Miika Mwamba vs. Pfunk Majani: Nani alikuwa na biti kali?

mwanamabadiliko

JF-Expert Member
Oct 30, 2010
843
1,363
Hawa wote Wana asili ya uzungu uzungu, Kila mmoja alitengeneza hits nyingi, Ila pfunk alikuwa akisaidiwa na bizman kwa Sana , Sasa he Nani Alikuwa Mkali zaidi, nimesahau track nyingine lakini hizi ni baadhi

Miika Mwamba
1.Mabinti wa Kitanga - misosi
2.Twenzetu - chegge
3.Wanok nok - mandojo
4. Fagio la chuma
5. Elimu mitaani D knob
6. Wange
7. Kikongwe.
8. Pia sebene kibao

Majani
1. Nikusaidieje
2. Zali la Mentali
3. Namba 8 Daz baba
4. Pamba nyepesi inspector
5.nitoke vipi misosi
6. Chagua moja
7. Kibanda Cha simu
8. Wife
9. Mikasi
Embu tajeni ngoma zao nyingine, Ila naona Kama majani anashindwa, Ila Mika Mwamba alikuwa hatari
 
Kwakweli she got gwan ni kati ya beat zangu bora kutoka kwa majani, ila lile beat hakulitengeneza yeye bali alilitengenza soggy na mzungu kichaa majani akamleta sijui jamaa gani kuweka keyboard. Na wakati wananza kulitengeneza hakuwa studio alilikuta likiwa tayari.
Soggy alikuwa ana idea nzuri za beat hata beat zake zilikuwa za kipekee.

Kuna beat moja ya nini mnataka mazee mle ndani majani aliua, halafu kuna beat ya down town records ya wimbo kaimba p 1 black ni kali balaaa jina siujui.
Ila kuna lyrics kama
Nisikize me
....
Watoto wadogo hawanisomi
....
Narepresent me...


Verse ya kwanza anaanza sijui smahani samahani nyingi sana. Nautafuta sana huu wimbo
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom