figganigga
JF-Expert Member
- Oct 17, 2010
- 25,658
- 55,485
Hapa sipati Picha,
Rais Magufuli ni rafiki wa Rais Mstaafu Benjamin Mkapa, Benjamin Mkapa anamiliki mashamba ya Miwa ya kutengeneza Sukari. Mkapa anahofia iwapo Sukari itaagizwa kutoka nje, basi miwa yake itakosa soko. Bila shaka alienda Ikulu siku ile kumuomba afute vibari vya Sukari kutoka nje. Kwanini apige marufuku kwenye sukari tu wakati kuna viwanda vya nondo, saruji na vinginevyo na vinaleta bidhaa kutoka nje. Ingekuwa ni Kulinda Bidha za ndani isingekuwa Sukari tu, Hapa kuna zaidi ya Sukari.
Sasa Sukari imeadimika watu wamemuacha Rais peke yake akihangaika. Ama kweli Rais anashauriwa Vibaya. Rais amewaomba Mashirika ya hifadhi ya Jamii yasaidie kuleta Sukari kutoka nje. Je Hao hifadhi ya Jamii Wamejisajili kwenye bodi ya Sukari? na waliokuwa naleta Sukari kutoka nje wafanye kazi gani? Hata hivyo alisema walikuwa wanaleta sukari iliyoisha muda wake na tumetumia sukari hiyo miaka yote tangu enzi za Mwinyi.
Rais Mstaafu wa Awamu ya tatu Benjamin William Mkapa alipomtembelea Rais magufuli Ikulu Dar 07 Januari, 2016.
Baada ya kukutana Wakubwa hawa, Tarehe 19 Feb, rais Magufuli akapiga Marufuku na kufuta vibari vyote vya kuagiza sukari kutoka nje. Kwamba analinda Viwanda vya ndani.
Hii imenifanya nikubariane na Habari iliyoandikwa na Nipashe leo.
========================
Sukari imemshinda Magufuli
Wadai amekurupuka kuzuia vibali vya uagizaji sukari, wamhusisha Mkapa, Rais mwenyewe atoa ruksa kwa mifuko ya hifadhi ya jamii kuleta sukari, kamata kamata yaendelea nchini. KAMBI Rasmi ya Upinzani Bungeni, imesema tatizo la sukari nchini limetokana na uamuzi usio sahihi wa Rais Dk. John Magufuli, kwa kupiga marufuku uingizwaji wa bidhaa hiyo kutoka nje ya nchi bila kufanya tathmini.
Akizungumza jana na waandishi wa habari, Waziri Kivuli wa Wizara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Anthony Komu, alisema agizo hilo lilitolewa kwa kukurupuka na ndilo lililosababisha sukari kuadimika.
Komu ambaye pia ni Mbunge wa Moshi Vijijini, alisema kama malengo ni kulinda viwanda vya ndani, basi lisifanyike kwa sukari pekee kwa sababu viwanda vipo vingi na bado bidhaa zinaingia kutoka nje nchi.
Alisema kuna harufu ya upendeleo kutokana na Rais kuwa swahiba wa Rais mstaafu wa awamu ya tatu, Benjamin Mkapa, ambaye ni mmiliki wa mashamba ya Mtibwa, hivyo amefanya hivyo kwa kupewa ushauri mbaya huku nchi ikiingia kwenye upungufu mkubwa wa sukari.
Alihoji kwa nini apige marufuku kwenye sukari tu wakati kuna viwanda vya nondo, saruji na vinginevyo na vinaleta bidhaa kutoka nje.
Alisema kilichofanywa na Rais ni kukurupuka na ni kuvunja sheria.
Komu alisema kitendo cha Rais kutoa amri ya walioficha sukari wany’ang’anywe, ni kupora haki za watu na kuua mitaji yao kibiashara.
“Hakuna sheria ambayo inaruhusu kwenda kukagua maghala ya wafanyabiashara na kugawa bidhaa bure, hii hali hata wawekezaji wataogopa kuja kuwekeza nchini kwa sababu wataona mazingira ya hapa nchini ni hatarishi," alisema Komu.
Alisema serikali iandae njia mbadala ya kuwafidia watu walionyang’anywa maana wengine wamekopa kwenye taasisi za kifedha.
“Agizo la Rais lina walakini, kwani ni nani katika biashara za watu...tunakokwenda ni kubaya kwani upungufu wa sukari ulijulikana tangu Februari, lakini akapiga marufuku sukari kutoka nje,” alisema Komu.
