Mika Mwamba ndiye Producer mwenye uwezo mkubwa wa kutengeneza beats kali kuwahi kutokea kwenye historia ya Bongofleva

NetMaster

JF-Expert Member
Sep 12, 2022
1,454
4,853
1670880858177.png


Jina lake ni Miikka Kari, Hapo kwenye Kari alibadili iwe kwa kiswahili na tafsiri yake ni Mwamba, hivyo aliamua kujiita Miikka Mwamba ila wengi tukaizoea Mika Mwamba

miika-png.558523



Ngoma za huyu mwamba zilikuwa na vinanda vyenye ma-vibe ya kufa mtu:
  • Tamara + ni wewe - Hard Mad
  • Eno maiki - Ziggy Dee (Uganda)
  • Nakupenda Mpenzi - Dudu Baya
  • get down - Prezo ft Naziz (Kenya)
  • Twenzetu - Chege
  • Baby Gal + wange - Mad Ice
  • Maria Salome - Saida Karoli
  • Kamanda + barua - Daz Nundaz
  • wanoknok + Taswira + dingi - Mandojo na domokaya
  • Picco - Kikongwe
  • Kwenye Chati - Balozi
  • Mtoto wa geti kali - Inspector Haroun
  • Elimu mtaani + sauti ya gharama - D knob
  • Mkiwa - K sal ft Ferooz
  • Salome + Julieta + Hi - Dully Sykes
  • Raha tu - AY
  • Mambo vipi - Mchizi Mox
  • Solid Ground Family - Bush party
  • Nini mnataka mazee- Pig black

Najua wengi mmekariri ni P Funk na Master J, na hata mimi nakubali linapokuja suala la kuwatoa wasanii wengi hawa jamaa hawana mpinzani hasa ukizingatia walivyokuwa na connections nyingi kwenye media, walisaidia kazi kibao za wasanii zitufikie na waliifanya kazi kama full time job iwe kazi yao rasmi. lakini kwa upande mwengine tunapomzungumzia Mika Mwamba hizo ni level nyingine na hata wao walijua, Mikka alikuwa na uwezo binafsi wa juu sana kwenye kubuni biti, alikuwa mtundu zaidi kwenye kucheza na vyombo kwa ubunifu ulioshangaza wengi.

Mzungu alikuwa ni Full Package ambae vitu vingi kwenye upande wa biti alikamilisha mwenyewe tofauti na kina Pfunk na Master J ambao waliwatumia wagonga beat wengi waliochangia idea na kutengeneza beats ila credit zikaenda kwa hao jamaa wawili. Mfano sehemu za vinanda wanamtumia bizzman, sehemu za gitaa wanamtumia mzungu kichaa, n.k. "She got a gwan" Gitaa ni Mzungu Kichaa, strings ni Bizz man, Kick zile ni Soggy Doggy, Majani kaja kumalizia mixing na mastering. Kwa upande wa Master J aliweza kuajiri kabisa watasha kama kina Ludigo na Said Comorie na walioandaa kazi kibao ila credit ikaishia kwa Master J.

Nimgusie pia Mkongwe Ludigo, huyu mtasha ndie kahusika kwenye ngoma kibao za hip hop zilizofanywa Bongo records na Mj Reecords, Ludigo hakuwa na Studio maalum ila mikono yake ipo kwenye hits kibao, pale bongo records kapika beats za Ngwea kama Mikasi, Kimya kimya, Aka mimi na Weekend, alihusika pia kwenye Mgambo ya juma nature, Aquelina ya Ocq ft Juma nature, kibanda cha simu ya Soggy, Bijou ya Dully sykes, kwa uchache tu. Kwa Master J ameandaa Album ya Wagosi, Album ya Mr Ebo , Mapacha, Fid Q na kina profesa Jay (ikiwemo Bongo Dsm) Kifupi Ludigo ndie alikuwa master mind wa ngoma kibao za hiphop ila ndio vile ngoma ikipikwa bongo records tunajua ni Majani na akifanya kwa MJ records sifa zote zinaenda kwa Master J

Tukija kwa upande wa kaka yao kiumri na kiuwezo Mika Mwamba huyu alikuwa ni next level na hata hao kina Pfunk na Master J walijua hilo, Ila tatizo ni kwamba Mika alikuwa hapendi kufahamika na ndio maana watu wengi hawakuweza hata kumfahamu kwamba ni mzungu kutokea Finland na sio raia wa Tanzania, hiyo yote ni kwasababu aliamua toka kitambo asionekane kwenye Media wala kupigwa picha, hakupenda umaaufu wala kufanya matukio ya watu kuanza kumfatilia, Interview aliyowahi kuifanya ni kwa millard ayo ipo Youtube ilikuwa 2017, hapo ni baada ya kukaa nje ya muziki mda mrefu sana.

Mika Mwamba alikuwa anakaa ulaya na bongo, anaweza akaja bongo akakaa miezi sita anapiga kazi pale Fm Studio kisha anasepa kurudi kwao, alikuwa hakai sana hapa bongo. ilikuwa ni kumvizia + timing, yaani akija tu watakaompata ndio hao watarikodi nae na kiukweli waliobahatika walipiga mshindo.


Aliachana na mambo ya mziki kwa muda mrefu ila alijaribu kutest mitambo walau mara moja na akathibitisha uzoefu wake hauozi, ee bwana eeh!! Alitubless na mkwaju ulioenda shule - Mashaallah ya Chid Benz ft Mzee Yusuf.

Inasemekana kuna watu wenye roho zao mbaya kwa kushirikiana walileta figisu mpaka Mika Mwamba akasepa ili wao na studio zao wapate majina ila nao wakaishia kushuka zaidi.
 
Sikujua Eno mic ilitencenezwa Bongo

Ziggy D kakaa sana Bongo tangu yuko underground. Naweza kusema katoka kimuziki akiwa TZ . Japo anaimba kiganda lakini wabongo ndio wameanza kumfahamu kimuziki kabla ya waganda. Sasa hivi sijui yuko wapi, lakini mara ya mwisho kumwona alikuwa anapiga mishe Arusha.
 
Ziggy D kakaa sana Bongo tangu yuko underground. Naweza kusema katoka kimuziki akiwa TZ . Japo anaimba kiganda lakini wabongo ndio wameanza kumfahamu kimuziki kabla ya waganda. Sasa hivi sijui yuko wapi, lakini mara ya mwisho kumwona alikuwa anapiga mishe Arusha.
Sio marehemu kweli huyo,,?
 
Mwamba mkali sana, sema ndiyo hivyo industry ya muziki mara nyingi haiwapi credits producers wanaowapa samples maproducer wakubwa. Na siyo TZ tu, ni ulimwengu mzima.

Kuna jamaa wanaitwa Cubeatz, ni mapacha, wapo very lowkey lakini wameshiriki kuandaa zaidi ya 80% ya nyimbo za HipHop marekani kwa miaka sita iliyopita, lakini credits wanapewa maproducer wanaonunua samples kutoka kwa hawa jamaa.

Umefanya jambo la msingi sana kumpa heshima yake, jamaa anatengeneza mziki mzuri.
 
Back
Top Bottom