MIGONGANO YA KIFIKRA: Kujinyonga - "Ajinyonga Kwa Udanganyifu Katika Mitihani " | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

MIGONGANO YA KIFIKRA: Kujinyonga - "Ajinyonga Kwa Udanganyifu Katika Mitihani "

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Steve Dii, Oct 12, 2007.

 1. Steve Dii

  Steve Dii JF-Expert Member

  #1
  Oct 12, 2007
  Joined: Jun 25, 2007
  Messages: 6,416
  Likes Received: 67
  Trophy Points: 145
  WanaJF, sijui mnazichukuliaje hizi habari za mwanafunzi kujinyonga? Hisia zangu kwa kweli baada ya kusoma tu hii habari zilikuwa za masikitiko, na ni maombi yangu Mwenyezi Mungu Amlaze Pahala Pema Peponi. Lakini pia hisia nyingine zilizo nijia moja kwa moja ni zile za viongozi wabadhirifu na mafisadi na uwajibikaji wao.

  Naomba usome kwanza hii habari hapa chini:

  Source: HabariLEO.

  Sasa ndugu zangu lile ambalo ningependa kuuliza ni kuwa;
  --Je, huyu kijana amekufa kishujaa au kinyonge?!

  --Je, kujinyonga baada ya kughafirika ki aibu ni kitu cha kutetea?!

  --Je, kijana huyu alivyofanya ni sawa na kujitoa mhanga?!

  Pia kuna habari kama ifuatayo:
  Pia kuna hii ya CEO Uchina:
  Pamoja na kuwa hata huko kwenye nchi zenye corporate responsibility ya hali ya juu kabisa matukio haya kuwa nadra, siishi kujiuliza: Is there a way out?!

  I don't understand how commiting suicide can rectify a situation, but again, you cannot really fit yourself in the shoes of a desperate and guilty person. Anyhow, to me, commiting suicide may seem to be the honourable way out by many, but it does not fix the situation that is left behind.

  Kwa sisi walalahoi, is this a means of escaping one's individual misery and wretched life or a way of rejecting completely the miserable and wretched social conditions and society one lives in?!

  Lakini kuna lile la kujitoa mhanga kama linavyotokea Mashariki ya Kati kila mara; is suicide a way of saving face, gaining honour and redemption for oneself and one's family and associates?!

  But even troubling, je baadhi ya wanasiasa wetu wengi wanaotajwa na wengi wanaojijua kuwa wameshiriki katika matendo ya kiuhujumu uchumi wafuate mfano wa huyo kijana huko Msoma kwa aibu wanazo zipatia familia zao na jamii zao kiujumla?!

  SteveD.
   
 2. Dua

  Dua JF-Expert Member

  #2
  Oct 12, 2007
  Joined: Nov 14, 2006
  Messages: 2,481
  Likes Received: 26
  Trophy Points: 135
  SteveD

  Naona viongozi wetu wengi bongo wanashangaa haya kwa sasa lakini yanakuja Tanzania kwa kasi kama umeme.
   
