: 493
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Mkuu swala la kuwa mtakatifu au kutokuwa hiyo ni kazi ya Mungu vipi watu leo wanajipa madaraka ya kutangaza wenzao kuwa ni watakatifu!!?
   
 14. kukomya

  kukomya JF-Expert Member

  #14
  Feb 12, 2012
  Joined: Sep 20, 2011
  Messages: 344
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 35
  Utakatifu? kwa imani ipi? Maana kwa mujibu wa madhehebu yanayoamini juu ya utakatifu hanazo sifa za kutangazwa hivyo. Maana ninavyofahamu yeye bado ni mkomunisti safi, haamini kwamba kuna Mungu, na ni wakala mzuri wa CIA
  tokea tumboni mwa mamake! Ndiyo, anaweza kuwa mtakatifu, lakini ni kwenye dhehebu lenu la wanaosali uchi usiku tu na si vinginevyo.
   
 15. J

  Jasusi JF-Expert Member

  #15
  Feb 12, 2012
  Joined: May 5, 2006
  Messages: 11,484
  Likes Received: 165
  Trophy Points: 160
  Orthodoxy wanatoa utakatifu? Hasa kwa watu ambao hawakutumikia kanisa au dini?
   
 16. p

  punainen-red JF-Expert Member

  #16
  Feb 12, 2012
  Joined: Nov 18, 2010
  Messages: 1,735
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 0
  @Kipis...
  Haahaaaa! Mkuu, swali lako linaniweka mahali ambapo ili nilijibu vizuri, ingebidi niwe m-roman au ningepaswa kujua kwa undani misingi ya imani yao hiyo juu ya utakatifu... Na pia hiyo unayoita kuwa ni kazi ya Mungu, inategemea imani na mafundisho ya mhusika! Nitakupa mfano, ktk Bible kuna sehemu nyingi ambapo wanaomwamini Yesu wameitwa Watakatifu. Sasa watu wanaoamini maandiko ya Biblia hata ufanyeje wanaamini yeyote anayemwamini Yesu ni mtakatifu! Sasa hii ya waroman ni imani yao na bila shaka wana mafundisho yao juu ya hili, sisi tusio wa imani hiyo hatuwezi kuwazuia kutekeleza imani yao hata tungewadharau vipi.
   
Loading...