Migomo mashuleni

hilbajojo2009

Member
May 25, 2009
46
1
Migomo mingi imekuwa ikitokea katika shule na vyuo mbalimbali nchini. Hivi karibuni katika chuo kimojawapo cha ualimu baadhi ya wanachuo walichukua hatua ya kuwashawishi wanachuo wenzao wasipige kura ya kuchagua rais wa serikali yao; Msisitizo ulikuwa wanachuo wagome kupiga kura. Wanchuo hao walifanya mikutano isiyo halali usiku na kubandika mabango yenye maneno yanayochochea mgomo. Sababu inayotolewa ni kuwa wanachuo wanahitaji Demokrasia ya kuchagua viongozi wao bila kuingiliwa na wakufunzi. Inasemekana wanachuo hao walishindwa kutambua taratibu za uendeshaji uchaguzi ambazo zinataka wakufunzi kuwafanyia usaili wagombea na kupitisha majina ya wagombea.

Je taratibu za uchaguzi ndizo chanzo cha migomo katika shule za sekondari na vyuo? au kuna vyanzo vingine vya migomo? Je nini kifanyike ili migomo isitokea mashuleni?
 
Back
Top Bottom