Alisema katika tafiti mbalimbali ikiwamo ripoti iliyotolewa na Shirika la BBC, mahitaji ya sukari nchini kwa mwaka ni tani 590,000, lakini uwezo uliopo ni tani 300,000, hivyo serikali ilikuwa ni busara iruhusu kuingizwa kwa sukari kwa sababu viwanda vya ndani vimekosa uwezo.
Alisema Rais anatakiwa kukemewa na kuambiwa kwamba anakwenda kinyume na kwamba wao kambi ya upinzani hawatetei wanaoficha sukari, lakini serikali itafute namna ya kukabili hali hiyo.
Naye Mbunge wa Ubungo, Saed Kubenea, alisema taifa lina viwanda vinne vikubwa vya sukari, lakini bado havina uwezo wa kuzalisha sukari ya kutosha.
Alisema serikali imefanya sukari ionekane kama dawa za kulevya kutokana na kuadimika huko.
Alisema sukari hadi iletwe nchini, ni takriban wiki tano na wanaoingia kwenye Mwezi Mtukufu wa Ramadhani watahitaji sukari kushinda vitu vingine.
“Sisi hatutetei walioficha, lakini wamenunua ili kuuza kwa taratibu kulingana na bei ya soko wasibughudhiwe maana kuna hatari ya benki kushindwa kurejeshewa fedha zilizokopwa,” alisema Kubenea.
TANI 622 ZAKAMATWA MOROGORO
Siku mbili baada ya vyombo vya dola kumkamata mfanyabiashara Harun Zakaria, akidaiwa kuficha kilo takriban milioni tano za sukari jijini Dar es Salaam, vyombo vya usalama mkoani Morogoro vimekamata sukari nyingine ya mfanyabiashara huyo ikiwa imehifadhiwa katika maghala matatu tofauti mjini hapa.
Sukari hiyo iliyokamatwa ni tani 622.4 ikiwa imehifadhiwa katika maghala matatu ikiwamo moja katika Manispaa ya Morogoro katika Stesheni ya Kampuni ya Reli (TRL) na maghala mawili ya Kampuni ya Sukari ya Illovo yaliyopo wilayani Kilombero na Kilosa.
Akizungumza na waandishi wa habari mjini hapa jana, Mkuu wa Mkoa wa Morogoro, Dk. Kebwe Steven Kebwe, alisema sukari ya mfanyabiashara huyo ilikamatwa baada ya kuunda kikosi kazi cha kufuatilia wafanyabiashara wa bidhaa hiyo mkoani Morogoro.
“Niliunda kikosi kazi wakiwamo wajumbe wa Kamati ya Ulinzi na usalama wa Mkoa wa Morogoro na tulianza kufanya kazi siku ile ile aliyotoa agizo Rais John Magufuli, kwa kutembelea maghala mbalimbali ya wafanyabiashara," alisema.
Alisema walifanya hivyo kutokana na Mkoa wa Morogoro kuwa na viwanda vitatu vya sukari ambavyo ni Mtibwa Sugar kilichopo wilayani Mvomero na viwili vya Kampuni ya Sukari ya Illovo vilivyopo Wilaya ya Kilosa na Kilombero.
Mkuu huyo wa mkoa alisema katika operesheni hiyo walibaini ghala lililopo eneo la stesheni lilikuwa limefichwa kiasi cha tani 58.4 na ghala lingine katika Kiwanda cha Sukari cha Kampuni ya Illovo la Kilombero likuwa limehifadhiwa tani 429 wakati lile lilopo wilayani Kilosa likiwa limehifadhiwa tani 135 zote zikielezwa kuwa ni mali ya Kampuni ya Alneem Enterprises ambayo ni mali ya Zakaria.
Kutokana na hali hiyo, Mkuu huyo wa Mkoa, alimwagiza Kamanda wa Polisi mkoani hapa kumkamata mara moja mfanyabiashara huyo na kumfungulia kesi mahakamani kutokana na kitendo hicho cha kuficha sukari kwa makusudi katika maghala yake ili baadaye aiuze kwa bei ya juu.
Kadhalika , aliagiza Mamlaka ya Mapato (TRA) Mkoa wa Morogoro kwenda kwenye maghala hayo mara moja kukagua sukari hiyo kama imelipiwa kodi ya serikali na endapo haijalipiwa mfanyabiashara huyo kabla ya kufikishwa katika vyombo vya sheria awe amelipa.
Hata hivyo, alisema sukari hiyo yote itachukuliwa na serikali na kusambazwa katika maduka ili wananchi wauziwe kwa bei elekezi ya serikali kuanzia Sh. 1,800 hadi 2,000 kwa kilo katika wilaya zote za Mkoa wa Morogoro.
Aliwataka wananchi kutoa taarifa kwa vyombo vya usalama ikiwamo, Polisi, Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa(Takukuru) pindi wanapoona wafanyabiashara wakubwa wakificha sukari katika maghala.
Kwa upande wake, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Morogoro, Urlich Matei, alisema tayari kikosi cha jeshi lake kinalinda maghala yote matatu ya mfanyabishara huyo huku likiendelea kumtafuta ili kumfikisha mbele ya vyombo vya sheria.
KIWANDA BUBU CHAGUNDULIKA MBEYA
Serikali mkoani Mbeya imekamata kiwanda bubu cha kufungasha sukari, ambacho kinadaiwa kufungasha upya sukari ya ndani kwenye mifuko yenye ujazo wa kati ya nusu kilo na kilo moja na kisha sehemu ya sukari hiyo kuuzwa nje ya nchi na nyingine kusambazwa mitaani.
Kukamatwa kwa kiwanda hicho kunatokana na hatua ya Mkuu wa Wilaya wa Mbeya, Nyerembe Munasa, akiwa ameongozana na Polisi kuingia mwenyewe mitaani kutekeleza agizo la Rais Magufuli la kuwasaka wafanyabiashara ambao wameficha sukari kwenye maghala.
Akiwa mitaani, ndipo akabaini uwapo wa kiwanda hicho kikiwa katika nyumba moja ya makazi ya watu iliyopo maeneo ya Soweto, huku mifuko inayotumika kufungashia sukari hiyo ikiwa na nembo isiyoonyesha mahali sukari hiyo ilipotengenezewa.
Akizungumza baada ya kubaini kiwanda hicho, Munasa alisema viwanda vya aina hiyo ndivyo vinavyotumika kufungasha sukari ambayo wakati mwingine huwa imepitwa na wakati na kuwauzia wananchi, hali ambayo inaweza kuwasababishia madhara kiafya.
“Viwanda vya aina hii ndivyo vinavyotumika kufungasha sukari feki, iliyopitwa na wakati, wao kwenye mifuko hii wanaandika tarehe nyingine ya sukari kumaliza muda wake wa matumizi, hali ambayo inaweza kuwadhuru watumiaji,” alisema Munasa.
Aidha, Munasa alimuuliza mmiliki wa kiwanda hicho, Bushir Sanga, kama ana kibali kutoka kwenye viwanda vya ndani vinavyompa mamlaka ya kubadilisha jina la sukari, na kukiri kutokuwa na kibali cha kufanya hivyo.
Hata hivyo, Sanga ambaye pia ni mfanyabiashara maarufu wa sukari jijini Mbeya alidai kuwa ana kibali cha kufanya shughuli hiyo kutoka Mamlaka ya Chakula na Dawa (TFDA) na pia anatambuliwa na TRA kwa kuwa huwa analipa kodi.
“Ninayo leseni ya TFDA na pia huwa nalipa kodi hivyo natambuliwa hata na TRA, hivyo shughuli yangu ya kufungasha sukari ni halali kisheria,” alisema Sanga.
Maelezo hayo hayakutosha kumshawishi Mkuu wa Wilaya kuwa mfanyabiashara huyo hana kosa, hivyo akaliamuru Jeshi la Polisi kumkamata na kumfikisha kituoni ili achukuliwe maelezo na baadaye afikishwe kwenye vyombo vya sheria.
Bei ya sukari mkoani Mbeya kwa sasa ni kati ya Sh. 2,400 na 2,500.
MAGUFULI ARUHUSU MIFUKO YA HIFADHI KUAGIZA SUKARI
Rais Dk. Magufuli, amesema iwapo mashirika hayo yatapenda kuagiza sukari, yupo tayari kutoa kibali yaagize badala ya biashara hiyo kuachwa ikihodhiwa na watu wachache.
“Nitawapeni kibali kununua sukari kama mnataka, lakini mjipange kujenga viwanda, hata mashamba ya kulima miwa nitawapa ili vijana wapate ajira, alisema Rais Magufuli wakati wa ufunguzi wa majengo ya vitega uchumi ya PPF na
NSSF jijini Arusha jana.