 3. Idimi

  Idimi JF-Expert Member

  #3
  Oct 12, 2007
  Joined: Mar 18, 2007
  Messages: 10,222
  Likes Received: 2,086
  Trophy Points: 280
  Huu mgongano ni mgumu kuutolea maamuzi! Lakini hebu tuchambue hoja ya kujinyonga hatua kwa hatua. Mimi naanza hivi:-
  Ni kweli kuwa huwezi kuwa katika mawazo ya yule anayejinyonga, kwamba anajisikiaje, hasa kujua kama anawajibika kwa kitendo chake ama kama anakwepa wajibu. Lakini mimi nadhani kuwa kujinyonga ni sehemu ya kukwepa kuwajibika kwa yale uliyotenda, ingawa ni ukatili na wala nisingependa mtu ajinyonge. Kwa mantiki hii, mimi nadhani kuwa kama mtu anajitoa uhai wake mwenyewe, atashindwaje kutoa uhai wa mwingine? (kumwajibisha). Mitazamo ya jamii na vyombo vya haki kama mahakama kuhusu wakosefu huweza kumsababishia mtu ajinyonge (humwajibisha kisaikolojia). Kwa mfano, mtu kama alibaka na akakamatwa na anajua kuwa kuna ushahidi wa kumtia hatiani, anaweza kujinyonga kwa kuogopa kwenda kukaa jela kwa maisha yake yote yatakayosalia hapa duniani baada ya hukumu, kwa hiyo kama anafahamu ama kasikia kuhusu mateso ya jela hatakuwa tayari kwena kuteseka. Mtuhumiwa huyu huyu wa ubakaji naweza pia kujinyonga kwa kuogopa aibu ya kuzomewa katika jamii kwa kitendo chake cha kinyama. Je anakwepa wajibu ama anawajibika?
  Mtu X anatokea na kumpiga mwenzake Y, huyu mwenzake anazirai! Kwa kutojua, jamaa X aliyempiga mwenzie Y anajinyonga, kwa kuhisi kaua, kwa hiyo nae huenda akahukumiwa kunyongwa! Huyu anawajibika ama anakwepa wajibu?
  Hali kadhalika, tumeshasikia mara kadhaa waathirika wa ukimwi wakijinyonga, ama kwa kuogopa unyanyapaa ama kwa kuogopa mateso yatokanayo na ukimwi. Wanakwepa wajibu ama wanawajika?
  Tunafahamu kuwa kwa nchi kama China, kosa la rushwa hupelekea mtu kunyongwa kama atakutwa na hatia. Sasa hapa mtu anakwepa wajibu ama anawajibika?
  Hata hivyo, wataalamu wa saikolojia wanasema kwamba, mtu anapokabiliwa na matatizo makubwa, uwezo wa kufikiri hupungua sana, na mara nyingi anakimbilia njia za mkato, ambazo hata hivyo hazitoi utatuzi wa kudumu wa shida za mhusika. Mnasemaje?
  Naomba tuendelee kulumbana kuhusu kujinyonga.
   
 4. Steve Dii

  Steve Dii JF-Expert Member

  #4
  Oct 12, 2007
  Joined: Jun 25, 2007
  Messages: 6,416
  Likes Received: 67
  Trophy Points: 145
  Dua ahsante, lakini je, yanakuja kwa kasi kutokana na ugumu wa maisha au uwajibikaji (kukua umetenda kosa hivyo kujinyonga)?!

  SteveD.
   
 5. Steve Dii

  Steve Dii JF-Expert Member

  #5
  Oct 12, 2007
  Joined: Jun 25, 2007
  Messages: 6,416
  Likes Received: 67
  Trophy Points: 145
  Mtupori, ahsante kwa maelezo yako, lakini hilo swali lako juu naona ni gumu tu zaidi, maana ukishalijibu itabidi uingilie mambo ya euthanasia pia. Labda nisubiri tu maelezo ya wengine...

  SteveD.
   
 6. Idimi

  Idimi JF-Expert Member

  #6
  Oct 12, 2007
  Joined: Mar 18, 2007
  Messages: 10,222
  Likes Received: 2,086
  Trophy Points: 280
  sawa Steve, labda tusubiri mawazo ya wengine. Ila tuna mengi ya kujifunza katika suala zima la kujitoa uhai, iwe kwa kujinyonga kwa kamba, kujisababishia ajali, kunywa vidonge nk.
   
 7. Quemu

  Quemu JF-Expert Member

  #7
  Oct 13, 2007
  Joined: Jun 27, 2007
  Messages: 986
  Likes Received: 69
  Trophy Points: 145
  Good topic Steve.

  In my opinion, commiting suicide is what seem to be aftermath of crying for help for quite sometime. Usually, one, who ends up commiting such act, has helplessly try to seek rescue from the society. Each human being has demon(s) within. So when our demons try to take contol of our soul/energy, that is when we cry for help. However, the problem arises when the society is either not listening or ignoring our cry for help. When it gets to that point, that is when one's demon is succeeding in taking control of the soul/energy. As a result, whatever that demon decides to do, is going to happen...

