Hii ndiyo tofauti ya Kikwete na Magufuli

Interest

JF-Expert Member
Apr 11, 2015
3,434
7,055
KUMEKUWA na kiu kubwa ya kumlinganisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. John Pombe Magufuli na mtangulizi wake, Dk. Jakaya Mrisho Kikwete. Kwamba nani ni nani? Si kwa hoja ya kimaumbile kuwa JK ni mrefu na mweupe wakati Magufuli ni mweusi na mfupi, la hasha!

Haiangaliwi mantiki ya kifamilia, kwani inaeleweka JK mkewe ni Salma na Magufuli wake ni Janeth. Hatupo huko, hapa kinachozungumzwa ni uongozi wao.

Kosa la kimsingi ni kutafsiri matokeo ya mafanikio ya sasa kama makosa au udhaifu wa serikali iliyopita.
Watanzania wamekuwa wepesi kuhukumu. Wazuri mno katika kushabikia michakato. Halafu hukumu zinakuwa za jumla mno.

Usimlaumu JK kama huwezi kuchanganua mtindo wake wa uongozi. Usimsifu tu Magufuli ikiwa hujatambua anatumia aina ipi ya uongozi. Na usipende kuongozwa na hoja za jumla (general), penda kushika kitu halisi (be realistic). Ni kwa kutambua vizuri mtindo wa uongozi ambao JK aliutumia ndiyo utaweza kubaini makosa ambayo yalifanyika, vilevile utaweka tahadhari kuhusu mwenendo wa Magufuli, kwamba asipokuwa makini wapi ataanguka.

Kuna dhana nne za uongozi. Ukizielewa hizo itakurahisishia kutambua nani ni kiongozi mzuri, anapatikanaje, kipi kinaweza kumfanya mtu kuwa kiongozi mzuri na chanzo kinachoweza kumpa nguvu kiongozi.

Dhana ya hulka (trait theory); Hii inachambuliwa katika Sayansi ya Siasa (Political Science) kama moja ya vigezo vya kutambua aina ya kiongozi. Ndani ya somo la saikolojia, inatafsiriwa kama kipimo cha kung?amua hulka, hisia, fikra na uhusika wa kiongozi. Katika dhana hii, kinachoangaliwa ni aina gani ya mtu anaweza kuwa kiongozi mzuri.

Dhana ya kitabia (behavioral theory); Je, kiongozi ana mwenendo gani kitabia? Kiongozi mzuri anafanyaje mambo yake? Katika dhana hii ndipo ambapo unaweza kung'amua nyenendo za viongozi. Katika dhana hii ndipo utaweza kuona tofauti ya JK wa 2005-2015 na Magufuli 2015-2020 au mpaka 2025, vilevile tutawamulika na watangulizi wao. Nakuomba twende pamoja.

Dhana ya dharura (contingency theory); Kwamba hajulikani kitabia na hakuna mwenye kutambua atakwenda kufanya nini, yaani hatabiriki lakini anapitishwa kwenda kushika hatamu. Anayepatikana kupitia dhana hii, matokeo chanya hushangaza zaidi kuliko hasi. Na zaidi, mazingira ndiyo yanaweza kusababisha kiongozi aonekane mzuri. Kupitia dhana hii nitaeleza jinsi Magufuli anavyong'ara kama ilivyotokea kwa Rais wa Awamu ya Tatu, Benjamin Mkapa alivyong'ara mwaka 1995.

Dhana ya nguvu na ushawishi (power and influence theory); Kama Waziri Mkuu wa zamani, Edward Ngoyai Lowassa, angeshinda urais mwaka huu, angekuwa amebebwa na dhana hii. Dhana hii pia ndiyo iliyomuingiza JK mwaka 2005. Kwamba mtu anakuwa na mtandao mkubwa wenye nguvu na ushawishi kiasi kwamba inakuwa vigumu kumzuia.

Kuhusu dhana ya dharura inavyombeba Magufuli kama ilivyotokea kwa Mkapa, ni mazingira ambayo wahusika waliyakuta.
Magufuli ameikuta nchi ikiwa na nidhamu mbaya ya matumizi ya fedha na udhibiti wa rasilamali za umma. Kuingia kwake na kasi kubwa ya kudhibiti matumizi mabaya ya fedha za serikali, kuahirisha shughuli zenye kutumia fedha nyingi kinyume na kipaumbele cha wananchi pamoja na kushughulikia ufisadi, vimemfanya ang'are kwa haraka mno.

Magufuli pia amerejesha nidhamu ya utumishi wa umma. Sasa mfanyakazi serikalini anatambua maana ya kuwajibika, kwani asipofanya hivyo anakuwa jipu.

Mkapa alikuta nchi watu binafsi walikuwa na uwezo mkubwa kuliko serikali. Akarejesha meno serikalini, akawabana wafanyabiashara na kukusanya kodi vizuri, akajenga miundombinu, akatanua wigo wa soko huria na kadhalika. Mkapa akaonekana malaika!

Ndani ya dhana ya kitabia ndipo unaweza kuiona tofauti ya kiuongozi kati ya JK na Magufuli. Mwanasaikolojia wa Kijerumani, hayati Kurt Zadek Lewin, aliwahi kuandika aina tatu za viongozi ambao wanaweza kupatikana kutokana na tabia zao.

Kiongozi anayetaka lake litimie (autocratic leader); Huyu wakati mwingine hutafsiriwa kama kiongozi wa kiimla. Si mwenye kutaka sifa, anachokifanya ni kutimiza maono yake tu. Watu wamchukie lakini dhamira yake itimie. Hapa ndipo unapoweza kumuona Magufuli.

Kiongozi mwana demokrasia (democratic leader); Kiongozi ambaye hafanyi mambo yake peke yake. Anashirikiana na timu yake kupanga na kutekeleza mipango ya kila siku. Huyu ni kiongozi ambaye anawaamini mno wasaidizi wake. Anawaacha wenzake waamue na kutekeleza majukumu yao ya kila siku kwa uhuru mkubwa. Na yeye binafsi hatendi mpaka yawepo makubaliano ya kitimu. Hapa ndipo unamuona JK.

Kiongozi mtegemea wasidizi (laissez-faire leader); Wasaidizi wanakuwa wanafanya kazi kubwa na wenye nguvu kuliko kiongozi mkuu. Yaani rais wa nchi anakuwa kubwa jinga (figure head) kwa sababu watu wake wanaweza kufanya chochote pasipo yeye kutia neno.

Tanzania hatujawahi kuwa na rais kubwa jinga. Wote pamoja na makosa ya hapa na pale, wamesimama vizuri kama marais na viungo muhimu (key figures) wa nchi kila mmoja kwa zama zake. Sababu ya kutegemea wasaidizi inaweza kutokana na uvivu wa kiongozi mkuu au uwezo mdogo alionao, kwamba wasaidizi wanakuwa na uwezo mzuri kiutendaji kuliko yeye, kwa hiyo anaona bora awape uwanja mzuri wa kutenda.

Ukiachana na aina hizo tatu za viongozi kama zilivyoletwa na Lewin mwaka 1930, katika somo la uongozi, wanatajwa viongozi aina sita.

Kiongozi mmbeba mamlaka yote (authoritarian), na ndani yake ndimo unaweza kumpata mwenye kutaka lake tu (autocratic). Rais anataka kila jambo lipate usimamizi wake wa karibu na aone matokeo. Magufuli yupo hapa!

Aina nyingine ya kiungozi ambayo Magufuli anakwenda nayo ni kuwa kiongozi mleta mabadiliko (transformational), kwamba habanwi na wasaidizi wake kuamua na kupanga kile ambacho yeye anaona kinafaa. Kwa kawaida kiongozi anayefanya mambo yake kwa mitindo hiyo miwili, ndani yake huongozwa na hali ya kutoamini mtu, kwamba wakati wowote wanaweza kumsaliti kwenye harakati zake za kutimiza malengo aliyojiwekea.

Faida kubwa katika mitindo hiyo miwili ni kwamba kisiasa, kama kiongozi mkuu anakuwa na utashi wa kweli wa kuwahudumia wananchi wake na kuwapa matokeo yenye kuonekana, huutikisa mfumo wote ili utende kama yalivyo matakwa yake. Ona Magufuli anavyotikisa hivi sasa.

Hasara za mitindo hiyo ni kuwafanya viongozi wa nchi waishi kama maroboti. Hawatajiamini na kufanya kazi kwa sura ambayo wanaona ni bora, wao wanajielekeza katika kumfurahisha kiongozi mkuu. Zaidi hawaishi kama viongozi, wanatenda tu mawazo ya kiongozi mkuu. Yaani wanakuwa watu wa kupokea maagizo na kufanya jinsi kiongozi wao anataka. Wanakuwa wazee wa 'kukopi' na 'kupesti'.

Na kwa sababu serikali ni taasisi kubwa, husababisha baadhi ya mambo ambayo siyo kipaumbele cha kiongozi mkuu kudumaa, wakati yangeweza kufanyiwa utekelezaji na viongozi wa chini kama wangekuwa huru na wenye kutimiza majukumu yao ipasavyo.

Ifahamike kuwa mifumo ya uongozi, kifaida na kihasara huzalishwa na saikolojia. Watendaji wa chini wanaweza kufanya mambo yao kama watu wasio na akili zinazojitegemea. Wanategemea akili za mkuu.
Kama kiongozi akiwa na haiba pendwa (charismatic leader), inaweza kuwasisimua na wasaidizi wake kujituma, kwani nao wanakuwa wanavutiwa naye kiuongozi na kitabia.

Aina hizo za uongozi, wakati mwingine huzaa kiongozi wa kiimla (dictator), hivyo kupitiliza na kuwafanya wasaidizi wake kumuogopa. Yaani badala ya kufanya kazi kulingana na mahitaji yao ya kiuongozi, wanakuwa watekeleza majukumu kwa hofu. Wakipigiwa simu na bosi mkuu, wanatetemeka kwa sababu hawajui wataambiwa nini.

Mafanikio ya Magufuli ndani ya muda mfupi ni kuwa nchi ilikuwa tenge. Watumishi wengi wa umma walikosa Utanzania, kwa hiyo wao wenyewe wakawa wahujumu uchumi badala ya kujenga uchumi. Kiongozi kama baba wa familia (paternalistic). JK na Magufuli kama ilivyokuwa kwa watangulizi wao, ni vichwa vya serikali na uhusika wao unaonesha hivyo.

Hata hivyo, mafanikio ya kiongozi wa aina hii husababishwa na hulka binafsi na aina ya watu ambao anafanya nao kazi. Akiwa kiongozi mwana demokrasia, anahitaji watu waaminifu, wachapakazi na wakweli mno. Kama watu ambao kiongozi anafanya nao kazi wakiwa siyo waaminifu, waongo na wavivu, kiongozi wa mtindo wa demokrasia kama alivyokuwa anakwenda nao JK ni vigumu mno kupata mafanikio stahili.

JK katika mtindo wake wa kidemokrasia, alitengeneza mfumo wa mamlaka huru kwa wasaidizi wake (free rein), kwamba nao wanaweza kufanya uamuzi kwa namna ambavyo wanaona inafaa. Wengi waliitumia vibaya nafasi hii ya kuaminiwa.

Rais Magufuli siku alipokabidhiwa cheti cha ushindi na Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (Nec), Jaji Damian Lubuva, ikiwa ni wiki moja kabla hajaapishwa, alimweleza JK: "Kuna watendaji wako walikusaliti, hao ndiyo nitaanza nao".
Kauli ya Magufuli ilikuwa na maana kuwa aliutambua usaliti wa kiungozi kwa umma ndani ya serikali ya JK na ulikuwa ukimkereketa lakini aliunyamazia kimya kwa sababu hakuwa na mamlaka.

Tatizo ni nini hapo? Lipo wazi, mara nyingi kiongozi wa kidemokrasia, hulinda zaidi mfumo wake usitetereke na wakati mwingine anapopewa taarifa za udhaifu wa wasaidizi wake, huchukulia kuwa ni majungu. Na anapoamua kuchukua hatua, huenda taratibu kwa sababu hufanya mchakato. Kiongozi mwana demokrasia hukataa kuchuakua uamuzi ambao mwisho ataonekana amekurupuka au kufanya uonevu.

Magufuli amekuwepo ndani ya Baraza la Mawaziri la JK kwa kipindi chote cha miaka 10, kwa hiyo anajua dhamira, maono pamoja na utendaji wa JK. Hiyo ndiyo sababu alisema kilichomuangusha JK ni watendaji wake wanafiki.

Kwa kawaida kiongozi anapoingia madarakani, kunakuwa na utangulizi wake, hivyo inakuwa rahisi kujua pa kuanzia kwa sababu anafahamu kasoro ambazo zilijiri kwa mtangulizi wake.

Mathalan, Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Nyerere, aliikuta Tanzania ikiwa mkusanyiko wa makabila na koo kubwa kubwa. Akaiunganisha na kujenga taifa moja. Akataka maendeleo ya pamoja kwa kila Mtanzania, hivyo akaasisi mfumo wa Ujamaa na Kujitegemea.

Hakutaka watu wachache watajirike wengi wabaki hohehahe (upebari), alishachungulia matatizo ya viongozi wengine kutumia madaraka yake vibaya, akaweka miiko ya uongozi, kisha kuunda Azimio la Arusha.

Mwalimu Nyerere alijenga viwanda kwa lengo la kumpa nguvu Mtanzania, aweze kuzalisha bidhaa zake ili asiuze malighafi nje kabla ya kuziongezea thamani. Maendeleo yalikuwa mazuri lakini kwa kusuasua. Miaka 25 ya falsafa za Nyerere, Mtanzania hakutoka kwenye umaskini.

Rais wa Awamu ya Pili, Ali Hassa Mwinyi aliposhika nchi, alifanya uthubutu kwa kuondoa vigingi wa kijamaa vilivyowekwa na Nyerere dhidi ya upebari. Bila kubadili mfumo, Tanzania ikibaki kuwa ya Ujamaa na Kujitegemea, wafanyabiashara wakawa na nguvu mno.

Rais Mwinyi ndiye mwanzilishi wa soko huria katika nchi. Hata hivyo, hakuweka misingi mizuri ya ukusanyaji kodi, matokeo yake serikali ikakosa uwezo mzuri wa kifedha. Wafanyabiashara wakajiona wapo kwenye neema.

Katika kuipa nguvu serikali, Rais Mwinyi alianzisha chombo cha kukusanya mapato ya serikali kuu ambayo ni Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA). Na mpaka alipomkabidhi nchi Rais Mkapa mwaka 1995, nchi ilikuwa inakusanya kodi wastani wa shilingi bilioni 25 kwa mwezi.

Rais Mkapa alipochukua nchi, pamoja na uwepo wa TRA, aliona bado kulikuwa na udhaifu wa ukusanyaji mapato, akaanzisha kodi ya ongezeko la thamani (VAT) na kudhibiti mianya ya ukwepaji kodi. Mwaka 2004, Rais Mkapa aliweka lengo la kukusanya shilingi bilioni 150 kwa mwezi lakini mpaka anakabidhi nchi, mapato ya mwezi yalikuwa shilingi bilioni 170.

Uhuru wa soko ulioanzishwa na Rais Mwinyi, ulisababisha wafanyabiashara wafanye fujo na kupandisha mfumuko wa bei mpaka asilimia 27 mwaka 1995, Rais Mkapa alishughulikia tatizo hilo na kupunguza mpaka asilimia 4.2.

JK alipochukua nchi, aliona mapato hayo, shilingi bilioni 170 kwa mwezi ni kidogo mno, akaweka utaratibu mzuri wa kutanua fursa za kibiashara kwa nchi. Kila mtu anaweza kuwa shuhuda ukuaji wa kibiashara katika miaka 10 ya JK. Aliona kasoro kwenye sekta ya madini, kwamba nchi ilikuwa inapunjwa na wawekezaji walikuwa wananeemeka kama vile wanavuna shambani kwao. Matokeo ya jumla yakawa kuongeza mapato ya nchi mpaka kufikia shilingi bilioni 900 kwa mwezi.

Utaona kuwa Mkapa alikabidhi nchi ikiwa inakusanya mapato zaidi ya mara sita ya alivyoachiwa na Mwinyi, JK pia amemkabidhi hatamu Magufuli, akiwa ameongeza mara sita ya Mkapa. Na takwimu za TRA zinaonesha kuwa miezi mitatu ya Julai mpaka Oktoba, makusanyo yalikuwa shilingi trilioni 3.77, sawa na wastani wa shilingi trilioni 1.25 kwa mwezi.

Mpaka hapo unaweza kuona kazi nzuri iliyofanywa na JK, mbali na kukusanya mapato, aliweza kuimarisha mfumo wa utawala bora. Angalau tukaweza kuona hata vigogo wanawajibishwa na mnyonge anasikilizwa.

JK aliweza kuimarisha ukaguzi katika hesabu za serikali, kuifanya Ofisi ya Taifa ya Ukaguzi wa Hesabu za Serikali (NAOT) kuwa taasisi huru ikiongozwa na Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG).

Akachochea mabadiliko ya kibunge kuanzia mwaka 2007, yaliyowafanya wapinzani kuwa wenyeviti wa kamati za kusimamia hesabu za serikali, kuanzia ile ya Hesabu za Serikali Kuu (PAC), Hesabu za Serikali za Mitaa (LAAC) na Hesabu za Mashirika ya Umma (POAC). Kwa sasa POAC imeingizwa ndani ya PAC.

Ni kupitia uwazi huo ambao JK aliuanzisha, uliweza kuimarisha hadhi na mamlaka ya bunge, hivyo kusaidia kugundulika kwa ufisadi mbalimbali serikalini. Rejea Tegeta Escrow, Richmond, EPA na nyinginezo.

Ni kipindi cha JK ndipo baadhi ya vigogo wa jeshi la polisi wenye hulka ya kubambikia watu kesi walifukuzwa kazi. Kashfa ya sukari iliibuliwa, mawaziri waliwajibishwa kwa kashfa ya tokomeza ujangili.

Ukipiga hesabu ya idadi ya mawaziri ambao walipoteza kazi kipindi cha JK, utagundua namna ambavyo kulikuwa na muundo mzuri wa uwazi serikalini. Ukifanya madudu unagundulika.

Weka pembeni Daraja la Kigamboni na Barabara za Mabasi Yaendayo Kasi (RBT Roads), JK ndiye rais ambaye ametekeleza miradi mingi ya maendeleo katika kipindi chake cha uongozi kuliko wote waliomtangulia. Ameiwezesha mikoa iliyokuwa inafikika kwa tabu, sasa inafikika kwa urahisi. Leo hii nchi inaunganishwa na barabara za lami mkoa kwa mkoa kwa zaidi ya asilimia 80. Magufuli ataunganisha kufikia asilimia 100.

Hata hivyo, kutokana na mfumo wa JK wa demokrasia ya uongozi, aliwaamini watendaji wake, kumbe pamoja na shilingi bilioni 900 au trilioni 1.25 nyakati za mwisho za utawala wake, bado kumekuwa na fujo kubwa ya wizi na ukwepaji kodi.

Ni rahisi sasa kuamini kuwa kumbe JK angeachana na demokrasia ya uongozi kisha kushika mtindo wa kusimamia na kufuatilia kila kitu kama afanyavyo Magufuli sasa, pengine angekabidhi nchi ikiwa inakusanya hata zaidi ya shilingi trilioni 1.5 kwa mwezi.

Ukiwa nje ya mchezo unaona vizuri zaidi, Magufuli aliyaona makosa ya JK, kuwa bandarini na TRA kuna fujo kubwa inayofanywa na watumishi wa mamlaka hizo pamoja na wafanyabiashara wakwepa kodi. Magufuli aliona kasoro za matumizi mabaya ya fedha za serikali, alipoingia tu akaanza kushughulikia udhibiti. Akazuia safari za nje na shughuli zisizo na tija.

Kwa kudhibiti ukwepaji kodi, Magufuli ameweka uelekeo wa serikali kukusanya shilingi trilioni 1.3 ndani ya Desemba hii.
Utaona kuwa Magufuli aliona mianya ya udhaifu wa JK, kuwa mfumo wake wa demokrasia ya utawala, umemgharimu. Angeweza kufanya zaidi lakini alihujumiwa na watendaji wezi walioruhusu wafanyabishara kujitanua.

Hata hivyo utaona kuwa Magufuli hajafanya kitu kikubwa kutanua wigo wa upatikanaji wa mapato, kwani alichokifanya ni kubana matumizi, kudhibiti kodi na kuwashughulikia watendaji wa serikali wezi na wafanyabishara wahuni. Yaani anashughulikia kwanza zile kasoro alizoziona wakati wa JK.

By Luqman Maloto
 
JK amekuzwa kipwani pwani
magufui jitu la bara......hapa kazi tu....tunataka kazi na si maneno
 
...Mkuu hii ni masterpiece.. Then mwanzo ulisema utaonesha aina ya uongozi wa magufuli na ni wapi anaweza kuangukia, nimefuatilia hadi mwisho sijaweza kuliona hili..!
 
Tofauti kubwa kati ya JK na JPM ni kuwa JK alikuwa msanii wa hali ya juu, kwa maana ya kuwa anayoyasema siyo yale anayoyatenda na JPM yuko more realistic, kwa maana anayoyasema ndiyo hayo anayoyatekeleza.
Mfano halisi ni kuwa wakati wa kampeni JPM aliahidi kuwa atadhibiti upotevu mkubwa wa fedha huko bandarini, alipoingia madarakani akatekeleza kwa vitendo ahadi yake hiyo kwa kutumbua majipu kwa kwenda mbele.
 
... ,umefafanua ila kama ilivyo kwa wengi, wanaandika/wanachambua badaeeeeee sana hasa baada ya mikono kuuma kutokana na kupiga makofi muda mrafu na sauti kukauka kwa kushangilia,
 
Mkuu Interest,

Basi nalazimika kuacha kuendelea na article yangu ambayo nilishafikia nusu kuiandika! Hapa ndipo wanamuziki huwa wanatuhumiana kuibiana nyimbo kumbe wakati mwingine ni maono tu!!! Ila naomba niongeze kidogo hapo kwenye demokrasia ya JK!

Ni kweli kabisa JK alijitahidi kuunda taasisi na sio uongozi wa mtu mmoja. Pale penye uwajibikaji ambacho alifanya JK ndicho hasa kinatakiwa... TAASISI! Mistake kubwa ambayo aliifanya ni ile kuamini kila mtu anafahamu wajibu wake na atatekeleza-- ali-assume anaongoza a PERFECT COMMUNITY.. UTOPIA STATE ambayo kila mmoja anafahamu wajibu wake na atautekeleza tu!

Style ya uongozi wa Magufuri ni mzuri sana kwa nchi kama yetu ambayo haina uwajibikaji lakini ina athari pale anapoondoka madarakani, manake ndani ya muda mfupi mambo huwa yanarudi kuwa shaghalabaghala kwavile yalitegemea usimamizi wa moja kwa moja wa mtu mmoja na sio usimamizi wa kitaasisi na mfumo. Inakuwa ni mfumo unaofanya watendaji watende si kwa kuwajibika bali kwa hofu!

Style ya JK ukikuta kuna mtu ni mwajibikaji basi ni mwajibikaji by nature... ana hiyo spirit ya kuwajibika lakini style ya Magufuri tutapata wawajibikaji fake... wanaowajibika kwavile wanaogopa kukutwa cha kuwakuta pindi wasipowajibika!

Hili lilitokea wakati wa Utawala wa Awamu ya Kwanza... kwa kuwa watendaji enzi za Mwalimu Nyerere walikuwa ni wenye hofu zaidi dhidi ya Nyerere badala ya kuwa na spirit ya uwajibikaji; pale Nyerere alipotoka tu madarakani, wale wale ambao walionekana wachapa kazi na wenye maadili ndio ghafla walibadilika na kuwa wala rushwa wakubwa!
 
Mkuu Interest,

Basi nalazimika kuacha kuendelea na article yangu ambayo nilishafikia nusu kuiandika! Hapa ndipo wanamuziki huwa wanatuhumiana kuibiana nyimbo kumbe wakati mwingine ni maono tu!!! Ila naomba niongeze kidogo hapo kwenye demokrasia ya JK!

Ni kweli kabisa JK alijitahidi kuunda taasisi na sio uongozi wa mtu mmoja. Pale penye uwajibikaji ambacho alifanya JK ndicho hasa kinatakiwa... TAASISI! Mistake kubwa ambayo aliifanya ni ile kuamini kila mtu anafahamu wajibu wake na atatekeleza-- ali-assume anaongoza a PERFECT COMMUNITY.. UTOPIA STATE ambayo kila mmoja anafahamu wajibu wake na atautekeleza tu!

Style ya uongozi wa Magufuri ni mzuri sana kwa nchi kama yetu ambayo haina uwajibikaji lakini ina athari pale anapoondoka madarakani, mambo yanarudi kuwa shaghalabaghala kwavile yalitegemea usimamizi wa moja kwa moja wa mtu mmoja na sio usimamizi wa kitaasisi na mfumo.

Ni kweli kabisa...JPM akiondoka kila kitu kinaweza kurudi kama mwanzo labda tuachane na Rasimu ya Katiba ya sasa, tukae miaka kama miwili, tuwe na vision nzuri, tujipime kwanza alafu tutunge katiba itakayokuwa comprehensive....
 
Mkuu Uchambuzi mzuri, nilikua na wazo pia lakuleta uchambuzi kama huu, ila umeshaleta, vizuri sana mkuu, kilichobaki ni wao kunywa wakikataa ujinga wao
 
...Mkuu hii ni masterpiece.. Then mwanzo ulisema utaonesha aina ya uongozi wa magufuli na ni wapi anaweza kuangukia, nimefuatilia hadi mwisho sijaweza kuliona hili..!

Hujaona hapo amesema Kuhusu Authoritan leadership ambapo anaweza kusalitiwa na watendaji wake
 
...nimetoa pongezi zangu kwa hii masterpiece, na kaushauri ka editorial kadogo, ambako pia umekafanya the least you could do is reciprocate what i did and not just edit my comment.

Of cause i agree ushauri wa editorial hauna mashiko tena baada ya wewe kuutekeleza but..hata PM tu kuwa respectifully "i am editing your comment"!
 
KUMEKUWA na kiu kubwa ya kumlinganisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. John Pombe Magufuli na mtangulizi wake, Dk. Jakaya Mrisho Kikwete. Kwamba nani ni nani? Si kwa hoja ya kimaumbile kuwa JK ni mrefu na mweupe wakati Magufuli ni mweusi na mfupi, la hasha!

Haiangaliwi mantiki ya kifamilia, kwani inaeleweka JK mkewe ni Salma na Magufuli wake ni Janeth. Hatupo huko, hapa kinachozungumzwa ni uongozi wao.

Kosa la kimsingi ni kutafsiri matokeo ya mafanikio ya sasa kama makosa au udhaifu wa serikali iliyopita.
Watanzania wamekuwa wepesi kuhukumu. Wazuri mno katika kushabikia michakato. Halafu hukumu zinakuwa za jumla mno.

Usimlaumu JK kama huwezi kuchanganua mtindo wake wa uongozi. Usimsifu tu Magufuli ikiwa hujatambua anatumia aina ipi ya uongozi. Na usipende kuongozwa na hoja za jumla (general), penda kushika kitu halisi (be realistic). Ni kwa kutambua vizuri mtindo wa uongozi ambao JK aliutumia ndiyo utaweza kubaini makosa ambayo yalifanyika, vilevile utaweka tahadhari kuhusu mwenendo wa Magufuli, kwamba asipokuwa makini wapi ataanguka.

Kuna dhana nne za uongozi. Ukizielewa hizo itakurahisishia kutambua nani ni kiongozi mzuri, anapatikanaje, kipi kinaweza kumfanya mtu kuwa kiongozi mzuri na chanzo kinachoweza kumpa nguvu kiongozi.

Dhana ya hulka (trait theory); Hii inachambuliwa katika Sayansi ya Siasa (Political Science) kama moja ya vigezo vya kutambua aina ya kiongozi. Ndani ya somo la saikolojia, inatafsiriwa kama kipimo cha kung?amua hulka, hisia, fikra na uhusika wa kiongozi. Katika dhana hii, kinachoangaliwa ni aina gani ya mtu anaweza kuwa kiongozi mzuri.

Dhana ya kitabia (behavioral theory); Je, kiongozi ana mwenendo gani kitabia? Kiongozi mzuri anafanyaje mambo yake? Katika dhana hii ndipo ambapo unaweza kung'amua nyenendo za viongozi. Katika dhana hii ndipo utaweza kuona tofauti ya JK wa 2005-2015 na Magufuli 2015-2020 au mpaka 2025, vilevile tutawamulika na watangulizi wao. Nakuomba twende pamoja.

Dhana ya dharura (contingency theory); Kwamba hajulikani kitabia na hakuna mwenye kutambua atakwenda kufanya nini, yaani hatabiriki lakini anapitishwa kwenda kushika hatamu. Anayepatikana kupitia dhana hii, matokeo chanya hushangaza zaidi kuliko hasi. Na zaidi, mazingira ndiyo yanaweza kusababisha kiongozi aonekane mzuri. Kupitia dhana hii nitaeleza jinsi Magufuli anavyong'ara kama ilivyotokea kwa Rais wa Awamu ya Tatu, Benjamin Mkapa alivyong'ara mwaka 1995.

Dhana ya nguvu na ushawishi (power and influence theory); Kama Waziri Mkuu wa zamani, Edward Ngoyai Lowassa, angeshinda urais mwaka huu, angekuwa amebebwa na dhana hii. Dhana hii pia ndiyo iliyomuingiza JK mwaka 2005. Kwamba mtu anakuwa na mtandao mkubwa wenye nguvu na ushawishi kiasi kwamba inakuwa vigumu kumzuia.

Kuhusu dhana ya dharura inavyombeba Magufuli kama ilivyotokea kwa Mkapa, ni mazingira ambayo wahusika waliyakuta.
Magufuli ameikuta nchi ikiwa na nidhamu mbaya ya matumizi ya fedha na udhibiti wa rasilamali za umma. Kuingia kwake na kasi kubwa ya kudhibiti matumizi mabaya ya fedha za serikali, kuahirisha shughuli zenye kutumia fedha nyingi kinyume na kipaumbele cha wananchi pamoja na kushughulikia ufisadi, vimemfanya ang'are kwa haraka mno.

Magufuli pia amerejesha nidhamu ya utumishi wa umma. Sasa mfanyakazi serikalini anatambua maana ya kuwajibika, kwani asipofanya hivyo anakuwa jipu.

Mkapa alikuta nchi watu binafsi walikuwa na uwezo mkubwa kuliko serikali. Akarejesha meno serikalini, akawabana wafanyabiashara na kukusanya kodi vizuri, akajenga miundombinu, akatanua wigo wa soko huria na kadhalika. Mkapa akaonekana malaika!

Ndani ya dhana ya kitabia ndipo unaweza kuiona tofauti ya kiuongozi kati ya JK na Magufuli. Mwanasaikolojia wa Kijerumani, hayati Kurt Zadek Lewin, aliwahi kuandika aina tatu za viongozi ambao wanaweza kupatikana kutokana na tabia zao.

Kiongozi anayetaka lake litimie (autocratic leader); Huyu wakati mwingine hutafsiriwa kama kiongozi wa kiimla. Si mwenye kutaka sifa, anachokifanya ni kutimiza maono yake tu. Watu wamchukie lakini dhamira yake itimie. Hapa ndipo unapoweza kumuona Magufuli.

Kiongozi mwana demokrasia (democratic leader); Kiongozi ambaye hafanyi mambo yake peke yake. Anashirikiana na timu yake kupanga na kutekeleza mipango ya kila siku. Huyu ni kiongozi ambaye anawaamini mno wasaidizi wake. Anawaacha wenzake waamue na kutekeleza majukumu yao ya kila siku kwa uhuru mkubwa. Na yeye binafsi hatendi mpaka yawepo makubaliano ya kitimu. Hapa ndipo unamuona JK.

Kiongozi mtegemea wasidizi (laissez-faire leader); Wasaidizi wanakuwa wanafanya kazi kubwa na wenye nguvu kuliko kiongozi mkuu. Yaani rais wa nchi anakuwa kubwa jinga (figure head) kwa sababu watu wake wanaweza kufanya chochote pasipo yeye kutia neno.

Tanzania hatujawahi kuwa na rais kubwa jinga. Wote pamoja na makosa ya hapa na pale, wamesimama vizuri kama marais na viungo muhimu (key figures) wa nchi kila mmoja kwa zama zake. Sababu ya kutegemea wasaidizi inaweza kutokana na uvivu wa kiongozi mkuu au uwezo mdogo alionao, kwamba wasaidizi wanakuwa na uwezo mzuri kiutendaji kuliko yeye, kwa hiyo anaona bora awape uwanja mzuri wa kutenda.

Ukiachana na aina hizo tatu za viongozi kama zilivyoletwa na Lewin mwaka 1930, katika somo la uongozi, wanatajwa viongozi aina sita.

Kiongozi mmbeba mamlaka yote (authoritarian), na ndani yake ndimo unaweza kumpata mwenye kutaka lake tu (autocratic). Rais anataka kila jambo lipate usimamizi wake wa karibu na aone matokeo. Magufuli yupo hapa!

Aina nyingine ya kiungozi ambayo Magufuli anakwenda nayo ni kuwa kiongozi mleta mabadiliko (transformational), kwamba habanwi na wasaidizi wake kuamua na kupanga kile ambacho yeye anaona kinafaa. Kwa kawaida kiongozi anayefanya mambo yake kwa mitindo hiyo miwili, ndani yake huongozwa na hali ya kutoamini mtu, kwamba wakati wowote wanaweza kumsaliti kwenye harakati zake za kutimiza malengo aliyojiwekea.

Faida kubwa katika mitindo hiyo miwili ni kwamba kisiasa, kama kiongozi mkuu anakuwa na utashi wa kweli wa kuwahudumia wananchi wake na kuwapa matokeo yenye kuonekana, huutikisa mfumo wote ili utende kama yalivyo matakwa yake. Ona Magufuli anavyotikisa hivi sasa.

Hasara za mitindo hiyo ni kuwafanya viongozi wa nchi waishi kama maroboti. Hawatajiamini na kufanya kazi kwa sura ambayo wanaona ni bora, wao wanajielekeza katika kumfurahisha kiongozi mkuu. Zaidi hawaishi kama viongozi, wanatenda tu mawazo ya kiongozi mkuu. Yaani wanakuwa watu wa kupokea maagizo na kufanya jinsi kiongozi wao anataka. Wanakuwa wazee wa 'kukopi' na 'kupesti'.

Na kwa sababu serikali ni taasisi kubwa, husababisha baadhi ya mambo ambayo siyo kipaumbele cha kiongozi mkuu kudumaa, wakati yangeweza kufanyiwa utekelezaji na viongozi wa chini kama wangekuwa huru na wenye kutimiza majukumu yao ipasavyo.

Ifahamike kuwa mifumo ya uongozi, kifaida na kihasara huzalishwa na saikolojia. Watendaji wa chini wanaweza kufanya mambo yao kama watu wasio na akili zinazojitegemea. Wanategemea akili za mkuu.
Kama kiongozi akiwa na haiba pendwa (charismatic leader), inaweza kuwasisimua na wasaidizi wake kujituma, kwani nao wanakuwa wanavutiwa naye kiuongozi na kitabia.

Aina hizo za uongozi, wakati mwingine huzaa kiongozi wa kiimla (dictator), hivyo kupitiliza na kuwafanya wasaidizi wake kumuogopa. Yaani badala ya kufanya kazi kulingana na mahitaji yao ya kiuongozi, wanakuwa watekeleza majukumu kwa hofu. Wakipigiwa simu na bosi mkuu, wanatetemeka kwa sababu hawajui wataambiwa nini.

Mafanikio ya Magufuli ndani ya muda mfupi ni kuwa nchi ilikuwa tenge. Watumishi wengi wa umma walikosa Utanzania, kwa hiyo wao wenyewe wakawa wahujumu uchumi badala ya kujenga uchumi. Kiongozi kama baba wa familia (paternalistic). JK na Magufuli kama ilivyokuwa kwa watangulizi wao, ni vichwa vya serikali na uhusika wao unaonesha hivyo.

Hata hivyo, mafanikio ya kiongozi wa aina hii husababishwa na hulka binafsi na aina ya watu ambao anafanya nao kazi. Akiwa kiongozi mwana demokrasia, anahitaji watu waaminifu, wachapakazi na wakweli mno. Kama watu ambao kiongozi anafanya nao kazi wakiwa siyo waaminifu, waongo na wavivu, kiongozi wa mtindo wa demokrasia kama alivyokuwa anakwenda nao JK ni vigumu mno kupata mafanikio stahili.

JK katika mtindo wake wa kidemokrasia, alitengeneza mfumo wa mamlaka huru kwa wasaidizi wake (free rein), kwamba nao wanaweza kufanya uamuzi kwa namna ambavyo wanaona inafaa. Wengi waliitumia vibaya nafasi hii ya kuaminiwa.

Rais Magufuli siku alipokabidhiwa cheti cha ushindi na Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (Nec), Jaji Damian Lubuva, ikiwa ni wiki moja kabla hajaapishwa, alimweleza JK: "Kuna watendaji wako walikusaliti, hao ndiyo nitaanza nao".
Kauli ya Magufuli ilikuwa na maana kuwa aliutambua usaliti wa kiungozi kwa umma ndani ya serikali ya JK na ulikuwa ukimkereketa lakini aliunyamazia kimya kwa sababu hakuwa na mamlaka.

Tatizo ni nini hapo? Lipo wazi, mara nyingi kiongozi wa kidemokrasia, hulinda zaidi mfumo wake usitetereke na wakati mwingine anapopewa taarifa za udhaifu wa wasaidizi wake, huchukulia kuwa ni majungu. Na anapoamua kuchukua hatua, huenda taratibu kwa sababu hufanya mchakato. Kiongozi mwana demokrasia hukataa kuchuakua uamuzi ambao mwisho ataonekana amekurupuka au kufanya uonevu.

Magufuli amekuwepo ndani ya Baraza la Mawaziri la JK kwa kipindi chote cha miaka 10, kwa hiyo anajua dhamira, maono pamoja na utendaji wa JK. Hiyo ndiyo sababu alisema kilichomuangusha JK ni watendaji wake wanafiki.

Kwa kawaida kiongozi anapoingia madarakani, kunakuwa na utangulizi wake, hivyo inakuwa rahisi kujua pa kuanzia kwa sababu anafahamu kasoro ambazo zilijiri kwa mtangulizi wake.

Mathalan, Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Nyerere, aliikuta Tanzania ikiwa mkusanyiko wa makabila na koo kubwa kubwa. Akaiunganisha na kujenga taifa moja. Akataka maendeleo ya pamoja kwa kila Mtanzania, hivyo akaasisi mfumo wa Ujamaa na Kujitegemea.

Hakutaka watu wachache watajirike wengi wabaki hohehahe (upebari), alishachungulia matatizo ya viongozi wengine kutumia madaraka yake vibaya, akaweka miiko ya uongozi, kisha kuunda Azimio la Arusha.

Mwalimu Nyerere alijenga viwanda kwa lengo la kumpa nguvu Mtanzania, aweze kuzalisha bidhaa zake ili asiuze malighafi nje kabla ya kuziongezea thamani. Maendeleo yalikuwa mazuri lakini kwa kusuasua. Miaka 25 ya falsafa za Nyerere, Mtanzania hakutoka kwenye umaskini.

Rais wa Awamu ya Pili, Ali Hassa Mwinyi aliposhika nchi, alifanya uthubutu kwa kuondoa vigingi wa kijamaa vilivyowekwa na Nyerere dhidi ya upebari. Bila kubadili mfumo, Tanzania ikibaki kuwa ya Ujamaa na Kujitegemea, wafanyabiashara wakawa na nguvu mno.

Rais Mwinyi ndiye mwanzilishi wa soko huria katika nchi. Hata hivyo, hakuweka misingi mizuri ya ukusanyaji kodi, matokeo yake serikali ikakosa uwezo mzuri wa kifedha. Wafanyabiashara wakajiona wapo kwenye neema.

Katika kuipa nguvu serikali, Rais Mwinyi alianzisha chombo cha kukusanya mapato ya serikali kuu ambayo ni Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA). Na mpaka alipomkabidhi nchi Rais Mkapa mwaka 1995, nchi ilikuwa inakusanya kodi wastani wa shilingi bilioni 25 kwa mwezi.

Rais Mkapa alipochukua nchi, pamoja na uwepo wa TRA, aliona bado kulikuwa na udhaifu wa ukusanyaji mapato, akaanzisha kodi ya ongezeko la thamani (VAT) na kudhibiti mianya ya ukwepaji kodi. Mwaka 2004, Rais Mkapa aliweka lengo la kukusanya shilingi bilioni 150 kwa mwezi lakini mpaka anakabidhi nchi, mapato ya mwezi yalikuwa shilingi bilioni 170.

Uhuru wa soko ulioanzishwa na Rais Mwinyi, ulisababisha wafanyabiashara wafanye fujo na kupandisha mfumuko wa bei mpaka asilimia 27 mwaka 1995, Rais Mkapa alishughulikia tatizo hilo na kupunguza mpaka asilimia 4.2.

JK alipochukua nchi, aliona mapato hayo, shilingi bilioni 170 kwa mwezi ni kidogo mno, akaweka utaratibu mzuri wa kutanua fursa za kibiashara kwa nchi. Kila mtu anaweza kuwa shuhuda ukuaji wa kibiashara katika miaka 10 ya JK. Aliona kasoro kwenye sekta ya madini, kwamba nchi ilikuwa inapunjwa na wawekezaji walikuwa wananeemeka kama vile wanavuna shambani kwao. Matokeo ya jumla yakawa kuongeza mapato ya nchi mpaka kufikia shilingi bilioni 900 kwa mwezi.

Utaona kuwa Mkapa alikabidhi nchi ikiwa inakusanya mapato zaidi ya mara sita ya alivyoachiwa na Mwinyi, JK pia amemkabidhi hatamu Magufuli, akiwa ameongeza mara sita ya Mkapa. Na takwimu za TRA zinaonesha kuwa miezi mitatu ya Julai mpaka Oktoba, makusanyo yalikuwa shilingi trilioni 3.77, sawa na wastani wa shilingi trilioni 1.25 kwa mwezi.

Mpaka hapo unaweza kuona kazi nzuri iliyofanywa na JK, mbali na kukusanya mapato, aliweza kuimarisha mfumo wa utawala bora. Angalau tukaweza kuona hata vigogo wanawajibishwa na mnyonge anasikilizwa.

JK aliweza kuimarisha ukaguzi katika hesabu za serikali, kuifanya Ofisi ya Taifa ya Ukaguzi wa Hesabu za Serikali (NAOT) kuwa taasisi huru ikiongozwa na Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG).

Akachochea mabadiliko ya kibunge kuanzia mwaka 2007, yaliyowafanya wapinzani kuwa wenyeviti wa kamati za kusimamia hesabu za serikali, kuanzia ile ya Hesabu za Serikali Kuu (PAC), Hesabu za Serikali za Mitaa (LAAC) na Hesabu za Mashirika ya Umma (POAC). Kwa sasa POAC imeingizwa ndani ya PAC.

Ni kupitia uwazi huo ambao JK aliuanzisha, uliweza kuimarisha hadhi na mamlaka ya bunge, hivyo kusaidia kugundulika kwa ufisadi mbalimbali serikalini. Rejea Tegeta Escrow, Richmond, EPA na nyinginezo.

Ni kipindi cha JK ndipo baadhi ya vigogo wa jeshi la polisi wenye hulka ya kubambikia watu kesi walifukuzwa kazi. Kashfa ya sukari iliibuliwa, mawaziri waliwajibishwa kwa kashfa ya tokomeza ujangili.

Ukipiga hesabu ya idadi ya mawaziri ambao walipoteza kazi kipindi cha JK, utagundua namna ambavyo kulikuwa na muundo mzuri wa uwazi serikalini. Ukifanya madudu unagundulika.

Weka pembeni Daraja la Kigamboni na Barabara za Mabasi Yaendayo Kasi (RBT Roads), JK ndiye rais ambaye ametekeleza miradi mingi ya maendeleo katika kipindi chake cha uongozi kuliko wote waliomtangulia. Ameiwezesha mikoa iliyokuwa inafikika kwa tabu, sasa inafikika kwa urahisi. Leo hii nchi inaunganishwa na barabara za lami mkoa kwa mkoa kwa zaidi ya asilimia 80. Magufuli ataunganisha kufikia asilimia 100.

Hata hivyo, kutokana na mfumo wa JK wa demokrasia ya uongozi, aliwaamini watendaji wake, kumbe pamoja na shilingi bilioni 900 au trilioni 1.25 nyakati za mwisho za utawala wake, bado kumekuwa na fujo kubwa ya wizi na ukwepaji kodi.

Ni rahisi sasa kuamini kuwa kumbe JK angeachana na demokrasia ya uongozi kisha kushika mtindo wa kusimamia na kufuatilia kila kitu kama afanyavyo Magufuli sasa, pengine angekabidhi nchi ikiwa inakusanya hata zaidi ya shilingi trilioni 1.5 kwa mwezi.

Ukiwa nje ya mchezo unaona vizuri zaidi, Magufuli aliyaona makosa ya JK, kuwa bandarini na TRA kuna fujo kubwa inayofanywa na watumishi wa mamlaka hizo pamoja na wafanyabiashara wakwepa kodi. Magufuli aliona kasoro za matumizi mabaya ya fedha za serikali, alipoingia tu akaanza kushughulikia udhibiti. Akazuia safari za nje na shughuli zisizo na tija.

Kwa kudhibiti ukwepaji kodi, Magufuli ameweka uelekeo wa serikali kukusanya shilingi trilioni 1.3 ndani ya Desemba hii.
Utaona kuwa Magufuli aliona mianya ya udhaifu wa JK, kuwa mfumo wake wa demokrasia ya utawala, umemgharimu. Angeweza kufanya zaidi lakini alihujumiwa na watendaji wezi walioruhusu wafanyabishara kujitanua.

Hata hivyo utaona kuwa Magufuli hajafanya kitu kikubwa kutanua wigo wa upatikanaji wa mapato, kwani alichokifanya ni kubana matumizi, kudhibiti kodi na kuwashughulikia watendaji wa serikali wezi na wafanyabishara wahuni. Yaani anashughulikia kwanza zile kasoro alizoziona wakati wa JK.

By Luqman Maloto
sijasoma yote ungefupisha..ila 'hapa kazi tu' ndio maneno ya mujini. lazima kitaeleweka.
 
Kwenye barabara hapo nadhani hujamtendea haki Mkapa. Mpango wa kujenga barabara zetu wenyewe.ni ubunifu wa.serikali ya mkapa. Jk alikuta miradi mingi iliyohitaji kukamilishwa tu.
 
...tofauti kubwa ni moja tu....kwamba mmoja ni mnafiki (hypocrite) na mwingine ni mkweli(realistic)....
 
Back
Top Bottom