Alisema hatawavumilia wafanyabiashara wanafiki wanaoshindwa kuwajali watu maskini kwa kuamua kuficha sukari, huku akiwataka Watanzania kutokuwa na wasiwasi kwani nchi itakwenda vizuri.
Aidha, amepiga marufuku mashirika ya hifadhi ya jamii kuwekeza katika majengo na badala yake ametaka yakite katika ujenzi wa viwanda mbalimbali vikiwamo vya sukari.
Alisema sukari imekuwa kama biashara ya dawa ya kulevya ambayo inafanywa na kundi fulani tu watu lakini akataka mashirika ya hifadhi ya jamii kuagiza sukari.
“Unajua sukari ni kama dawa ya kulevya, wapo kundi fulani fulani tu la watu. Baadhi yao hawawajali Watanzania, hao ni wanafiki kabisa…wanaagiza sukari iliyokwisha muda wake toka Brazil na kuja kuuza hapa. Wafanyabiashara wa namna hii siwezi kuwavumilia iwe wanatoka CCM, Chadema, CUF kwangu ni mkong’oto tu," alisema na kuongeza:
“Wapo wanaotaka kukwamisha maendeleo, hao nina uhakika watashindwa, tena watalegea, sisi ni mbele kwa mbele. Simung’unyi maneno, nitadili nao mpaka mwisho.”
Akiwatoa hofu Watanzania alisema: “Msiwe na wasiwasi nchi itakwenda. Nina uhakika tutafanikiwa, kwa mshikamano huu waliouonyesha Watanzania tutafika mbali na hao watachoka tu. Nawahakikishia tutajipanga na kuwahakikishia Tanzania inasonga mbele.”
Akizungumzia zaidi kuhusu uwekezaji katika viwanda, alisema zaidi ya Sh. bilioni 60 zilizotumika kwa ujenzi wa majengo hayo mawili, kama zingewekezwa katika viwanda Watanzania wengi wangepata ajira, mashirika hayo yangepata wanachama wengine zaidi na serikali ingepata
mapato.
“Leo (jana) mngekuwa umewekeza katika viwanda ya sukari, hata wanaoficha sukari wasingetuchezea. Hakuna mtu atakayetoka nje kuja kuwekeza hapa,” alisema.
Alisema mifuko ya hifadhi ya jamii ipo saba na yupo tayari kutotoza kodi kwa muda fulani (tax holiday) kama wanayopata wawekezaji wengine iwapo watajikita katika viwanda.
“Hiyo ndiyo Tanzania ninayoitaka mimi…ninayoiota mimi, Tanzania ya viwanda,” alisema na kuongeza: “Mngekuwa mmejenga viwanda leo hapa mngejipanga barabarani kuandikisha vijana wa kufanya kazi.”
Akizungumzia kero za wakazi wa Arusha, alisema wanachohitaji ni kutatuliwa kero zao na siyo vyama vya siasa walivyonavyo.
“Uchaguzi umekwisha na ninawashukuru sana kwa kunipa kura nyingi za ushindi, tutafanya kazi kuwaletea maisha bora. Kitu kikubwa wanachohitaji Arusha ni kuondoa kero zao, wamechoka kuwa na kero. Watanzania wote tushikamane pamoja kwenda mbele. Tanzania ina kila kitu lakini wachache wanatuumiza,” alisema.
Mapema, Waziri wa Fedha na Mipango, Dk. Philip Mpango, alisema PPF litazingatia uwekezaji wa miradi itakayowafaa wastaafu na taifa kwa ujumla.
Naye Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge, Kazi, Ajira, Vijana na Watu wenye Ulemavu, Jenista Mhagama, alisema NSSF tayari imetenga Sh. bilioni 34 kwa ajili ya kufufua vinu vya kusaga nafaka vya Shirika la Usagaji la Taifa (NMC) vya mikoa ya Mbeya, Iringa, Dodoma na Mwanza.
Awali, Msemaji Mkuu wa CCM, Christopher Ole Sendeka, alimpongeza Dk. Magufuli kwa kazi kubwa anayoifanya ambayo imeiletea heshima taifa ndani na nje ya nchi.
Katika kuchangia elimu, PPF ilitoa madawati 2,000 na NSSF ilitoa madawati 4,000.
RC DODOMA AAGIZA TANI 154 ZILIZOKAMATWA KUUZWA
Siku moja baada ya Taasisi ya Kuzua na Kupambana na Rushwa (Takukuru) kwa kushirikiana na Kamati ya Ulinzi na Usalama mkoani Dodoma kukamata na kuzifungia tani 154 (kilo 154,000) za sukari katika ghala la mfanyabiashara Haidary Gulamali, Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Jordani Rugimbana, amelifungua ghala hilo na kuagiza kuanza kutoa huduma kwa wananchi.
Tani hizo154 zilidaiwa na Takukuru kukamatwa usiku wa Mei 7, mwaka huu zikiwa zimefichwa na mfanyabiashara na msambazaji huyo mkubwa wa sukari mkoani hapa kwenye ghala lake lililopo eneo la Kizota, Manispaa ya Dodoma.
Akizungumza na waandhishi wa habari katika ghala hilo jana, Rugimbana ambaye aliambatana na Kamati ya Ulinzi na Usalama ya mkoa, alisema wameamua kufungua ghala hilo kuanza kutoa huduma kwa wananchi kwa bei elekezi ya serikali kutokana uhitaji mkubwa kwa sasa wa bidhaa hiyo.
Aidha, alisema Kamati ya Ulinzi na Usalama ya mkoa inatoa onyo kwa wafanyabiashara wote mkoani Dodoma kuacha kuficha sukari waliyonayo, kwani serikali haitawafumbia macho bali itawachulia hatua kali za kisheria.
TANGA WAHAHA
Maeneo vinara yaliyokuwa yakitumika kuingiza sukari ya magendo mkoani Tanga ndiyo yamekuwa ya kwanza kuadimika bidhaa hiyo, huku wananchi wakilalamikia hali hiyo na kuiomba serikali kuingilia kati.
Mkoa wa Tanga unakabiliwa na changamoto ya uwapo wa bandari bubu 19 kwenye wilaya zilizopitiwa na Bahari ya Hindi za Tanga, Mkinga na Pangani, huku bidhaa kama sukari na mchele zikiingizwa kwa njia ya magendo kutoka nje ya nchi kupitia Zanzibar.
Baadhi ya wananchi wa eneo la Kigombe waliliambia Nipashe kuwa wanalazimika kuagiza sukari kutoka Tanga mjini au Pangani ambako wanainunua kwa zaidi ya Sh. 2,500 kwa kilo moja.
Walisema sukari ilianza kuadimika kwenye maeneo yao tangu serikali ilipobana waingizaji hususan kwenye bandari bubu ambako awali walikuwa wakinunua sukari kwa Sh. 800 kwa kilo moja.
UHABA BARA WAIBUA MAGENDO ZANZIBAR
Uhaba wa sukari uliyojitokea Tanzania Bara umeibua biashara ya magendo Zanzibar, kutokana na bidhaa hiyo kuendelea kupatikana kwa gharama nafuu visiwani humo.
Uchunguzi wa Nipashe mjini Zanzibar umebaini sukari imekuwa ikisafirishwa kwa njia za magendo kupitia bandari bubu tangu kuibuka kwa uhaba wa sukari na mfuko wa kilo 50 kuuzwa kwa Sh. 90,000 baada ya kuingizwa sokoni Tanzania Bara.
Sukari hiyo imekuwa ikisafirishwa kutoka Zanzibar na kuingizwa katika mikoa ya Tanga na Dar es Salaam kutokana na bidhaa hiyo kupatikana kwa bei poa Zanzibar.
Bei ya sukari Zanzibar mfuko wa kilo 50 unauzwa kwa Sh. 66,000 kwa sukari nyeupe na nyekundu Sh. 65,000, wakati katika soko la rejareja kilo moja ni Sh.1,500 mpaka Sh. 1,600 kwa sukari nyekundu.
Mfanyabiashara wa duka la sukari, Juma Ali, aliliambia Nipashe jana kuwa, wateja wanaonunua bidhaa hiyo kwa bei ya jumla wameongezeka Zanzibar tofauti na miaka ya nyuma.
Alisema wanaonunuzi sukari ya jumla kuanzia mifumo 10 mpaka 50 wameongezeka katika maduka ya jumla tofauti na siku za nyuma wateja walikuwa wa maduka ya rejareja kuanzia mifuko miwili hadi mitatu.
“Kazi yetu kubwa kuuza hatuhitaji kufahamu kama mteja katoka Zanzibar au Tanzania Bara, si kazi yetu, lakini wateja wa jumla wamekuwa wengi Zanzibar,” alisema Saleh Ali Mfanyabiashara katika duka la sukari Darajani.
Uchunguzi wa gazeti hili umebaini maeneo matano ya bandari yasiyokuwa rasmi yanatajwa kutumika kwa biashara ya kusafirisha sukari ya magendo, ikiwamo Bandari ya Mifungo ya Kisakasaka, Chukwani, Maisara, Mtoni na Micheweni, kisiwani Pemba.
Meneja wa Forodha wa Mamlaka ya Kodi ya Mapato Tanzania (TRA) Zanzibar, Ali Bakary, alisema doria zimekuwa zikifanyika, lakini mpaka sasa hakuna watu waliokamatwa kwa kusafirisha sukari tangu kujitokeza kwa uhaba wa bidhaa hiyo Tanzania Bara.
SUKARI KAMA ‘KAKAKUONA’ MWANZA
Kuadimika kwa bidhaa ya sukari nchini hususan katika mikoa ya Kanda ya Ziwa, kumekuwa kama mnyama maarufu ‘Kakakuona’, kutokana na kuadimika na kusababisha kupaa kwa bei ya bidhaa hiyo kila kukicha.
Uchunguzi wa Nipashe jijini Mwanza, Magu na Kahama umeonyesha kuwa, bei ya kilo moja ya sukari imekuwa mwiba kwa walaji kutokana na kupaa kwa kiasi kikubwa.
Katika jiji la Mwanza hadi kufikia jana, kilo moja ya sukari ilifikia Sh. 5,000 kwa baadhi ya maeneo, wakati sehemu nyingine ikiwa Sh. 4,000.
Baadhi ya wakazi wa Mwanza waliohojiwa na Nipashe jana, akiwamo mjumbe wa serikali ya mtaa wa Nera, Ezekiel Rufurungo, alisema sukari ipo katika baadhi ya maduka, lakini ikiuzwa kwa kujuana kwa Sh. 5,000 kwa kilo moja.
“Sukari ipo ila inauzwa kwa kujificha sana, maduka mengi yanaficha sukari, wauzaji hawataki kujulikana kama wanauza bidhaa hiyo, ndiyo maana wanakuuzia kwa kukujua, iwapo hufahamiki ukiuliza kama ipo utaambiwa haipo,” alisema Rufurungo.
Alisema kuuziana kwa kujuana kunatokana na hofu ya kukamatwa na maofisa wa TRA, Polisi, Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru) na Mamlaka ya Chakula na Dawa (TFDA), wanaotekeleza agizo la serikali la kuwasaka na kuwabaini wanaoficha sukari na kuuza kwa bei isiyo elekezi.
Naye mnunuzi na mfanyabiashara wa sukari ambaye ni mkurugenzi wa kampuni ya Birchand Group ya jijini Mwanza, Mohamed Shariff, alisema kwa muda mrefu hajapata bidhaa hiyo toka Oktoba, mwaka jana, baada ya kiwanda alichokuwa akinunua bidhaa hiyo kupunguza uzalishaji na kuongezeka kwa wanunuzi kuliko uwezo wa uzalishaji wa kiwanda.
“Hali ni ngumu kuliko kawaida, kila mahali wameweka makufuli, hivyo serikali inatakiwa kuwabana wenye nia mbaya na wanaotaka kujinufaisha na janga hili,” alisema Sharif.
Jijini Mwanza, polisi walikamata tani 26.5 za sukari yenye thamani ya Sh. milioni 53, ambazo polisi wanazifanyia uchunguzi iwapo mfanyabiashara husika alizificha au alikuwa akizigawa.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mwanza, Ahmed Msangi, alisema sukari hiyo ilikamatwa katika lori lililokuwa na trela aina ya Scania lililokamatwa mtaa wa Rufiji, wilayani Nyamagana.
TANI MBILI ZAKAMATWA KAHAMA
Kamanda wa Polisi Mkoani Shinyanga, Michael Nyange, alisema wamefanya ukaguzi katika wilaya ya Kahama na kukagua maghala ya wafanyabiashara John Hango, Nyorobi Kisabu, Mashaka Kaziro na Alex Magina.
Alisema katika ukaguzi huo uliofanywa kwa kushirikiana na kikosi kazi cha wilaya kinachojumuisha polisi, kamati ya ulinzi na usalama, TRA na Halmashauri ya mji, walikamata tani mbili za sukari (kilo 2,100).
Kwa sasa sukari kilo moja katika wilaya hiyo inauzwa kwa Sh. 3,000.