  Sasa tukiangalia hili tukio la kijana mwanafunzi wetu:

  My take
  Ukisoma kwa makini hofu yake utagundua kuwa pengine demons wake walikuwa wanamvuruga/wanamtia uoga sana katika maandalizi yake ya mtiani huo. Huwezi jua, pengine alishawasilisha matatizo ya upeo wake wa kuelewa masomo kwa walimu au wanafunzi wake kwa nia ya kuomba msaada, lakini either hawakumtilia maanani au hawakuelewa tatizo lake lilikuwa ni nini. Matokeo yake, demons wake wakaiteka nafsi yake...
   
 8. Steve Dii

  Steve Dii JF-Expert Member

  #8
  Oct 13, 2007
  Joined: Jun 25, 2007
  Messages: 6,416
  Likes Received: 67
  Trophy Points: 145
  QM, thanks a lot for your good shot,

  However, I have another concern brought about by your very expression above. The issue of demons, don't you see that this is rather another broad subject that some of us believe in and some don't?! Or in your opinion, is this thing for really (phyiscal) or is it a mere kind of 'thought forms'?!

  Personally, I somewhat believe in 'thought forms' type of demons, just like your example above in red, they are mere personifications of concepts like fear, rage, desire/lust, envy and other emotions that someone would like to cast out of themselves.

  Na nikikubaliana na hiyo form ya demons, basi kama unavyosema labda huyo kijana wa Musoma alikumbwa na hii type... tatizo swali lipo pale pale, ni kufa kishujaa au kinyonge?

  (naomba kuto limit aina za hiki kifo, kama kuna khali nyinginezo zaidi ya ushujaa au unyonge naomba mtu aongezee).


  SteveD.
   
 9. Mbu

  Mbu JF-Expert Member

  #9
  Oct 13, 2007
  Joined: Jan 11, 2007
  Messages: 12,729
  Likes Received: 187
  Trophy Points: 160
  --Je, kujinyonga baada ya kughafirika ki aibu ni kitu cha kutetea?!
  --Je, huyu kijana amekufa kishujaa au kinyonge?!
  --Je, kijana huyu alivyofanya ni sawa na kujitoa mhanga?!


  `

  Labda tuangalie makundi matatu kwanza ya watu wanaoamua kujiua;

  1. Kundi la mwanzo linahusisha wanaojiua kwa sababu ya kumuumiza/kumkomoa mtu mwingine mfano mzazi wake, mpenzi'we, rafiki'ye nk kwa matarajio kitendo chake hicho 'huenda' kitamsononesha maisha yote huyo alomkusudia kwa kujilaumu na kulaumiwa na jumuia, nk.

  --Je, kujinyonga baada ya kughafirika ki aibu ni kitu cha kutetea?!
  Hapana, si la kutetea; ila la msingi tukumbuke kwamba mara nyingi wanaokuwa na tendency za kujidhuru, iwe kutishia kujiua, kujiunguza na sigara ama kujikata kata na visu, ama kujiua kweli, iwe kwa kusaga chupa, kujinyonga ama kunywa sumu nk, hawa wote wana hitilafu fulani katika ubongo. kwa maana nyingine ni, wenye tabia hii hurudia rudia kauli zao mpaka pale wanapotimiza azma yao hiyo. Kubwa panahitajika mental health consultancy ili kuweza kuwafariji na kuwapa nasaha za kuboresha fikra za watu wenye tendecy hizo.

  2.Kundi la pili ni wale wanaoamua kujiua ama kutokana na maradhi ya muda mrefu pengine yasokuwa na tiba, (yakiwemo UKIMWI, Akili na ulemavu) , ulevi kupita kupindukia, utumiaji wa madawa ya kulevya nakadhalika, na walokumbwa na depression, kiasi kwamba hawaoni njia nyingine yeyote ya kujitoa katika matatizo hayo ila kwa njia hiyo ya mkato, na kwa kudhani hivyo wanauhakika kifo hakitaacha pengo lolote kwa jamii husika.

  --Je, huyu kijana amekufa kishujaa au kinyonge?!
  Kinyonge; kwa mtazamo wa 'hadithi' yenyewe,Hatuwezi jua msukumo ulompelekea kufikia uamuzi wa kutumia mlungula ili tu aweze kufaulu mtihani wake huo, kiasi kwamba hata alipokamatwa alionelea bora tu kujiua kuliko hatma ya kufutiwa mitihani yote baada ya kubainika na majibu ya mtihani.

