Miji (sehemu) mizuri kwa mapumziko TZ

ahahahaa..mkuu suala la vacation ni suala nyeti katika upangaji wake umakini na hasa lengo kuu la mapumziko inabidi lijulikane...say unataka mapumziko kwa minajili ya kupunguza stress za kazi...say unataka mapumziko ya kurekebisha mahusiano na familia/mpenzi wako?... au unataka mapumziko kwa ajili ya ku-jitafakari kwa ajili ya next move/steps in ur life..kama ulivyosema upo single...inawezekana ukataka mapumziko kwa ajili ya kufanya maamuzi kati ya madem wako wa-3 ulonao umuoe nani hiyo next year......zingatia haya

1- kupunguza stress za kazi-- nenda maeneo yenye shamrashamra za starehe..say arusha, morogoro, mwanza, haphapa dar pia panafaa.. na zenji ila wakati wa festival ya music and films i mean maeneo vibrant ni rahisi kukusahaulisha misukosuko ya kikazi

2- mapumziko ya kifamilia kurekebisha mahusiano- nenda moshi/ kilimanjaro..panda mlima , tembelea vivutio vidogo vya watalii kama waterfalls nenda bagamoyo na kwengineko ambako miji sio soo vibrant

3- maamuzi magumu kama ya ndoa na engagement, kuacha kazi, kujivua gamba, kuhama nchi, kukana uraia etc... haya nakushauri nenda maeneo tulivu kama visiwa vilivyo maeneo ya zenji na pemba kaa hotel nzuri na tulivu, nenda mbugani, etc

4- mapumziko kwa maana ya kujutia madhambi etc- nenda makha, israel etc sehemu za mahujaji unakoweza kujutia madhambi yako na mungu atakusamehe...ila kama fungu halitoshi jiwekee ratiba ya kutembelea watu wenye uhitaji na jitolee kwa kila hali na mali yako atleast mungu atakupunguzia mzigo wa dhambi na itakujenga ki-imani zaidi.

ni maoni tuuu
 
Bahasha la Jairo naona limeanza kukulevya, kumbe hata usafiri wako binafsi huna halafu unawaza vacation? kweli mswahili ngozi ya makalio.
Kuwa mpole ndugu, kwa hiyo unataka Zanzibar niende na usafiri wangu? Pia hizo long safaris sio vizuri kwenda na usafiri wako ukiendesha, utachoka zaidi! Halafu nani alikuambia starlet inaweza kufika Bukoba ikarudi nzima!
 
  • Thanks
Reactions: Nzi
Nenda Mwanza Malaika beach, ukitoka hapo nenda Serengeti stop over halafu baadaye Bilila kempisky Serengeti huko huko, utaenjoy Ziwa victoria, ukarimu wa wasukuma, Wanyama wa porini na jinsi Tanzania ilivyobarikiwa kuwa vivutio vingi, tena usiende kwa ndege, panda basi kutokea Ubungo ili uone pia jinsi watu wanvyoishi maisha magumu humo njiani wakati unaenda, Barabara ni lami yote hadi utakapoingia Serengeti.

Umeteleza mkuu! Hilo eneo ulilolitaja wasukuma sio wenyeji...huko wanapatikana waikoma na wamaasai sana sana, na wakurya kiasi fulani.
 
Karibu lushota tanga mkuu, kuna mambo mengi ya kiutalii na hayana gharama kubwa
 

Attachments

  • IMG_0073.JPG
    IMG_0073.JPG
    873 KB · Views: 59
  • snaa 041.jpg
    snaa 041.jpg
    742.6 KB · Views: 48
Kuwa mpole ndugu, kwa hiyo unataka Zanzibar niende na usafiri wangu? Pia hizo long safaris sio vizuri kwenda na usafiri wako ukiendesha, utachoka zaidi! Halafu nani alikuambia starlet inaweza kufika Bukoba ikarudi nzima!
Kweli waswahili kazi ipo, yaani mbwembwe zote hizi kumbe unamiliki kistarlet?
 
Kweli waswahili kazi ipo, yaani mbwembwe zote hizi kumbe unamiliki kistarlet?
Kumbe ndio maana utalii wa ndani TZ ni zero! Unadhani ili kwenda kutalii lazima uwe na gari kubwa, helicopter na private boat! Inaelekea utaniuliza kama mimi ni mzungu, kwa akili yako hii unafikiria mtalii lazima awe mzungu!
 
NENDA BAGAMOYO KWA MIGUU ukifika pumzika siku nne
then endelea mpaka msata pumzika siku moja,
endelea chalinze pumzika siku mbili,
...........misugusugu siku moja............picha ndege siku moja...
..kibaha mjini siku mbili,..... then bongo ,,,,,,,:A S 103:

LIKIZO ITAKUWA IMEISHA!!!!!
 
nenda Bukoba ufanye community tourism. huu mkoa ni very rich in culture, natumaini utajifunza mambo mengi sana.
 
Mkuu ukienda Mtwara utafurahia kuona asili ya mwafrika, nenda kaone jinsi tulivyojaliwa ardhi yenye gas and oil.
 
Kaa bongo wiki nzima usikilizie mgao..halaf nenda kijijini ukaonane na babu na bibi zako..na kwa kuwa upo single unaweza kwenda dodoma, kule sasa hv kuna mademu kibao si unajua bunge..ukifika dom unaweza kupata bongo flava kimtindo..kama likizo bado serereka zenji ukaone muafaka na serikali ya umoja wa kitaifa inavyopiga mzigo..nadhani ni ratiba nzuri..jaribu na utaniambia
 
Nenda Mwanza Malaika beach, ukitoka hapo nenda Serengeti stop over halafu baadaye Bilila kempisky Serengeti huko huko, utaenjoy Ziwa victoria, ukarimu wa wasukuma, Wanyama wa porini na jinsi Tanzania ilivyobarikiwa kuwa vivutio vingi, tena usiende kwa ndege, panda basi kutokea Ubungo ili uone pia jinsi watu wanvyoishi maisha magumu humo njiani wakati unaenda, Barabara ni lami yote hadi utakapoingia Serengeti.


Masuke hapo kwenye red hapo!
 
Umeteleza mkuu! Hilo eneo ulilolitaja wasukuma sio wenyeji...huko wanapatikana waikoma na wamaasai sana sana, na wakurya kiasi fulani.

Mkuu mimi sitaki kubishana na wewe, lakini nataka na mimi nikueleweshe, nilisema hivyo nikizingatia kwamba ataanzia Mwanza na atasafiri kwa barabara kuanzia Mwanza hadi sehemu moja inaitwa Ramadi ukienda mbele kidogo utakuta gate la kuingilia Serengeti na Stop Over iko maeneo hayo hayo, Sasa toka Mwanza hadi Ramadi ni maeneo ya wasukuma yote yale, Bilila ndo iko wilaya ya Serengeti hapo sawa atakutana na Waikoma lakini wamasai atawapata wapi kwa njia ile?

Kwa reference zaidi gonga hapo chini.

Serengeti Stop Over
 
Masuke hapo kwenye red hapo!

Mama D usiogope, Kashasema mwenyewe anataka Vacation maanake ana hela za kutumia, aende tu Bilila asiogope hata kama ataishia kunywa Soda kwenye matent sio lazima aingie ndani na kulala kabisa.
 
nenda iringa ukajionee mashamba ya miti na maisha ya watu iringa, ni wakarim sana pia utajifunza biashara ya hewa ukaa, unaijua wewe? basi ni muda mzuri wa kupumzika huko na kujifunza mengi.
 
Back
Top Bottom