Migodi ya dhahabu ya ushirombo shinyanga kumirikiwa na ridhiwani au kikwete kuna dhambi gani?

DUNIANGUMU JR

Member
Apr 20, 2011
43
14
Rais mkapa alifanya biashara akiwa ikulu ingawa alikatazwa na baba wa taifa mwalimu nyerere, akauza nyumba za serikali kwa wahindi kwa bei poa huku akiweka 10% mifukoni, ameuza mashirika ya umma, naye akanunua kiwira kwa bei poa, sasa rais wa sasa hivi na kijana wake wanamiriki migodi ya dhahabu kule shinyanga, je kuna ubaya gani kama wakimiriki? mbona Mkapa ana kiwira?
 
hakuna ubaya wowote; lakini kwa nchi kuongozwa na viongozi wa namna hii walalahoi wa Tanzania watakiona cha moto.

tuendelee kusubiri fulana, kofia na viremba.
 
Kikwete alisema yeye hajui kufanya biashara ila anajua kulima analima mananasi kule Bagamoyo.

Leo biashara ya dhahabu kaijuaje, au ndiyo matokeo ya ugeni wa Sinclair aliyofanya pale Ikulu mwaka 2006 na ku-mute kelele zote za Kikwete za kutaka kupitia mikataba ya madini upya.

Kumbukeni kuwa viongozi dhalimu huisha kwa udhalimu pia. Inaonekana Kikwete atakuwa anawazidi kwa udhalimu wote waliomtangulia hapa Tanzania
 
kama Mkapa na wanawe wanamiriki kiwanda cha kiwira hii ni moja ya sera za biashara kutoka marais wa CCM wakiwa ikulu tofauti na baba wa taifa alivyowaonya
 
Hili jukwaa si la kujadili threads zisizo na mashiko wala vina, jirekebishe na jiepushe na huu ufasta fasta!
 
Mod futa hii topic, ni Diblicate au bado unajivua gamba?
 
Hamna shida...ni baraka tupu kwa waTanzania...sawa na tulivyopata wenye magamba kua viongozi wetu!
 
Zamani tulikuwa na kanuni ya "sitatumia cheo changu kujitajirisha." Ukitaka kujua ubaya wa Kikwete na mwanae kumiliki migodi ya dhahabu baada ya Kikwete kuingia Ikulu ni hiyo ya kutumia cheo cha rais kujitajirisha yeye na familia yake. Kama hilo ni poa tu kwa Watanzania basi tuanze mjadala mwingine.
 
Du kweli binadamu wote ni vichaa ila ukichaa wetu unatofautiana.Upo juu kwa mawazo mgando.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom