Steve Dii
JF-Expert Member
- Jun 25, 2007
- 6,402
- 1,254
- Thread starter
- #21
--Je, kujinyonga baada ya kughafirika ki aibu ni kitu cha kutetea?!
--Je, huyu kijana amekufa kishujaa au kinyonge?!
--Je, kijana huyu alivyofanya ni sawa na kujitoa mhanga?!
`
Labda tuangalie makundi matatu kwanza ya watu wanaoamua kujiua;
1. Kundi la mwanzo linahusisha wanaojiua kwa sababu ya kumuumiza/kumkomoa mtu mwingine mfano mzazi wake, mpenzi'we, rafiki'ye nk kwa matarajio kitendo chake hicho 'huenda' kitamsononesha maisha yote huyo alomkusudia kwa kujilaumu na kulaumiwa na jumuia, nk.
--Je, kujinyonga baada ya kughafirika ki aibu ni kitu cha kutetea?!
Hapana, si la kutetea; ila la msingi tukumbuke kwamba mara nyingi wanaokuwa na tendency za kujidhuru, iwe kutishia kujiua, kujiunguza na sigara ama kujikata kata na visu, ama kujiua kweli, iwe kwa kusaga chupa, kujinyonga ama kunywa sumu nk, hawa wote wana hitilafu fulani katika ubongo. kwa maana nyingine ni, wenye tabia hii hurudia rudia kauli zao mpaka pale wanapotimiza azma yao hiyo. Kubwa panahitajika mental health consultancy ili kuweza kuwafariji na kuwapa nasaha za kuboresha fikra za watu wenye tendecy hizo.
2.Kundi la pili ni wale wanaoamua kujiua ama kutokana na maradhi ya muda mrefu pengine yasokuwa na tiba, (yakiwemo UKIMWI, Akili na ulemavu) , ulevi kupita kupindukia, utumiaji wa madawa ya kulevya nakadhalika, na walokumbwa na depression, kiasi kwamba hawaoni njia nyingine yeyote ya kujitoa katika matatizo hayo ila kwa njia hiyo ya mkato, na kwa kudhani hivyo wanauhakika kifo hakitaacha pengo lolote kwa jamii husika.
--Je, huyu kijana amekufa kishujaa au kinyonge?!
Kinyonge; kwa mtazamo wa 'hadithi' yenyewe,Hatuwezi jua msukumo ulompelekea kufikia uamuzi wa kutumia mlungula ili tu aweze kufaulu mtihani wake huo, kiasi kwamba hata alipokamatwa alionelea bora tu kujiua kuliko hatma ya kufutiwa mitihani yote baada ya kubainika na majibu ya mtihani.
3. Kundi jingine ni wale ambao wanaona hawana budi kujitoa mhanga kwa ajili ya watu wengine, hawa ni wale wenye mitizamo ya kidini zaidi mfano wanaopigania haki zao kwa mujibu wa itikadi zao za dini mfano; Budha's Monks, Religious Extremists, nk... na kisiasa; mfano wale wanaotetea maslahi ya kundi, nchi au sehemu fulani dhidi ya utawala wa kikandamizaji toka tabaka fulani la watawala mfano Extremists Sikhs walomuua Rajiv Gandhi, au 'Kamikaze Pilots' wakati wa vita vikuu vya dunia).
--Je, kijana huyu alivyofanya ni sawa na kujitoa mhanga?!
Hapana, sidhani kama kwa sababu tu amekamatwa na mlungula na kufukuzwa kwenye chumba cha mtihani ni sababu tosha ya kuamua kujitolea mhanga, kwani kosa linamuelekea yeye mwanafunzi.
Mchongoma, Ahsante sana kwa maelezo yako.
Lakini hapo kwenye kijani, nikichukulia mfano mwingine wa 'sects' ambao hurubuniwa au kujirubuni na hivyo wote kujiua kama vile ilivyo wahi kutokea kule Amerika na hapa Africa (Uganda na Kenya kama sikosei); hawa wote nao wana kufa kinyonge au kishujaa ukihusisha imani yao?!
SteveD.