Yoda
JF-Expert Member
- Jul 22, 2018
- 37,597
- 46,206
Kumekuwepo na mazoea au utamaduni wa muda mrefu wa waumini kuleta malalamiko hapa jukwaani kuhusiana na migogoro mbalimbali ambayo imakeuwa ikitokea hasa katika makanisa ya KKKT, Anglican na TAG.
Malalamiko haya sio hapa jukwaani tu bali hata katika mitandao mingine ya kijamii.
Malalamiko au migogoro hiyo mara nyingi huelezewa kuhusunia na kugombania vyeo, matumizi fedha na rasilimali nyingine, maadili na mambo yanayohusiana na siasa.
Kuleta migogoro ya makanisa mitandaoni au sehemu nyingine nje ya kanisa ni ujinga, ujuha na uwezo duni wa kufikiri. Kama kanisa ulilopo lina migogoro kwa nini msimalize wenyewe huko ndani ya kanisa washiriki na viongozi wenu husika ? Kama imeshindikana kabisa kufikia muafaka kwa nini msiachane na hilo kanisa mkaenda madhehebu mengine, kama hilo nalo ni gumu pia kwa nini msianzishe kanisa lenu wenyewe?
Tanzania ina uhuru mkubwa wa kiimani, mtu unaweza kuhamia dhehebu lingine au dini nyingine kabisa wakati wowote bila kikwazo. Pia Tanzania ni sehemu rahisi sana kuanzisha kanisa lako tofauti na nchi kama Rwanda, kama mnaona mnashindwana na wenzenu anzisheni kanisa lenu msiparuane na kulazimisha upande wenu mnaoona ni sahihi kwenu.