  3. Kundi jingine ni wale ambao wanaona hawana budi kujitoa mhanga kwa ajili ya watu wengine, hawa ni wale wenye mitizamo ya kidini zaidi mfano wanaopigania haki zao kwa mujibu wa itikadi zao za dini mfano; Budha's Monks, Religious Extremists, nk... na kisiasa; mfano wale wanaotetea maslahi ya kundi, nchi au sehemu fulani dhidi ya utawala wa kikandamizaji toka tabaka fulani la watawala mfano Extremists Sikhs walomuua Rajiv Gandhi, au 'Kamikaze Pilots' wakati wa vita vikuu vya dunia).

  --Je, kijana huyu alivyofanya ni sawa na kujitoa mhanga?!
  Hapana, sidhani kama kwa sababu tu amekamatwa na mlungula na kufukuzwa kwenye chumba cha mtihani ni sababu tosha ya kuamua kujitolea mhanga, kwani kosa linamuelekea yeye mwanafunzi.
   
 10. Idimi

  Idimi JF-Expert Member

  #10
  Oct 13, 2007
  Joined: Mar 18, 2007
  Messages: 10,222
  Likes Received: 2,086
  Trophy Points: 280
  Samahani kwa makala ndefu, lakini tuendelee na uchambuzi wa hoja hii ambayo inaleta sana utata katika jamii zetu. Angalia sababu za watu hao kujinyonga, nimeziwekea wino mweusi sana makusudi kuonyesha msisitizo.
   
 11. Mbu

  Mbu JF-Expert Member

  #11
  Oct 13, 2007
  Joined: Jan 11, 2007
  Messages: 12,729
  Likes Received: 187
  Trophy Points: 160
  -Kuchoshwa na maradhi yanayomsumbua'
  -Kuchoshwa na maisha, kukata tamaa ya maisha, mzigo wa madeni...nk...

  ...Hivi, depression kwa kiswahili sanifu/tafsiri yake ni nini?
   
 12. Idimi

  Idimi JF-Expert Member

  #12
  Oct 14, 2007
  Joined: Mar 18, 2007
  Messages: 10,222
  Likes Received: 2,086
  Trophy Points: 280
  Niweke wazi kuwa sina uhakika na tafsiri ya neno depression kwa kiswahili, ila kuna neno linaitwa msongo wa mawazo ambalo mara nyingi watu hupenda kulitumia kumaanisha kitu kama depression. Labda Steve atusaidie tafsiri hii.
   
 13. Mbu

  Mbu JF-Expert Member

  #13
  Oct 14, 2007
  Joined: Jan 11, 2007
  Messages: 12,729
  Likes Received: 187
  Trophy Points: 160
  Depression

  -Persistent sad, anxious, or "empty" mood
  -Feelings of hopelessness, pessimism
  -Feelings of guilt, worthlessness, helplessness
  -Loss of interest or pleasure in hobbies and activities that were once enjoyed, including sex
  -Decreased energy, fatigue, being "slowed down"
  -Difficulty concentrating, remembering, making decisions
  -Insomnia, early-morning awakening, or oversleeping
  -Appetite and/or weight loss or overeating and weight gain
  -Thoughts of death or suicide; suicide attempts
  -Restlessness, irritability
  -Persistent physical symptoms that do not respond to treatment, such as headaches, digestive disorders, and chronic pain

  ...na kwa kipengele hiki;...
  ...naweza jibu ifuatavyo;...


  ...Kwa mtazamo wangu, kuna uwezekano mkubwa wa mlipuko wa 'msongo huo wa mawazo' unawakumba wengi tu, ila Diagnosis ya kinyumbani (Tz) bado sana. Treatment na counselling yake haijaboreshwa, ndio maana matukio haya 'machache' yanayoripotiwa sasa yanaashiria kwa kiasi fulani huko tunakoelekea 'yatazidi'! (pia, iwapo hakutakuwa na 'ahueni' kwenye maisha ya mwananchi).
   
 14. K

  Kasana JF-Expert Member

  #14
  Oct 14, 2007
  Joined: Apr 3, 2007
  Messages: 414
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 35
  Depression pia inaitwa sonono.

