Migogoro ya makanisani kujaa mitandaoni au nje ya kanisa hakuna mashiko, ni tabia ya hovyo

Acha waweke madudu yao wazi
Wamepiga sana hela na wengine wamebadili kitega uchumi

Zamani kulikuwa hakuna utandawazi ndio maana mambo yakikuwa chini chini na yanafichwa ila sasa technology haifichi kitu na watu wamepevuka sio wale wajinga

Hela zinapigwa sana
IMG_4717.jpg
 
Acha waweke madudu yao wazi
Wamepiga sana hela na wengine wamebadili kitega uchumi

Zamani kulikuwa hakuna utandawazi ndio maana mambo yakikuwa chini chini na yanafichwa ila sasa technology haifichi kitu na watu wamepevuka sio wale wajinga

Hela zinapigwa sana View attachment 2164798
Kama kanisani kwako help zinapigwa acha kutoa sadaka au hamia kanisa lingine, hakuna haja ya kuleta vurugu na migogoro.
Huo ni ujinga mtupu
 
Migogoro chanzo ni ulaji,maslahi tu

Acha wararuane wakichoka wataacha

Ova
 
Na siku mkipunguza kwenda huko makanisani hamtosikia migogoro

Ova
 
Hata kabla ya kuwepo mfumo wowote wa utawala, wafalme, mafarao n.k dini ilikuewepo.

Dini ilikuwepo hata kabla binadamu hawajawa na utaratibu wa kukaa pamoja kama jamii ndogo inayoshirikiana.

Mtawala wa kwanza kabisa duniani ni Mungu muumba mbingu na nchi, yeye ndiye mfalme wa wafalme cheo ambacho ni cha kisiasa (utawala).

Kama nakuelewa vizuri, ukisema dini ilikuwako kabla ya siasa basi ijikite huko kwenye uumbaji na sio hizi porojo za kina Bagonza sijui Mwamakula.
 
Baada ya kutuvuna KWA muda mrefu fedha zetu Mungu kachukia kaamua kuwaumbua na kuwaponya watu wake KWA kuonyesha yeye hana njaa wala si omba omba kama wao wanaooomba pesa kea kivipi cha Mungu!!!
 
Kama kanisani kwako help zinapigwa acha kutoa sadaka au hamia kanisa lingine, hakuna haja ya kuleta vurugu na migogoro.
Huo ni ujinga mtupu

Hapana wao ndio wakatafute kazi za halali maana siku hizi wanapiga hata za sadaka
But I don’t care nachangia tu kama member humu ila hayanihusu acha wapigane tu kama wanaibiana

Humu tunatoa maoni tu haijalishi kama ni dini gani bali natoa maoni kutokana na tunayoyasikia tu
 
ITAMBUE DINI YA KWELI
1. upendo miongoni mwao, (viongozi na waumini)
2. Dini ya kweli haiungi mkono siasa... (iepuke kuruhusu kuwa wanachama wa chama fulani cha kisiasa)
3. Dini isiunge mkono vita. ( wazia UKRAINE vs RUSSIA). Kiongoz wa dini X Anaongoza ibada ukraine kuombea jesh lao likashinde. Dini X Pia ipo urusi, nayo inaombea jesh lake. Mungu ni mmoja? Atajibu sala ipi?
4. Dini ifundishe, ionye, na ikaripie kwa kutumia BIBLIA, Sio falsafa zao binadam...
JE? UPO DINI YA KWELI?
visit, www.jw.org/sw
Kwa hiyo unataka kusema kuwa
-Waumini na viongozi wa dini wasiteuliwe, wasigombee wala kupiga kura, maana yote hayo ni mambo ya siasa, na wewe hutaki wachika dini wasishiriki siasa.

-Washika dini wasijiunge na jeshi, maana kufanya hivyo ni kuunga mkono vita.

Hayo ni mawazo ya ajabu.
 
Ikiwa umewahi funua pazia la kisiasa ujue undani wake, hutaitetea... Mauaji, mateso na kusalitiana ni kawaida., . Kaa mbali nayo. Chama kimoja, vyama vingi, ujamaa, ubepari, vyote vimeshndwa kutatua matatizo ya binadamu,..Chanzo cha matatizo ya binadamu wa leo kipo waz
2TIMOTHEO 3:1~5
 
Kumekuwepo na mazoea au utamaduni wa muda mrefu wa waumini kuleta malalamiko hapa jukwaani kuhusiana na migogoro mbalimbali ambayo imakeuwa ikitokea hasa katika makanisa ya KKKT, Anglican na TAG.
Malalamiko haya sio hapa jukwaani tu bali hata katika mitandao mingine ya kijamii.

Malalamiko au migogoro hiyo mara nyingi huelezewa kuhusunia na kugombania vyeo, matumizi fedha na rasilimali nyingine, maadili na mambo yanayohusiana na siasa.

Kuleta migogoro ya makanisa mitandaoni au sehemu nyingine nje ya kanisa ni ujinga, ujuha na uwezo duni wa kufikiri. Kama kanisa ulilopo lina migogoro kwa nini msimalize wenyewe huko ndani ya kanisa washiriki na viongozi wenu husika ? Kama imeshindikana kabisa kufikia muafaka kwa nini msiachane na hilo kanisa mkaenda madhehebu mengine, kama hilo nalo ni gumu pia kwa nini msianzishe kanisa lenu wenyewe?

Tanzania ina uhuru mkubwa wa kiimani, mtu unaweza kuhamia dhehebu lingine au dini nyingine kabisa wakati wowote bila kikwazo. Pia Tanzania ni sehemu rahisi sana kuanzisha kanisa lako tofauti na nchi kama Rwanda, kama mnaona mnashindwana na wenzenu anzisheni kanisa lenu msiparuane na kulazimisha upande wenu mnaoona ni sahihi kwenu.
Ni ngumu sana kwa sasa kuthibiti taarifa kuvuja maana watu wanapenda sambaza taarifa na usambazaji umekuwa rahisi sana
 
ITAMBUE DINI YA KWELI
1. upendo miongoni mwao, (viongozi na waumini)
2. Dini ya kweli haiungi mkono siasa... (iepuke kuruhusu kuwa wanachama wa chama fulani cha kisiasa)
3. Dini isiunge mkono vita. ( wazia UKRAINE vs RUSSIA). Kiongoz wa dini X Anaongoza ibada ukraine kuombea jesh lao likashinde. Dini X Pia ipo urusi, nayo inaombea jesh lake. Mungu ni mmoja? Atajibu sala ipi?
4. Dini ifundishe, ionye, na ikaripie kwa kutumia BIBLIA, Sio falsafa zao binadam...
JE? UPO DINI YA KWELI?
visit, www.jw.org/sw
Hizi Sifa umezitoa wapi hasa?
 
Write your reply...
1. Waumini wa dini ya kweli hupendana, hawabaguani...(upendo)
YOHANA 13:35
2. Dini ya kweli haiungi mkono siasa...
YOHANA 18:36
3. Dini ya kweli haiungi mkono vita, . Haitaombea wanajeshi waendapo vitani..haitaruhusu waumin wake kuwa wanajeshi (askari)...wala kuhubiri waumini kushika siraha kulinda nchi

4. Dini ya kweli inategemea biblia kwa kufundisha, kukaripia, kuonya, kunyoosha mambo na kutia nidhamu. Sio falsafa za kibinadamu..
2timotheo 3:16,17
5.Waumini watamuabudu MUNGU Peke yake, sio vitu..watamtukuza MUNGU Sio mali, umaarufu au pesa
UFunuo4:11, mathayo 4:10
 
Hapa ndipo Kanisa Catholic linapojichukuliaga Sifa.

Migogoro ya hovyo uminywa ndani kwa ndani.

Ukiruhusu Demokrasia Kanisani Umekwisha.
 
Mbona harambee huwa mitandaoni,
Ibada na misa huwa mitandaoni,
Ujenzi wa makanisa na ofisi za chadema huwa mitandaoni,
 
Kumekuwepo na mazoea au utamaduni wa muda mrefu wa waumini kuleta malalamiko hapa jukwaani kuhusiana na migogoro mbalimbali ambayo imakeuwa ikitokea hasa katika makanisa ya KKKT, Anglican na TAG.
Malalamiko haya sio hapa jukwaani tu bali hata katika mitandao mingine ya kijamii.

Malalamiko au migogoro hiyo mara nyingi huelezewa kuhusunia na kugombania vyeo, matumizi fedha na rasilimali nyingine, maadili na mambo yanayohusiana na siasa.

Kuleta migogoro ya makanisa mitandaoni au sehemu nyingine nje ya kanisa ni ujinga, ujuha na uwezo duni wa kufikiri. Kama kanisa ulilopo lina migogoro kwa nini msimalize wenyewe huko ndani ya kanisa washiriki na viongozi wenu husika ? Kama imeshindikana kabisa kufikia muafaka kwa nini msiachane na hilo kanisa mkaenda madhehebu mengine, kama hilo nalo ni gumu pia kwa nini msianzishe kanisa lenu wenyewe?

Tanzania ina uhuru mkubwa wa kiimani, mtu unaweza kuhamia dhehebu lingine au dini nyingine kabisa wakati wowote bila kikwazo. Pia Tanzania ni sehemu rahisi sana kuanzisha kanisa lako tofauti na nchi kama Rwanda, kama mnaona mnashindwana na wenzenu anzisheni kanisa lenu msiparuane na kulazimisha upande wenu mnaoona ni sahihi kwenu.

Mkuu Yoda

Wewe inakuuma nini mkianikwa uozo wenu humu?

Mbona kwenye kutafuta waumini mnajitangaza kote kote na namba ya kutumia pesa mnatuma?

Je humu mitandaoni inawauma kwa sababu inawaharibia kwa wafadhili wenu huko nje ambao huwasaidia kwa nia nzuri bila kujua wanawafadhili Fisi?

Je huku mitandaoni hakuna waumini wanaopaswa kuhabarishwa kama raia wengine huko nje ya mitandao?

Mbona wanasiasa wao mnawatupia migogoro yao humu kila uchao?

Ni haki ya waumini kuhabarishwa kupitia njia zozote zile ikiwemo ya mitandaoni ili tujuwe maovu ya wale tunaoaminishwa kuwa ni wema na kutoa sadaka ili kulijenga kanisa,na wao wanadokoa ili kujenga mahekalu yao.
 
Kumekuwepo na mazoea au utamaduni wa muda mrefu wa waumini kuleta malalamiko hapa jukwaani kuhusiana na migogoro mbalimbali ambayo imakeuwa ikitokea hasa katika makanisa ya KKKT, Anglican na TAG.
Malalamiko haya sio hapa jukwaani tu bali hata katika mitandao mingine ya kijamii.

Malalamiko au migogoro hiyo mara nyingi huelezewa kuhusunia na kugombania vyeo, matumizi fedha na rasilimali nyingine, maadili na mambo yanayohusiana na siasa.

Kuleta migogoro ya makanisa mitandaoni au sehemu nyingine nje ya kanisa ni ujinga, ujuha na uwezo duni wa kufikiri. Kama kanisa ulilopo lina migogoro kwa nini msimalize wenyewe huko ndani ya kanisa washiriki na viongozi wenu husika ? Kama imeshindikana kabisa kufikia muafaka kwa nini msiachane na hilo kanisa mkaenda madhehebu mengine, kama hilo nalo ni gumu pia kwa nini msianzishe kanisa lenu wenyewe?

Tanzania ina uhuru mkubwa wa kiimani, mtu unaweza kuhamia dhehebu lingine au dini nyingine kabisa wakati wowote bila kikwazo. Pia Tanzania ni sehemu rahisi sana kuanzisha kanisa lako tofauti na nchi kama Rwanda, kama mnaona mnashindwana na wenzenu anzisheni kanisa lenu msiparuane na kulazimisha upande wenu mnaoona ni sahihi kwenu.
Umejaa tope la kisiasa kichwani chezea kitu ingine si imani.
Yesu mwenyewe Mwana wa Mungu mlimwuza kwa vipande 30 vya fedha!
 
BARAZA la Vijana wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania KKKT, Dayosisi ya Konde, limemtupia lawama Mkuu wa kanisa hilo nchini, Askofu Dk. Fredrick Shoo, likidai kuongoza mkutano wa kumwondoa Askofu wa dayosisi hiyo, Dk. Edward Mwaikali, badala ya kutafuta njia sahihi ya kumaliza mgogoro ....

[https://res]

unaofukuta.

Akisoma taarifa ya msimamo wa vijana wa dayosisi hiyo jana, Marko Mahenge, alidai Askofu Dk. Shoo amekuwa sehemu ya kukuza mgogoro huo badala ya kutafuta njia sahihi ya kujadili namna ya kushughulika na jambo hilo ambalo linaendelea kuyumbisha Dayosisi ya Konde.

Alisema kwa muda mrefu vijana walikuwa kimya wakifuatilia mwenendo ya mgogoro huo huku wakitarajia kufanyika kwa hekima na busara katika kushughulikia maridhiano ya kuhamisha makao makuu ya dayosisi hiyo kutoka mjini Tukuyu katika Wilaya ya Rungwe na kupelekwa Halmashauri ya Jiji la Mbeya.

“Sisi vijana wa Jimbo hili la Mbeya na maeneo mengine ya dayosisi hii tunapinga vikali uamuzi wa Mkuu wa Kanisa kumwondoa Askofu Mwaikali kwenye kiti chake kwa sababu mkutano uliofanyika Machi 22, katika Ushirika wa Uyole ulikuwa batili, tunamtambua Dk. Mwaikali kuwa ndiye askofu wetu na hapa jimboni haondoka wala mchungaji au Mkuu wa Jimbo,” alisema Mahenge.

Aidha, Mahenge aliliomba Baraza la Maaskofu wa kanisa hilo nchini kuingilia kati mgogoro huo kwa kuiita halmashauri kuu ya dayosisi na viongozi wengine ili kukubaliana mambo ya kufanya.

Akizungumza wakati wa ibada ya Jumapili katika Kanisa Kuu la Ruanda, yalipo makao makuu ya Dayosisi ya Konde, Mkuu wa Jimbo, Mchungaji Nyibuko Mwambola, alisema Halmashauri Kuu haitambui mkutano ulioitishwa na Askofu Dk. Fredrick Shoo kwa madai kuwa ulikuwa batili.

Alimtupia lawama Askofu Dk. Shoo kama mkuu wa kanisa kwa kushindwa kusuluhisha mgogoro huo na kuwa sehemu ya kuchochea hali ambayo alidai inazidi kuongeza chuki na mfarakano.

Kadhalika, alisema baada ya mkutano wa kumchagua askofu mwingine, Geofrey Mwakihaba, Askofu Dk. Shoo alituma waraka kwa taasisi zote za kifedha kufunga akaunti za dayosisi.

Alisema hatua hiyo imewasababishia kushindwa kufanya malipo yoyote ikiwamo mishahara ya wachungaji na watumishi wengine wa dayosisi hiyo.

Vile vile, alidai kuwa Dk. Shoo amewatumia barua wachungaji wote wa Dayosisi ya Konde kuhudhuria kikao kinachofanyika kesho jijini Dodoma, bila kumpa taarifa Askofu wa Jimbo Dk. Mwaikali, na kwamba Halmashauri Kuu imesema naye atashiriki kikao hicho.

“Mkuu wa Kanisa ameonyesha dhahiri upande alipo kwa sababu ameshindwa kutukutanisha pamoja viongozi wa dayosisi na kujadili pamoja namna bora ya kumaliza huu mgogoro badala yake ameonesha wazi kushindwa kusimamia jambo hilo na kuchangia kuchochea suala hili, sisi tunamtambua bado Askofu Mwaikali ndiyo anasimamia dayosisi yetu ya Konde,” alisisitiza.

“Haiwezekani Mkuu wa Kanisa aitishe mkutano na kufanya uchaguzi wa kumchagua askofu mwingine, tena kwa siku moja, inaonyesha dhahiri kuna chuki binafsi na sio suala la kuhamisha makao mkuu ya dayosisi.”

Machi 22 mwaka huu Mkuu wa Kanisa la KKKT nchini, Askofu Dk Fredrick Shoo, pamoja na wajumbe 201 walifanya mkutano katika Usharika wa Uyole jijini Mbeya kwa lengo la kumaliza mgogoro huo ambapo liliibuka suala la wajumbe kutokuwa na imani na Askofu Dk. Edward Mwaikali.

Katika mkutano huo ambao uliendeshwa na Askofu Dk. Shoo na kudumu kwa saa 10, ulitumika kumchagua Askofu mwingine Mchungaji Geofrey Mwakihaba, ambaye alitangazwa mbele ya wajumbe wa mkutano.

Kutokana na uamuzi huo baadhi ya vijana wa KKKT mkoani Mbeya walieleza kuwa mchakato uliotumika kuwa ulikuwa batili.

Hata hivyo, Askofu Dk. Shoo alipotafutwa na Nipashe kwa simu jana, muda wote hakupatikana kuzungumzia suala hilo.

Mgogoro wa kwanini yahamishwe makao makuu ya dayosisi kutoka mjini Tukuyu katika Wilaya ya Rungwe na kwenda Halmashauri ya Jiji la Mbeya, ulianza kufukuta tangu mwaka 2017 hadi sasa.

Back
Top Bottom