  Diagnosis ipo wazi, nafikiri tatizo ni jinsi ya kutibu, kwani matibabu yake mengi yanategemea 'social welfare' pamoja na support ya community.
   
 15. Bubu Msemaovyo

  Bubu Msemaovyo JF-Expert Member

  #15
  Oct 15, 2007
  Joined: May 9, 2007
  Messages: 3,436
  Likes Received: 43
  Trophy Points: 145
  HAO WAMEFANYA HIVYO BAADA YA KUONA WANA HATIA NA HAWANA SABABU YA KUISHI, KWA VIONGOZI WETU WA SERIKALI YA TANZANIA NANI KATI YENU ANAWEZA KULIONA HILO, NANI KATI YENU WALA RUSHWA MAFISADI MNAWEZA KUONA THAMANI YA MAISHA YAMEKWENDA KWA SABABU TU YA WOGA KUITWA MLA RUSHWA HUYU MWANAFUNZI ALIONA AIBU KWANI AKIPITA MITAANI ATAITWA MGANDAMIZIAJI. WEWE KAMA KIONGOZI WA SERIKALI HUNA AIBU KUIKUMBATIA RUSHWA
   
 16. Mushobozi

  Mushobozi JF-Expert Member

  #16
  Oct 16, 2007
  Joined: Aug 20, 2007
  Messages: 543
  Likes Received: 14
  Trophy Points: 35
  pia watu huchukua uamuzi wa kujinyonga pale wanapojiridhisha wenyewe kuwa ulimwengu umewatenga na hivyo hauwataki tena.

  wakati mwingine hudhani kila wanayekutana naye anajua jambo walilolifanya, au kuwa anawakinai.

  hujiridhisha kuwa milele na milele hatatokea mtu wa kuwafariji na hivyo kuchukua uamuzi wa kukatisha maisha yao.
   
 17. Idimi

  Idimi JF-Expert Member

  #17
  Oct 16, 2007
  Joined: Mar 18, 2007
  Messages: 10,222
  Likes Received: 2,086
  Trophy Points: 280
  Heshima mbele wana JF kwa mada hii nzuri.
  Kasana, kama ulivyodai hapo, 'social welfare' ina nafasi yake kubwa sana katika maisha ya kawaida ya wanajamii. Tulishaliongelea hili katika mifano mada mama hapo juu, hasa tulipoangalia mifano ya matukio ya sababu za watu kujinyonga. Kwamba mtu anajihisi kama jamii imemtenga ama haimtendei vile anavyotaka. Maisha ya kibepari yanayosisitiza sana 'ubinafsi' ama 'kutotegemeana' yanasababisha vifo vingi vingi sana ktk nchi tajiri. Idadi ya watu wanaojiua kwa nchi zilizo na maendeleo ya juu ni kubwa mno kwa sasa kutokana na mfumo wa huu wa maisha.
  Kuna wazungu wanatamani maisha ya Afrika hata kama ni ya kimasikini. Kisa? Watu wanajuliana hali, wanasaidiana katika sida na raha wanajaliana. Katika nchi zilizoendelea, hasa Ulaya Magharibi, ukiwa na tatizo kama kufiwa ama kuishiwa, hilo ujue unajitwisha, kwani hakuna kushirikiana kama ilivyo kwa jamii nyingi za Afrika.
  Ndio hapa ambapo ummuhimu wa 'social integration' unapoonekana.
  Kwa hitimimisho langu, maisha ya kibepari ni mojawapo ya sababu za watu kujiua.
  Tuendelee kujadili, ningependa kupata mawazo kutoka kwa wenzangu kuhusu namna ya kukabili tatizo hili la watu kujiua.
   
 18. Gaijin

  Gaijin JF-Expert Member

  #18
  Oct 17, 2007
  Joined: Aug 21, 2007
  Messages: 11,850
  Likes Received: 57
  Trophy Points: 0
  kujinyonga kunaweza kutafsiriwa kutokana na historia ya pahala.

  kwa nchi kama Japani, kujinyong'a kwa kiongozi kunachukuliwa kama kitendo cha kishujaa. hii haikuanza leo wala jana, katika enzi za samurai, walipokuwa wakienda vitani na wakishindwa kulinda kile walichokiamini, badala ya kurudi kijijini na aibu ya kushindwa, walikuwa wakifanya 'harikiri' ambayo ni kujikata kwa upanga wako sehemu ya tumboni ili kujiuwa.

  samurai alikufa vitani na yule alikufa kwa kujiuwa mwenyewe wote walichukuliwa kama mashujaa katika jamii.

  historia hii imekuwa ikirithishwa vizazi hadi vizazi, na hadi sasa kwa japani, kujiuwa si jambo la ajabu sana.

  mtendaji wa serikali anaposhindwa moja kwa moja kutetea makosa yake, anaweza kuchukua hatua ya kujiuwa, ambayo haionekani kama mbaya kwa jamii

  mtoto wa kijapani anapojiuwa, jamii inasikitika kwa kukosa uhai wa mtoto yule, ila haishangai kwa kujiuwa huko, kwa vile anafata vitendo vya ma bibi na mababu zake

  tunapokuja kwa upande wa tanzania sasa
  sisi hatuna mila za namna hiyo. kujiuwa ni kosa na wala hakuna sehemu yoyote kitendo hicho kilipowahi kusifiwa.

  anaejiuwa, anatenda makosa kijamii, na kwa mawazo yangu, watanzania hujiuwa kwa kukosa mtu wa kumuhadithia matatizo yao.

  chukua mfano mtoto huyo, labda kwake yeye ameingiziwa akilini kuwa ni lazima apasi mtihani, apate kuendelea ili waweze kujikomboa kimaisha yeye na wazee wake. familia yake yote pengine inamtegemea kwa yeye kufaulu mtihani huo.

  kila mtoto na uwezo wake kisaikolojia, kwa mwengine ni jambo zito kisaikolojia kulikomnyima raha ya kufikiri na kutafakari, na hasa ukitazama hana wa kusema nae kuwa anahisi hawezi kufaulu kwa vile wazee wanamtegemea. baada ya kukamatwa na "kibomu" kwenye mtihani, anaona matumaini yake yameisha na ni aibu kwa wazee wake, anaamua kujiuwa.

  nafikiri kujiuwa kunatokana na ukosefu wa mtu wa kusema nae matatizo yako wakati matatizo hayo yanapokuwa mazito zaidi kwenye akili yako
   
 19. Steve Dii

  Steve Dii JF-Expert Member

  #19
  Oct 19, 2007
  Joined: Jun 25, 2007
  Messages: 6,416
  Likes Received: 67
  Trophy Points: 145
  Gaijin,
  Kwanza kabisa, ahsante kwa mchango wako. Kwenye hilo nililoweka wekundu, kama sijakosea, mbona nakumbuka kwenye historia yetu kuna mtemi (Mkwawa) alijiua ili asikamatwe akiwa hai na Wajerumani, na tendo hili kama jinsi vitabu vyetu vingi vya historia vilivyo andika ni tendo la kishujaa... au una maanisha jamii ya maisha ya hivi karibuni tu?! Ahsante.

  SteveD.
   
 20. Steve Dii

  Steve Dii JF-Expert Member

  #20
  Oct 19, 2007
  Joined: Jun 25, 2007
  Messages: 6,416
  Likes Received: 67
  Trophy Points: 145
  Mtupori, Ahsante sana kwa mchango wako.
  Kwenye wekundu hapo nami nakuunga mkono. Sababu alizoelezea mchongoma zifuatazo mojawapo naona inahusika na hilo:
  Wengi wanaojiua katika nchi zilizoendelea ambao hawaonyezi dalili nyinginezo za SONONO na wana maisha ya kuweza kuitwa 'matajiri', wanajiua kutokana na kujiona wamekamilisha yote maishani na hawana cha nyongeza 'bali kujaribu kifo'.

  Hebu fikiria uwemwanadamu uliyebarikiwa na kuwa na yote, (apart from hilo la kuondoa hisia za kujiua), unapesa, umefanya mapenzi utakavyo, umesafiri na kuona yote ulikopenda, kwenye Mwezi pia umeenda, kwenye space station pia umefika, kwenye chemichemi za maji baharini umefika, myth za aliens nazo unajua jibu lake, imani ya kidini nayo huna... kilichobakia nini hapa duniani?!

  SteveD.
   
Loading...